Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
ah. yale yale. ya juz, jana na sasa leo.

nyerere alisifika sana huko nje. na mpaka leo tunamkumbuka kwa misimamo yake ya maana kwa mwafrika (kama kusaidia harakat za upatikanaj uhuru kusin mwa afrika). lakin huku ndan matatizo yalikuwa mtindo mmoja. lakin masifa alijipatia kibao

baadae mkapa. akajulikana nje mpaka kupewa cheo cha 'uglobalization'. mtu wa kimataifa. naye akapata sifa huko nje si haba

sasa kikwete. inaandikwa kafanya mkubwa na ya maana sana huko nje

lakin hayo masifa ya huko yanatatuaje hamu yetu ya maendeleo? ndo kwamba tunavutia misaada mingi? ndo kwamba watz wenzetu wengi watakuwa kwenye nafas nzur kimataifa? halaf then what? barabara zetu zitajengwa? shule zetu za yeboyebo ndo zitapata vitabu na vifaa vya kufundishia? wanafunz vyuon watapata 'mikopo' asilimia mia? ndo kilimo chetu tutakiendeleza zaid kuwa cha kisasa?

mi naona bora wasikazanie kujitafutia misifa huko nje. wawwe bize kuangalia matatizo yetu, wawe bize kubuni mbinu za kukabiliana na matatizo kisayans then ndo tuwape hiyo miujiko

binadamu wa kawaida hata presidaa hawez kuwa bize na mambo kibao na yote akaweza kuya handle ipasavyo na akafanikiwa kwa yote. kuna sehemu utaelemea tu. wakiwa bize huko wanapunguza muda wa kushughulikia matatizo yetu ya ndani
 
Ingawa kuna English version, lakini Muungwana kaisoma hii ya kiswahili. Amemaliza kuisoma dakika chache zilizopita


HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUKABIDHI UENYEKITI WA UMOJA WA AFRIKA WAKATI WA MKUTANO WA 12 WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA UMOJA WA AFRIKA ADDIS ABABA, ETHIOPIA,
TAREHE 1 HADI 3 FEBRUARI, 2009

Mheshimiwa Meles Zenawi, Waziri Mkuu wa Ethiopia;
Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika;
Mheshimiwa Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa;
Mheshimiwa Jean Ping, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika;
Waheshimiwa Mawaziri;
Waheshimiwa Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana:

Awali ya yote naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana hapa leo hii. Kwa kuwa ndio tunakutana kwa mara ya kwanza mwaka huu, niruhusuni nitumie fursa hii kuwatakieni nyote kheri ya mwaka mpya. Tumuombe Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema mwaka 2009 uwe wa baraka na mafanikio tele kwa Bara letu.

Natumaini mtaungana nami katika kumshukuru Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Meles Zenawi, kwa mapokezi mazuri na ukarimu ulioonyeshwa na serikali yake na watu wa Ethiopia. Ukarimu ambao tumetokea kuuzoea na kuutarajia.

Waheshimiwa Viongozi wenzangu;
Tangu tulipokutana mjini Sharm el Sheikh, Misri tarehe 30 Juni, 2008, Umoja wetu umepata pigo kubwa kwa kuondokewa na viongozi wenzetu wawili. Wenzetu hao ni Mheshimiwa Levy Mwanawasa, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Zambia na Mheshimiwa Jenerali Lansana Conte, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Guinea. Kwa niaba ya Umoja wa Afrika naomba tusimame kwa dakika moja kuwakumbuka viongozi na ndugu zetu hawa. Tumuombe Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.

Napenda pia kutumia nafasi hii kuwakaribisha rasmi Mheshimiwa Rupiah Banda, Rais mpya wa Zambia, Mheshimiwa Kgalema Motlanthe, Rais mpya wa Afrika Kusini na Mheshimiwa Sheikh Sharif Ahmed Said, Rais mpya wa Somali ambao hiki ni kikao chao cha kwanza kuhudhuria katika nyadhifa zao za Wakuu wa Nchi na Serikali za nchi zao tukufu. Nina hakika kuwepo kwao na mchango wao vitazidi kuimarisha umoja wetu.

Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali;
Tarehe 31 Januari, 2008 mlinichagua kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika. Hii ilikuwa heshima kubwa kwangu mimi binafsi na kwa nchi yangu ya Tanzania. Wakati nikikubali heshima mliyonipa, nilitaja maeneo manne ambayo niliahidi kuyapa kipaumbele katika kipindi cha Uenyekiti wangu. Maeneo hayo ni (a) ulinzi na usalama (b) kutetea maslahi na kutafuta fursa za kiuchumi na kisiasa zitakazoleta maendeleo na ustawi wa bara letu (c) kushughulikia masuala ya jamii na utamaduni na (d) kuimarisha Umoja wa Afrika na taasisi zake.

Leo, wakati wa kumaliza kipindi changu cha uongozi na kukabidhi kijiti kwa kiongozi mwenzetu mwingine kuongoza Umoja wa Afrika, nawiwa na wajibu wa kuelezea jinsi kwa pamoja tulivyotekeleza majukumu yetu katika maeneo haya muhimu. Ni matumaini yangu kwamba tathmini hii itatusaidia kuweka wazi changamoto zilizokuwepo wakati ule, mafanikio tuliyopata na changamoto zilizobaki mbele yetu ambazo hatuna budi kuendelea kuzikabili siku za usoni kwa nguvu zetu zote.

Waheshimiwa Viongozi;
Wakati nakubali Uenyekiti nilisema kuwa mimi ni mtu wa matumaini. Leo hii ninapokamilisha kipindi cha Uenyekiti wangu nafurahi kuona kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja, Umoja wa Afrika unajivunia mafaniko tuliyopata katika maeneo kadhaa.

Utatuzi wa Migogoro
Katika jitihada za kutatua migogoro inayolikabili Bara letu, mtakumbuka kuwa kwenye kikao chetu cha 11 mjini Sharm el Sheikh, nilieleza mafanikio makubwa ambayo Umoja wetu ulikuwa umepata kwa kutatua migogoro katika nchi za Kenya na Comoros. Nchini Kenya, tuliweza kuzipatanisha pande zilizokuwa zikivutana na kufikia makubaliano ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Serikali hiyo ilirejesha amani nchini humo na hali ya maelewano na maridhiano imeendelea kushamiri Kenya hadi hii leo. Kwa niaba yenu narudia kuwapongeza wananchi wa Kenya na viongozi wao, akiwamo Rais Mwai Kibaki ambaye tunaye hapa leo, kwa mafanikio hayo.

Aidha, nchini Comoro Umoja wa Afrika katika operesheni ya kwanza ya aina yake, ulituma majeshi kutoka Libya, Sudan na Tanzania na kufanikiwa kukomesha uasi katika Kisiwa cha Anjouan na hivyo kuweza kurejesha umoja wa kitaifa katika nchi hiyo. Hadi sasa mshikamano huu umedumu nchini Comoro.

Tumepata pia mafanikio ya kutia moyo katika kutafuta suluhu nchini Burundi, kufuatia juhudi za nchi za Kanda na usuluhishi wa Serikali ya Afrika Kusini. Tarehe 4 Desemba 2008, Serikali ya Burundi na Kikundi cha PALIPEHUTU-FNL zilikubaliana kumaliza tofauti zao na kuanza kutekeleza vipengele vya mwisho vya Mkataba wa Kusitisha Mapigano kati ya pande hizo mbili.

Katika makubaliano hayo Kikundi cha PALIPEHUTU-FNL kimekubali kubadilisha jina lake ili kuondoa muonekano wa kikabila. Aidha, Chama hicho kimekubali kupeleka wapiganaji wake kwenye makambi ya kukusanyia wapiganaji ili kuwezesha zoezi la kuwanyang’anya silaha kufanyika na mchakato wa kuwatangamanisha na jamii ya Burundi uanze. Kwa upande wake, Serikali imeandaa kambi kubwa huko Rubira kwa ajili ya kuwakusanya wapiganaji wa FNL. Aidha, Serikali ya Burundi imekwishatoa nafasi 20 za uongozi kati ya 33 ilizokubali kutoa kwa viongozi wa FNL. Ni mategemeo yangu kwamba pande zote husika zitaheshimu na kutekeleza ipasavyo makubaliano yao hayo.

Napenda kutumia nafasi hii, kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushirikiana na Umoja wa Afrika kusaidia kujenga nchi hiyo upya. Kwa kuanzia, jumuiya ya kimataifa haina budi kutekeleza ahadi yake ya kutoa msaada wa kuanzisha makambi ya kukusanyia wapiganaji, pamoja na chakula
kwa nchi ya Burundi. Pili, kutoa misaaada ya maendeleo ambayo ilisitishwa kusubiri hatua hii.

Waheshimiwa Viongozi wenzangu;
Mwaka 2008 pia tumeshuhudia mambo ya kutia moyo yakiendana na changamoto kadhaa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (JKK). Hali ya amani na mafanikio ambayo ilipatikana nchini JKK iliingia dosari mwezi Agosti kufuatia kuzuka upya kwa mapigano kati ya majeshi ya Serikali na vikosi vya Jenerali Laurent Nkunda. Mapigano hayo yamesababisha vifo vya watu wengi na uharibifu wa mali na mateso kwa raia wengi wasiokuwa na hatia. Watu wapatao milioni moja na laki saba wamekuwa wakimbizi ndani ya nchi yao.

Katika jitihada za kusuluhisha mgogoro huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Ban Ki-moon kwa mashauriano nami nikiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais Mwai Kibaki wa Kenya ambaye ni Mwenyekiti wa Ushirikiano wa Nchi za Kanda ya Maziwa Makuu aliitisha mkutano wa Wakuu wa Nchi za Ushirikiano huo tarehe 7 Novemba 2008, mjini Nairobi, Kenya. Mkutano huo uliofanyika chini ya uenyekiti wangu ulijadili hali ya usalama na mapigano katika Jimbo la Kivu. Kwa kauli moja mkutano huo ulizitaka pande husika kusitisha mapigano mara moja na kuruhusu misaada ya kibinadamu kupelekwa kwa wananchi wanaohitaji. Pia, ilizitaka pande hizo zianze mazungumzo ya kutatua tofauti zao.

Aidha, Wakuu hao walimteua Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Tanzania, kuungana na Mhe. Olesegun Obasanjo, Rais Mstaafu wa Nigeria aliyeteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufanya kazi ya kusuluhisha mgogoro huo. Nafurahi kueleza kuwa Wasuluhishi hao tayari wamefanya mazungumzo na pande zote zinazohusika na mgogoro huo. Jitihada zao zimeanza kuzaa matunda kwani pande husika zilikubali kusitisha mapigano na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia wananchi.

Nafurahi kusema kuwa, pande zinazohasimiana zimeingia kwenye mazungumzo yanayoendelea hivi sasa huko Nairobi, Kenya. Nashauri Umoja wa Afrika utambue na kuwapongeza Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa na Wakuu wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu kwa uamuzi wao wa busara na hatua wanazoendelea kuchukua. Pia, kikao kiwatake waendelee kusimamia juhudi za kupata amani mashariki mwa Kongo.

Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali, Mabibi na Mabwana;
Pamoja na mafanikio haya bado Bara letu limeendelea kukabiliwa na migogoro sugu na mingine iliyozuka hivi karibuni. Miongoni mwa migogoro hiyo ni pamoja na ile ya Somalia, Jimbo la Darfur nchini Sudan, Zimbabwe, Mauritania na Guinea.

Kuhusu Zimbabwe mtakumbuka kuwa wakati wa kikao chetu mjini Sharm el Sheikh, tulikubaliana kuikabidhi Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) jukumu la kuendelea kusuluhisha mgogoro kati ya Serikali ya Zimbabwe na Chama cha Movement for Democratic Change (MDC) kinachoongozwa na Bw. Morgan Tsvangirai. SADC.

Kupitia msuluhishi wake Mheshimiwa Thabo Mbeki, aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, ilifanikiwa kuanzisha mazungumzo kati ya Chama cha Zanu-PF na Chama cha MDC kinachoongozwa na Bwana Tsvangirai kama tulivyoagiza. Katika mazungumzo hayo pia kilishirikishwa Chama cha MDC kinachoongozwa na Profesa Arthur Mutambala. Tarehe 15 Septemba 2008, pande hizo zilifikia makubaliano ya kumaliza uhasama na kuanzisha Serikali ya Umoja wa kitaifa. Katika makubaliano hayo, ilikubalika kuwa Rais Robert Mugabe aendelee kuwa Rais wa Zimbabwe na Bwana Morgan Tsvangirai awe Waziri Mkuu na Profesa Arthur Mutambara awe Naibu Waziri Mkuu. Pia walikubaliana kuwepo Naibu Waziri Mkuu wa pili kutoka Chama cha MDC cha Bwana Morgan Tsvangirai. Hali kadhalika pande hizo zilikubaliana kugawana nafasi za Mawaziri kwa uwiano wa nafasi 15 kwa Zanu-PF, 13 kwa MDC- Tsvangirai na nafasi 3 kwa MDC-Mutambara.
Maelewano hayo yaliingia dosari tarehe 11 Oktoba 2008 baada ya kutangazwa mgao wa wizara kwa vyama ambapo Chama cha MDC kilipoelezea kutokuridhika na jinsi mgao ulivyofanywa. Kilidai kuwa nafasi zote nyeti zilienda kwenye Chama cha Zanu-PF. Hali hiyo ya kutokuelewana imechelewesha utekelezaji wa makubaliano hayo.

Viongozi wa SADC wameendelea na juhudi za kuzipatanisha pande husika ili ziweze kufikia makubaliano kuhusu nafasi za Uwaziri. Juhudi hizo zimezaa matunda, Bw. Morgan Tsivangirai na Chama chake cha MDC wamekubali kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Taarifa ya uamuzi wa Chama cha MDC kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni ya kutia moyo. Sisi katika AU tunafurahi kuwa uamuzi wetu wa Sharm al Sheikh umezingatiwa. Wakati tunawapongeza viongozi wenzetu wa SADC kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa niaba yetu, tuwaombe viongozi wa Zimbabwe kuweka mbele maslahi ya taifa lao na watu wake. Nawaomba wenzangu wote na hasa Umoja wa Afrika uendelee kuwa pamoja na watu wa Zimbabwe hasa wakati huu wa kazi ngumu ya kuunda na kuendesha Serikali ya pamoja inayojumuisha wanasiasa ambao wanatofautiana na kuhasimiana.

Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali;
Namaliza Uenyekiti wakati hali ya Somalia ikiwa bado ni changamoto kubwa kwa Umoja wa Afrika na kwa dunia kwa jumla. Uharamia wa utekaji nyara wa meli kati ya Ghuba ya Aden unaufanya mgogoro huo sasa uchukue sura ya kimataifa badala ya kuwa ni wa ndani ya Somalia au wa ukanda wa pembe ya Afrika pekee. Hali hii inasisitiza hoja ya jumuiya ya kimataifa kwa pamoja kujihusisha kwa karibu na juhudi za kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa mgogoro wa Somalia. Kwa maneno mengine, tungependa kuona Umoja wa Mataifa ukichukua nafasi yake stahiki ya uongozi ikishirikiana na Umoja wa Afrika. Mgogoro huu umefikia mahali ambapo hauwezi kuachiwa Umoja wa Afrika pekee. Sisi tumetimiza wajibu wetu kwa uwezo wetu na tutaendelea kufanya hivyo. Tunaomba jumuiya ya kimataifa nayo ikiongozwa na Umoja wa Mataifa itusaidie. Tunausubiri kwa hamu uamuzi utakaofanywa na Baraza la Usalama mwezi Aprili, 2009.

Waheshimiwa Viongozi wenzangu;
Napenda kuitumia nafasi hii kuwapongeza wenzetu wa Uganda na Burundi kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika juhudi za kutafuta amani nchini Somalia. Mchango wao wa wanajeshi wa kulinda amani katika AMISOM unathaminiwa na kupongezwa sana. Aidha, sina budi kusema neno la pongezi kwa Serikali na watu wa Ethiopia kwa uamuzi wa busara kupeleka majeshi nchini Somalia. Uamuzi ule wa kishujaa ndiyo uliosaidia Somalia kuendelea kuwa taifa moja na lenye Serikali tunayoiona leo. Kama si hivyo, sijui hali ingekuwaje. Tunawapongeza tena kwa uamuzi wao wa busara na kuondoa majeshi yao baada ya kutoa mchango wao muhimu.

Kwa niaba yenu napenda kuwapongeza sasa Wabunge wa Somalia kwa uamuzi wa hivi karibuni wa kumchagua Sheikh Sharif Ahmed Said kuwa kiongozi wa nchi yao. Tumeupokea kwa furaha uamuzi huo na kuwataka wanasiasa na wananchi wote wa Somalia kuunga mkono uamuzi huo. Wampe ushirikiano Kiongozi wao mpya kwa maslahi yao na nchi yao.

Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali;
Kuhusu Darfur, napenda kuelezea faraja yangu kwamba muelekeo ni mzuri kuhusu kupelekwa kwa vikosi vya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (UNAMID). Bado hali ya amani ya Darfur ni tete lakini naamini vikosi vya UNAMID vikikamilika hali ya amani itadhibitiwa na kutengemaa.

Wakati naipongeza Serikali ya Sudan kwa ushirikiano wake, niombe wahusika kwa upande wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuongeza juhudi ya kupatanisha vikundi vya waasi ili mazungumzo na Serikali yaanze mapema iwezekanavyo. Hatima ya amani ya kudumu ya Darfur ipo katika kufanyika na kufanikiwa kwa mazungumzo hayo.

Changamoto mpya kwenye mgogoro wa Darfur inahusu ombi la Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Kimataifa (ICC) la kutaka Rais Omar Al-Bashir wa Sudan kufunguliwa mashtaka ya makosa ya kivita. Kimsingi, Umoja wa Afrika hauna pingamizi kuhusu watuhumiwa wa makosa ya kivita kuwajibishwa. Hoja yetu ni kwamba mchakato wa kutafuta suluhu huko Dafur unastahili kupewa kipaumbele na ili kuhakikisha usalama wa watu walio wengi katika jimbo hilo. Rais Al-Bashir ni mdau muhimu sana katika kufanikisha hayo.

Umoja wa Afrika umewasiliana na mamlaka, taasisi na wadau husika kutaka ombi hilo kusitishwa kwa sasa. Hadi sasa jitihada hizo bado hazijafanikiwa. Ni vyema basi Umoja wa Afrika ukaendelea na juhudi zake, kwa kushirikiana na pande zote zinazohusika, kutafuta amani katika nchi hiyo. Ninaiomba jumuiya ya kimataifa iendelee kuunga mkono juhudi zetu.

Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali;
Kama nilivyosema awali, Bara letu pia limeshuhudia kuzuka kwa migogoro mipya kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika katika nchi za Mauritania na Guinea. Mapinduzi hayo ni kinyume na Katiba ya Umoja wa Afrika, Mkataba wa kuanzisha Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, pamoja na Tamko la Lome la mwaka 2000. Umoja wa Afrika unakataa kubadilisha Serikali za nchi kwa kutumia njia zisizokuwa za kidemokrasia. Kwa kuzingatia misingi tuliyoiweka, nchi hizo mbili zimesimamishwa kushiriki shughuli za Umoja wa Afrika mpaka zitakaporudishwa katika utawala wa kidemokrasia.

Naomba kutumia fursa hii kutoa mwito kwa viongozi wa kijeshi katika nchi hizo kuheshimu katiba za nchi zao na kurudisha utawala wa kiraia haraka iwezekanavyo. Aidha, naziomba nchi wanachama za Umoja wa Afrika kukataa kuunga mkono viongozi hao wa kijeshi kwani kufanya hivyo ni kukiuka Katiba ya Umoja wetu. Pia jumuiya ya kimataifa haina budi kutuunga mkono kwa kukemea mapinduzi hayo na kutowatambua viongozi wa kijeshi wa nchi hizo.

Kwa misingi hiyo tunasikitishwa na hali ya wasiwasi inayoendelea sasa nchini Madagascar. Harakati za kuiondoa Serikali iliyochaguliwa kidemodrasia hazikubaliki. Tunawasihi wahusika waache kutumia njia za ghasia bali wazingatie na kuheshimu misingi ya kidemokrasia.

Waheshimiwa Viongozi;
Kwa jumla hali ya amani na utulivu Barani Afrika ni ya kuridhisha. Ni nchi chache tu zenye migogoro siku hizi ukilinganisha na miaka ya nyuma. Mimi naamini inawezekana kukawa na amani na utulivu katika nchi zote Barani Afrika. Siku hiyo haiko mbali kadri demokrasia inavyozidi kuimarika, utawala bora unavyozingatiwa, haki za binadamu zinavyoheshimiwa na uchumi wa nchi za Afrika unavyozidi kukua na umaskini kupungua. Hata hivyo, hatuna budi kufanya kila tuwezalo kuhakikisha hayo yaendelee kufanyika katika nchi zetu.

Mafanikio ya kiuchumi
Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali;
Namaliza kipindi changu cha uongozi nikiacha nyuma yangu changamoto kubwa ya maendeleo ya kiuchumi na kijamaa ikiwa ndilo suala la msingi ambalo hatuna budi kuendelea kulipa kipaumbele cha kwanza. Afrika ndilo Bara maskini kuliko mabara yote duniani. Katika nchi 50 maskini sana duniani 34 zipo Afrika.

Bado upatikanaji wa huduma za kiuchumi na kijamii kama vile elimu, afya, maji, barabara, reli, usafiri wa anga, umeme n.k. ni wa kiwango cha chini sana.

Kwa upande wa usalama wa chakula, hali ya Afrika bado siyo nzuri. Kwa sasa, duniani kuna nchi 36 zinazokabiliwa na tatizo la upungufu wa chakula. Kati ya hizo, 21 ziko Afrika. Nayasema mambo haya tunayoyajua sote kusisitiza ukubwa wa tatizo la kujiletea maendeleo katika nchi zetu moja moja na kwa Bara zima la Afrika. Tuna safari ndefu na ngumu mbele yetu kufikia maendeleo tunayoyatarajia sote. Hatuna budi kutoa uzito unaostahili kwa masuala ya kukuza uchumi wa nchi zetu na kuwaletea maendeleo watu wetu.

Bahati mbaya sana, tunatumia muda mwingi kutatua migogoro na kuzungumzia masuala ya kisiasa tena kuhusu kugawana madaraka miongoni mwa wanasiasa au baadhi yetu kujiongezea madaraka au umaarufu. Nawaomba wenzangu tubadilike. Tupange vipaumbele vyetu vizuri na kuweka masuala ya maendeleo ya uchumi katika kipaumbele stahili.

Ndugu zangu, Viongozi wenzangu;
Pamoja na hali kuwa ngumu lakini nafurahi kusema kuwa muelekeo wetu ni mzuri. Lililo muhimu ni kuhakikisha haturudi nyuma bali tunasonga mbele. Mwaka wa jana uchumi wa Afrika ulikuwa kwa wastani wa asilimia 5.8. Hii ni kasi nzuri lakini haitoshi hasa kwa vile tuko nyuma sana kimaendeleo. Isitoshe, kiasi hicho ni pungufu ya lengo la asilimia 7 linalotakiwa kutuwezesha kutekeleza lengo la Milenia la kupunguza umaskini kwa nusu ifikapo mwaka 2015. Lazima tuongeze juhudi za kukuza uchumi wa nchi zetu kwa kasi kubwa zaidi. Naomba nipendekeze kuwa, tutafute nafasi siku za usoni tulizungumze suala hili. Tena itakuwa bora tuwe na kikao maalum kuzungumzia mikakati na mbinu za kukuza uchumi wa Bara la Afrika haraka ili kujiondoa katika aibu ya kuwa Bara la nchi na watu maskini kuliko wote duniani.

Uhusiano kati ya Afrika na Nchi na Kanda nyingine
Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali, Wageni Waalikwa; Mabibi na Mabwana;
Kwa ajili ya kuendeleza shughuli za Umoja wetu na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo la nchi zetu na Bara letu mahusiano mazuri na mataifa na mashirika ya kimataifa duniani ni jambo muhimu sana. Katika mwaka mmoja wa uongozi wangu kulikuwa na shughuli nyingi za namna hiyo. Tulianzisha rasmi ushirikiano wa kiuchumi na India na Uturuki na tumefanya mikutano ambayo ilitushirikisha sisi na wakuu wa nchi na Serikali wa nchi hizo. Nafurahi kwamba katika mikutano hiyo yaani tarehe 8-9 Aprili, 2008 na India na tarehe 18-20 Agosti 2008 na Uturuki makubaliano muhimu yahusuyo maendeleo na uhusiano wa kibiashara yenye maslahi kwetu yalifikiwa. Nawaombeni wenzangu tuchangamkie kufuatilia.

Katika mwaka uliopita kulifanyika mikutano muhimu nchini Japan na kwenye Umoja wa Mataifa New York iliyohusu maendeleo ya Afrika. Wa kwanza ni Mkutano wa Nne wa Ushirikiano kati ya Africa na Japan (TICAD IV) uliofanyika tarehe 28 - 30 Mei, 2008 huko Yokohama, Japan. Kama mtakavyokumbuka katika mkutano ule Mheshimiwa Takeo Fukuda aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan wakati ule alitangaza fursa nyingi za misaada ya maendeleo, uwekezaji na biashara.

Hatuna budi kujipanga vizuri katika ufuatiliaji ili tuzitumie fursa hizo kwa maendeleo yetu. Bahati nzuri marafiki zetu wa Japan walikubali, kwa mara ya kwanza, kuwapo utaratibu wa kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya TICAD IV. Naomba Uongozi ujao wa Umoja wetu na sote kwa jumla tuzichangamkie fursa hizo na kuzitumia. Ni muhimu kwetu, zitatusaidia sana.

Waheshimiwa Viongozi Wezangu;
Tarehe 07 hadi 09 Julai, 2008, nilishiriki Mkutano wa G8 uliofanyika huko Japan. Nilipata fursa, pamoja na Waziri Mkuu Meles Zenawi wa Ethiopia, Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini wakati ule, Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria, Rais Abdoulaye Wade wa Senegal na Rais Yaradua wa Nigeria kuzungumzia masuala muhimu kwa maendeleo ya Afrika. Kama ilivyo kawaida ya viongozi wa nchi wanachama wa G8, walikuwa wakarimu kwa ahadi za kutusaidia. Naomba tuendelee kwa umoja wetu kufuatilia ahadi hizo na zile za nyuma walizotoa katika mikutano iliyopita. Ahadi nyingi zilizotolewa na Wakuu wa Nchi za G8 zikitekelezwa, hali ya maendeleo ya Bara letu itafikia mahali pazuri.

Waheshima Wakuu wa Nchi na Serikali;
Mwaka wa jana, Umoja wa Mataifa umetutendea wema sana. Kulifanyika mikutano mitatu maalum kuhusu Afrika. Tarehe 22 Septemba, 2008 kulikuwa na mkutano kuhusu mahitaji maalum ya maendeleo ya Afrika (High Level Meeting on Africa’s Development Needs). Mkutano huo uliitishwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Padri Miguel Brockmann. Tarehe 25 Septemba, 2008 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Ban Ki-Moon aliitisha mkutano wa kuzungumzia kutekeleza Malengo ya Milenia Bara la Afrika. Mikutano hiyo imeleta faraja kubwa kwetu sote viongozi na wananchi wa Afrika kwamba, Umoja wa Mataifa unajali mambo yenye maslahi kwa Afrika. Kwa niaba yenu napenda kumshukuru Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa moyo wao wa upendo kwa Afrika na watu wake. Naomba yaliyoamuliwa na kukubaliwa na mikutano hiyo miwili yatekelezwe ipasavyo. Tunasubiri utekelezaji wake kwa hamu. Naomba Kamisheni ya Umoja wa Afrika na sisi viongozi mmoja mmoja na kwa umoja wetu tuwe makini kufuatilia.

Waheshimiwa Viongozi;
Mkutano wa Pili wa Ushirikiano baina ya Afrika na Amerika ya Kusini ambao ulikuwa ufanyike tarehe 01 Desemba, 2008 huko Caracas, Venezuela uliahirishwa. Sababu ya kufanya hivyo, ilikuwa kutoa nafasi kwa washiriki wa pande zote mbili waweze kushiriki mkutano wa kutathmini utekelezaji wa makubaliano ya Monterey kuhusu kugharimia maendeleo (Follow up Conference on Financing for Development)ya nchi zinazoendelea uliofanyika Doha, Quatar tarehe 29 Novemba hadi 02 Desemba, 2008. Mkutano kati ya Afrika na Amerika Kusini sasa utafanyika mapema mwaka huu. Napenda kuchukua nafasi hii kuhimiza nchi za Afrika kujiandaa vyema ikiwa ni pamoja na kutayarisha miradi ambayo itatekelezwa kwa pamoja na washirika wetu wa Amerika Kusini.

Aidha, ushirikiano wetu na Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika na Jumuiya ya Ulaya zimeendelea kuwa wahimili wakubwa wa maendeleo ya Afrika. Tunawashukuru sana. Tunaomba waendelee kutusaidia. Afrika inawahitaji sana.

Mkutano wa 10 wa Utatu wa Mawaziri (Troika Ministerial Meeting) wa Afrika na Ulaya ulifanyika tarehe 20 na 21 Novemba 2008 hapa Addis Ababa kuhakiki maendeleo ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Pamoja kati ya Afrika na Ulaya. Pande hizo zimeunda Timu za Pamoja za Wataalamu katika maeneo yote ya ushirikiano. Kazi ya kuandaa miradi ya pamoja inaendelea na nina imani kuwa mafanikio yatapatikana mapema kabla ya Mkutano wetu na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Ulaya utakaofanyika mwaka 2010. Ni matumaini yangu kuwa nchi wanachama zitachangamkia fursa hizi zilizopatikana ili kukuza uchumi na kuondoa umaskini kwa raia wetu.

Waheshimiwa Viongozi wenzangu;
Changamoto kubwa iliyopo sasa ni namna ya kutumia fursa zilizojitokeza katika ushirikiano wetu na mataifa na mashirika mbalimbali ya kimataifa duniani kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa nchi zetu za Afrika. Nataka nitumie fursa hii kuihimiza Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuendelea kuratibu shughuli za ushirikiano na kuandaa tathmini za mara kwa mara ili tuweze kufahamu maendeleo yanayopatikana na changamoto zilizopo.

Waheshimiwa Viongozi;
Vilevile, wakati wa Uenyekiti wa Tanzania, ilifanyika pia mikutano mingi ya kisekta ambayo iliratibiwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika. Tumepiga hatua kubwa katika mchakato wa kuanzisha taasisi za fedha za Umoja wetu, hususan Benki ya Rasilimali ya Afrika. Aidha, Mawaziri wa Viwanda walikutana mwezi Oktoba mjini Durban, Afrika Kusini na kupitisha Mkakati wa Kutekeleza Mpango Kazi wa Kuendeleza Viwanda Afrika. Mkakati huo ukitekelezwa vyema, utaliwezesha bara la Afrika kujikomboa kutoka kwenye mtego wa kuuza malighafi duniani kwa nchi za Magharibi kwa bei nafuu. Vilevile, suala la uhaba wa chakula lilipewa nafasi yake ambapo Mawaziri wa Chakula walikutana mwezi Desemba 2008 mjini Sirte, Libya na kujadili namna ya kutumia rasilmali maji kwa ajili ya umwagiliaji mashambani na uzalishaji wa nishati kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa chakula na maendeleo ya vijijini.

Misukosuko ya Mfumo wa Fedha Kimataifa
Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali;
Kama tunavyojua, mwaka 2008 ulikuwa na misukosuko mingi ya kiuchumi duniani iliyotuathiri hata sisi katika Bara la Afrika. Tulianza na tatizo la kupanda sana kwa bei za mafuta, baadae bei za chakula na sasa mgogoro wa fedha na uchumi. Matatizo hayo yameathiri uchumi wa nchi zetu kwa namna mbalimbali na kutishia kupoteza mafanikio tuliyoyapata katika utulivu wa uchumi na maendeleo. Bei za mafuta na chakula zimeshuka lakini athari za mgogoro wa fedha na uchumi tutakuwa nazo mpaka hapo migogoro hiyo itakapoisha. Tuna kila sabubu za kuhofia matokeo yake kwa uchumi wa nchi zetu changa.

Nusura yetu inategemea ni kwa kiasi gani mataifa makubwa kiuchumi yaliyo chanzo cha kuwepo migogoro hiyo yatafanikiwa kukabiliana na matatizo haya. Tunawapongeza kwa juhudi kubwa wazifanyazo kurekebisha mambo katika nchi zao na tunawatakia mafanikio. Hata hivyo ni muhimu Afrika nayo ishirikishwe katika mikutano waifanyayo kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili kubwa. Na sisi pia ni sehemu ya uchumi wa dunia na athari zinazotokana na misukosuko ya fedha na uchumi na sisi tunazipata.

Waheshimiwa Viongozi Wenzangu;
Kwa vile athari zinatupata sote hatuna budi na sisi wenyewe kujiwekea mikakati ya kuziepuka na kuzikubali. Nawapongeza sana Mawaziri wa Fedha wa Afrika kwa uamuzi wao waliofanya kukutana Tunis, Tunisia Novemba, 2008 na kwa maamuzi yao muafaka waliyoafikiana. Naamini yakitekelezwa ipasavyo yatasaidia kutuepusha au kutupunguzia makali ya tatizo. Nawaomba viongozi wenzangu tuyatafakari na kuchukua hatua zipasazo.

Kuhusu masuala ya jamii na utamaduni, chini ya Uenyekiti wangu Baraza la Uchumi, Jamii na Utamaduni lilizinduliwa rasmi tarehe 9 Septemba 2008 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Mtakumbuka kuwa Asasi zisizo za Kiserikali zilizopo Barani ni wanachama wa Baraza hili. Kuanza kazi rasmi kwa Baraza hili ni fursa nzuri kwa raia wa kawaida kushiriki kwenye shughuli za kiuchumi, jamii na utamaduni ambazo zinahusu Bara letu. Ni matumaini yangu kuwa asasi zote zisizo za kiserikali zitatumia Baraza hili katika kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake.

Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Jambo lingine nililolishughulikia wakati wa Uenyekiti wangu ni suala la matumizi mabaya ya dhana ya uwezo wa kufungua kesi za makosa ya jinai yanayofanywa mahali popote ulimwenguni na ambayo yamekuwa yakitumika na baadhi ya majaji wa nchi za Ulaya, kufungua mashtaka dhidi ya viongozi wa nchi za Afrika.

Kufuatia uamuzi wetu tuliofikia wakati wa kikao chetu cha Sharm el Sheikh kuwa suala hili lijadiliwe kwa kina na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, niliwasilisha uamuzi huo wakati nilipohutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba, 2008. Suala hili sasa lipo kwenye Kamati ya Sita ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Aidha, Mwenyekiti wa Kamisheni, amewasiliana na Rais wa Kamisheni ya nchi za Ulaya kupendekeza kuwa suala hili lijadiliwe baina ya taasisi hizo mbili, kwa sababu matumizi mabaya ya dhana hii, yanaonekana zaidi kwenye nchi za Ulaya. Nategemea kuwa Mwenyekiti mpya tutakayemchagua, atahakikisha kuwa shughuli hii inakamilika mapema iwezekanavyo.

Uimarishaji wa taasisi za AU
Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali; Mabibi na Mabwana;
Mtakumbuka kwamba katika kipindi cha Uenyekiti wangu tulifanya uchaguzi wa Kamisheni mpya na nilikuwepo kushuhudia Mwenyekiti aliyemaliza muda Mheshimiwa Prof. Alpha Omar Konare akimkabidhi Mwenyekiti mpya Mheshimiwa Jean Ping. Nilipata fursa ya kuzungumza na Makamishna wapya kuhusu majukumu yao na mategemeo yetu kwao.

Aidha, nilizungumza na wafanyakazi wa Kamisheni ya Afrika ambapo walinieleza matatizo mbalimbali yanayowakabili. Nafurahi kwamba katika kikao kilichomalizika juzi cha Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika, uamuzi wa kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa AU umefanywa. Ahadi yangu kwao imetimia sasa ni wajibu wao kutimiza ahadi yao kwangu ya kufanya kazi kwa bidii.

Pamoja na hayo kazi ya kuimarisha Kamisheni kwa nyenzo na vifaa haina budi iendelee. Kazi hiyo ingefanikiwa zaidi kama nchi zote zitalipa michango yao kwa wakati. Naomba niwasihi viongozi wenzangu tuzingatie wajibu wetu huu wa msingi. Wenye kudaiwa malimbikizo walipe na tujenge mazoea ya kulipa michango yetu kwa wakati. Uimara wa chombo chetu hiki muhimu unategemea sana ulipaji wetu wa michango. Hili si jambo ambalo ninalazimika kulifafanua zaidi. Sote tunalielewa vyema.

Viongozi wenzangu;
Jambo lingine muhimu kuhusu Kamisheni yetu lililotokea katika kipindi cha Uenyekiti wangu ni ule uamuzi wetu jana. Tumeazimia kuongezea mamlaka na uwezo wa kiutendaji wa Kamisheni yetu kwa kuifanyia mageuzi ya kimfumo na kimuundo na kuibadili kuwa Mamlaka ya Umoja wa Afrika. Uamuzi ule ni hatua kubwa kuelekea kutumia ndoto yetu ya Serikali ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa ya Afrika. Hatuna budi kujipongeza kwa uamuzi ule ambao unalihakikishia Bara letu umoja na mshikamano.

Mapendekezo
Waheshimiwa Viongozi;
Katika kipindi changu cha uongozi nimejifunza mambo mengi. Yapo baadhi nimeona yakifanyiwa marekebisho fulani fulani yatasaidia kuimarisha ufanisi wa shughuli za Umoja wa Afrika. Naomba niyataje mambo matatu.

Kwanza kabisa, ni suala la nchi ambayo ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kutokuwa mjumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika naona ni kasoro ambayo hatuna budi kuirekebisha. Bahati mbaya sana bara letu lina migogoro mingi na miongoni mwa mambo ambayo Mwenyekiti wa Umoja wa Arika anajikuta anatumia muda wake mwingi ni kushughulikia usuluhishi wa migogoro. Katika kufanya hivyo anastahili kufanya kazi na Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika. Inapotokea nchi Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika si mjumbe wa Baraza hilo anaikosa fursa hiyo. Mimi naamini kazi ya Mwenyekiti ya kusuluhisha migogoro ingerahisishwa sana kama ungewekwa utaratibu wa nchi yake kuwa mjumbe wa Baraza hilo. Kama ni mjumbe tayari kwa utaratibu wa kawaida tatizo linakuwa halipo.

Pili, napendekeza tuangalie uwezekano wa kuanzisha utaratibu wa Troika katika mtiririko wa vikao vyetu. Pendekezo langu limesukumwa na ukweli kwamba baada ya kikao cha Wakuu wa Nchi, kikao rasmi anachoweza kukitumia kupata ushauri au kujadili na kufanya maamuzi kwa mambo ambayo lazima Mwenyekiti ashughulikie. Nashauri tuutumie utaratibu huu tumuondolee Mwenyekiti upweke na kumuongezea uwezo wa kutimiza majukumu yake. Vinginevyo anakuwa Mwenyekiti anayepwaya tu anayesubiri kuongoza vikao viwili cha Januari na Julai.

Na la tatu, naomba niwakumbushe tu kuwa utekelezaji wa majukumu ya Uenyekiti wa Umoja wetu ni mzigo mkubwa. Ni vyema tukafikiria namna ya kupunguza mzigo unaobebwa na nchi-Mwenyekiti, hususan rasilimali fedha, wakati wa kutekeleza majukumu yake. Nashauri tuangalie uwezekano wa kutenga fedha maalum kwa ajili ya kugharamia baadhi ya shughuli za Mwenyekiti. Bila kufanya hivyo, tunaweza kukosa mchango wa uongozi wa baadhi ya nchi wanachama, kwa kuhofia gharama kubwa zinazoendana na majukumu ya uenyekiti.

Hitimisho
Waheshimiwa Wakuu wa Nchi na Serikali;
Wakati ninapomalizia Uenyekiti wa Umoja wetu, napenda kwa mara nyingine tena kutoa shukrani zangu za dhati kwa imani na heshima kubwa ambayo mmeonesha kwangu mimi binafsi na kwa nchi yangu. Nimepata faraja kubwa kulitumikia Bara letu la Afrika kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.

Kwa namna ya pekee, naomba niwashukuru nyinyi viongozi wenzangu kwa ushirikiano mlionionesha katika kipindi chote cha uongozi wangu. Naamini bila ushirikiano wenu mafanikio niliyoyataja ambayo tumeweza kuyapata katika mwaka mmoja uliopita yasingeweza kupatikana. Vilevile napenda kuwashukuru viongozi wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa ushirikiano walionipatia wakati wa kipindi chote cha uongozi wangu. Namshukuru Mhe. Jean Ping, Mwenyekiti wa Kamisheni, Makamu wake Mheshimiwa Erastus Mwencha na Makamishna kwa ushauri waliokuwa wakinipatia tangu walipochaguliwa katika nafasi hiyo. Naondoka nikiwa na kumbukumbu nzuri ya kufanya kazi na watu makini, mahili na wachapa kazi hodari.

Natoa shukrani za pekee ziende kwa Mhe. Alpha Oumar Konare, Mwenyekiti wa zamani wa Kamisheni kwa kunisaidia katika masuala mbalimbali hususan katika kipindi cha mwanzo cha uongozi wangu. Nilipoanza Uenyekiti wangu yeye alikuwa Mwenyekiti wa Kamisheni mpaka alipoingia Mheshimiwa Jean Ping. Nawashukuru wakurugenzi pamoja na wafanyakazi wote wa Kamisheni kwa msaada waliotoa katika kufanikisha shughuli mbalimbali za Umoja wetu katika kipidi chote cha Uenyekiti wangu. Nawashukuru pia viongozi mbalimbali wa taasisi na asasi za Umoja wetu kwa ushirikiano wao. Naamini ushirikiano mlionipa utaendelea pia kwa Mwenyekiti wetu ajaye ambaye tutamchagua hivi punde.

Kwa kumalizia, naomba wenzangu mnikubalie tutume salamu maalum za pongezi kwa Rais Barack Obama wa Marekani, kwa ushindi alioupata katika uchaguzi uliopita. Tunampongeza kama ambavyo tunastahili kufanya kwa kiongozi yeyote wa taifa lolote ambalo tuna uhusiano nalo mzuri. Lakini pia tunampongeza kwa sababu ya kuwa Mmarekani mwenye asili ya Afrika hususan Kenya. Kwetu sisi ni jambo la fahari na kujivunia.

Mungu ibariki Afrika!
Mungu ubariki Umoja wa Afrika!
AHSANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA
 
Nabii mzuri hakubaliki Kwao.
Mh. JK ongeza juhudi zaidi Tz lakini siyo kwa sababu vuguvugu la uchaguzi limeanza nukia. Maana jukumu la AU umeshamaliza, kaza msuli kwa watanzania!
Hongera.
 
Nimefurahishwa sana na kitendo cha Rais wetu Hon. JMK kuhutubia viongozi wa Afrika kwa kutumia Lugha ya Kiswahili.

Thiss one of the crutial steps in building nationalism, self esteem and the core strength of our nation, the nation of Swahili speakers.

Take the same spirit to Geneva, Davos, New York, Beijing and all over the world.

God bless Tanzania.

I salute.
 
Kabla hatujamwaga sifa kemkem, je ni nini haswa JK ameweza kukifanya wakati akiwa mwenyekiti AU?

Zimbabwe watu wanauana, Mugabe anazidi kuleta udikteta - where was JK
Congo wanauana - Where was JK
Sudan wanauana - Where was JK
Somalia wanauana - Where was JK
Kenya wameuana - Where was JK. Record has it ni Kofi Anan na NIgeria Ex-president ndio walio broker ile Kenyan peace deal, na power sharing. JK was a spectator.
plus many more examples.

Wakati umefika kwa waafrika tusikubali mazingaombwe tunayofanyiwa na viongozi wetu ambao ni selfish, lets start holding them accountable.

Angalia hotuba, imejaa mazingaombwe, na maneno yakupamba pamba. Watu wanakufa,vita imetandaa bara zima, hawa viongozi waache blaa blaa, tunataka kuona actions.
 
Jamboni wote kwa mpigo.Jana baada ya kuona kipindi maalumu usiku kilicho rushwa na TBC ikiwa na marudio ya tukio la sherehe za kuzaliwa Mfaume Kawawa mengin nimeyaona lakini nikajawa na maswali .Mojawapo ya haya maswali ni haya .

1.Lowasa alijiondoa hakufukuzwa lakini ana hadhi ya waziri Mkuu mstaafu , mbona sikumuona pale wakati wakuu zote wa zamani kama yeye walitinga pale kwenye makulaji na kujidai ?

2.Gharama za jana TBC kurusha matangazo yale kama kipindi maalumu zililipwa na nani ?

3.Watanzania kwa kuonyeshwa kipindi maalumu kuliwasaidia kulijenga Taifa hili masikini kwa maneno lakini kwa matendo ni tajiri ?

4.Je kuna siku wataonyesha hata tukio la uchaguzi la CUF la uchaguzi na kikao chao in details kama walivyo fanya jana kwa Kawawa ?Maana CUF pia ni Watanzania wanao lipa kofi na kuiendesha TBC .

Naombeni msaada tafadhali .
 
Tatizo la kuchagua kiongozi asiye na mwelekeo, uelewa , wala kujua nini la kufanya hata katika maisha yake mwenyewe ni hili tulionalo kwa rais kikwete.

Ndugu huyu anaonyesha udini bila soni, mbaguzi , mkumbatia wezi, hana maadili (hata ya ndoa tu) na zaidi hana uwezo wa kuongoza.
Ndiyo maana amekuwa akijaza waislamu kwenye uteuzi wa nafasi zote muhimu.

Mfano; jundu ni wakili ambaye hakuonyesha mafanikio yoyote kwenye fani kama wakili, leo jaji kiongozi. Mataka daudi ambaye hata tabia zake za kimemde zinafahamika kapewa kuua atcl wakati awali alipewa kuua bima. Sasa amemrudisha kuizika bima.

Huyu rais ni mzigo. Kwanini bado yupo?

Ngeleja anataka kuiba palepale ambapo lowassa na karamagi wameiba na bila aibu anatuona wajinga. Rais naye anaangalia.

Ingekuwa mtu anamwibia kimada kweli angekaa kimya hivi nchi akibakwa? Anakaa kimya kwa vile yeye haelewi. Anafikiri yeye ni mcheza filamu wakati yeye ni rais. Mungu wangu!!!!

Na zitto kabwe amekuwa mpumbavu. Kisha lipiwa yule!

Ni kwavile watanzania wajinga mno
 
Ndiyo maana amekuwa akijaza waislamu kwenye uteuzi wa nafasi zote muhimu.
Mfano; jundu ni wakili ambaye hakuonyesha mafanikio yoyote kwenye fani kama wakili, leo jaji kiongozi. Mataka daudi ambaye hata tabia zake za kimemde zinafahamika kapewa kuua atcl wakati awali alipewa kuua bima. Sasa amemrudisha kuizika bima.

Ngeleja anataka kuiba palepale ambapo lowassa na karamagi wameiba na bila aibu anatuona wajinga. Rais naye anaangalia.

Na zitto kabwe amekuwa mpumbavu. Kisha lipiwa yule!

Unapotaka kutoa hoja ama michango, acha lugha za matusi. Changia kwa mifano halisi ili tujue ukweli wa unayoyasema. Werevu wako tunaweza kuupima kwa maneno unayotumia.
 
Tatizo la kuchagua kiongozi asiye na mwelekeo, uelewa , wala kujua nini la kufanya hata katika maisha yake mwenyewe ni hili tulionalo kwa rais kikwete.

Ndugu huyu anaonyesha udini bila soni, mbaguzi , mkumbatia wezi, hana maadili (hata ya ndoa tu) na zaidi hana uwezo wa kuongoza.
Ndiyo maana amekuwa akijaza waislamu kwenye uteuzi wa nafasi zote muhimu.

Mfano; jundu ni wakili ambaye hakuonyesha mafanikio yoyote kwenye fani kama wakili, leo jaji kiongozi. Mataka daudi ambaye hata tabia zake za kimemde zinafahamika kapewa kuua atcl wakati awali alipewa kuua bima. Sasa amemrudisha kuizika bima.

Huyu rais ni mzigo. Kwanini bado yupo?

Ngeleja anataka kuiba palepale ambapo lowassa na karamagi wameiba na bila aibu anatuona wajinga. Rais naye anaangalia.

Ingekuwa mtu anamwibia kimada kweli angekaa kimya hivi nchi akibakwa? Anakaa kimya kwa vile yeye haelewi. Anafikiri yeye ni mcheza filamu wakati yeye ni rais. Mungu wangu!!!!

Na zitto kabwe amekuwa mpumbavu. Kisha lipiwa yule!

Ni kwavile watanzania wajinga mno

Heri yako umeona kama alikuwa na hoja... mimi sikuona kila kitu!!!

Alafu wa ndugu... haya mauteuzi wakati mwingine hata sio ya Rais wakuu... ni kwa kuwa katiba tu inasema isemwe hivyo... wakati kuniambia Rais anawafahamu wakuu wa wilaya wote nchini...

Practically Nadhani ofisi ya Waziri mkuu ndio kwa mfano inajua wakuu wa wilaya kuliko ofisi ya Rais.
 
Jamboni wote kwa mpigo.Jana baada ya kuona kipindi maalumu usiku kilicho rushwa na TBC ikiwa na marudio ya tukio la sherehe za kuzaliwa Mfaume Kawawa mengin nimeyaona lakini nikajawa na maswali .Mojawapo ya haya maswali ni haya .

1.Lowasa alijiondoa hakufukuzwa lakini ana hadhi ya waziri Mkuu mstaafu , mbona sikumuona pale wakati wakuu zote wa zamani kama yeye walitinga pale kwenye makulaji na kujidai ?

2.Gharama za jana TBC kurusha matangazo yale kama kipindi maalumu zililipwa na nani ?

3.Watanzania kwa kuonyeshwa kipindi maalumu kuliwasaidia kulijenga Taifa hili masikini kwa maneno lakini kwa matendo ni tajiri ?

4.Je kuna siku wataonyesha hata tukio la uchaguzi la CUF la uchaguzi na kikao chao in details kama walivyo fanya jana kwa Kawawa ?Maana CUF pia ni Watanzania wanao lipa kofi na kuiendesha TBC .

Naombeni msaada tafadhali .

Jibu

  • Kama Rais wa Jamhuri alikuwa kwenye hilo tukio.. hilo linatosha kama justification ya kurusha hicho kipindi bila... kulipiwa.
  • Swali la Lowassa lilishajibiwa kwamba tatizo ni katiba... haikuwahi kusema waziri mkuu akiachia mwenyewe, akijiuzulu etc atakuwa nani... hivyo kamlaumu Mbunge wako Kwanza kwa kulala mpaka kusababisha katiba kuwa na matobo.
 
Tatizo la kuchagua kiongozi asiye na mwelekeo, uelewa , wala kujua nini la kufanya hata katika maisha yake mwenyewe ni hili tulionalo kwa rais kikwete.

Ndugu huyu anaonyesha udini bila soni, mbaguzi , mkumbatia wezi, hana maadili (hata ya ndoa tu) na zaidi hana uwezo wa kuongoza.
Ndiyo maana amekuwa akijaza waislamu kwenye uteuzi wa nafasi zote muhimu.

Mfano; jundu ni wakili ambaye hakuonyesha mafanikio yoyote kwenye fani kama wakili, leo jaji kiongozi. Mataka daudi ambaye hata tabia zake za kimemde zinafahamika kapewa kuua atcl wakati awali alipewa kuua bima. Sasa amemrudisha kuizika bima.

Huyu rais ni mzigo. Kwanini bado yupo?

Ngeleja anataka kuiba palepale ambapo lowassa na karamagi wameiba na bila aibu anatuona wajinga. Rais naye anaangalia.

Ingekuwa mtu anamwibia kimada kweli angekaa kimya hivi nchi akibakwa? Anakaa kimya kwa vile yeye haelewi. Anafikiri yeye ni mcheza filamu wakati yeye ni rais. Mungu wangu!!!!

Na zitto kabwe amekuwa mpumbavu. Kisha lipiwa yule!

Ni kwavile watanzania wajinga mno

Tizo
Join Date: Mon May 2008
Posts: 12
Rep Power: 0

Thanks: 0
Thanked 7 Times in 3 Posts
Credits: 1,310


Mkuu Heshima mbele, Karibu sana JF,

Unaweza ukawa upo sawa kabisa kwenye maada na mchango ulioutoa kwenye hii thread maaana "JF WE DARE TO TALK OPENLY" lakini sasa Mkuu wangu sio kihivyo kama huwezi kuweka uhalisia kwa maana ya ushahidi ilituweze kujua umesimamia wapi kwenye hoja yako nasi tuweza kuchangia.

Humu ndani tunaamini kwamba JF ni THE HOME OF GREAT THINKERS sasa kama ni hivyo hatunabudi kuwa tofauti na watu wa vijiweni. WEKA NONDO KWA MIFANO WATU TUINGIE KAZINI. Haya unayoyasema yapo ila sasa mwaga nyuki tuone mifano.
 
Jibu

  • Kama Rais wa Jamhuri alikuwa kwenye hilo tukio.. hilo linatosha kama justification ya kurusha hicho kipindi bila... kulipiwa.
  • Swali la Lowassa lilishajibiwa kwamba tatizo ni katiba... haikuwahi kusema waziri mkuu akiachia mwenyewe, akijiuzulu etc atakuwa nani... hivyo kamlaumu Mbunge wako Kwanza kwa kulala mpaka kusababisha katiba kuwa na matobo.

Kwa kuongezea nafikiri kama kafa wanaweza kuwa na kiasi cha kulipia kipindi sidhani kama wanaweza kushindwa kurusha vipindi vyao kwenye TBC maana ile ni Televisheni ya Taifa na sio ya CCM
 
Jana baada ya kuona kipindi maalumu usiku kilicho rushwa na TBC ikiwa na marudio ya tukio la sherehe za kuzaliwa Mfaume Kawawa mengin nimeyaona lakini nikajawa na maswali .Mojawapo ya haya maswali ni haya .

1.Lowasa alijiondoa hakufukuzwa lakini ana hadhi ya waziri Mkuu mstaafu , mbona sikumuona pale wakati wakuu zote wa zamani kama yeye walitinga pale kwenye makulaji na kujidai ?.

Huenda alikuwa na udhuru kwa majukumu mengine ya kifamilia ama ya kazi yake ya ubunge, naye ni binadamu kama tulivyo. Kutinga kwa wakuu wengine hakumfanyi naye lazima awepo, jee yeye angekuwepo na mwingine asiwepo?, lingekuja swali kwanini yupo?.
 
Kasheshe if they went LIVE siku ya tukio je kulikuwa na haja tena ya kutumia pesa zetu jana kuwa na kipindi Maalumu ?Mbona alikuwa haonyeshwi huyo Rais kwa kiasi hicho and again what was so special ? Mbona akiwa anafungua mahali tunamuona mara moja na si katika kipindi maalumu ?Je nia ilikuwa kumuonyesha JK kwamba alikuwepo ama kufaya watanzania wamjue JK kwamba hawamjui so we needed kipindi maalumu kama jana usiku ?
 
Tatizo la kuchagua kiongozi asiye na mwelekeo, uelewa , wala kujua nini la kufanya hata katika maisha yake mwenyewe ni hili tulionalo kwa rais kikwete.

Ndugu huyu anaonyesha udini bila soni, mbaguzi , mkumbatia wezi, hana maadili (hata ya ndoa tu) na zaidi hana uwezo wa kuongoza.
Ndiyo maana amekuwa akijaza waislamu kwenye uteuzi wa nafasi zote muhimu.

Mfano; jundu ni wakili ambaye hakuonyesha mafanikio yoyote kwenye fani kama wakili, leo jaji kiongozi. Mataka daudi ambaye hata tabia zake za kimemde zinafahamika kapewa kuua atcl wakati awali alipewa kuua bima. Sasa amemrudisha kuizika bima.

Huyu rais ni mzigo. Kwanini bado yupo?

Ngeleja anataka kuiba palepale ambapo lowassa na karamagi wameiba na bila aibu anatuona wajinga. Rais naye anaangalia.

Ingekuwa mtu anamwibia kimada kweli angekaa kimya hivi nchi akibakwa? Anakaa kimya kwa vile yeye haelewi. Anafikiri yeye ni mcheza filamu wakati yeye ni rais. Mungu wangu!!!!

Na zitto kabwe amekuwa mpumbavu. Kisha lipiwa yule!

Ni kwavile watanzania wajinga mno

Ndugu yangu ungekuwa mkuu wa wilaya tungesema kwanza ufutwe kazi kisha ukapimwe afya.
 
Ndugu yangu ungekuwa mkuu wa wilaya tungesema kwanza ufutwe kazi kisha ukapimwe afya.

Nadhani mkuu huyu alitaka kusema kwamba JK ana udini na kujuana .Nadhani huu ndiyo ujumbe wake kwetu .Na mimi nasema naacha yale yakwazayo naungana nawe kujiuliza na hata kuamini kwamba JK ni mdini na mpenda urafiki anafanya lolote kuendeleza haya .
 
Tizo
Join Date: Mon May 2008
Posts: 12
Rep Power: 0

Thanks: 0
Thanked 7 Times in 3 Posts
Credits: 1,310


Mkuu Heshima mbele, Karibu sana JF,

Humu ndani tunaamini kwamba JF ni THE HOME OF GREAT THINKERS sasa kama ni hivyo hatunabudi kuwa tofauti na watu wa vijiweni. WEKA NONDO KWA MIFANO WATU TUINGIE KAZINI. Haya unayoyasema yapo ila sasa mwaga nyuki tuone mifano.

Ya mifano ni muhimu sana.
 
Nadhani mkuu huyu alitaka kusema kwamba JK ana udini na kujuana .Nadhani huu ndiyo ujumbe wake kwetu .Na mimi nasema naacha yale yakwazayo naungana nawe kujiuliza na hata kuamini kwamba JK ni mdini na mpenda urafiki anafanya lolote kuendeleza haya .


ktk wachangiaji wa muda mrefu hapa JF ambae bado ana ubwege kichwani mwake wewe ni miongoni mwao....

kaka u need to grow kimawazo na unaishushia Heshima JF, ambapo imeandikwa ni Home of Great thinkers. sasa Lunyungu hii ndio thinking capacity yako?...tunaokujua hapa JF umekuwa mzushi na umekuwa na Majina mengi tu unayatumia.
 
ktk wachangiaji wa muda mrefu hapa JF ambae bado ana ubwege kichwani mwake wewe ni miongoni mwao....

kaka u need to grow kimawazo na unaishushia Heshima JF, ambapo imeandikwa ni Home of Great thinkers. sasa Lunyungu hii ndio thinking capacity yako?...tunaokujua hapa JF umekuwa mzushi na umekuwa na Majina mengi tu unayatumia.


Chuma uliyo yaandika sasa ndiyo ya ma thinkers na si ubwege ? Kaka dwell kwenye hoja wacha kulia lia hapa .Unapingana na udini na urafiki wa JK na teuzi zake ama unataka kusemaje ?
What is the connection of my writing na uzushi wako wewe ambao unaniita mimi mzushi ?

Hoja imewekwa inakosolewa mie nimechukua niliyo yaona na wewe si kuniita bwege bali uje uonyeshe mawazo yako endelevu kaka .Nangoja kuona hoja na si vioja .
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom