Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Wewe unasound kama mdini vile? Ulipata wapi muda wa kuwajua hawa kwa dini zao na sio umaarufu wao!!!!!!!!!!

Kwani Mwanakijiji alipata wapi muda wakujua kuwa wajumbe wa kamati kuu ni waislam?
Mdini ni mimi au alieanzisha mada hii ya udini?
 
Kwani Mwanakijiji alipata wapi muda wakujua kuwa wajumbe wa kamati kuu ni waislam?
Mdini ni mimi au alieanzisha mada hii ya udini?

YEYE NI UDINI NA WEWE NI UKABILA..UJUMBE HUO WENU NI WA KUMNUFAISHA MFISADI NA KUMYIMA MTANZANIA HAKI!

Wewe kama ni WANGWE...Basi karibu sana jf!

Wewe na mwenyekiti wenu mmesababisha tuendelee kuwajadili nyie badala ya matatizo yanayotukabili Tanzania!

Wananchi wa TARIME...MWAMBIENI HUYU WANGWE AULIZIE RIPOTI ZA EPA NA MADINI NA SI KUPIGA KELELE ZA RUZUKU NA UKABILA KABLA HATA YA UCHUNGUZI AMA RIPOTI ZA UCHUNGUZI!

NANI ALIYEWAAMBIA KUWA MTAPIGIWA KURA KABLA YA WANANCHI KUELEWESHWA?

Uamuzi wenu unamnufaisha fisadi na hivyo sichelei kusema kuwa mmetumwa!
 
Mdaku uliyeleta habari ya UDAKU ukashindwa kuleta facts, ulidhani umepata kumbe umepatikana. Siku ingine ukifungua thrad hakikisha una DATAZ za kutosha.

Chonde, chonde, Mama! Naona haumtendei haki Mgaya kwenye hili. Yeye ameambatanisha kielelezo kinachomfanya aseme kuwa kuna udini CCM. Ili kumpinga katika mada yake ni aidha umuonyeshe kuwa hicho kielelezo si sahihi au kuwa kielelezo hicho hakitoi picha halisi au huyo anayetaka aondoe udini hana mamlaka ya kufanya hivyo ( kama kuna udini). Kumuuliza swali nje ya mada na kudai kwa vile ameshindwa kulisimamia basi hata hii mada yake ni udaku, ni kupotosha mambo. Swali la watu wa dini gani ndiyo waliohusika katika kugombea uhuru lina utata kwa sababu liko based kwenye assumption kwamba waliopigania uhuru walikuwa ni wale wanachama wa TAA na baadae TANU tu. Umeelezwa, mwanzoni kabisa, kuwa kutokana na TAA ( ambacho hakikua na itikadi ya kugombea uhuru kabla ya Nyerere) na baadae TANU vilianzishwa na kukuzwa pwani basi bila shaka wanachama wake wengi na viongozi walikuwa waislamu. Lakini vilevile ikumbukwe kuwa wakristu wenye uwezo wengi wao walikuwa wameajiriwa na serikali ya mkoloni ( walimu n.k) kwa hiyo wasingeweza kujitokeza wazi wazi kutetea msimamo wa TANU. Wakati waislamu wengi waasisi walikuwa wafanya biashara ( wakina Sykes n.k.) kwa hiyo kwao hilo halikuwa tatizo. Wafanya biashara wakristo kama Mzee Rupia waliweza kujitokeza kwa sababu hizo hizo. Karibu na baada ya uhuru ambapo uwezo wa ku'manage' ukapewa kipaumbele na ndipo wasomi wakaanza kujitokeza. Again, for historical reasons, wasomi wengi walikuwa wakristo.
Swali la Mgaya ni pertinent na ni lazima lijadiliwe kwa uwazi ili kama kuna kamzizi ka udini katika jamii tuushughulikia kabla haijawa taabu. Kwa mkristo kukaa na kuhesabu idadi ya waislamu katika nafasi ya uongozi haiashirii mema kama vile walivyokuwa wakifanya waislamu wakihesabu wakristo katika nafasi za uongozi. Vilevile kuangalia vyama kwa misingi ya dini. Lakini kusema hivi hakuwaondolei wajibu viongozi wa vyama hivyo kuhakikisha kuwa masuala ya dini, kabila, jinsia, umri, ulemavu havina nafasi katika vyama vyao. Wakiona hali inajitokeza wafanye jitihada za kuikabili. Vyama vya upinzani(UDP,CHADEMA,CUF, TLP, NCCR-Mageuzi n.k) ni lazima vifanye jitihada za ziada kukaribisha na kuvutia wanachama na viongozi kutoka sehemu ambazo sio core constituencies zao. CCM kutokana na kuwa na wigo mkubwa zaidi, kinabidi kuhakikisha masuala haya hayajitokezi. Wanapopuuzia kufanya hivi ndipo shutuma kama hizi zinapojitokeza.
 
Hakuna udini Raisi aondoe udini gani?CCM haiteuwi wajumbe bali wanapigiwa kura!

First Lady...Nilikuwa nikirekebisha kuhusu EPA ilivyoanzishwa makusudi kuchafua baada ya migodi na mali nyingine za mabilioni ya dola za kimarekani kuuzwa na kumilikiwa isivyo halali.

Na nikasema kuwa ni mpango maalum wa ccm KWANI IDDI SIMBA NA WENZAKE NI WAISLAM Lakini mtiririko wa PESA ZA EPA ULIWALENGA WATU FLANI FLANI ESPECIALLY WACHAGGA NA WAKRISTO...Na sasa hoja ya ccm ni uchagga na ukristo vs uislam na si migodi na mali nyingine!

EPA NI MCHEZO MCHAFU WA KISIASA NA KIMAFIA ULIOANDALIWA NA MWENYEKITI WA ccm WAZAZI..IDDI SIMBA....Akishirikiana na mawakili wa MALEGESI pamoja na familia ya LUKAZA..Mbinu hii ya ccm ni Kama silaha ya kujikinga na vita vyetu vya kudai uhuru wetu!
 
Huu Nimuda Wa Kuangalia Maendeleo Ya Nchi, Tumo Kwenye Ushndani Wa Viama Vingi Tukianza Kuleta Udini Kwenye Chama Tawala Tutajigawa Utakuwa Mwanya Kwa Wapinzani. Muhimu Wenye Cheo Anaweza Kutuletea Maendeleo Na Tumpe Support Kwa Nguvu Zote Tusiangalie Dini Wala Kabila Lake.
wakati Wa Utawala Wa Rais Mkapa Ukiristo Ulitawala Sehemu Zote Waislamu Hawakusema Kitu Iweje Leo Yamekuwa Hayo?tukiangalia Hayo Amani Itatoweka Nchi.

Tusiwe disingeneous. Waislamu walisema sana wakati wa Mkapa kama vile wakristo walivyomlalamikia Mwinyi.
 
mgagagigikoko.. unathibitisha hoja kuwa ukimuona mtu anaitwa Kimaro haina maana ana ukabila! Na ukiona mama anaitwa mama Mushi haina maana ni Mchagga! Na ukimkuta mchagga aliyezaliwa na kukulia usukumani na anaitwa Massawe usije ukakimbilia na kusema anatoka Kilimanjaro! of course, kwenu mtasema anatoka Kilimanjaro kwa sababu ndicho kilichotumiwa kwa Mdee hicho siyo?

Nilikuwa namjibu Mgaya ambaye nilimwambia kitu cha kwanza ni kufanya utafiti kuwa jina la mhusika ni ni dini gani? kuna msemo maarufu unasema'no research no right to speak' hajafanya utafiti anaongea bila kuwa na uhakika na anachokiongea,

ndio maana nimetoa majina hayo kuonesha kuwa hoja hoja ya MGAYA ni lemavu isiyo na mashiko(baseless).

Wachaga wa Chadema tumewafanyia utafiti wa kina,Grace Kihwelu ni mchaga na mtu wa karibu sana na Mbowe.Lucy Owenya ni mtoto wa Ndesamburo ambaye ni kigogo wa wachagga na wengine wote,umefanywa utafiti wa kina hadi mahusiano ya familia hizo.

Anna KOMU nae ana link kubwa Kilimanjaro ingekuwa unaweza kusema kuwa ni raia wa kilimanjaro by naturalisation, hujawahi kuona mhindi kazaliwa India anaomba uraia kwa kupitia naturalisation?, anasema kama kuna mtu ana kipingamizi akipeke wizaya ya mambo ya Ndani,ANNA KOMU amejipa hadi jina la kichagga ni zaidi ya naturalisation citizen.
 
Tusiwe disingeneous. Waislamu walisema sana wakati wa Mkapa kama vile wakristo walivyomlalamikia Mwinyi.

Msilete mambo yenu ya kuuwa issue!
Mlijificha kwenye mijadala ya kimataifa na sasa bado tuko na nyie huku kwani nilishawaambia before!Wewe kama hutaki tukate issue nyeti basi na wewe una maslahi ya kifisadi!
EPA ILIANZIA ccm kwenye utitiri wa waislam...Sasa IDDI SIMBA NI MKRISTO?AMA MCHAGGA?
ccm MSILETE UCHAWI HAPA JF HAUFANYI KAZI!
 
Iddi Simba Alitumwa Na Waislam Kwenda Kuiba Pesa Za Epa?
Pesa Za Epa Unajuwa Mtiririko Wake? We Mtu Gani Na Ruzuku Wakati Huu? Kweli Halafu Ni Msomi?
Mi Nakwambia Ukipoteza Uhuru Wako Kama Umenunuliwa Basi Na Utashi Unapotea Na Unajikuta Unaongea Kama Uko Programmed!
Yani Maneno Yako Ni Kama Umetumwa Lakini Si Wangwe Tuliyekuwa Tukimfahamu!
Tanzania Ya Sasa Ni Tofauti Na Pia Naomba Uzingatie Hilo!
 
Nilikuwa namjibu Mgaya ambaye nilimwambia kitu cha kwanza ni kufanya utafiti kuwa jina la mhusika ni ni dini gani? kuna msemo maarufu unasema'no research no right to speak' hajafanya utafiti anaongea bila kuwa na uhakika na anachokiongea,

ndio maana nimetoa majina hayo kuonesha kuwa hoja hoja ya MGAYA ni lemavu isiyo na mashiko(baseless).

Wachaga wa Chadema tumewafanyia utafiti wa kina,Grace Kihwelu ni mchaga na mtu wa karibu sana na Mbowe.Lucy Owenya ni mtoto wa Ndesamburo ambaye ni kigogo wa wachagga na wengine wote,umefanywa utafiti wa kina hadi mahusiano ya familia hizo.

Anna KOMU nae ana link kubwa Kilimanjaro ingekuwa unaweza kusema kuwa ni raia wa kilimanjaro by naturalisation, hujawahi kuona mhindi kazaliwa India anaomba uraia kwa kupitia naturalisation?, anasema kama kuna mtu ana kipingamizi akipeke wizaya ya mambo ya Ndani,ANNA KOMU amejipa hadi jina la kichagga ni zaidi ya naturalisation citizen.

Unazungumza kwa hekima lakini ni hekima iliyopotoka... kwenye hao uliowataja unashindwa kusema wote ni wachagga kwa sababu unajua si wote ni wachagga. Tukiwabana kuhusu makabila yao mnahama na kusema mikoa, tukisema si wote wanatoka mikoa hiyo mnasema mtu kaolewa huko so by extension ni mtu wa kilimanjaro na by extension ni mchagga!!

Lakini hata kwa jitihada hiyo kweli mnaweza kusema watu sita wanaweza kukifanya chama kizima kiwe cha kikabila?
 
Hii ni nafasi nyingine kwa Mwenyekiti wa ccm kuweka usawa kwenye chama kinachoongoza nchi yetu. Suala la kuwa na viongozi wengi wa kamati kuu ya ccm ambao ni kutoka dini moja linaleta picha ambayo haionyeshi usawa wa dini mbili kubwa Tanzania za Ukristo na Uislam.

Huu ni ushauri tu, ni muhimu sana kwa Kikwete kushawishi wanaccm kuwa na katiba ambayo itaweka usawa wa kidini kwenye chama tawala.

Majina haya yanaonyesha kile kinachoendelea CCM:

1. Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete - Mwenyekiti - Muslim
2. Ndugu Pius Msekwa - Makamu Mwenyekiti (Bara) -
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar) - Muslim
4. Ndugu Yussuf R. Makamba - Katibu Mkuu - Muslim
5. Capt. (mst) George Huruma Mkuchika - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)- Muslim
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe - Muslim
8. Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe - Muslim
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe - Muslim
11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe
12. Mzee Rashid Mfaume Kawawa - Mjumbe - Muslim
13. Dr. Salmin Amour - Mjumbe - Muslim
14. Ndugu John Samwel Malecela - Mjumbe
15. Capt. (mst) John Zefania Chiligati - Mjumbe
16. Ndugu Amos Gabriel Makala - Mjumbe
17. Ndugu Bernard Kamilius Membe - Mjumbe
18. Ndugu Kidawa Hamid Saleh - Mjumbe - Muslim
19. Ndugu Samwel John Sitta - Mjumbe
20. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe - Muslim
21. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
22. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe - Muslim
23. Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe - Muslim
24. Ndugu Pindi Hazara Chana - Mjumbe
25. Ndugu Andrew Chenge - Mjumbe
26. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe - Muslim
27. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe - Muslim
28. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe - Muslim
29. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe - Muslim
30. Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe - Muslim
31. Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe - Muslim
32. Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe -
33. Ndugu Fatuma Said Ali Mchumo - Mjumbe - Muslim
34. Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe - Muslim
35. Ndugu Omar Yussuf Mzee - Mjumbe - Muslim
36. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
37. Ndugu Ali Ameir Mohamed - Mjumbe - Muslim
38. Ndugu Yussuf Moh’d Yussuf - Mjumbe - Muslim

Majibu nilikupa mapema soma hapa na ukurasa wa 18 labda huelewi tizama rekodi ya Mkapa.
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=15199&page=17
 
First Lady...Nilikuwa nikirekebisha kuhusu EPA ilivyoanzishwa makusudi kuchafua baada ya migodi na mali nyingine za mabilioni ya dola za kimarekani kuuzwa na kumilikiwa isivyo halali.

Na nikasema kuwa ni mpango maalum wa ccm KWANI IDDI SIMBA NA WENZAKE NI WAISLAM Lakini mtiririko wa PESA ZA EPA ULIWALENGA WATU FLANI FLANI ESPECIALLY WACHAGGA NA WAKRISTO...Na sasa hoja ya ccm ni uchagga na ukristo vs uislam na si migodi na mali nyingine!

Iddi Simba sio mwenyekiti wa wazazi Tanzania, na sio mchagga kama rais Mkapa sio Mchagga ila mke wake ni mchagga ndio aliemuharibu MKAPA na kujiingiza kwenye huu uhuni na wezi.

fuatilia labda Idd Simba ana mke mchagga.
inajulika kuwa wakili MALEGESA alitumiwa na mama MKAPA kwenye EPA,Subiri Report sijakataa wala kukubali kama Simba ni Epa ILA MAREGEZA line ya mama MKAPA.
 
Unazungumza kwa hekima lakini ni hekima iliyopotoka... kwenye hao uliowataja unashindwa kusema wote ni wachagga kwa sababu unajua si wote ni wachagga. Tukiwabana kuhusu makabila yao mnahama na kusema mikoa, tukisema si wote wanatoka mikoa hiyo mnasema mtu kaolewa huko so by extension ni mtu wa kilimanjaro na by extension ni mchagga!!

Lakini hata kwa jitihada hiyo kweli mnaweza kusema watu sita wanaweza kukifanya chama kizima kiwe cha kikabila?

yupo Suzan Lyimo nae ni mchagga, watu sita na kule kwenye kamati kuu unakutana na MTEI na Ndesapesa hao ndio wenye kauli ya chama, fukuza WANGWE kweli anaondoka.
 
First Lady...Nilikuwa nikirekebisha kuhusu EPA ilivyoanzishwa makusudi kuchafua baada ya migodi na mali nyingine za mabilioni ya dola za kimarekani kuuzwa na kumilikiwa isivyo halali.

Na nikasema kuwa ni mpango maalum wa ccm KWANI IDDI SIMBA NA WENZAKE NI WAISLAM Lakini mtiririko wa PESA ZA EPA ULIWALENGA WATU FLANI FLANI ESPECIALLY WACHAGGA NA WAKRISTO...Na sasa hoja ya ccm ni uchagga na ukristo vs uislam na si migodi na mali nyingine!

Iddi Simba sio mwenyekiti wa wazazi Tanzania, na sio mchagga kama rais Mkapa sio Mchagga ila mke wake ni mchagga ndio aliemuharibu MKAPA na kujiingiza kwenye huu uhuni na wezi.

fuatilia labda Idd Simba ana mke mchagga.
inajulika kuwa wakili MALEGESA alitumiwa na mama MKAPA kwenye EPA,Subiri Report sijakataa wala kukubali kama Simba ni Epa ILA MAREGEZA line ya mama MKAPA.

Wangwe sikiliza..Ukisema Mama Anna Mkapa ndiye aliyemsababisha Mkapa akauza nchi umekosea na umewakosea wachagga na wewe umetumwa na mafisadi!

Yeye Mkapa kama CHINGA...KAOA MCHAGGA...NANI KASEMA WACHAGGA WOTE AMA CHINGA WOTE NI MAFISADI?

WASUKUMA WOTE NI MAFISADI KWASABABU YA CHENGE?

KWANINI KAMA KWELI UNA MASLAHI YA TAIFA USIANZE NA RIPOTI HIZO ILI SASA TUJUWE KAMA HAO MAFISADI NI MAKABILA GANI NA DINI GANI?

KWANI HUONI KUWA KWASABABU NI KWELI ccm INA UDINI..SASA MULIWAGAWIA wakristo wengine na wachagga wengine?

Unamjua Aggrey Marealle? Ama unamjuwa NJAKE? Mimi nakwambia pesa hizo zilitoka kwa waislam wa ccm na si mama Anna Mkapa!

Yeye piya kama ametuhumiwa basi hana tofauti na atakavyotuhumiwa mtu wa Mtwara!

Ama hata MMASAI LOWASSA!

AMA MZARAMO KIKWETE? OR..OK MUISLAM KIKWETE? NA MKRISTO MKAPA?

UFISADI HAUNA DINI WALA KABILA...SHERIA NDIO KIBOKO YAKE!

SASA MWANASHERIA GANI WEWE?

NB:IDDI SIMBA ALIKUWA KAMA MWENYEKITI WA ccm WAZAZI WAKATI WAKITOA PESA ZA EPA WAO NA MALEGESI NA LUKAZA.
 
Katafute makala hii niliyosema kuwa "Kikwete Mdini kwa kuwapeleka mahujaji Makkah kwa ndege za serikali". Sijawahi kusema hivyo.

Niko upande wa reason. Soma post ya kwanza utaelewa ninasema nini.

Hakutoa siri yoyote ya mteja acha kupotosha watu. As a matter of fact in the interests of full disclosure (kama unaelewa hiyo concept) alitakiwa kusema alichosema.

Nani alikuambia KLH News ni taasisi? Na hii Marekani ndugu yangu siyo nchi ya Kikomunisti kuna mambo yanawezekana hapa ambako kwingine hayawezekani.

Hiki ndicho kichekesho cha mwaka. Kwanza hakuna siri ya mteja iliyotolewa. Pili wakienda mahakamani wana namba yangu wanipigie tu 1 248 556 6748 na waniulize mimi ni nani Bin Nani.. So waende tu mahakamani. Hivi kweli unafikiri watu wote ninaozungumza nao kwa kutumia "mwanakijiji" hawanijui mimi ni nani? duh! unaiunderestimate serikali yako sana. Wakitaka kuandika wasifu wangu wanaweza kuandika kuanzia wapi nilizaliwa hadi ninapofanya kazi sasa. Wanaheshimu ninachofanya ndiio maana wako tayari kuzungumza nami na kupokea simu zangu siyo Wangwe na Lissu tu hadi Rais Kikwete mwenyewe. Tofauti yetu siyo uadui. Haya ni mambo ya kisiasa, kama wewe unataka kufanya iwe personal utapotea kweli.

Marekani sio nchi ya kijamaa lakini sheria zinafuatwa, jana kulikuwa na kesi mahakamani kati ya kampuni ya GOOGLE na YOU TUBE imefanyika marekani fuatilia kesi hiyo.

Siamini kama Rais Kikwete amewahi kuongea na KLH NEWS ukinipa ushahidi wa jambo hilo nitakuwa Chadema na kadi nitalipia ada ya miaka kumi,naomba uthibitisho wa hilo la Interview ya JK na Klh News?
 
Mgagagigikoko.. soma mtu anachoandika kabla ya kuanza kudai "uthibitisho". duh..! wengine tunapima kila neno tunalotumia.
 
Ndugu zangu samahani kidogo naomba kuelimishwa kitu kimoja kabla ya kuchangia kiundani maada hii. Wajumbe wa kamati kuu ya CCM wanapatikanaje?. ( Wajumbe hao wanachaguliwa na Raisi ama wanapigiwa kura na wananchi?).

Asanteni
 
Wabunge wa Kamati Kuu wanachaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya CCM. Hata hivyo kufuatia mabadiliko ya mwisho ya Katiba hiyo kuna wanaoingia kutokana na nafasi walizowahi kuwa nazo na hao hawapigiwi kura. Ukiondoa wale wanaoiongia kutokana na nafasi zao (au walizowahi kushika) wajumbe wengine hupigiwa kura kwenye mkutano mkuu wa CCM.
 
Asante sana kwa kunijibu.

Sasa hapa suala la udini linaingiaje?. Ukiangalia kwa haraka haraka utaona watu kama Kawawa, Salmini na Mwinyi wanaingia kutokana na nafasi zao walizowahi kuwa nazo. Na nafasi hizo walikuwa nazo toka enzi za Nyerere.

Na hao wanaopigiwa kura kwenye mkutano mkuu utaona wazi kwamba wanapigiwa kura na wajumbe wote wa mkutano mkuu, na wajumbe hao ni wakristo, waislamu, wahindi na wapagani. Suala la udini linaingiaje hapa?.
Kama kuna mtu (mkristo) aligombea nafasi hiyo na katika alienguliwa tokana na imani ya dini yake basi ajitokeze hapa ama kama kuna mtu hapa JF anajua kuna mtu alifanyiwa hivyo basi atuletee ushaidi hapa JF.

Hili suala si dogo kama mnavyodhani baadhi yetu hapa JF. Ni suala zito ambalo linaweza kabisa kuleta mgawanyiko ndani na nje ya Chama na pia kwa Watanzania wote. Ubaguzi wa kidini ni mbaya kuliko ubaguzi wa namna nyingine yoyote ile, hivyo kama hakuna ushaidi katika hili ningeomba wana JF tuache kabisa kuzungumzia maada chochezi kama hizi.
 
Kidatu nakubaliana na wewe kwa asilimia 100 Tatizo ni kuwa nilichoelezea mimi siyo udini unavyouelewa wewe. Angalia maana ya Udini nilivyoiweka hapa. Haihusiani na imani ya mtu. Ukisoma tafsiri yangu ya udini na ukabila utaona kuwa hazihusiani actually na kabila la mtu au imani ya mtu.

I'm still trying to make a point.
 
Marekani sio nchi ya kijamaa lakini sheria zinafuatwa, jana kulikuwa na kesi mahakamani kati ya kampuni ya GOOGLE na YOU TUBE imefanyika marekani fuatilia kesi hiyo.

Siamini kama Rais Kikwete amewahi kuongea na KLH NEWS ukinipa ushahidi wa jambo hilo nitakuwa Chadema na kadi nitalipia ada ya miaka kumi,naomba uthibitisho wa hilo la Interview ya JK na Klh News?

Mgagagigikoko,

Google itakuwa vipi na kesi na You tube wakati Google iliwanunua You tube 2006?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom