Nikirudi kwako mleta mada, uislamu umetoa muongozo wa kuwapenda watu na kuwachukia wengine vilevile, ama wasiokuwa waislamu sisi hatujakatazwa kuamiliana nao muda wa kuwa hawatufanyii uadui kwenye dini yetu wala hawatupigi vita na kututoa kwenye nyumba zetu.
Ama kwa asili ni kweli tunawachukia kwasababu nyinyi mmemkufuru mola wenu aliewaumba na muongozo aliowateremeshia kutoka kwake kwa huruma yake na mapenzi juu yenu.
Lakini chuki hii ni ibada hivyo ina vidhibiti na masharti yake na kiwango pia kinatofautiana na ndio maana mtume swala na salaam ziwe juu yake aliamiliana na wasiokuwa waislamu na aliandikiana nao mikataba, ama wale waliofanya chuki na kumpiga vita aliwapiga vita vilevile.
Lighton