Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Kama mwenyekiti wa chama anapaswa kuchukua hatua badala ya kuzira.Kama atawaidhiria na jamaa wa EPA na Richmond kwamba wagawane wenyewe hali itakuwa mbaya sana.

Kila kitu kina mwanzo wakuu. Suala la EPA halimpi raha kabisa mkuu wa kaya na ni kweli atawashughulikia mafisadi kama alivyooanza.

Kumbukeni kwamba Jakaya amekutana na machafu yaliyofanywa na Mkapa, na ameanza kuwashughulikia wahusika. Ni nani alitegemea kuona ama kusikia Pesambili Mramba na Mgonja kupelekwa rumande?. Jamani tusione haya kumpongeza mkuu wa kaya pale anapofanya kitu kizuri kama vile ambavyo hatuoni haya kumbwatukia pale anapochemsha.

Utendaji una utaratibu wake, yeye kama mkuu wa nchi hawezi kuanza kusema mbovu hadharani. Pale Arusha alipoona uchafu ule kususa kwake kugawa zile baiskeli ni fundisho kubwa kwa watendaji wake wa chini kwamba mambo kama yale si mazuri na hayatakiwa kufanywa tena. Ki-ustaarabu ndiyo maana aliwaita chemba wahusika na kuwapaka choo.
 
Halafu ndio Malecela anasema CCM haina uhusiano na mafisadi? Utamwekaje fisadi, ambaye emshitakiwa na serikali kwa wizi kwenye meza kuu ya viongozi?

JK haitoshi kukataa kugawa hizo pikipiki, ilitakiwa kuwawajibisha pia hao waliotaka kukutumia kugawa mali hizo ambazo huenda zimepatikana kwa kutuibia kwenye miradi mbalimbali.

CCM na ufisadi ni mtu na ndugu yake, kama kuna wasafi mle ndani sidhani kama wanazidi 20%.

Aibu kweli, kama mpaka wanataka kumuingiza rais wa nchi kwenye michezo yao? kweli maadili yameporomoka TZ.

JK naye inaonekana ni weak mno, hao jamaa angewasemea hovyo hapo hapo. Kuna haja gani ya kuwaonea haya wababaishaji?
 
Tinga Tinga naye anaongee nini hapa chini? CCM inakumbatia wazi Mafisadi, hiyo ni ishara tosha kwamba CCM kama chama kina uhusiano na ufisadi TZ

Malecela: Ufisadi usihusishwe na chama
Merali Chawe, Mbeya
Daily News; Sunday,January 11, 2009 @21:15

Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Malecela amesema upungufu na dosari za mtu mmoja mmoja ikiwamo tuhuma za ufisadi na rushwa, zisihusishwe na chama hicho.

Malecela aliyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili mkoani Mbeya kushiriki kampeni za kumnadi mgombea wa CCM, Mchungaji Luckson Mwanjale katika kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini, unaofanyika Januari 25, mwaka huu.

Alisema Katiba ya CCM inataka mambo maovu yashughulikiwe na kupigwa vita, na kuongeza kuwa kila palipo na viongozi lazima kuna dosari zinazoweza kujitokeza na kwamba dosari za mtu binafsi zisihusishwe na chama ambacho kipo mstari wa mbele kupiga vita vitendo viovu ikiwamo masuala ya ufisadi.

Alisema Serikali ya CCM itahakikisha kila panapokuwa na dosari inashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizopo. "Mapungufu ya mtu mmoja yasihusishwe na chama" alisema mwanasiasa huyo mkongwe.

Aidha, alisema hata vyama vya upinzani ambavyo vimekuwa mstari wa mbele kukituhumu Chama Cha Mapinduzi, navyo vimekuwa vikikabiliwa na migogoro huku viongozi wake wakituhumiana kutumia vibaya fedha za vyama vyao.

Akizungumzia sababu za kuja kushiriki kampeni za uchaguzi wa jimbo hilo, Malecela alisema wenye jukumu la kuendesha kampeni za uchaguzi huo ni Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Mbeya na kwamba wao wamekuja kusaidia.

"Kule kwetu ukichinja ngo'mbe au mbuzi, wakati wa kuchuna ngozi unamwita mtu akusaidie kushika miguu ili uchune vizuri," alisema na kuongeza kuwa amekuja kusaidia kampeni katika kuhakikisha CCM inaibuka na ushindi Januari 25.

Alipuuza shutuma na kebehi ambazo zimekuwa zikitolewa na viongozi wa vyama vya upinzani, ambapo kazi ya CCM ni kuwaonyesha wananchi kazi walizozifanya, na kwamba wananchi wamekuwa wakishiriki katika shughuli za maendeleo na wanafahamu mafanikio wanayoyapata. Alivitaka vyombo vya habari kuwafichua watu wanaowarubuni wananchi na kununua shahada za kupigia kura ili wachukuliwe hatua za kisheria. "Ukiona watu wananunua shahada za wapiga kura ujue hao hawana sera," alisema.
 
wakuu naona hamkubali kwamba mkuu wa kaya kaanza kuwalia mingo mafisadi. Kukataa zawadi zao waziwazi ni dalili tosha kwamba Jakaya ametambua kwamba waliompigia kura wanataka afanye nini.

Sasa ndo tunauliza kwa nini tumpongeze?
 
Wakati mwingine "Retreat" ni mkakati mzuri wa kushinda. Si lazima kila wakati kumshambulia mtu uso kwa uso, hasa kama hujui unapingana na nguvu kiasi gani.
Sijasema kwamba lazima JK amefanya safi kabisa lakini pia nampa haki ya angalau kutambua kuwa kuna tatizo hapa, ndio maana akaacha. Baada ya hapo ndio labda atafanya utafiti, labda hakujua kuwa amepangiwa kugawa pikipiki akiwa hapo akashitukizwa tu nae akashituka, lakini akawa jasiri wa kukataa. "Some times give the devil his due rigths"
 
wandugu,

..hizo pikipiki zimetolewa na mafisadi ambao hawako kundi moja na Raisi Kikwete.

..zingetolewa na wale mafisadi wanaomuunga mkono basi angetoa baraka zake na kuzikabidhi kwa wanachama.

..Sophia Simba amechaguliwa kwa kutumia rushwa ya fedha za mafisadi walioko ktk kundi la Raisi Kikwete. hiyo ndiyo sababu iliyomfanya Raisi aivumilie rushwa ktk uchaguzi wa mwenyekiti wa UWT.

NB:

..ukitaka ufanikiwe ktk masuala ya ufisadi inabidi uwe ktk kundi linamuunga mkono Raisi Kikwete ndani ya CCM.

..kujifanyia ufisadi kivyako-vyako kama Mramba,Yona,na Mgonja, is too risky these days.
 
QUOTE"Pikipiki ni zenu mnajua mlipozipata mimi nimezishuhudia…gawaneni wenyewe," alisema Rais Kikwete. QUOTE

Hii ni rushwa sawa na rushwa zingine, hakutosha kukataa angeomba takukuru walifanyie kazi na kubaini kama haikuwa mbinu ya kushawishi rushwa.
 
Wakati mwingine "Retreat" ni mkakati mzuri wa kushinda. Si lazima kila wakati kumshambulia mtu uso kwa uso, hasa kama hujui unapingana na nguvu kiasi gani.
Sijasema kwamba lazima JK amefanya safi kabisa lakini pia nampa haki ya angalau kutambua kuwa kuna tatizo hapa, ndio maana akaacha. Baada ya hapo ndio labda atafanya utafiti, labda hakujua kuwa amepangiwa kugawa pikipiki akiwa hapo akashitukizwa tu nae akashituka, lakini akawa jasiri wa kukataa. "Some times give the devil his due rigths"

asante mkuu kwa kunisadia kuelewesha kwani nilikuwa nina maanisha kama ulivyoandika.

Watanzania waliompa kura 2005 walikuwa na kiu ya maisha bora ikiwa ni pamoja na kuupiga vita ufisadi. Mkuu alipoingia kitini alilielewa hilo lakini taratibu akaanza kujisahau, lakini baada ya matokeo ya hivi karibuni na kelele za wananchi toka kila pande amesituka na kukosa usingizi katika hili suala. Ameanza kulishughulikia hivi karibuni baada ya kujua nani ni nani na ana nguvu gani?. Kwa hilo jamani tusione haya kumpa hongera.
 
Huo ni unafiki mkubwa sana.Kwa nini hakuzikataa zile za za Somaia kwa UVCCM?? Kwa nini hakukataa michango ya Sophia Simba na mafisadi waliowezesha kampeni zake
chafu hadi kushinda?? Unataka kuniambia JK hakujua kama kuna michango michafu ilitolewa kwa Sophia??? Sema kuwa Njake si katika wale ambao ni marafiki wa JK??? Angezitoa Rostam au Manji angezikataa??? Asituletee sinema hapa.
 
Habari za Kitaifa Habari zaidi!
Kikwete aonya dhidi ya siasa za chuki, uhasama
Mgaya Kingoba, Pemba
Daily News; Wednesday,January 21, 2009 @09:32

RAIS Jakaya Kikwete amesema siasa za chuki na uhasama hazifai, na badala yake ushindani wa kidemokrasia unatakiwa kuwapo katika mfumo wa vyama vingi.Amesema ni vyema wanasiasa wakapiga maneno majukwaani na kushawishi kura za wananchi na kukubali kushindwa, badala ya siasa za chuki zikiwamo za uchomaji wa majengo na kuhatarisha amani.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akihutubia wananchi wa Jimbo la Konde, Wilaya ya Micheweni, Kaskazini Pemba, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika risala yao, uongozi wa tawi hilo la CCM ulieleza kwamba ofisi ya awali ilichomwa moto Novemba mosi, 2005 na watu waliowaita maharamia wa Chama cha Wananchi (CUF), baada ya kushindwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huo. “Ni vyema wanasiasa wakapiga maneno jukwaani na kuwashawishi wananchi, na pia kujenga utamaduni wa kukubali kushindwa.

Lakini hili la kuchoma moto ofisi halionyeshi ushindani, ni siasa za chuki na uhasama, hizi hazifai,” alisema. Mwenyekiti huyo wa CCM alisema siasa za namna hiyo ni za uhasidi na chuki, na CCM kama baba, itaendelea kuwa darasa la kufundisha siasa za kidemokrasia za kushindana bila kuvunja amani na utulivu nchini.

“CCM hatuchomi nyumba za watu, hatuweki watu ngeu. Siasa gani za kuchoma nyumba za watu? Sisi hatubagui na tutaendelea kutoa darasa kwa kuwa ndio baba anavyopaswa kuwa. Tujifunze kukubali matokeo,” alisema Rais Kikwete. Aliwaahidi wanachama wa tawi hilo kuwa atachangia ujenzi wake kwa kutoa bati, saruji, madirisha na dari.

Kwa mujibu wa taarifa ya CCM tawi hilo, ujenzi wake ulianza Novemba 17, 2005 kwa nguvu za wananchi na kuchangiwa na viongozi mbalimbali na hadi sasa wametumia Sh milioni 4.59. Ilieleza taarifa yao kuwa katika uchomaji huo, pikipiki ya VESPA iliteketezwa kwa moto pamoja na mali nyingine za chama
 
Hongera Kikwete kwa kazi nzuri AU
Mhariri
Daily News; Sunday,February 01, 2009 @21:15

Tanzania leo inamaliza uenyekiti wake wa mwaka mmoja wa Umoja wa Afrika (AU) uliokuwa ukishikiliwa na Rais Jakaya Kikwete, tangu Februari mwaka jana. Rais Kikwete anamaliza muda wake wakati wa mkutano wa kawaida wa viongozi wa nchi na serikali wa Afrika watakapoanza rasmi mkutano wao leo mjini Addis Ababa, Ethiopia, yalipo makao makuu ya AU.

Rais Kikwete anafanya hivyo kutokana na utaratibu wa kawaida wa Katiba ya AU ambayo inaeleza kuwa nafasi hiyo itakuwa ya kuzunguka baina ya nchi wanachama kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Tanzania chini ya Rais Kikwete inakabidhi uenyekiti huo wa AU, ikiwa na mengi ya kujivunia iliyoyafanya wakati wa mwaka wake mmoja wa kushika wadhifa huo mzito na wenye majukumu mengi. Rais Kikwete amefanya mengi ya kukumbukwa chini yake akiwa Mwenyekiti wa AU.

Tanzania, kwa msaada wa AU ilikwenda katika kisiwa cha Anjouan nchini Comoro ambako iliweza kumwondoa madarakani kiongozi muasi, Kanali Mohamed Bakar baada ya kujitangazia madaraka kinyume cha Katiba katika kisiwa hicho.

Majeshi hayo ya Tanzania ya vijana 700 waliweza kuhakikisha muasi huyo anaondoka nchini humo na anawaacha wananchi wa Anjouan wakifurahia maisha katika kisiwa chao kwa amani, bila ya umwagaji damu. Hongera Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Hongera Rais Kikwete.

Si hilo tu. Kwa juhudi zake na kwa kuwa mstari wa mbele, Rais Kikwete alikwenda Kenya na kumaliza mzozo na machafuko yaliyotokana na Uchaguzi Mkuu wa Desemba 2007, ambao ulisababisha mauaji ya Wakenya zaidi ya 2,000.

Mwenyekiti huyo wa AU kwa busara na uwezo wake, alizishawishi pande zilizokuwa zikivutana katika mzozo huo wa uchaguzi, kukaa meza moja na kufikia makubaliano ambayo sasa Kenya ni moja na wanaijenga nchi yao.

Jingine alilolifanya katika kuleta amani ni suala la mgogoro wa muda mrefu wa Burundi ambako amewezesha kusitishwa kwa mapigano na kufikiwa kwa mkataba wa amani baada ya mauaji na vita ya muda mrefu kati ya waasi na jeshi la serikali.

Juzi, siku chache kabla ya kukabidhi madaraka leo, alikuwa Afrika Kusini, ambako kwa wadhifa wake wa uenyekiti wa AU, alishirikiana na viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuzishawishi pande zinazovutana Zimbabwe kutekeleza makubaliano ya kugawana madaraka yaliyofikiwa Septemba mwaka jana baada ya uchaguzi uliokuwa na kasoro.

Yapo pia ya kuleta mabadiliko katika Sekretarieti ya AU mjini Addis Ababa ambako kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Rais Kikwete amemaliza tatizo la muda mrefu lililokuwa likiwakabili watumishi katika Sekretarieti ya AU kwa kufanikisha kuongezwa mishahara ikiwamo kulipwa malimbikizo, posho za matibabu na elimu ambazo walikuwa wanadai kwa miaka mitano iliyopita.

Tunajua kuwa yapo masuala kadhaa ambayo pengine aliahidi au yalipaswa kutekelezwa katika kipindi chake cha uongozi wa mwaka mmoja, lakini ni ukweli usiofichika kuwa Rais Kikwete amefanya makubwa katika kipindi hicho.Ikumbukwe kuwa chini ya uongozi wake, ameweza pia kuifanya Tanzania na Afrika kwa ujumla, kuwa na sauti katika medani ya kimataifa, hali ambayo imeongeza ushawishi wa mataifa makubwa kwa Afrika.

Tunaamini Rais Kikwete anamaliza uenyekiti wa AU akiwa ametekeleza kwa ufanisi mkubwa na kwa umakini majukumu yake, kiasi kuwa ameliweka jina la Tanzania na Afrika kwa ujumla katika ajenda za mataifa makubwa. Tunampongeza Rais Kikwete kwa kazi nzuri na kumtakia kila la heri katika jukumu lake la kuwahudumia Watanzania baada ya jukumu kubwa na zito la kuwaongoza Waafrika kwa mwaka mmoja uliopita.
 
Kwa kweli ingawa sikubaliani nae kwa mambo mengi,lakini anastahili pongezi.Amejitahidi sana kuitangaza Tanzania,Ni opportunist mzuri ambaye kwa kweli ameweza kuitumia fursa yake vizuri huku akilitangaza bara la Africa na Tanzania kwa ujumla

Ni matumaini yangu kwamba ataelekeza nguvu zake kwa taifa lake sasa.Hongera sana Jk,Mungu akuzidishie Nguvu.Tanzania imeonyesha uwezo mkubwa kiongozi katika bara hili na dunia kwa ujumla.Kuanzia UN kwa Migiro,Bunge la Afrika kwa Mongela,Common wealth Dr.Shija,UNHABITAT kwa Prof.Anna Tibaijuka,Bunge la SADDC La Mhe.Sitta nk.

Mungu Ibariki Afrika,Mungu Ibariki Tanzania
 
Kwa kweli JK ni Mwenyekiti Bora kabisa wa EU tangu kuanzishwa OAU hadi kuzaliwa AU. Hongeara sana JK, na kwa kweli anastahili pongezi.

Hata hivyo, Mkuu wetu alionekana zaidi kama kiongozi wa Afrika kuliko Tanzania na hapa Tanzania hajafanya kama tunavyomtarajia na sipendi aje kuwa kama vile mwana JF aliwahi kusema huko nyuma kuwa huenda akaawa the worst president ever in Tanzania.

Kwa kuwa JK amemaliza Wenyekiti AU naamini nguvu hizo hizo atazirudisha hapa TZ ili tuwe na sababu ya kumuenzi kama tunavyomuenzi kwenye AU.
 
Mkuu Ibrah kama vp fanya marekebsho kidogo hapo juu,umeandika EU badala ya AU,maana nadhani EU inaleta maana nyingine kabisa mkulu...be blessed
 
Hongera Kikwete kwa kazi nzuri AU
Mhariri
Daily News; Sunday,February 01, 2009 @21:15

Tanzania leo inamaliza uenyekiti wake wa mwaka mmoja wa Umoja wa Afrika (AU) uliokuwa ukishikiliwa na Rais Jakaya Kikwete, tangu Februari mwaka jana. Rais Kikwete anamaliza muda wake wakati wa mkutano wa kawaida wa viongozi wa nchi na serikali wa Afrika watakapoanza rasmi mkutano wao leo mjini Addis Ababa, Ethiopia, yalipo makao makuu ya AU.

Rais Kikwete anafanya hivyo kutokana na utaratibu wa kawaida wa Katiba ya AU ambayo inaeleza kuwa nafasi hiyo itakuwa ya kuzunguka baina ya nchi wanachama kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Tanzania chini ya Rais Kikwete inakabidhi uenyekiti huo wa AU, ikiwa na mengi ya kujivunia iliyoyafanya wakati wa mwaka wake mmoja wa kushika wadhifa huo mzito na wenye majukumu mengi. Rais Kikwete amefanya mengi ya kukumbukwa chini yake akiwa Mwenyekiti wa AU.

Tanzania, kwa msaada wa AU ilikwenda katika kisiwa cha Anjouan nchini Comoro ambako iliweza kumwondoa madarakani kiongozi muasi, Kanali Mohamed Bakar baada ya kujitangazia madaraka kinyume cha Katiba katika kisiwa hicho.

Majeshi hayo ya Tanzania ya vijana 700 waliweza kuhakikisha muasi huyo anaondoka nchini humo na anawaacha wananchi wa Anjouan wakifurahia maisha katika kisiwa chao kwa amani, bila ya umwagaji damu. Hongera Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Hongera Rais Kikwete.

Si hilo tu. Kwa juhudi zake na kwa kuwa mstari wa mbele, Rais Kikwete alikwenda Kenya na kumaliza mzozo na machafuko yaliyotokana na Uchaguzi Mkuu wa Desemba 2007, ambao ulisababisha mauaji ya Wakenya zaidi ya 2,000.

Mwenyekiti huyo wa AU kwa busara na uwezo wake, alizishawishi pande zilizokuwa zikivutana katika mzozo huo wa uchaguzi, kukaa meza moja na kufikia makubaliano ambayo sasa Kenya ni moja na wanaijenga nchi yao.

Jingine alilolifanya katika kuleta amani ni suala la mgogoro wa muda mrefu wa Burundi ambako amewezesha kusitishwa kwa mapigano na kufikiwa kwa mkataba wa amani baada ya mauaji na vita ya muda mrefu kati ya waasi na jeshi la serikali.

Juzi, siku chache kabla ya kukabidhi madaraka leo, alikuwa Afrika Kusini, ambako kwa wadhifa wake wa uenyekiti wa AU, alishirikiana na viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuzishawishi pande zinazovutana Zimbabwe kutekeleza makubaliano ya kugawana madaraka yaliyofikiwa Septemba mwaka jana baada ya uchaguzi uliokuwa na kasoro.

Yapo pia ya kuleta mabadiliko katika Sekretarieti ya AU mjini Addis Ababa ambako kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Rais Kikwete amemaliza tatizo la muda mrefu lililokuwa likiwakabili watumishi katika Sekretarieti ya AU kwa kufanikisha kuongezwa mishahara ikiwamo kulipwa malimbikizo, posho za matibabu na elimu ambazo walikuwa wanadai kwa miaka mitano iliyopita.

Tunajua kuwa yapo masuala kadhaa ambayo pengine aliahidi au yalipaswa kutekelezwa katika kipindi chake cha uongozi wa mwaka mmoja, lakini ni ukweli usiofichika kuwa Rais Kikwete amefanya makubwa katika kipindi hicho.Ikumbukwe kuwa chini ya uongozi wake, ameweza pia kuifanya Tanzania na Afrika kwa ujumla, kuwa na sauti katika medani ya kimataifa, hali ambayo imeongeza ushawishi wa mataifa makubwa kwa Afrika.

Tunaamini Rais Kikwete anamaliza uenyekiti wa AU akiwa ametekeleza kwa ufanisi mkubwa na kwa umakini majukumu yake, kiasi kuwa ameliweka jina la Tanzania na Afrika kwa ujumla katika ajenda za mataifa makubwa. Tunampongeza Rais Kikwete kwa kazi nzuri na kumtakia kila la heri katika jukumu lake la kuwahudumia Watanzania baada ya jukumu kubwa na zito la kuwaongoza Waafrika kwa mwaka mmoja uliopita.

Chumvi imezidi hapa. But all in all nina wasiwasi na mrithi wake Col. Ghadaffi..
 
Mkuu Ibrah kama vp fanya marekebsho kidogo hapo juu,umeandika EU badala ya AU,maana nadhani EU inaleta maana nyingine kabisa mkulu...be blessed

Asante Home boy, nlimaanisha AU=African Union na si EU.
 
Sifa njema ni kutoka kwako ulikolala.Hapa wadigo tunamaanisha kuwa endapo utasifiwa ugenini kwa mema uliyowatendea kule utokakko yapaswa sifa hizo zilishavuma muda mrefu.Sasa hapa kwetu hizo sifa hazipo.Msimpambe pambe sana kama hivyo,Nakuhakikishieni kweli kabisa sifa zilizopo sizo hizo kabisa.Muulizeni Mbeki kuhusu tatizo la Zimbabwe,Pia muulizeni Museveni na Kagame kuhusu swala la DRC-Kwamba role ya mwenyekiti wa AU ilikuwa nini na alifanya nini???Kule Somalia,na Mauritania!Jeshi letu JWTZ lilienda kwa ridhaa ya nani kule Anjwani,Si ni kwa ridhaa yake kama Mkuu wa Majeshi Tz???Lakini madhara yake si yanaiumiza Nchi????Mbona Kony wa Uganda,Vurugu za Eritrea,Djobout na kwingineko hakuziona?
Najua mnampamba kwa ushabiki tu kwa kuwa nanyi mnapenda disco kuliko maendeleo.
 
Mkuu Ibrah kama vp fanya marekebsho kidogo hapo juu,umeandika EU badala ya AU,maana nadhani EU inaleta maana nyingine kabisa mkulu...be blessed

You have an eye of details - hongera! You can edit me too.....ha ha haa
 
- Hapa tupo wote, kwenye AU amefanya kazi inayoridhisha kidogo kuliko hapa nyumbani, lakini anahitaji credit ingawa sasa tungetegemea arudishe nguvu zote hapa nyumbani.

Mungu Aibariki Tanzania.
 
Mimi si kwamba niko negative kihivyo ila kama Piemu napata tabu ya kujuwa ni kwanini hasa waliomwanga hizo sifa lukuki kwa msanii wetu wamefanya hivyo. Au ni huu utanzania wetu wa kuandama kumpongeza mtu kwa hotuba? AU imekuwa bonge la double standard katika kipindi chake. Tatizo moja hili hilo limekuwa treated tofauti kabisa kwa nchi moja na nyingine. Tukiwa makini mtaona kabisa sisi kama nchi tumepata hasara kwa huu uenyekiti wa AU. It would have been much better kama tusingelionja kabisa hiyo position.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom