Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Kamati Kuu ya CCM imejaa Udini?

--------------------------------------------------------------------------------

Nadhani mzee, huko kijijini njaa imezidi, ulikuwa wapi hukuuliza swali hili kwa zaidi ya miaka 10 Mkapa akiwa M/kiti Rais Sumai Mjumbe na W/mkuu magúla katibu.
kama utafanya uchunguzi utaona kwamba siku zote swala la UDINI linaibuka tuu pale, jamaa wa dini fulani wakionekana kwamba wamekua zaidi ya vile - watu wenye mawazo kama yako - wanavyotaka iwe!
Kuna kamati kadhaa ambazo zina watu wadini mmoja tu na kuna post kadhaa ambazo (km Makatibu wakuu na wakurugenzi ktk wizara) - hali kwa tafsiri ya msimamo wako zisinge kuwa na waliomo kwa sasa. hali kama hii ikijitokeza jibu la watu kama wewe huwa: "hii inatokana na 'merites"'
Kula la kheri kaka
Kiganj
Kaka KubwaJinga = you have made my Day Thanks soooo much. (smile) 'waarabu wa pemba.....'
 
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA


Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuondoka nchini leo (tarehe 05 Julai, 2008) kwenda Hokkaido, Japan kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa nchi tajiri zenye viwanda duniani (G8) utakaofanyika tarehe 7-8 Julai, 2008

Katika mkutano huo, Rais Kikwete ataongoza Viongozi Wakuu wa Nchi za Bara la Afrika ambazo ni Algeria, Afrika Kusini, Ethiopia, Ghana, Misri, Nigeria na Senegal.

Masuala makuu yanayotarajiwa kujadiliwa katika kikao hicho yatahusu Maendeleo ya Afrika, Utekelezaji wa Malengo ya Milenia na changamoto kadhaa zinazoikabili dunia ambazo ni kupanda kwa bei ya vyakula, kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Rais Kikwete anatarajiwa kuongoza hoja juu ya maendeleo ya Afrika ambapo viongozi watatoa wito kwa nchi hizo tajiri kutekeleza wajibu wao wa kulisaidia Bara la Afrika ili liweze kupiga hatua za maendeleo.

Akiwa nchini Japan, Rais Kikwete atafanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini humo ambapo atafanya mazungumzo na viongozi wa serikali ya Japan na wawekezaji wenye nia ya kuja kuwekeza nchini Tanzania

Rais anatarajiwa kurejea nchini Tarehe 11 Julai, 2008.

Imetolewa na
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

05 Julai, 2008
 

Attachments

Great Analysis, musipomshitukia Mzee Mwanakijiji atatupeleka pabaya!!! Namshauri kuwa makini sana wakati anabonyeza key board yake pale anapoandika kitu chochote kinachohusiana na imani.

Namkumbusha kwamba Tanzania hatutaweza gawanyika kwa ukabilia... lakini we are equally very vulnerable with UDINIs...

Please mwanakijiji... naomba uwe makini sana!!! ushabiki wa Wangwe na Mbowe... usitumike kwenda CCM na kuiligawa taifa kwa udini...

Kasheshe... wewe ni miongoni mwa watu wanaangalia mambo hapa kwa umakini sana. Bahati mbaya katika hili na wewe una react from an emotional point of view. Soma definition yangu ya Ukabila na Udini kwanza ndio utaelewa ni point gani ninayojaribu kuitoa.
 
Mgagagigikoko,

Google itakuwa vipi na kesi na You tube wakati Google iliwanunua You tube 2006?

Kesi inahusu Kampuni ya You tube na Google upande mmoja na kampuni ya VIACOM kwa upande mwingine inayomiliki MTV na NICKELODEN.

Kesi hii ya fidia ya dola billion moja,
naijua vizuri YOU TUBE ilianzishwa California Mwaka 2005 ikanunuliwa na Google kwa dola billion 1.65 mwaka 2006,Marekani pekee wana wateja million 72.
kesi hii ilianza mwezi machi 2007 na hukumu imetoka juzi na huyo jaji nilyemtaja juu LOUIS SANTON.

wanaosema kuwa Marekani sio wakomunisti na kila kitu kinawezekana sio kweli.
2006 the US Department of justice waliwaamuru Google kutoa information za mamillioni ya web searches.ikiwa ni part ya wide-ranging investigation into illegal activity on line.
 
Athari za bei kubwa za mafuta na chakula duniani ni kubwa sana kwa watu wote duniani lakini ni kubwa zaidi kwa nchi maskini na zinazoendelea (nyingi zikiwa Barani Afrika). Hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kutokana na kupanda sana kwa gharama za maisha. Uwezo wa Serikali zetu kuwahudumia wananchi wake unazidi kuathirika. Matatizo hayo ukichanganya na lile la kutetereka kwa mfumo wa fedha wa dunia lililoanzia Marekani na kuenea Ulaya yanatishia kudhoofisha kasi ya kukua kwa uchumi wa dunia nzima.
Mbona hakutaja kuwa matatizo mengine ya waafrika yanatokana na ufisadi?. Haya aliyoyataja ni yale yale ambayo kila siku wote wanayatumia kuwadanganya watu huku wakiwaibia kila siku. Ahhhh Waafrika tusivyo na huruma? Mungu atusaidie kutupa moyo wa huruma. Maana huruma yetu inajitokeza yanapotokea majanga lakini kwa kutuibia hakuna anayeona huruma.
 
Megapayne...this Is A Megga Move!
I Endorse The Idea!
 
Mwkjj,
Hapa watu wameanza jaziba zao badala ya kuzungumzia hoja iliyo mbele yao. Na hili ndilo linanifanya niwashangae hawa ndugu zetu waislamu. Wao ukishaongea jambo ambalo kuna maslahi yao hapo ndipo utaonekana umefilisika kifikra na kejeli nyingi nyingi tu.
Sikilizeni wana jf hapa kuna hoja ijibiwe kistaarabu na si kuipindisha na kuleta mambo mengine yasiyo katika hoja hii.
Kama kuna watu ambao wamekuwa mstari wa mbele kupigia kelele za domination ya ukristo katika siasa na serikali ya Tanzania ni waislamu. Kila leo wamekuwa wakija na hoja hii na ile ili kuonyesha kuwa uislamu unakandamizwa katika Tanzania. Na kwa kweli imefika mahali wamewaweka viongozi wa nchi hii katika mtego mkubwa sana na uangalifu kila wanapogawa posts mbali mbali katika nchi hii ili angalau wasionekane wako biased na dini fulani.
Na kila mara wamekuwa wakija na demands hii na ile na viongozi wetu wamekuwa katika hali ya kuona inawasaidia na wanaridhika.
Sasa hakuna shida na mkuu mwkjj akija katika mtililiko ule ule, mjibuni, badala ya kuja na majibu rahisi kwamba hii nchi haina udini au tusiujadili hapa. Kwanza ndiyo sababu hii inaitwa forum. Maana yake tujadili na si lazima wote tukubaliane lakini tunaweza kuona where the truth is.
Mwakjj. hujaishiwa kama wengine wanavyotaka kutusadikisha. Kuna point hapa.
Hata mimi nilishawahi kujiuliza swali hili hili. Sasa kama kamati kuu inachaguliwa na halmashauri kuu je huko kuna mgawanyiko upi kati ya wakristo na waislamu? mwenye data azilete hapa ili tujilidhishe. Watu wasitufanye hatuoni what is behind a curtain.
 
Sasa isn't that a grand example of upendeleo usio wa lazima. Iweje CCM Zanzibar ichangie asilimia 50 ya wajumbe wa NEC?

Kwa sababu waliunganisha vyama viwili - kimoja kutoka kila upande wa nchi inayoitwa Tanzania - sasa kama inatakiwa isiwe sawa nabidi Bara kungetoka vyama viwili au zaidi na Znz kimoja.

Hili ndilo suala llilo na mtazamo tafauti wa kila mmoja wetu kwani hata katika muungano wengi tunasahau tuliunganisha nchi mbili tafauti na kama kuna mgao basi ni nusu kwa nusu na kama ni mchango vile. Ninachotaka kusema kuwa share ni asilmia hamsini kwa kila upande kwa gharama na mapato ama pale ambapo upande mmoja hauwezi kugharamia hizo asilimia hamsini basi inaukopesha upande mmoja kiasi chochoe cha gharama na kutegemea kupata mgao wa faida kwqa asilimi ile ile iliyotoa gharama - lakini ikimbukwe kila upande una haki ya asilimia hamsini na unapopata uwezo wa kutoa mchango wa Muungano ( gharama) haki yao wapewe.

Hii najua ni ngumu kwa ndugu zetu wa upande wa pili lakini kama ni mashirikiano na nchi ndogo basi hilo ni lazima lizingatiwe kwani lilijulikana mwanzo bila hivyo - kigezo cha idadi ya watu naukubwa wa nchi havina msingi , mfano ni umoja wa Mataifa9 ambako Znz ilikuwa mwanachama kabla ya Tanganyika) kila nchi ina kiti kimoja tu bila kujali ukumbwa na idadi ya watu wa nchi hizo.

Kitu kingine cha kujiuliza ni kuwa kwa nini hii hoja inakuja sasa hivi tu na huko nyuma haikuja au kwa sababu wajumbe walikuwa wanatoka katika kundi la dini nyengine? ( mtoa mada hakuweza kupasua mojakwa moja ni dini gani - kwani mwenyewe kajua kuwa ni jambo duni kabisa kuanza kuangalia udini)

Kama nilivyombambia Mgaya; Mzee Mwanakijiji naomba usimalizie kwenye KK ya CCM tu endelea na Baraza la Mawaziri, Manaibu, Mkatibu, Wakuu n.k hadi madiwani itatoa picha nzuri.
 
Asante sana kwa kunijibu.

Sasa hapa suala la udini linaingiaje?. Ukiangalia kwa haraka haraka utaona watu kama Kawawa, Salmini na Mwinyi wanaingia kutokana na nafasi zao walizowahi kuwa nazo. Na nafasi hizo walikuwa nazo toka enzi za Nyerere.

Na hao wanaopigiwa kura kwenye mkutano mkuu utaona wazi kwamba wanapigiwa kura na wajumbe wote wa mkutano mkuu, na wajumbe hao ni wakristo, waislamu, wahindi na wapagani. Suala la udini linaingiaje hapa?.
Kama kuna mtu (mkristo) aligombea nafasi hiyo na katika alienguliwa tokana na imani ya dini yake basi ajitokeze hapa ama kama kuna mtu hapa JF anajua kuna mtu alifanyiwa hivyo basi atuletee ushaidi hapa JF.

Hili suala si dogo kama mnavyodhani baadhi yetu hapa JF. Ni suala zito ambalo linaweza kabisa kuleta mgawanyiko ndani na nje ya Chama na pia kwa Watanzania wote. Ubaguzi wa kidini ni mbaya kuliko ubaguzi wa namna nyingine yoyote ile, hivyo kama hakuna ushaidi katika hili ningeomba wana JF tuache kabisa kuzungumzia maada chochezi kama hizi.

Nakuunga mkono Mkuu kwani mimi ni mmoja wao niliosomathread chache za hii mada na ikanichoma sana hasa ukizingatia kuwa mtoa mada ni mtu ambaye wengi wetu tunaamini anaitakia mema nchi hii - lakini anapofanya analysis ya vitu vinavohusiana na ubaguzi wa kidini inatia mashaka kwani hiyo ni hatari kuliko huu ufisadi tunaoupigia kelele.
 
Naona hii ndiyo thread pekee nitakayoanza kuchangia kwani hata MEGAPAYNE MWENYEWE KANIKARIBISHA HAPA!
Ndugu zangu kuna watu wananichongea ili nifungiwe hapa kwasababu ya kitendo changu cha kupinga hoja za udini na ukabila!
Sasa nimepewa warning...Na mimi nimemwomba mod huyo anipe list ya watu ambao hawataki nichangie thread zao ili kuepuka kufungiwa...Na kwa hivyo basi...Kuna watu kama Mafuchila na Megapayne na wengineo ambao najuwa hawana noma nikichangia mijadala hii bila matusi wala kwenda personal!
Once again nashukuru MegaPAYNE kwa ukarimu wako na pia sasa ni muda wa kujiandaa na NONDOZ ili kieleweke!
Pia kama kuna yule asiyetaka nichangie kwenye thread yake naomba ani PM kabla ya kwenda kunichongea ili nifungiwe.
 
Tatizo inaonekana wengi wana react from an emotional angle and not an intellectual one. Nimewaomba tena msome hasa nilichosema kwenye post ya mwanzo badala ya kuproject mtiririko wa mada kuwa ni mawazo yangu. Haya mambo si magumu kiasi hicho.
 
Nikiwa mtu mwenye maslahi ya pekee kwenye CCM naona jambo hili si zuri na litazua manung'uniko yasiyo ya lazima. Kama kikundi, taasisi, au jumuiya fulani ina watu wenye sifa moja inayolingana, sifa ambayo inawatofautisha na watu wengine hasa ya vitu kama kabila, rangi, au dini basi mahali hapo ni pa kuangaliwa kwa karibu.

Tanzania aliyojenga JKN ilikuwa Tanzania ya kitu kimoja hakuna ukabila wala udini.......tofauti na nchi nying duniani......suala la ukabila na udini limeifanya hii dunia yetu ya sasa kuwa na migogoro isiyoisha.

Mara kwa mara suala la dini limetumika sana kama silaha kwa manufaa ya wachache...ukianzia wakoloni mpaka sasa ma neocon wanatumia udini kama silaha.

Mimi naona mwenzetu Mkjj, amekuja na hili issue na anajuwa wazi kuwa haileti maslahi yoyote kwa nchi yetu....mimi naamini kwetu kitu muhimu, ni wajibu wetu tukumbushane kuwa UTAIFA ndio mbele, haya ya ukabila au udini yasiwemo katika nyoyo zetu.

Mkjj sababu zako za kuanzisha hii thread, ndizo ukiona zimewafanya wa irish, protestant na catholic wakashindwa kuishi pamoja mpaka leo, au iraq kati ya mashia na masunni kuto kuishi pamoja.

Najua wengi mtasema ni vizuri lizungumziwe....ni sawa lakini ina faida gani?...au ndio kuanzisha chuki kati yetu?...kila mtu anajua issue za dini au ukabila inawafanya watu kuwa emotional...tusiende mbali angalieni Darfour ni udini....Kenya ni ukabila.....Soamlia ni ukabila.

Tusitoke kwenye mada muhimu, tuliyonayo ya kupigana na ufisadi uliyokithiri katika nchi yetu na kuanza kuingiza dini....hii inaogopesha sana....mkjj isiwe ndio spin ndio kitu unafanya hapa.....

Jamani udini ukabila ni ugonjwa mbaya sana nawaombeni msijiombee ugonjwa huu maanake dawa hakuna afadhali hata aids unaweza kujikinga
 
Nadhani hapa ndipo msingi mkubwa wa EPA ulipolala. Uwizi na kugushi. Bila kufumbua fumbo hili mengine yote yatabaki propaganda. Hakuna mlango wowote wala Safe iliyobomolewa, hakuna mlango uliovunjwa. iwapo Karatasi zimewekwa saini, fedha zimetoka, mathalan katika Kagoda, ni vema majibu ya kina yakapatikana. Majibu ya timu ya Mwanyika na wenzake yajiandae kwa maswali hayo muhimu, vinginevyo wajiandae kujibu kwanini wametumia fedha nyingi za watanzania ambazo zingelikuwa zinajenga shule,zahanati na barabara. Ushahidi wote wa Ernst and Young unahitaji kupatiwa majibu ya kina, siyo tu swala la kurudisha fedha, kama zinarudishwa!
 
Dr.W.Slaa Junior Member Join Date: Tue Jul 2008

1. Re: Kamati Kuu ya CCM imejaa Udini?

2. Nadhani hapa ndipo msingi mkubwa wa EPA ulipolala. Uwizi na kugushi. Bila kufumbua fumbo hili mengine yote yatabaki propaganda.

3. Hakuna mlango wowote wala Safe iliyobomolewa, hakuna mlango uliovunjwa. iwapo Karatasi zimewekwa saini, fedha zimetoka, mathalan katika Kagoda, ni vema majibu ya kina yakapatikana.

4. Majibu ya timu ya Mwanyika na wenzake yajiandae kwa maswali hayo muhimu, vinginevyo wajiandae kujibu kwanini wametumia fedha nyingi za watanzania ambazo zingelikuwa zinajenga shule,zahanati na barabara.

5. Ushahidi wote wa Ernst and Young unahitaji kupatiwa majibu ya kina, siyo tu swala la kurudisha fedha, kama zinarudishwa!

Kwakweli I need a help, kwa sababu niko confused kidogo jinsi udini unavyohusika na wizi wa EPA, please somebody help me maana I am lost!
 
ES,

You are not ALONE. Hata mimi sijaelewa. Labda alikuwa ana support maandiko hapo juu ya Mwanakijiji ..........labda.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom