Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Mie nadhani hapa pongezi atazipata atakapokuwa amefika mwisho na kupimwa kwa alichokifanya. Kelele zimepigwa nyingi, tusijekudanganyika kuwa kesha tenda wakati mambo makubwa wakati yote anayotakiwa kuhakikisha kwa mujibu wa katiba anayasimamia na kuyatekeleza hata kwa 20% bado. Mie nadhani ungeshauri tuendelee kumpigia kengele kuwa hapo alipofika ndio kwanza bado kabisa!
 
Tumpongeze Raisi wetu - MH. Jakaya Kikwete

Kwa lipi tumpongeze? Kwa kuleta Maximo na taifa stars kuifunga Sudan?
Maybe una intend kusema hilo MWIBA/THORN?
 
Mimi binafsi nikiridhishwa na utendaji wake sioni sababu ya kutotoa pongezi zangu kwake, lakini kwa sasa sioni sababu zozote za kufanya hivyo. Bado mikataba ya madini isiyo na maslahi kwa Tanzania haijashughulikwa, bado Mwanyika na Hosea wanapeta pamoja na kutolewa ushauri na Tume ya Mwakyembe kwamba waondolewe madarakani. EPA nayo bado imegubikwa na usanii wa hali ya juu. Bado anafanya kila njia kuukimbia utata wa mgodi wa Kiwira, sera za maisha bora kwa kila Mtanzania sijaziona. Bado sijaridhika kwa kweli. Hivyo sioni sababu ya kutoa pongezi zangu.
 
Ukimpongeza best lazima kichwa chako kina uwezo mdogo sana kwa kuona mambo yalivyo. Na kama huna taarifa zaidi ya hizi unazosikia na wewe ni mvivu wa kutafuta tarifa, lazima ujikute humu jamvini ukisema kama wale wazee wa kijijini, jamani saasa tumpongeze.

Amka uzingizini...! saidieni hivi vichwa jamani, ndo hawahawa waliipigia ccm kura.
 
Nahitaji maoni yenu zaidi kuhusika na uongozi wa Rais Mheshimiwa Jakaya Kikwete,kwa nionavyo mimi na baadhi ya wengi tu kuwa mheshimiwa anastahili kuongezwa nguvu ,hii ataipata ikiwa tutakuwa mstari wa mbele katika kumuunga mkono juu ya hatua aliyofikia katika kutatua matatizo ya wananchi.

Wengi wetu wanaona ni kazi rahisi na ya mara moja ,lala amka mambo powa kila mkoa na kijiji unapata mahitajio kamili na haya matamanio utayakuta kwa wale ambao hawawezi kupambambanua na wafinyu wa kufikiri wao kwao kila jambo ni rahisi ,hawa ndio wale waliokuwa hawaishi kumlaumu Mheshimiwa Raisi na serikali yake.

Si vibaya kumlaumu Raisi na zipo njia nyingi za kumlaumu yakiwemo maneno makali yenye kuudhi na kukatisha tamaa ila Raisi wetu ameweza kuyafahamu na kuwafahamu watu hao haraka nao pia wanauchungu wa Nchi hii na kama Raisi alitakiwa na ndivyo anavyofanya kutumia busara za hali ya juu sana ,japo wasiopenda maendeleo yake wanaona giza tu na kama hakuna linalofanyika kwa kuwa tu ile haraka wanayoitaka sivyo inavyotekelezwa na Mwenye Busara ambae ni Raisi Jakaya Kikwete,kuna watu hawapendi wakimwona anasafiri mara kwa mara ,watu hawa ni wale wasio mtakio ufanizi katika kuwajibika na majukumu ambayo kama Raisi na ambae ana uzoefu wa hali ya juu kuhusu nchi za nje kwa alivyokuwa akifanya kazi hiyo,Mheshimiwa Raisi kwa nionavyo ameona itakuwa rahisi majukumu kutekelezeka ikiwa atayavalia njuga mahitajio na kuyafuatia yeye mwenyewe.
Tumpongeze Raisi Kikwete na azidi kuwa mstari wa mbele yeye kama kiongozi Mkuu wa Watanzania.Sisi tukizidi kumpongeza na kumpa sifa anazostahili ndipo nae atakapozidi kuwa mwadilifu na kuhakikisha yale anayoyapanga yanathaminiwa na wananchi wake hivyo itakuwa rahiri kwa yeye kutekeleza amri zote ambazo zitaonekana nzito kwa wengine.

Hongera raisi Kikwete

Mimi nampongeza kwa sababu kipindi alichoingia kilikuwa kigumu na mitihani kibao.Kwanza kabisa alipambana na njaa na akahakikisha kuwa chakula kinapatikana.Hili halina mjadala.

Kutokana na matatizo makubwa ya umeme,mafisadi wakajiingiza na hakuna mtu asiyejua mambo yalivyokwenda hadi EL na mawaziri wengine wakatimuliwa.Zamani matokeo ya tume yalikuwa yakihifadhiwa kwenye kabati.period.na wananchi wanasahau.

Matatizo mengine aliyarithi kutoka awamu ya tatu,wengi wetu tumeyachanbua hapa JF na matokeo yake watuhumiwa wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria na kesi zipo.Hukumu zitatoka.Mengine yanaendelea kushughulikiwa kwa taratibu za nchi.

JK amejikuta yuko njia panda kwa sababu ya mapambano ya kisiasa ndani ya CCM.Nia yake ni kuiongoza nchi kwa njia za kistaarabu lakini kuna wahafidhina wanamrudisha nyuma.JK bado yupo na ni matumaini kuwa atakuwa kidedea dhidi ya wapinzani wake ndani ya CCM.

Amefanya mambo ambayo wananchi wanayataka ayafanye na hii ni credit upande wake.
Uhuru wa kutoa maoni bila kushughulikiwa umetanuka(Muulize Jenerali Ulimwengu)Uhuru wa kuandamana ndiyo huo hadi anarushiwa mawe.

Watu wa Pemba walipotangaza kuwa wanajitenga alichukua hatua za kidiplomasia badala ya mabavu.Hajaua mtu yeyote anayeandamana.(Waulize kina Lipumba na Maalim Seif)

Wamemsema sana kuwa ni weak lakini matukio ya hivi karibuni yemeonesha siyo hivyo.Kule kupanda kwa hali ya maisha kunatokana na hali ya uchumi wa dunia kwa jumla.Kupanda kwa bei za mafuta kulipandisha bei za bidhaa kadhaa lakini sasa bei zinashuka na mambo yanaekea kuwa afadhali.

Kapangua baraza la mawaziri ili ku accomodate matakwa ya wananchi na juzi kapanga makatibu wakuu ili kushinikiza utendaji bora serikalini.

Tuna sababu ya kumpongeza na kumpa moyo Rais wetu.

Unapoweza kuwa na appreciation kwa madogo unampa mtu nguvu kuweza kufanya makubwa,wanadamu si rahisi kuwasatisfy ktk yote,ufupi nampongeza RAIS kwa kias chake kwa sababu zifuatazo;
1.Ametoa uhuru japo kdogo ktk vyombo vya habari,waut sasa wanaongea bila kuingiliwa sana
2.Ameweza kutoa fikra potofu za viongozi waliokuwa nazo ya kuwa wakisha pata madaraka basi wanaweza kufanya chochote bila kuingiliwa na kuulizwa abuse of power and public funds
3.
4.
5.
Tujue mazuri makubwa alofanya tumpongeze na mengine tumshauri aboreshe vip lakini sio kusema ati hakuna kitu amefanya.


Stupidiest comments ever seen in JF in recently days!

Hivi huyo rais anpokuja kuomb kura anwaambia atafanya kitu gani?? mnapotok nyumbani kweni siku ya kupiga kura mnataka afanye nini?

hivi mbumbumbu kama nyie msi waza japo kidogo uwezo na wajibu wa rais si ndio mnafuga ujinga, wezi n.k

Hivi Kikwete akija leo na kuwaomba vitu fulani mtampa tu......

sura inawachanganya?? mtu anafanya kazi kwa presha za donors leo mnamsifia

mpeni basi wake AU waume zenu afurahi


NYIE NDIYO MAFISADI NAMBA MOJA ZERO BRAIN IN TANZANIA, TENA NGAU MNA UWEZO WA KUSURF INTERNET MNA UWEZO MDOGO WA KUFIKIRI KAMA WA PANYA JE, WALE WASIOSOMA KABISA SI NDO WANALEWA MATAPUTAPU KWA FURAHA NA 2010 ANAINGIA TENA IKULU.

BASI TU HAMUONEKANI,NINGEWACHAPA VIBAO

NYIE NDIYO MNAJUA VIONGOZI NI MIUNGU WAKATI NI WATUMISHI WETU

YAONE VILE UJINGA TU!1

ALA!!!!!!!
 
Unapoweza kuwa na appreciation kwa madogo unampa mtu nguvu kuweza kufanya makubwa,wanadamu si rahisi kuwasatisfy ktk yote,ufupi nampongeza RAIS kwa kias chake kwa sababu zifuatazo;
1.Ametoa uhuru japo kdogo ktk vyombo vya habari,waut sasa wanaongea bila kuingiliwa sana
2.Ameweza kutoa fikra potofu za viongozi waliokuwa nazo ya kuwa wakisha pata madaraka basi wanaweza kufanya chochote bila kuingiliwa na kuulizwa abuse of power and public funds
3.
4.
5.
Tujue mazuri makubwa alofanya tumpongeze na mengine tumshauri aboreshe vip lakini sio kusema ati hakuna kitu amefanya.


Swala ni kwamba tunarudi kwenye habari ya "low expectation" tuliyonayo na hii ni mbaya sana.Nchi yetu inahitaji mambo mengi sana kwahiyo kiongozi must take high scores not down score and we need to see the output.

Kuna watu walikuwa wanapongezwa na wazazi kwa kupata just 50% ya mtihani na wangine walikuwa wakipata 90% walikuwa wakiambiwa umejitahidi ila ungeweza kupata zaidi ya hii ongeza bidii you can do better than this son.
Tusiwe tuna spoil viongozi wetu kwa kupongeza kwa kufanya kidogo ktk wajibu wao na ndio maana hutufanyia sanaa wakijua tutalizika .

Wengine wanadai Rais kakutana na mambo magumu ! kwani urais mchezo,na ndio sisi wengine tutapongeza kwa ku overcome magumu yup!Na haya yanayotokea sasa hivi kwanza itabidi tusubiri tuone maana kutofautisha masuke na ngano kwa sasa si rahisi.Watanzaia waungwana matatizo yaliyopo yanajulikana akishughulikiwa hatuta sita kumsifia kama watu waliweza kumpa kura zote hizo .
Hebu fikiria sasa hivi bado tunapigana na system mbovu ya uongozi lini tutafika kwenye kutengeneza ajira just imagine pace tunayokwenda nayo kisha tupongezane.

Unadai vyombo vya habari viko huru ,its just time kama mtandao utazuiaje?Huwezi labda mwanahalisi sijui ndio waliweza inawa unapongeza.Jamani tuache pia habari ya ku compare ,ati uki compare na waliopita.....no sisi ni kizazi kingine tuamke tusukume viongozi si wafanye mema ila kazi zao kama inavyotatikana ,tusifananishe na walioshindwa.

Sisi tunafanya kazi kupigia kelele maovu,ufisadi,uzembe na tunahitaji ufanisi ndio support yetu.
 
Pongezi zangu zitakuja pindi haya yakifanyika:-

1. Watuhumiwa WOTE wakifikishwa mbele ya sheria na sheria KUACHWA kuchukua mkondo wake (na si vinginevyo).

2. Wezi wetu wote (pamoja na hawa waliofikishwa Kisutu) wakitendewa sawa na walivyolitendea Taifa bila kujali ushkaji na kulindana. Yani ikiwezekana adhabu yao iwe ni kunyongwa (kumradhi kama nahukumu vibaya as I believe ndiyo adhabu nzuri kwao). Rostam, Karamagi, Mkapa, Lowassa na wenzao ambao wamekuwa wakitajwa na tena kuoneshwa kwa vithibitisho kadha wa kadha wakifanyiwa uchunguzi wa kina na watanzania wakafahamishwa kwa ukweli na uwazi ili heshima zao ziendelee kupanda na kama ni kushuka zifikie ZERO!

3. Katiba ya nchi itafanyiwa marekebisho na kipengele kinachoweza kuwa kinamlinda rais ama kiongozi yeyote fisadi kikaondolewa na wote waliotupeleka kusiko wakahukumiwa sawa na matendo yao.

4. Rais akikubaliana nasi kuwa taifa hili ni letu sote na kufikiria kuwa na baraza dogo la mawaziri lenye 'wazalendo' wa kweli na hata kuwa na kiongozi walau mmoja ama wawili toka vyama vya upinzani.

5. Rais akiweza kudhibiti mfumko wa bei na kuangalia uwezekano wa kutimiza "Maisha bora kwa kila mtanzania" kabla ya mwaka 2010.

Tofauti na haya matano (kwa uchache) nina imani kubwa kuwa 'uzembe' wowote unaoweza kutendeka na kupelekea viongozi ambao ni wazi watanzania HAWATAKI HATA KUSIKIA MAJINA YAO wakaonekana hawakuwa na hatia kwa upindishwaji wa namna yoyote iwayo wa sheria ama kulindwa basi kutatupeleka kusiko kabisa.

Ni mawazo yangu tu
 
Raisi Gnassingbé Eyadema wa Togo aliwahi kusifiwa na baadhi ya wananchi wake kwa kuwezesha mvua kunyesha !! - ndivyo wengine wetu tulivyo.
 
Pongezi zangu zitakuja pindi haya yakifanyika:-

1. Watuhumiwa WOTE wakifikishwa mbele ya sheria na sheria KUACHWA kuchukua mkondo wake (na si vinginevyo).

2. Wezi wetu wote (pamoja na hawa waliofikishwa Kisutu) wakitendewa sawa na walivyolitendea Taifa bila kujali ushkaji na kulindana. Yani ikiwezekana adhabu yao iwe ni kunyongwa (kumradhi kama nahukumu vibaya as I believe ndiyo adhabu nzuri kwao). Rostam, Karamagi, Mkapa, Lowassa na wenzao ambao wamekuwa wakitajwa na tena kuoneshwa kwa vithibitisho kadha wa kadha wakifanyiwa uchunguzi wa kina na watanzania wakafahamishwa kwa ukweli na uwazi ili heshima zao ziendelee kupanda na kama ni kushuka zifikie ZERO!

3. Katiba ya nchi itafanyiwa marekebisho na kipengele kinachoweza kuwa kinamlinda rais ama kiongozi yeyote fisadi kikaondolewa na wote waliotupeleka kusiko wakahukumiwa sawa na matendo yao.

4. Rais akikubaliana nasi kuwa taifa hili ni letu sote na kufikiria kuwa na baraza dogo la mawaziri lenye 'wazalendo' wa kweli na hata kuwa na kiongozi walau mmoja ama wawili toka vyama vya upinzani.

5. Rais akiweza kudhibiti mfumko wa bei na kuangalia uwezekano wa kutimiza "Maisha bora kwa kila mtanzania" kabla ya mwaka 2010.

Tofauti na haya matano (kwa uchache) nina imani kubwa kuwa 'uzembe' wowote unaoweza kutendeka na kupelekea viongozi ambao ni wazi watanzania HAWATAKI HATA KUSIKIA MAJINA YAO wakaonekana hawakuwa na hatia kwa upindishwaji wa namna yoyote iwayo wa sheria ama kulindwa basi kutatupeleka kusiko kabisa.

Ni mawazo yangu tu



HAAAAAAAAAAA kaka umeongea vema ila pa blue panatisha ingawa wakina China ndivyo walivyotiana adabu.
Ndio maana unajaribu kuwaambia watu tuna kazi kubwa sisi kwa sehemu yetu na viongozi.Kweli akiyafanya/kuwezesha hayo ulisema ukiacha pa blue ahahaaa,kweli tutampa pongezi sasa ni mapema mno kwa pongezi.
 
HAAAAAAAAAAA kaka umeongea vema ila pa blue panatisha ingawa wakina China ndivyo walivyotiana adabu.
Ndio maana unajaribu kuwaambia watu tuna kazi kubwa sisi kwa sehemu yetu na viongozi.Kweli akiyafanya/kuwezesha hayo ulisema ukiacha pa blue ahahaaa,kweli tutampa pongezi sasa ni mapema mno kwa pongezi.
Unajua nini mkuu, kuna mjumbe humu kaandika kuwa tunapigana na watu hatari na akaomba Mungu atupe ustahimilivu. Sasa watu kama hawa njia pekee ya kuwamaliza ni kuwapa adhabu kali ya kuweza kuwafanya wengine 'wakome' mara moja michezo inayoligharimu taifa.

Yet, ni mawazo yangu tu
 
Unajua nini mkuu, kuna mjumbe humu kaandika kuwa tunapigana na watu hatari na akaomba Mungu atupe ustahimilivu. Sasa watu kama hawa njia pekee ya kuwamaliza ni kuwapa adhabu kali ya kuweza kuwafanya wengine 'wakome' mara moja michezo inayoligharimu taifa.

Yet, ni mawazo yangu tu

Nakuunga mkono kuwa adhabu kali ndio inayostahiki maana vinginevyo ni kuruhu makosa kuendelea.
 
Wakuu,

Tuchukulie mfano mdogo tu usiohitaji mawazo makubwa. Kama wewe ni mfanyakazi, unapoenda kuomba kazi na ukakubaliwa, unapewa majukumu na matazamio. Ukitimiza majukumu na matazamio yako, basi utaambiwa kuwa umefanya vizuri kutimiza majukumu yako. Hii si pongezi, bali ni neno la kukuashiria kuwa unafanya kazi unavyotakiwa. Pongezi inakuja pale unapofanya kuliko vile unavyotarajiwa kufanya.

Nikirudi kwenye hoja ya kumpongeza Rais Kikwete, binafsi sijaona kile alichofanya "above and beyond". Kama mkuu invinsible alivyosema, watu bado maskini, elimu hovyo, afya duni, mfumuko wa bei hauna spidi gavana...kama akiweza kuyageuza mambo haya, basi pongezi itatoka kwa mkono mkunjufu kwani si kazi lelemama kutimiza haya yote katika kipindi cha miaka mitano au hata kumi.

Kama muanzisha hoja hii anakusudia kumpongeza Rais kwa kumtimua Ballali, kuondoka kwa Lowassa, kuwashtaki Mramba na Yona, nk, basi mkuu huyu amepotoka. Huu ni wajibu wa Rais. Hakushikiwa bunduki akiambiwa aende kuchukua fomu za kugombea urais. Alitaka mwenyewe. Hata kwa yule mwenye kusema kuwa Kikwete aliingia madarakani kwenye wakati mgumu, kwa kweli hiki kisiwe kisingizio. Alijua anajiingiza kwenye kazi ya namna gani kwani yeye alikuwa kwenye baraza la mawaziri kwa zaidi ya miaka kumi kabla hajawa Rais.

Naomba niwakumbushe wakuu kuwa cheo ni dhamana. Maana yake ni kuwa, mtu mwenye wadhifa ana jukumu la kulinda katiba na maslahi ya wananchi. Pia, anatakiwa ahakikishe kuwa haki na sheria zinafuatwa. Sasa kama mafisadi (bila kujali vyeo vyao) wamevunja sheria, ni wajibu wa serikali (inayoongozwa na Rais) kuwashughulikia. Japo kinadharia hakuna aliye juu ya sheria, kwa mfumo tulio nao (hakuna uhuru wa mahakama, hakuna checks and balances, Rais ndio mwenyekiti wa chama, nk), Rais ndio mwenye mamlaka ya mwisho. Ni uamuzi wake tu wa kumwelekeza DPP amshtaki nani na amwache nani.

Nimalizie basi kwa kufafanua dhana ya kuwa Rais ndio mwenye mamlaka ya mwisho...hivi kweli tumesahau kuwa ni majuzi tu Rais Mkapa aliamua kuvunja hadhi ya urais na kujiuzia mwenyewe Kiwira huku akitumia Ikulu kama ofisi yake ya kibiashara? Huo si ulikuwa usemi wa mwisho? Nani alithubutu kumpinga? Kazi ya urais si lelemama na tusimjaze ujinga Rais kwa kumpongeza kwa kufanya wajibu wake.
 
Kikwete haihitaji pongezi ya aina yeyote ile kwani naye ni chanzo cha matatizo yetu.
Alikuwa wapi wenzeke wakiiba. kwani hakuona mbona kangoja mpaka watanzania tunataka kutoa mtu roho.
Aliyaona ya Hazina akiwa waziri wa fedha.
aliyaona ya nishati akiwa waziri wa nishati.
aliona wakiiba fedha kwa ajili yake ili awe rais.
Alikuwa nao kwenye baraza la mawaziri wakibariki kutupiga bakora za umasikini
Alisafiri nao alikula nao aliiimba nao, aliiba nao.
kikwete sio mwenzetu ni mwenzao, ila mkiwa mnazama husemi tuokoe unasema niokoe.
hata shetani ukimuuliza anasema ni binadamu na binadamu anasema ni shetani.
Huu mzunguko ukipelekwa vizuri naye yumu.
sadaka ya madaraka na utawala usio na sheria unaweka pazia jeusi na wadanganyika wanashindwa kujua kipi cheusi wanashangilia.
Aliwapa uwaziri, walipanga jinsi ya kutughilibu sasa wanacheza siasa za ukweli usanii juu ya kisahani ndani ya nyumba ya sanaa........kwi kwi kwi machozi yanatoka kwa uchungu
 
Stupidiest comments ever seen in JF in recently days!

Hivi huyo rais anpokuja kuomb kura anwaambia atafanya kitu gani?? mnapotok nyumbani kweni siku ya kupiga kura mnataka afanye nini?

hivi mbumbumbu kama nyie msi waza japo kidogo uwezo na wajibu wa rais si ndio mnafuga ujinga, wezi n.k

Hivi Kikwete akija leo na kuwaomba vitu fulani mtampa tu......

sura inawachanganya?? mtu anafanya kazi kwa presha za donors leo mnamsifia

mpeni basi wake AU waume zenu afurahi


NYIE NDIYO MAFISADI NAMBA MOJA ZERO BRAIN IN TANZANIA, TENA NGAU MNA UWEZO WA KUSURF INTERNET MNA UWEZO MDOGO WA KUFIKIRI KAMA WA PANYA JE, WALE WASIOSOMA KABISA SI NDO WANALEWA MATAPUTAPU KWA FURAHA NA 2010 ANAINGIA TENA IKULU.

BASI TU HAMUONEKANI,NINGEWACHAPA VIBAO

NYIE NDIYO MNAJUA VIONGOZI NI MIUNGU WAKATI NI WATUMISHI WETU

YAONE VILE UJINGA TU!1

ALA!!!!!!!
#

HA HA HAAAAAAAAAAAAAAAAAAA hakiyanani nimecheka sana!raha yake hatuonani manake wengine wangeambulia MAKONZI!...nyie watu mlio-quotiwa na huyu englisher jihesabuni mna bahati saaaana ha ha haaaaaaaaaaa mngeondoka na MANUNDU walahiii!
 
Hongera raisi Kikwete

nyie ndo wale wale mlioenda kwenye maandamano ya kumpongeza kwa kusafisha ufisadi kabla ht hajateka maji ya kusafisha???yani natafuta picha za wale waliokuwa wanaendesha maandamano naamini kuna rushwa iliendelea pale Takrima si imekataliwaaaa..,
 
Hongera Kikwete.umejaribu kiasi (NB.HUJAJITAHIDI). Hasa kwenye demokrasia,umejaribu kiasi lakini kwenye uchumi bado kabisa mkuu.Hapo sina la kukupongeza.

Kwanza hapo ninaposema umejaribu nimelinganisha na Mkapa.
 
Ndo tatizo letu si wabongo.
Tumpongeze kwa lipi kafanya nini?Huo si ndo wajibu wake wakati anaomba kura kwa wananchi sasa tuanze kumpongeza ili iweje?Ndo maaana si ni wadanganyika siku zote tumesha danganywa na akina Mramba na Yona basi move yote inapoa.
Mkuu mwiba usiharibu mistake.
Duhhh kali hyo ni mpemba nini asiyeridhika na choote kinachofanya na SISIM
 
JK hastahili pongezi yo yote bora tuwapongeze Dr. Slaa na
Wakili Tundu Lisu walioanika orodha ya mafisadi pale Temeke ambao wengine mpaka sasa wanakumbatiwa na JK.

_________________________________
Wars are caused by undefended wealth - Ernest Hemingway
 
2) Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili, laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji
Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili hawezi kumudu kazi zake. Baada ya kupokea azimio kama hilo, Jaji Mkuu atateua bodi ya utabibu ya watu
wasiopungua watatu atakaowateua kutoka miongoni mwa mabingwa wanaotambuliwa na sheria ya matababu ya Tanzania, na bodi hiyo itachunguza suala hilo na kumshauri Jaji Mkuu
ipasavyo, naye aweza, baada ya kutafakari ushahidi wa kitabibu kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba Rais kutokana na maradhi ya mwili au ya akili, hamudu kazi zake; na
iwapo Jaji Mkuu hatabatilisha tamko hilo ndani ya siku saba kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi itahesabiwa kwamba kiti cha Rais ki wazi, na masharti yaliyomo
katika ibara ndogo ya (3) yatatumika.

(3) Ikitokea kwamba Kiti cha Rais ki wazi kutokana na masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (2) au endapo kiti cha Rais kiwazi kutokana na sababu nyingine yoyote, na endapo
Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na shuhguli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo na wafuatao, kwa kufuata orodha kama ilivyopangwa, yaani-
(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yake iwazi au kama naye hayupo au ni mgonjwa; basi.
(b) Spika wa Bunge au, kama nafasi yake iwazi au kama naye hayupo au ni mgonjwa; basi
(c) Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.

(4) Endapo yeyote kati ya watu waliotajwa katika aya ya (b) na (c) za ibara ndogo ya (3) atatekeleza kazi na shughuli za Rais kutokana na sababu kwamba mtu mwingine anayemtangulia katika orodha hiyo hayupo, basi mtu huyo ataacha kutekeleza
kazi na shughuli hizo mara tu mtu huyo mwingine anayemtangulia atakaporejea na akashika na kuanza kuteleza kazi na shughuli za Rais.

(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa
kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya
40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua
asilimia hamsini ya Wabunge wote

Wadau acheni utani, mnataka kuanza kumpongeza kwa lipi hasa? Binafsi nilikuwa napitia Katiba yetu hapo kuona kama tunaweza kumtoa madarakani au kupata kitu chochote cha kumtoa madarakani na nafasi yake achukue Shein. /Kumbe hatuwezi kutumiia hizi safari zalke za mara kwa mara kumtoa, nasikitika sana
 
45.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, Rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a) kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, na aweza kutoa msamaha huo ama bila ya masharti au kwa masharti, kwa mujibu wa sheria;
(b) kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtu yeyote aliyehukumuwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au asitimize adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum;
(c) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu;
(d) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu ya kutoza, au kuhozi (au kuchukua) kitu cha mtu mwenye hatia ambacho vinginevyo kingechukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano

Na jinsi mnavyozidi kushusha upeo wenu wa kuelew na kfafanua mambo, sitashangaa siku ambayo maamuzi yoyote ya hakimu atakayotoa kwa hao mafisadi mfano kifungo maisha au vinginevyo, na raisi wenu huyu huyu mnayetaka kumpongeza sasa hivi kwa kukohoa tu, atakapokuja na kuwasamehe watuhumiwa wote hao wa ufisadi.


Eeenh tusishangae mamlaka hayo anayo hayo hapo, sasa sijui na hapo mtamsifu au laa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom