Nitakujibu mimi kama mimi,Nimefundishwa na kuelimishwa Elimu inayohusiana na Uganga,Yaani tiba za jadi, zinazohusiana kuanzia miti shamba, kitabu cha Mungu na Uchawi ndani yake.
Kila mtu atakubaliana na mimi kabla ya kuja wakoloni, jamii yetu ilijitibu kwa miti shamba, siyo dhambi wala uchawi, dhambi inaanza pale utakapoambiwa unapokunywa hii dawa usimame katikati ya mlango au uangalie jua linapochomoza na useme maneno haya,hii haichagui uwe mpagani au mkristo umeshaingia kwenye ushirikina,
Na Quruani ni tiba, kuna aya ukizisoma unapoingia kulala, Unalindwa na vitu vibaya vyote kuanzia majini mpaka wachawi, na vilevile kuna aya ukisoma kama unaumwa unapona,
Lakini kuna watu kwa kufata matamanio ya Dunia wanachanganya mambo ya Uisilamu na uchawi, ndiyo maana tukafundishwa ni jinsi gani nitamgundua mganga mchawi,kwanza anakuwa na vitambaa vyeupe na vyekundu,mikia ya wanyama,ngozi za wanyama, mapembe ya wanyama na mengineyo,
Halafu hupenda kukwambia mambo yajayo kama vile kukutabilia ya kesho au kukukwambia sijui unarogwa na nani na mengineyo huo ndiyo uchawi,haijalishi huyo mtu ni mkristo, Muisilamu au mpagani