Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Chuma uliyo yaandika sasa ndiyo ya ma thinkers na si ubwege ? Kaka dwell kwenye hoja wacha kulia lia hapa .Unapingana na udini na urafiki wa JK na teuzi zake ama unataka kusemaje ?
What is the connection of my writing na uzushi wako wewe ambao unaniita mimi mzushi ?

Hoja imewekwa inakosolewa mie nimechukua niliyo yaona na wewe si kuniita bwege bali uje uonyeshe mawazo yako endelevu kaka .Nangoja kuona hoja na si vioja .

Lunyungu ntaendelea kukuita bwege kwakua huwezi pambanua Hoja Makini na Dhaifu ni ipi...!!!

Huna dalili za kutosha za kuonesha JK ni mdini..., ila JK amekuwa mdini pale tu anapochagua mwislam....Bahati mbaya hao baadhi ya waislam wenyewe wanaoteuliwa kt teuzi hizo hata kuswali hawaswali...!!

JK kamchagua Jaji mpya Catherine Opiyo, lkn Hadi sasa hujaona watu kuweka News bulletin au watu kutaka wasifu wake au kujua Opiyo kachaguliwa kwa Dini yake au Uswahiba wake...au labda Lunyungu na Genge lako utupe data za Huyu Opiyo kateuliwa kwa Dini yake au uswahiba wake na JK au Mama Salma?

Alipochaguliwa Jundu, hata kabla waandishi wa magazeti hawajaweka au ku-updates news zao, usiku tu news iliwekwa hapa. kwa uzoefu hapa JF, ndugu zetu wakristo mpo so sensitive pindi tu teuzi kubwa akipewa Mwislam. na kwa utaratibu huu twendeni tu lile taifa mnalotaka kulijenga litakuwa na costs za taifa hilo kila mmoja wetu atalibeba.
 
i) hebu kweli tuangalie % ya aliowateua JK je wengi ni maswahiba Waislamu au wakristo?

May be JK anatekeleza Afirmative Action kuwapa upendeleo waislamu ktk nafasi za uteuzi wa juu kwani kwa mda mrefu walibaki nyuma kutokana na sababu za shule na historia..ila sasa wapo wengi wanaoqualify!

ii)Fikiria tu mama Mongela alieanda kwake akamlilia mwanae ana matatizo ya ndoa yake na karamagi..basi yule mtoto akepewa Ukuu wa Wilaya Kigoma yaani kufumba na kufumbua!
 
Mkuu Lunyungu, concern zako umeshazibainisha lakini majibu yanakuja aina aina. Ingekuwa vema iwapo ungeeleza maana nyuma na concern zako, mathalani kwa kuelea ni nini kimekusukuma kuwaza ulivyowaza, ili kutupa mwanga zaidi utakaotusaidia kupata majibu muruwa na concerns zako.
 
Namuunga mkono Lunyungu kwa kupembua na kuona kuwa licha ya lugha chafu iliyotumika lakini ni dhahili kuwa muungwana anaendeleza sana urafiki na udini; na hili ameambiwa point blank na pengo alipohudhulia silver jubilee yake kuwa si busara kwa Rais kushauriana na viongozi wa dini moja tu!! Ukitaka ushahidi angalia utendaji wa David Mattaka hapo ATCL halafu justification ya yeye kumteua kwenye task force ya NIC [wakati huko ATCL kazi inamshinda] not to mention the appointment ya Jundu kama jaji kiongozi!! Hii ni mifano michache, one could go on and on; huyu bwana analipeleka taifa pabaya!!
 
Lowasa huenda anaona soo hata angekaribishwa angeweza akaingia mitini!

Kule Moshi Lowasa alipita mahali..basi umati wa watu wakawa wanamkimbilia eti wamemwona mzee wa Richmond! Akaingia ktk gari na kuishia!

Lowasa anaonekana kama Fisadi Celebrity sasa hivi!!
 
Lunyungu, heshima mbele mkuu; Lowassa sio waziri mkuu mstaafu [ he never finished his term] bali ni waziri mkuu aliyejiuzulishwa[ forced to resign].
 
Masha hivi ni Mwislamu?, Karamagi je?, Chenge je?, Lowasa Je?, Hivi nyinyi mnataka kusema kitu gani? hivi hao walipata kuteuliwa na muungwana kwa sababu waliukana Ukristo wao? au kwamba Ukiristo wao uliwafanya wawe Watendaji wazuri?. Muungwana ana matatizo yake, lakini pasipo ushahidi haipaswi kueneza maneno yasiyo na uhakika. binafsi siungi mkono Uteuzi wa Mataka atcl, lakini msilete hoja za ajabu ajabu kwamba kwa sababu ni mwislamu ndo maana kateuliwa pale, Tz mbona kuna Waislamu kibao wenye uwezo kwa nini ateuliwe Mataka?, ndo maana hoja ya udini hapa naona haina mshiko
 
Jakaya ukweli ana uswahiba wa hali ya juu. Viongozi walio madarakani 90% ni marafiki wakubwa sana wa Jakaya na hili limekuwa ni moja ya sababu ya kushuka kwa maadili ya uwongozi na kushuka kwa uwajibikaji wa viongozi serikalini.

Viongozi hawaoni haya kutamka kwamba mkuu ni mtu wangu hata nikifanya madudu hakuna kitu nitafanywa. Hakukuwa na sababu yoyote ya kuendelea kuwa na Chenge, Iddris Rashid, Mataka, Rostam wengineo kama si uswahiba.

Kuhusu udini nadhani tuwe makini kidogo kwani Tanzania kuna dini nyingine zaidi ya ukristo na uislamu, kuna hindu,budhi, bohora nk. Sasa sijui mnaanzia wapi katika point hii?
 
Nadhani mkuu huyu alitaka kusema kwamba JK ana udini na kujuana .Nadhani huu ndiyo ujumbe wake kwetu .Na mimi nasema naacha yale yakwazayo naungana nawe kujiuliza na hata kuamini kwamba JK ni mdini na mpenda urafiki anafanya lolote kuendeleza haya .

Maada hii inaweza kuwa imewekwa vibaya na mtoa hoja lakini ni mhimi key words zikazingatiwa japo hazina nyama 'ushahidi kutoka kwa mtoa hoja''. Kashfa ya udini na uswahiba kwa rais wetu imekuwa ikimkabili toka alipoingia madarakani hivyo ni vema akabadirika na sio waungwana kutetea hoja hii ikiwekwa hapa
 
Sio ana udini hapana hilo nalikataa kabisa ,hana udini wala uswahiba,alichokuwa nacho ni mbovu wa kudhibiti uongozi wake ,ni mbovu yeye na Chama chake wote wameoza kila mmoja anahari mbaya kuliko mwenziwe ndio ikawa wanaogopana ogopana.
Kuna siku Kikwete alijikaza akasema Uraisi au uongozi wake hauna ubia.

Kwa kauli hiyo inaonyesha wazi kuwa Raisi Kikwete ni m'binafsi ,hapendi ushirika ,hapendi kuelekezwa ,hapendi kusaidiwa maamuzi ,kwa alivyolingana na kauli hiyo anaonyesha wazi hasikilizi mtu yeyote na zaidi akiona anazidiwa huwa cha watu wafanye watakavyo.

Kwa vile hana ubia huwa anajifanyia na kujisemea kivyakevyake kama tunavyoona katika kauli zake hasa za hivi karibuni amekuwa mkali na vitisho ,ameanza Pemba na sasa anamalizia huku Tanganyika.

Sababu za ukali na vitisho ni kuona kuwa mambo yameshamuharibikia na aliokuwa akiwategemea wote wanamatatizo ya ufisadi tokea mmoja mmoja mpka Chama Chake kizima chote kinahusishwa na ufisadi.

Na kila anapojaribu kupanga hakuna hata moja linalokuwa mwisho linaishia kuwa ni ahadi hewa na kuzidi kuonekana hatimizi ahadi anazoziweka na hana njia ya kuzifanya zikatimizika ,kwani CCM wote ni viluilui wenye njaa ,huna utakapowaweka wasidokoe na kula na kumaliza kabisa liwalo na liwe ,ndipo walipofikia CCM hivi sasa ,kila mmoja anaona bora akwibe akajikalie popote pale,hata akifukuzwa Chama huwaga ameshachukua chake mapema ,sasa huku kuchagua mashehe masharifu anaona labda kutamsaidia lakini hakuna cha shehe wala sharifu wote wezi ukienda kwa mapadire wanauwa maalbino ukija kwa mashehe wanakula feza ya bakwata ,hajui amshike nani,hamna kitu ,wizi mtupu.

Haoa tulipo CCM tayari imeshaigawa nchi katika makundi ya kibabe ,gangs mbali mbali zipo Tanzania zikiongozwa na wakubwa waliomo serikalini ,tumeona akina Zombe ,tumeona akina Mahita ,tunawaona wanaokuwa matajiri kwa muda mfupi tu wa Uongozi ,hakuna kitu kila mmoja anafanya anachokiweza kujipatia mapato ya wizi.

Kuna sehemu zinaingiza fedha sana hapa serikalini ,anaesimamia fedha hizo hafikishi zote na pengine hafikishi kabisa zinaishia katika mahesabu ya uwongo.
 
Masha hivi ni Mwislamu?, Karamagi je?, Chenge je?, Lowasa Je?, Hivi nyinyi mnataka kusema kitu gani? hivi hao walipata kuteuliwa na muungwana kwa sababu waliukana Ukristo wao? au kwamba Ukiristo wao uliwafanya wawe Watendaji wazuri?. Muungwana ana matatizo yake, lakini pasipo ushahidi haipaswi kueneza maneno yasiyo na uhakika. binafsi siungi mkono Uteuzi wa Mataka atcl, lakini msilete hoja za ajabu ajabu kwamba kwa sababu ni mwislamu ndo maana kateuliwa pale, Tz mbona kuna Waislamu kibao wenye uwezo kwa nini ateuliwe Mataka?, ndo maana hoja ya udini hapa naona haina mshiko

Ni mwislamu 🙂
 
Mnapoleta udini CCM itaendelea kupeta kwa sababu kule watu wa dini zote na makabila yote wananyonya kwa zamu.
 
Code:
Lunyungu ntaendelea kukuita bwege kwakua huwezi pambanua Hoja Makini na Dhaifu ni ipi...!!!

Huna dalili za kutosha za kuonesha JK ni mdini..., ila JK amekuwa mdini pale tu anapochagua mwislam....Bahati mbaya hao baadhi ya waislam wenyewe wanaoteuliwa kt teuzi hizo hata kuswali hawaswali...!!

JK kamchagua Jaji mpya Catherine Opiyo, lkn Hadi sasa hujaona watu kuweka News bulletin au watu kutaka wasifu wake au kujua Opiyo kachaguliwa kwa Dini yake au Uswahiba wake...au labda Lunyungu na Genge lako utupe data za Huyu Opiyo kateuliwa kwa Dini yake au uswahiba wake na JK au Mama Salma?

Alipochaguliwa Jundu, hata kabla waandishi wa magazeti hawajaweka au ku-updates news zao, usiku tu news iliwekwa hapa. kwa uzoefu hapa JF, ndugu zetu wakristo mpo so sensitive pindi tu teuzi kubwa akipewa Mwislam. na kwa utaratibu huu twendeni tu lile taifa mnalotaka kulijenga litakuwa na costs za taifa hilo kila mmoja wetu atalibeba.

Chuma better you have made yourself clear kwamba Uislam wako umekusukuma kunishushia tuhuma na kashfa ambazo huna ushahidi nazo .Mie mkuu nikisema kitu kinaanzia tetesi na kinakuwa ukweli .Sasa ngojea nakuletea nyingine karibuni itakuwa tetesi hadi utakapo ona kwamba mimi si mtu wa aina yako .

Mada ilisema ama Mdini ama Swahiba .Sasa kwenye udini anaonekana ana kunyoosha ila ushwahiba ndiyo zaidiiiiiii.Wote wanao lete mashida Nchini ni washikaji zake ama ndani ya Chama ama Baraza la mawaziri ama mtaani .Hoja ilikuwa kujadili mambo haya 2 na si kushusha tuhuma ambazo huna ukweli nazo .

Sasa tujadili ni Udini ama Uswahiba ?Ndiyo issue hapa .Tuanzie hapa .
 
Lunyungu,
Ni udini na uswahiba vyote viwili kwa pamoja.
 
Jamboni wote kwa mpigo.Jana baada ya kuona kipindi maalumu usiku kilicho rushwa na TBC ikiwa na marudio ya tukio la sherehe za kuzaliwa Mfaume Kawawa mengin nimeyaona lakini nikajawa na maswali .Mojawapo ya haya maswali ni haya .

1.Lowasa alijiondoa hakufukuzwa lakini ana hadhi ya waziri Mkuu mstaafu , mbona sikumuona pale wakati wakuu zote wa zamani kama yeye walitinga pale kwenye makulaji na kujidai ?

2.Gharama za jana TBC kurusha matangazo yale kama kipindi maalumu zililipwa na nani ?

3.Watanzania kwa kuonyeshwa kipindi maalumu kuliwasaidia kulijenga Taifa hili masikini kwa maneno lakini kwa matendo ni tajiri ?

4.Je kuna siku wataonyesha hata tukio la uchaguzi la CUF la uchaguzi na kikao chao in details kama walivyo fanya jana kwa Kawawa ?Maana CUF pia ni Watanzania wanao lipa kofi na kuiendesha TBC .

Naombeni msaada tafadhali .

Hata mimi nilikiona kipindi hicho kilichoitwa maalum. Kwangu ni sawa na Robert Mugabe alivyofanya kijisherehe chake kwa pesa ya serikali. It was personal using tax payers money, wala hatukutakiwa kuoneshwa. Kutuonesha wajukuu na wanae wanacheza sijui Lizombe na vijiotuba vya wakina Msekwa. Havikuwa na maana kwetu.
Nadhani there was a motive behind this program. Just rubish.
Ila mzee Kawawa kazeeka sana na nilimuona kama hana memory nzuri tena. Hata ile hotuba alitoa unaona haina mpangilio wowote na ni kama vile hakujua aseme nini na aache nini. Ndio maana aliona atuombe msamaha watanzania.
 
Sii vibaya kuwaenzi wazee wetu ..hivi nani tena mzee wa aina yake aliyebaki kama huyu?

Ni sehemu ya historia yetu!
 
David ana tabia za kimende? Hilo ni jambo ambalo sina habari nalo. I mean,kwa jinsi David alivyokuwa na sura nzuri,ungesema ana tabia za kishoga,ningeamini upesi zaidi.
Mimi sipendi discrimination,lakini kama mtu ana tabia za kimende au kishoga,nasema,asipewe cheo kama hicho kuongoza ATCL,na kama amepewa kazi kama hiyo,aambiwe kwamba hawezi kuendelea na kazi hiyo,mpaka aache tabia kama hizo.
Rais Mwinyi aliwakabili watu,aliwaita ofisini kwake,akawaambia,''Ni kweli kuhusu haya mambo nimesikia unayoyafanya? Acha kabisa mambo hayo.''
Kuhusu Rais Kikwete kutokuwa mwaminifu katika ndoa yake,haya mambo mimi pia nimesikia,from usually realible sources. Lakini hilo ni jambo ambalo halituhusu sisi,linamhusu Salma tu.
JK anapendwa na watu. And maybe it is safe to say kwamba atachaguliwa tena kuwa mgombea Urais wa CCM 2010.
Mtu kama Zitto,yupo katika system. Akiongea vizuri,anapata kuchaguliwa kuwa katika kamati au Bodi za Wakurugenzi,au anapata nafasi ya kusafiri[kwenda nchi nje ya Nchi],kwa hiyo,usitegemee kwamba atajali maslahi ya watu wa chini.
Hapa lazima tujue kuna mambo mawili ,movement and change. Do we want to get things moving or do we want to change things. Kama alivyosema Marx,"previous philosophers have explained the world,our job is to change it'' Tunataka more of the same,kwamba Kikwete aendelee kuwa Rais,au tunataka aache Urais ''sasa hivi.'' Hakuna precedent katika nchi hii ya Rais kuacha Urais ghafla,from a vote of no confidence. Kwa hiyo labda tunaweza kusema kwa uhakika kwamba Kikwete atakuwa mgombea Urais 2010. Kuhusu kuchaguliwa kwake,it is difficult to say. Watu wamekuwa na very strong feelings kuhusu ufisadi,ambalo ndilo jambo lililosababisha Rais awashukie mafisadi. Lakini if the people have been appeased with what has been done so far,it is not easy to determine.
Hili ndilo jambo ambalo ninalopenda kuhusu JF.ukisoma JF unajifunza mambo mengi,kwamba Zitto ni mpumbavu,kwamba David Mataka ni mende,kwamba Karamagi anataka kuiba,kwamba Watanzania ni wajinga.
Lakini Watanzania siyo wajinga. Mwaka jana nilikuwa nasikiliza kipindi cha TBC1 ambapo Esha Muhiddin alikuwa anawauliza wananchi kuhusu kero za Serkali. Na wananchi wote walikuwa na complaint moja,kwamba viongozi wakichaguliwa hawajali maslahi ya wananchi,wanajali maslahi yao. Na Esha Muhiddin alipokuwa anawauliza,wanadhani nini kifanyike,jibu wote lilikuwa moja tu,"Hawajui nini kufanyike ili kutanzua tatizo hili.'' Hiyo ilikuwa kabla Serikali haijaamua kuwakamata mafisadi. Lakini wananchi wanaweza kuamua kwamba Uchaguzi unaweza kuwa njia ya kuiwajibisha Serikali,na kama itakuwepo viable Opposition Party,CCM inaweza kuondolewa madarakani.
In other words,mimi naona kwamba ipo possibility ya CCM kushindwa katika Uchaguzi,au kujirekebisha sasa hivi kwa kufanya major changes katika uongozi.
Na wakibadili uongozi,siyo Lunyungu ambaye atachaguliwa kuwa Rais. Wapo viongozi waandamizi ambao watachaguliwa katika nafasi hizo.
Sisi hapa tunatoa maoni tu kuhusu mstakabali wa Taifa.
 
Sii vibaya kuwaenzi wazee wetu ..hivi nani tena mzee wa aina yake aliyebaki kama huyu?

Ni sehemu ya historia yetu!

Nani kasema asienziwe? Kuenziwa ni mpaka kutumia tax payers money? Hiyo pesa haina cha kufanya? Tunaitaji rais kichaa ili nchi ibadilike?
Ni haya haya yanayotumaliza waafrika. eti KUWAENZI WAZEE WETU.
Zimbabwe watu hawana chakula hawana dawa wanakufa kwa magonjwa viongozi mnajienzi kwa maelfu ya dolas.
Haya Bwana endeleeni kujienzi...........
 
Masha hivi ni Mwislamu?, Karamagi je?, Chenge je?, Lowasa Je?, Hivi nyinyi mnataka kusema kitu gani? hivi hao walipata kuteuliwa na muungwana kwa sababu waliukana Ukristo wao? au kwamba Ukiristo wao uliwafanya wawe Watendaji wazuri?. Muungwana ana matatizo yake, lakini pasipo ushahidi haipaswi kueneza maneno yasiyo na uhakika. binafsi siungi mkono Uteuzi wa Mataka atcl, lakini msilete hoja za ajabu ajabu kwamba kwa sababu ni mwislamu ndo maana kateuliwa pale, Tz mbona kuna Waislamu kibao wenye uwezo kwa nini ateuliwe Mataka?, ndo maana hoja ya udini hapa naona haina mshiko

Gamba La Nyoka nakupata.

Wengi, kama sio wote, wanaodai Kikwete mdini naona kama hawako coherent fulani hivi, kama wamechanganya madawa hivi, sijui kama umegundua.

Mmoja kasema Kikwete anapendelea Waislam, halafu hapo hapo akamchana Kikwete kwa ku replace cheo cha Nazir Mustafa Karamagi na William Ngeleje. Katoka Muislam kaingiza Mkristo! Huyo ndo mleta hoja huyo. Dopey! Halafu, listen to this, kwenye kichwa cha thread mawazo yake kwamba Kikwete ni mdini anayaita "tetesi"!

Kaja fuzzy act mwingine anasema kuna mtoto wa mkubwa alikuwa na matatizo ya ndoa Mama yake akaenda kumlilia Kikwete, Kikwete katika kutatua tatizo la kijana la ndoa akampa mtoto Ukuu wa Wilaya Kigoma! Imagine that! Halafu huyu act anasema inawezekana Kikwete anarekebisha kutowiana kwa nafasi za uongozi baina ya waislam na wakristo kulikojengeka miaka ya nyuma "ila sasa wapo wengi wanaoqualify." Kwa hiyo ina maana Kikwete anateua Waislam ambao wana qualify, sio? Yani incoherence tupu.

Kaja mwingine anasema "naacha yale yakwazayo... na kuamini kwamba JK ni mdini na mpenda urafiki." Sasa, topic nzima ya mleta mada ni dopey, haja substantiate hoja yake, yote yanakwaza, halafu mtu anakuja kusema anaacha yale yakwazayo ila anakubaliana na "ujumbe wake kwetu." Boloney.

Blowhard mmoja kadai kwamba ushahidi kuwa Kikwete ni mdini ni kwamba David Mattaka bado anapewa mashirika japo ni mbovu (I am assuming huyu David Mattaka ni mwislam). Lakini hajaeleza inakuwaje Kikwete anavumilia wakurugenzi wabovu wote? Kwa maneno mengine, ni mpaka utakapoonyesha kwamba kuna mkurugenzi mbovu Mkristo ambaye Kikwete kam fire akamwacha Mattaka, Muislam, na ubovu wake, hii pointi inabaki kuwa ni bangi bangi tu.

Na huyu jaji Jundu, akaongeza huyu blowhard, ni ushahidi wa udini wa Kikwete. Lakini ukimuuliza jaji Jundu ana uzoefu wa muda gani hajui! Ukimuuliza ni kwa nini Kikwete amewaruka majaji wengine Waislam wenye uzoefu kupita Jundu, amempendea nini Jundu hajui! Just blowhard blabber.
 
Hakuna sababu yoyote kwa nini Kawawa asifanyiwe Birthday Party Ikulu. Kawawa ni Simba wa Vita,alikuwa Waziri wa Ulinzi Tanzania ilipokuwa inapigana na Idi Amin.
Hii siyo njia ya CUF kupata umaarufu,kwa kusema pesa za Serikali zinapotea Kawawa akifanyiwa Party.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom