Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Tatizo ni Zenji Factor. Nadhani Zenji wanachangia 50% ya members wanaoingia kwenye CC. Hapo sijaweka wale ambao wanaingia huko kwa heshima ama kwa nyadhifa zao (viongozi wakuu wa Chama wa pande zote mbili, marais wastaafu na wazee wa chama kama akina Kawawa).

Ukishaweka hiyo Zenji factor automatically lazima utaishia kwenye conclusion ya Mwanakijiji.

Labda swali la kujiuliza ni kwanini Zenji inapewa nafasi sawa na Bara?

Kwa kweli kwa MAONI yangu hili ndilo JIBU linalojitosheleza sana kwenye MADA hii na MSINGI wake ni KATIBA yenyewe ya CCM. Na CC ya CCM imekuwa hivi nadhani tangu 1977 pale TANU yetu na ASP yao vilipoungana. Bara (Kwa maana ya TANGANYIKA) tuli- sacrifice mambo mengi sana kwa ajili ya MUUNGANO wetu. Si unajua hata TANGANYIKA haipo ingawa ZANZIBAR ipo?
 

Kwani mada yako hapa sio udini?:




Na ukiongolea udini Tanzania, huongelei Ukristo na Uislamu?

Mwnkjj, utajutia hii thread, I tell you!

Ofcoz mada sio udini. Mada yake ni UKABILA, na inamuhusu Mbowe na Wangwe. Soma katikati ya mistari ndugu. Ndio maana kule sehumu ya hoja ya SAM nilikwambia unamwelewa mtu kimaandishi...................
 
hivi dini ya mtu inakuja kwa jina lake?
na wale wanaoitwa diria au abdulrahman babu na ikisha wakawa wanasema kuwa hawaaamini mungu, tuwaite waislam kwa sababu majina yao yanaasili ya kiarabu?
jee wale watu wenye asili ya majina ya kiukoo ambao yaliundwa wakati bado watu hawakuwa na dini hizi zilizoletwa na wakoloni, tuwahesabu hawana dini japokuwa wanafuata dini fulani?

mwanakijiji hoja yako ni potofu kabisa, na imekosa uchambuzi.

tunaweza kukubali kuwa kuna baadhi ya watu wanaajiri wengine kutokana na dini zao, lakini kwa kutizama majina ya watu, hujasema bado chama fulani ni cha dini fulani.
 
Wakati mnaendelea na mjadala, wajumbe wenyewe ndo hawa hapa:

1. Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete - Mwenyekiti
2. Ndugu Pius Msekwa - Makamu Mwenyekiti (Bara)
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)
4. Ndugu Yussuf R. Makamba - Katibu Mkuu
5. Capt. (mst) George Huruma Mkuchika - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe
8. Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe
11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe
12. Mzee Rashid Mfaume Kawawa - Mjumbe
13. Dr. Salmin Amour - Mjumbe
14. Ndugu John Samwel Malecela - Mjumbe
15. Capt. (mst) John Zefania Chiligati - Mjumbe
16. Ndugu Amos Gabriel Makala - Mjumbe
17. Ndugu Bernard Kamilius Membe - Mjumbe
18. Ndugu Kidawa Hamid Saleh - Mjumbe
19. Ndugu Samwel John Sitta - Mjumbe
20. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe
21. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
22. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe
23. Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe
24. Ndugu Pindi Hazara Chana - Mjumbe
25. Ndugu Andrew Chenge - Mjumbe
26. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe
27. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe
28. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe
29. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe
30. Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe
31. Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe
32. Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe
33. Ndugu Fatuma Said Ali Mchumo - Mjumbe
34. Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe
35. Ndugu Omar Yussuf Mzee - Mjumbe
36. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
37. Ndugu Ali Ameir Mohamed - Mjumbe
38. Ndugu Yussuf Moh’d Yussuf - Mjumbe


Tatizo langu ni pale watu wa dini moja wanapokuwa wengi. Mfano hawa jamaa wakiamua kutumia principle ya tabi' yeh which is actually their concoction of an Islamic principle that permits them to lie whenever it's in their interest. OOOh hatutawalaumu tena wakija na uwongo wao sasa
 
1. Katiba ya CCM inatoa nafasi ya upendeleo kwa wa Zenj kujazwa zaidi ya wabara ilhali wabara ndio wengi. Katiba ya Chadema haitoi nafasi kwa wachaga kujazwa kwenye nafasi mbalimbali kuliko makabila mengine.

2. Zanzibar kutokana na point hiyo hapo juu; wengi wao ni waislamu. Kwahiyo ukiwapa nafasi ya upendeleo utakuta wengi ni waislamu. Hii ni tofauti Chadema ambao ukiwapa nafasi ya kuteuwa wabunge huteua wanaohusiana au wachaga.

3. Sio CCM tu inailea Zanzibar bali hata serikali yetu ya Muungano inailea Zenj. Swali, kwanini tusiwe na serikali ya TATU?, kwanini kamkoa kamoja kadogo kuliko hata Wilaya ya Ilala in terms of population ina representatives kibao?, Bungeni, Chama chetu na tena wana ka baraza la wawakilishi linalowakilisha mikoa miwili tu?. Think of this.

Ni sahihi wewe ku side na akina Mbowe, lakini sio sahihi wewe ku spin mambo.

Naomba nionyeshe hapa chini Zanzibar wanapendelewa vipi zaidi ya vile viti 2 vya Wanawake:

Ibara ya 109(1)
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itakuwa na wajumbe wafuatao:-


(a) Mwenyekiti wa CCM.
(b) Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayetokana na CCM.
(c) Makamu wawili wa Mwenyekiti wa CCM.
(d) Rais wa Zanzibar anayetokana na CCM.
(e) Katibu Mkuu wa CCM.
(f) Manaibu Katibu Mkuu wa CCM.
(g) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizasheni.
(h) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi.
(i) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
(j) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha.
(k) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano anayetokan a na CCM, na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar anayetokana na CCM.
(l) Wajumbe wengine wasiozidi kumi na wanne waliochaguliwa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa wakiwemo wanawake wasiopungua wanne, wawili kutoka Tanzania Bara na wawili kutoka Tanzania Zanzibar.
 
mwanakijiji, nafikiri uliulizwa suala, iwapo mbwa atakung'ata na wewe utachuchumaa umng'ate?

ikiwa ccm wanachukua vigezo ovyo kusema kuwa cuf ni chama cha udini na chadema ni chama cha kikabila, ukumbi huu haupaswi kujishusha kama wao.

asante
 
Ofcoz mada sio udini. Mada yake ni UKABILA, na inamuhusu Mbowe na Wangwe. Soma katikati ya mistari ndugu. Ndio maana kule sehumu ya hoja ya SAM nilikwambia unamwelewa mtu kimaandishi...................

Mada sio udini vipi wakati ametumia analogy ya uwezekano wa udini ndani ya CCM ili aje kujenga hoja kuhusiana na ishu za ukabila ndani ya CHADEMA?

Mwisho wa siku anataka kurudi kwenye ishu ya ukabila lakini hapa ni analysis ya kuwepo au kutokuwepo na udini CCM. Sasa utasemaje mada sio udini hapa?
 
Kumbe 'mkuki kwa nguruwe'. Hwa jamaa waCCM wameguswa tu na la udini wanalalamika sana! Nadhani hii hoja imekuwa mtego hata wasio wanaCCM wameingia bila kujijua kulaani hoja! Mimi nadhani Mkjj ametumia mfano mzuri sana kuweka point ya Chadema na ukabila. Kwa kadri hoja ya udini ilivyodhaifu ndivyo hivyohivyo hoja ya ukabila ilivyodhaifu. Haya mambo yakiachiwa yote mawili ni hatari kw akiwango kilekile. Lakini cha msingi hakuna mifano hai ya maamuzi ya CCM yenye sura ya udini, vivyohivyo hakuna mifano hai ya maamuzi ya chadema ya kikabila.

Itafika mahali tutasema DSM wabunge wote lazima wawe wazaramo na waislam!!
 
Mgaya.

Utafiti wako ni finyu nakupa msaada labda upeo wako unaweza kutanuka.
1-Michael Tyson-muislam jina lake limekaa vipi?
2-Freddy Kanute mchezaji wa kimataifa ni muislam jina lake la kiislam?
3-Frank Riberry mchezaji wa Timu ya Taifa ya Ufaransa ni muislam jina lake linaweza kukusaidia kusema yuko dini gani?
4-Bondia Danny Williams ni muislam jina lake linakaa kidini gani?
5-Nicholas Anelka mchezaji wa Chelsea ni muislam jina lake linaelekea kuwa la kiislam?
6-Waziri Sophia Simba jina lake linaoekana kama muislam lakini ni mkristu,
7-DR.Batilda burian jina lake limekaa kidini ipi?

8-Ramadhan Mtoro Ongora ni mkristu muda wote kwa utafiti wako ungesema ni mtoto wa sheikh wa msikiti wa Mtoro,

9-Stephen Nemes masajage kipa wa Yanga na Taifa Stars ni muislam kwa jina utamjua?
10-Tariq Aziz aliyekuwa waziri wa karibu sana na Sadam Hussein ni mkristu wa kuzaliwa,kwa jina lake bila kuwa na utafiti utasema ni muslam(a) utasema ni mwarabu lazima awe muslam(b) jina lake utasema ni la kiislam kwa mujibu wa ubishi wako usio na hoja.

Umsimsahau Malcom X alikuwa kiongozi wa kiislam kwa jina utasemaje? nimekupa sample kidogo kama nisingekutajia watu hao dini gani katika hao 11 niliwataja ungeweza labda wawili tu.


Wewe unasound kama mdini vile? Ulipata wapi muda wa kuwajua hawa kwa dini zao na sio umaarufu wao!!!!!!!!!!
 
...Kwa kadri hoja ya udini ilivyodhaifu ndivyo hivyohivyo hoja ya ukabila ilivyodhaifu.

...Lakini cha msingi hakuna mifano hai ya maamuzi ya CCM yenye sura ya udini, vivyohivyo hakuna mifano hai ya maamuzi ya chadema ya kikabila.

Sio kweli.

Amelinganisha vitu tofauti. Udini CCM ni kweli hakuna lakini mazingira ya Uchaguzi wa wajumbe wa Kamati Kuu ni tofauti na wa CHADEMA. Wa CCM wako pre-determined. Katiba inasema kamati itakuwa na wajumbe wafuatao: Rais ya Jamhuri kutoka CCM. Huyo Rais hata akiwa ni m-Budha atakuwa mjumbe.

Uchaguzi wa Wabunge wa CHADEMA ni handpicked. Mwanakijiji ametengeneza a false comparison.
 
presentation yake haikuwa kama ni mfano, ilikuwa kama ni hoja iliyojitegemea. kwa maana hiyo watu wana haki ya kujadili 'ccm ni chama cha udini' au la.

kama angetaka watu wajadili hoja ya chadema, angepangilia mistari yake uzuri ili watu wachangie huko.

kuibua hoja za kibaguzi za aina yote, hata kama ni kwa ajili ya kuitega ccm, sio njia sahihi
 
Mada sio udini vipi wakati ametumia analogy ya uwezekano wa udini ndani ya CCM ili aje kujenga hoja kuhusiana na ishu za ukabila ndani ya CHADEMA?

Mwisho wa siku anataka kurudi kwenye ishu ya ukabila lakini hapa ni analysis ya kuwepo au kutokuwepo na udini CCM. Sasa utasemaje mada sio udini hapa?

Katika kusoma maandishi wa MKJJ nilihisi issue ni udini, baadae nikajaribu kuangalia ana-support nini katika michango ya watu(Thanks zake ziko katika mtazamo gani baada ya mada yake) . Nilichogundua ni kuwa second mind yake haikuwa katika dini kama KUHANI alivyoeleza hapo juu, MKJJ jaribu kurudi na kutuelimisha watu juu ya kile kilicho ktk akili yako.

Matazamo wangu: MKJJ anajaribu kutufanya kufikiri juu ya yale yaliojili katika CHADEMA na yaliopo katika vyama vingine. Ukiangalia kwa undani unaweza kwenda mbele zaidi na kusema mbona chama fulani kimejaa watu waliomaliza chuo fulani mwaka fulani, je, hili nalo tutaita uchuo au u-mwaka? Hvy nalazimika kuamini kuwa mtazamo wake ni zaidi ya kile kilichoandikwa.
 
Je kuna sababu yoyote ya msingi ya kwanini watu 25 kati ya 38 wawe ni wa dini moja? Je imeshindindikana kwa CCM kutafuta njia ya kuweza kugawa nafasi hizi kwa kuangalia uwiano wa dini?
[/QUOTE]

Ikumbukwe kwamba idadi ya wajumbe wa kutoka Zanzibar na Bara ni sawa!Kutokana na kwamba abaout 99% ya Zanzibar ni waislam!mimi sioni kama ni ajabu kuwa na waislam wengi kwenye kamati kuu!Maana wajumbe wote kutoka Zanzibar ni waislam!
Haitawezekana because of Zanzibar in nature ni waislam!Refer to the history!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Burundi, Comoro na Kenya
zamshukuru Rais Kikwete

Na Mwandishi Maalum,


NCHI tatu za Afrika zimetoa shukurani rasmi kwa Tanzania, na hasa kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kwa mchango wake mkubwa katika kutatua migogoro ya kisiasa katika nchi hizo.

Shukurani hizo zilitolewa na nchi za Burundi, Comoro na Kenya wakati wa Kikao cha 11 cha Wakuu wa Nchi za Afrika kilichofanyika mwanzoni mwa wiki hii katika eneo la kitalii la Sharm El Sheikh, Sinai, Misri.

Nchi zote tatu zilieleza kuwa bila Tanzania na hasa bila kujihusisha moja kwa moja kwa Rais Kikwete katika migogoro ya nchi hiyo, ingezichukua nchi hizo muda mrefu zaidi kwa migogoro hiyo kuweza kutatuliwa.

Shukurani za nchi hizo zilitolewa wakati wakuu wa nchi za Afrika walipokuwa wanajadili hoja ya kuanzishwa kwa serikali ya Umoja wa Afrika, moja ya ajenda kuu za kikao hicho cha siku mbili kilichofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha International Congress Center cha Hoteli ya Maritim Peninsula kuanzia Jumatatu, Juni 30, 2008, mwaka huu.

Makamu wa Rais wa Burundi, Yves Sahinguvu aliuambia mkutano huo: “Sisi wa Burundi, tunamshukuru sana Rais Kikwete kwa juhudi zake za miaka mingi kuweza kusuluhisha mgogoro katika Burundi ambao umefikia mwisho wake kwa kuhakikisha kuwa viongozi wa chama cha FNL-PALIPHEHUTU wanarejea nyumbani karibuni.”

“Tanzania, na hasa Rais Kikwete, tokea alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje, imehangaika na mgogoro wa Burundi kuliko nchi nyingine yoyote. Tunawashukuru sana Watanzania kwa mchango wao wa kindugu sana,” alisema Makamu huyo wa Rais.

Rais Kikwete ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho, alimjibu Makamu huyo wa Rais wa Burundi, “Hakuna shaka kuwa nchi zote katika eneo letu la Afrika zimechangia katika kusuluhisha mgogoro wa Burundi, lakini tunapokea shukurani hizo kwa “mchango wetu mdogo na wa unyenyekevu” tuliotoa katika Burundi. Tanzania ilijihusisha na mgogoro wa Burundi kwa kiasi cha miaka 14.

Naye Rais Sambi wa Comoro alitoa shukurani kwa jumuia ya kimataifa, na hasa kwa Rais Kikwete na viongozi wa Sudan na Libya kwa kuweza kusaidia kutatua mgogoro wa kisiasa visiwani humo uliosababishwa na uasi wa Kanali Mohammed Bakari katika Kisiwa cha Anjouan.

“Natoa shukurani za pekee kabisa kwa Mheshimiwa Rais Kikwete wa Tanzania, Rais wa Sudan, Omar El Bashir na kiongozi wa Libya, Brother-Leader kwa kuliwezesha tatizo la Anjouan kufikia mwisho. Bila damu yao, tungekuwa bado tunakabiliwa na uasi, na kwa kweli natoa heshima kubwa kwa umoja wa bara letu, AU, kwa kupitisha uamuzi uliowawezesha viongozi hao watatu kumaliza tatizo la Anjouan.”

Naye Naibu Waziri Mkuu wa Kenya, Uhuru Kenyatta alitoa shukurani kwa Rais Kikwete, katibu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Dk, Kofi Annan; Rais Museveni wa Uganda, Umoja wa Afrika (AU) na Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kuchangia katika usuluhishi wa mgogoro wa Kenya mwishoni mwa mwaka uliopita na mwanzoni mwa mwaka huu.

“Kama mnavyojua, mazungumzo ya usuluhishi yalianza Januari 28, mwaka huu, chini ya usimamizi wa Mheshimiwa Kofi Annan na kwa kweli tunamshukuru sana kwa uvumilivu wake katika kufanikisha mazungumzo haya.”

Aliongeza: “Lakini kwa kweli Kofi Annan angelazimika kuhangaika sana bila mchango muhimu sana wa Mwenyekiti wa AU, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania. Lakini pia lazima tuwashukuru watu wengine – Rais Museveni, aliyekuwa mwenyekiti wa EAC, na taasisi zetu za AU na EAC yenyewe, kwa kusaidia kurejesha hali ya amani na usalama katika Kenya.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

03 Julai, 2008
 

Attachments

Tutegemee nini katika hii thread? Hotuba, ratiba?
Unategemea mchango wowote toka kwa wana jf?

Tegemea chochote tutakachokipata kinachomhusu Rais wetu, kama ni hotuba, ratiba na vinginevyo.

Kama jina la thread linavyosema "Monitoring" dicho sisi tutakuwa tunakifanya hapa.
 
It is playing cheap politics kuanza ku-uquestion ujumbe wa mtu kwa msingi wa dini. I can question ujumbwe wa uanachama wa baadhi ya wajumbe kama RA, kwa sababu hayuko mle kwa maslahi ya Taifa, maslahi ya chama na wala maslahi ya watanzania. He is there for his own interest na ni kama immunity kwake kwa uovu anaofanya. Kimsingi hana maadili ya kuwa mjumbe wa CC. Tusiwe wajinga siasa za dini ni siasa za kijinga, watu waingie kwa uwezo wao, uzalendo wao, na utu wao. Tu-question uanachama wao kwa misingi hiyo na sio kwa misingi ya rangi, dini, kabila na ujinga kama huu.
Mwizi ni mwizi tu, hana dini. Segerea kuna wakristo, wapagani na waislam kibao. Si dini zao zinazowafanya wawe common kule. Ni wizi.
Issue inayolikabili taifa letu ni ufisadi. Sijui mzee wa visenti ni dini gani, sijui MZee wa Dowans ni dini gani, lakini ukiangalia unaweza kuona dini zao tofauti lakini kinachowafanya wawe wamoja ni kashfa za ufisadi.
 
Matazamo wangu: MKJJ anajaribu kutufanya kufikiri juu ya yale yaliojili katika CHADEMA na yaliopo katika vyama vingine. Ukiangalia kwa undani unaweza kwenda mbele zaidi na kusema mbona chama fulani kimejaa watu waliomaliza chuo fulani mwaka fulani, je, hili nalo tutaita uchuo au u-mwaka? Hvy nalazimika kuamini kuwa mtazamo wake ni zaidi ya kile kilichoandikwa.

Ni kweli mwisho wa siku hoja yake ya msingi ni swala la ukabila ndani ya CHADEMA. Lakini hapa anataka tu analyze swali moja tu: je kuna udini ndani ya CCM?

Tukishajibu hilo swali ndio atalitumia hilo jibu kurudi kwenye mada ya Ukabila/kutokuwa na Ukabila CHADEMA. Kwa hiyo hapa ishu ni udini au kutokuwepo na udini ndani ya CCM. Hilo ndilo swali la thread. FairPlayer ananiambia ni read between the lines kuona kwamba ishu sio Udini hapa. Yes and No. Yes ni udini, ndilo swali la thread. Ndio analysis ya thread. No kwa maana kwamba mwisho wa siku utarudishwa kwenye hoja ya CHADEMA, kutoka na jibu lako la je, kuna udini CCM?

Tatizo ni kwamba analogy anayotumia kati ya uchaguzi wa wajumbe wa Kamati Kuu na Wabunge wa CHADEMA ni distorted.
 
Sio kweli.

Amelinganisha vitu tofauti. Udini CCM ni kweli hakuna lakini mazingira ya Uchaguzi wa wajumbe wa Kamati Kuu ni tofauti na wa CHADEMA. Wa CCM wako pre-determined. Katiba inasema kamati itakuwa na wajumbe wafuatao: Rais ya Jamhuri kutoka CCM. Huyo Rais hata akiwa ni m-Budha atakuwa mjumbe.

Uchaguzi wa Wabunge wa CHADEMA ni handpicked. Mwanakijiji ametengeneza a false comparison.

Nisingependa kujitumbukiza kwenye mjadala wa uislam na ukristo. Mimi hii mada sijaitafsiri kwa dini hizo.

Pamoja na nafasi za CCM kuwa predetermined inawezekana watu (wa dini fulani) waka predetermine namna ya kupata hizo nafasi. Suala la Zanzibar kupendelewa, mimi nadhani halina mjadala. Zanzibar ina population ndogo sana (about a million) hapo kama watoto (chini ya 18%) ni zaidi ya asilimia 60% basi una watu wazima wasiozidi laki nne na kama hapo kuna wazee na wapemba wanaobaguliwa, wazee na akina mama wasioactive sana katika siasa (usinielewe vibaya) utajua Zanzibar wanapata share kubwa mno. Hao wastaafu (eg. marais wa Zanzibar) ni wajumbe. Idadi itazidi kukuwa Karume akistaafu! Nadhani ni wazi Zanzibar wakati mwingine imetumia hii number kuinfluence mambo. Kwa mfano Butiama (pamoja na kwamba ile ilikuwa sanasana ni NEC)!

Sipendi kuingia sana kwenye dini kwa sababu naamini Mkjj aliitoa hii hoja kwa ajili tu wa ku make a point (ndivyo nilivyomuelewa). Hata Chadema nadhani hawana kigezo cha upendeleo wa kikabila katika taratibu zao. Sanasana naona hii ya CCM inaweza (probabilistically) siku moja ikaresult kuwa na wajumbe wa dini moja au kabila moja! Lakini hivi vyama at the end of the day ni flexible, hizi taratibu zinaweza kubadilishwa kuaddress unlikely events kama hizo!

Logically pia sioni kwa nini Chadema kiwe cha kikabila pamoja na kuwa na watu wengi toka makabila mengi kuwa viongozi na watu wenye calibre ya juu tu. Kwa nini walee ukabila, logic haipo.
 
Jinsi ya kupata jibu hili ni rahisi. swali la msingi linapaswa liwe je members wa kamati kuu ya CCM wanapatikana vipi?
Mchakato unaowawezesha wanachama kupata uanachama wa kamati kuu umeelezewa vizuri kwenye katiba na hakuna influence ya yeyote kupinga wale walioshinda kwa kura nyingi. That way sioni kama kuna udini katika uundwaji wa kamati kuu.
In general ninaweza kusema kuwa institutionally hakuna udini katika CCM, ila ndani ya mioyo ya wanachama na viongozi mmojammoja SIJUI.
 
Wana-JF tujaribu kuwa tunajikita kwenye HOJA/MADA iliyotolewa badala kuziunganisha hoja/mada hizi ambazo mara nyingi huwa zimetolewa na WATU tofauti na zina MAUDHUI tofauti kabisa. Kwa nini tunairudisha mada hii kule CHADEMA na kujaribu kufikiri anachofikiri MTOA mada?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom