Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Hivi kuna mtu anaweza kunieleza sifa alizonazo Makamba mpaka akaonekana anafaa kuwa katibu mkuu wa ccm, mbali na dini yake?
 
Hivi kuna mtu anaweza kunieleza sifa alizonazo Makamba mpaka akaonekana anafaa kuwa katibu mkuu wa ccm, mbali na dini yake?

mbali na dini yake umemaanisha nini? au tayari umeshaweka conclusion kuwa dini ya ccm ni uislam?
 
Naomba nionyeshe hapa chini Zanzibar wanapendelewa vipi zaidi ya vile viti 2 vya Wanawake:

Ibara ya 109(1)
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itakuwa na wajumbe wafuatao:-


(a) Mwenyekiti wa CCM.
(b) Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayetokana na CCM.
(c) Makamu wawili wa Mwenyekiti wa CCM.
(d) Rais wa Zanzibar anayetokana na CCM.
(e) Katibu Mkuu wa CCM.
(f) Manaibu Katibu Mkuu wa CCM.
(g) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizasheni.
(h) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi.
(i) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
(j) Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha.
(k) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano anayetokan a na CCM, na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar anayetokana na CCM.
(l) Wajumbe wengine wasiozidi kumi na wanne waliochaguliwa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa wakiwemo wanawake wasiopungua wanne, wawili kutoka Tanzania Bara na wawili kutoka Tanzania Zanzibar.

Mheshmiwa,

Angalia idadi ya wananchi/wananchama wa CCM bara na visiwani. Utagundua (kama hujagundua) kuwa Bara ni kama over 90%. Sasa hawa watu unapowapa nafasi zilizo sawa unamaanisha nini?
Mfano, katika hao watu kuna makatibu pande zote. Spika etc. Kama umesoma heasbu za uwiano kidogo utaona kuwa probability ya wazanzibar kuwemo/kuongezeka ni kubwa sana ukilinganisha na population yao. Kwa urahisi ni kuwa kama wa Zenji wapo million 2 wakawakilishwa na watu 10 na wabara wapo million 20 wakawakilishwa na watu 28 bado uwiano ahiingii akilini.

Nadhani utakuwa umeelewa sasa.
 
anayesema kuwa znz wanapendelewa kwa vile wanawanachama kidogo, kwa hiyo wasipewe nafasi zote hizo za juu anakosea.

zanzibar ina wananchi kidoogo lakini imepewa serikali nzima, kwa hiyo idadi nafikiri haijalishi, muundo wa muungano umesababisha zanzibar kupewa asilimia 50 japo inawatu kidogo mno kulinganisha na bara.

ccm bara haiwezi kupunguza nafasi ya ccm zanzibar kwa sababu wanajua wakijaribu kufanya hivyo watawatishia kuhusu muungano.

kwa maana hiyo, zanzibar itaendelea kuwa na nafasi kubwa kwenye ccm na serikali unless kuwe na serikali moja tu, na kitu kinachoitwa zanzibar kitokomee.
 
Mwanakijiji,

This is the argument I am also trying to make here whilst expanding the scope of your question. By just looking at numbers and observations, anyone can say anything about anybody at anytime.

Do we have now to hire or choose incompetent leaders to balance tribes, sex or gender, regions, religion, etc? Why should we make it so big that 30 out of 38 or 5 out of 6 are people of the same group?

Can it happen that all are competent irrespective or their tribes or religions?

Nampongeza Mwanakijiji kwa kuamsha hisia na akili zetu .Sikuwahi kufikiri kuwa tunaongozwa na kundi linaloelemea upande mmoja tu.

Then I have to think again. Hadi leo America wanauhusisha terrorism na Uislam . Very unfortunate though.

If we are getting poor every comming day, due to ufisadi , unproffesional handling of matters like Zanzibar issue, etc can we link it with our NEC profile?

Dr Slaa amefanya kazi kubwa kufichua ufisadi akiwa Chadema. Now should we link this with Chaggas? Then what is the conclusion if you put the two together? Foolish but food for thought.
 
asante tunasubiri mengi,
yanayosemwa na/au kufanywa nae.
 
Nitakubaliana na wewe kwenye udini kuwa wewe huamini kuwepo, lakini ukabila hapa umetudanganya. Hii thread yenyewe nia yake ni ku-deflate ile ya ukabila ndani ya CHADEMA, but that will never go away untill solved, it is just as simple as that.

Mkuu Chadema imekuaffect vipi na ukabila wao? Hebu tupe profile yao kama ilivyotolewa ya NEC tuone ukubwa wa hilo.

Sijui kama NEC ya CCM inakuaffect wewe. If it does then discuss hows ,and whys you getting affected. Mwkjj anathani one reason is one religious sect dominance. Upo hapo?
 

Hivi kama Zenji Karume`s ambao wamedominate politics za huko..ingekuwaje kama ingekuwa ni upinzani? Leo mtoto wa mwinyi ana ambitions za kuwa rais, mdogo wa Karume ana ambitions za kuwa rais...no body is saying what, lakini watanzania hao hao leo tunamsulubu bwana Mbowe kisa? kuna wabunge wakuteuliwa toka MOSHI Uchagani... conclusion? Mbowe na Chadema ni wakabila! Talk of double standards! (sasa kama hao waislamu wa CCM wamepata au kuteuliwa kwa merit, kwa nini tusiassume kwamba hata hao wabunge wachaga wa Chadema wameteuliwa kwa merit? au kwa vile ni wapinzani?)

Tanzania udini, ukabila upo na haupo...upo kama unamsaidia mtu kufanikisha agenda zake, haupo kama haumsaidii, kwa critics wa Chadema, ukabila upo kwa sababu unawasaidia kuonyesha kwamba CHADEMA ni chama cha wachaga hakiwajali makabila mengine..lakini hao hao critics..hata siku moja huwezi wasikia wakisema kwamba Karume ambaye alipata uraisi kwa kubebwa anaendekeza umwinyi kwani zanzibar siyo family property... (si wazenji walimkataa...na wakubwa Dodoma ndo wakampatia uraisi?) mbona hatujasikia watu wanaongea hapa? Na badala yake tunaambiwa as long as ni MERIT basi tumuache? Merit ipi kama wananchi walikukataa ukabebwa?? To me as long as mtu anapata madaraka on merit..it doesnt bother me, kinachonisumbua ni double standards. (wilaya yangu haijawahi kuwa na waziri hata siku moja hata naibu waziri..but I have never complained kwamba tunaonewa...I just assume as ndugu zetu walio huko Dodoma na Dar Es Salaama wanavyotwambia..ni MERIT! perhaps sisi wabunge wetu hawana merit...wilaya yangu..tuna bara bara ya LAMI haizidi KM 20....hatulalamiki..tunaambiwa ni mipango ya kitaifa..ukienda huko Moshi na kwingineko..hali ni tofauti..wazee watu tuko kimya ila siyo wajinga...CCM and its supporters should be the last people to accuse others on the lines of ukabila au udini!

Kwa hiyo kama ni ukabila au undugunization, ni hakika umejaa CCM kuliko chama kingine chochote..lakini kwa vile wengi wetu ndo hivyo ni wanafiki..hatupendi kulisema hilo..ukilisema unaambiwa wewe ni mkabila. Fine agreed. lakini hao hao wanaokwambia hivyo...ikija kwa mpinzani wao..wanajisahau wanaanza kuaccuse wengine kwamba ni wakabila...Watanzania wenzangu especially ruling class na mlio karibu nao..inabidi muache unafiki, mjue kwamba sasa dunia inabadilika na sisi watoto wa wakulima tumeanza kuuona mwanga..tumechoka kudanganywa na tumeuchoka unafiki wenu! Huu wimbo wa amani na umoja, tanzania hakuna udini wala ukabila...tumeuchoka we need A REAL DEAL TO BRING FOOD ON THE TABLE..siyo kuwa mnafaidika kwa migongo ya wengine....Na kibaya zaidi mnajisahau


Nadhani Mwanakijiji akiyafikiria yote hayo..ndo anajaribu kuwauliza watanzania wenzake..kama alivyowauliza kwa kutumia "akili"..Whither udini?
 
Mwanakijiji wewe ni mchokonozi sana kwa mabo ambayo umekaa nayo muda mrefu sana na nilijua utakuja nayo hapa leo tu,ila bado nasimamia pale Wangwe Doctrine...Wangwe ana Hoja na asikilizwe

Sijui ushauri wangu Viongzoi wa CHADEMA wameufuata kwa hisia au vipi?

1.Mnyika Rudi ukamalize Shule na ujiendeleze zaidi na ikiwezekana utafute kazi nyingine ya Proffesional yako ili mpate pesa za Kampeni..

Hii siyo kwako na uwaambie na wenzako mfanye hivyo,Mmshauri na Mwenyekiti wenu wa taifa Atuambie kamaa shule amemaliza au vipi?
 
Shadrack Sagati, Dodoma

HabariLeo; Ijumaa,July 04, 2008 @09:17


MKURUGENZI Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Ephraem Mrema ameumbuliwa bungeni, kuwa amepewa wadhifa huo kinyume cha taratibu.

Mbunge wa Kasulu Magharibi, Kilontsi Mporogomyi (CCM) alisema Mrema hana taaluma ya uhandisi ujenzi, huku analipwa mamilioni ya fedha za Watanzania.

Mporogomyi ndiye aliyeweka hadharani habari za Mkurugenzi huyo kuingizwa kwenye madaraka hayo kupitia mlango wa nyuma; huku wataalamu ambao walipendekezwa na jopo la usaili wakiwekwa pembeni.

“Ninavyojua huyu Mrema hakuwa amependekezwa na jopo la usaili, hatujui alikotokea hadi akawekwa pale…naomba waziri useme juu ya ajira ya mkurugenzi huyu,” alisema wakati akichangia katika hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa.

Mporogomyi aliliambia Bunge kuwa sifa za mkurugenzi huyo ni kwamba ni mshauri wa mambo ya ununuzi na kabla ya kushika wadhifa huo, alikuwa anafanya shughuli zake visiwani Zanzibar.

Hata hivyo, Mrema mwenyewe alijitetea kuwa ana shahada ya kwanza ya ukandarasi uchumi (Construction Economics) na shahada ya pili ya Menejimenti ya miradi (Project Management) aliyoipata mwaka 1987. Hata hivyo, hakutaja vyuo alikopata shahada hizo.

Aliwataja wahandisi ambao walipendekezwa na jopo la usaili kuwa ni Boniface Nyiti, Venance Ndyamkama na mwingine aliyemtaja kwa jina la moja la Chacha. “Hawa ndiyo ambao walipendekezwa na ni wahandisi wa siku nyingi pale Tanroads; lakini huyu mkurugenzi alikotolewa na kuwekwa pale haijulikani.”

Mrema alichukua wadhifa wa mkurugenzi aliyekuwa anatokea Ghana ambaye alimaliza muda wake mwaka 2006. Mporogomyi alisema mkurugenzi wa sasa aliingizwa kwa misingi ya ufisadi.

Mbunge huyo aliongeza kuwa mara tu baada ya kupata wadhifa huo, alianza kuwanyanyasa wahandisi hao wenye sifa na akawahamishia wizarani ambako pia walirudishwa na wizara Tanroads. “Wizara ilisema hawa ni mawakala wa ujenzi wa barabara wakawarudisha.”

Alisema Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu wakati inawarejesha kwa Tanroads, ilishauri wapewe mikoa ya kuongoza, lakini kuwa tayari nafasi hizo zilishajazwa na watu wengine Mrema hakuweza kutekeleza agizo hilo.

Alisema alibaki nao makao makuu na wanalipwa fedha nyingi huku wakiwa hawana kazi za kufanya. Alisema kuwa mkurugenzi huyo baada ya kuona wahandisi hao ni tishio katika ajira yake, sasa ameingiza utaratibu mpya wa ajira za mikataba.

Mporogomyi alisema mpango huo mpya unafanywa na mkurugenzi huyo kwa nia ya kuwaengua wafanyakazi wote ambao anaona kama ni tishio kwake, hasa wale wahandisi wenye sifa za kushika wadhifa wake huo.

“Kibaya zaidi pamoja na kuingia kwa mlango wa nyuma, lakini ananyanyasa wafanyakazi,” alisema mbunge huyo huku akimtaka Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu amweleze namna mkurugenzi huyo alivyoingizwa kwenye nafasi hiyo nyeti na ikiwezekana aondolewe haraka.

Lakini pia alisema mkurugenzi huyo analipwa fedha nyingi kama vile ni mtaalamu ambaye ameajriwa kutoka nje ya nchi.

Aliweka hadharani viwango hivyo kuwa Mrema alipoanza kazi alipewa posho ya kuanza (Commencement allowance) dola za Marekani 9,000 kwa siku 60 (sawa na Sh milioni 10.8), mshahara wake kwa mwezi ni dola za Marekani 8,500 (Sh milioni 10.2), posho ya nyumba kwa mwezi ni dola 2,200 (Sh milioni 2.6), posho ya matibabu dola 400 kwa mwezi (Sh 480,000), posho ya usafiri dola 500 (Sh 600,000).

Pia analipwa pensheni kwa mwaka kiasi cha dola za Marekani 10,200 (Sh milioni 12.4), akienda likizo analipwa dola 3,000 (Sh milioni 3.6), bonasi yake kwa mwaka analipwa dola 102,000 (Sh milioni 122.4) na mwisho wa mkataba wake analipwa dola 10,000 (Sh milioni 12) kama malipo ya kumaliza kazi.

Mporogomyi alisema pamoja na fedha nyingi anazolipwa mkurugenzi huyo; lakini bado anajihusisha na vitendo vya ufisadi zinavyosababisha wakati mwingine awanyanyase na kuwafukuza wafanyakazi ambao wanatenda haki.

Mbunge huyo alitoa mfano kuwa kuna mfanyakazi aliyemtaja kwa jina moja la Mabuye ambaye alikuwa anafanya kazi katika mizani ya Kibaha. Alisema siku moja mfanyakazi huyo alikamata malori ambayo yalikuwa yamezidisha uzito wa bidhaa walizobeba.

Alisema aliyazuia na kuwataka walipe faini ya Sh milioni 18, lakini matajiri wa yale malori walipoambiwa kukamatwa kwa magari yao walimpigia simu na yeye akaamuru Mabuye afukuzwe kazi.

Mporogomyi alisema Mrema alimpigia simu meneja wa Tanroads mkoa wa Pwani ili amfukuze na aliposita alimtishia kwa simu kuwa afanye hivyo haraka, kwani hataki kumwona huyo mfanyakazi akiendelea na kazi.

“Kama siyo ufisadi hiki nini, yaani mfanyakazi ambaye anafanya kazi kwa misingi ya sheria unamfukuza kazi, sababu ni nini hapa? Alihoji mbunge huyo na kusisitiza kutaka maelezo ya kina kutoka kwa Waziri wa Miundombinu.
 
Ikiwa inahusu CCM inauma ila ni kigezo gani kilitumika kuwasema CUF?
Ni kigezo gani kilitumika kuisema CHADEMA?

Hapa ni hoja imeletwa japo sio nzuri kwa mustakabali wa nchi ila ni lazima ijadiliwe kama nyingine zilivyojadiliwa.

Mwingine aende kwenye baraza la mawaziri atajionea mengi juu ya hili pia.
 
Ikiwa inahusu CCM inauma ila ni kigezo gani kilitumika kuwasema CUF?
Ni kigezo gani kilitumika kuisema CHADEMA?

Hapa ni hoja imeletwa japo sio nzuri kwa mustakabali wa nchi ila ni lazima ijadiliwe kama nyingine zilivyojadiliwa.

Mwingine aende kwenye baraza la mawaziri atajionea mengi juu ya hili pia.

Tatizo siyo udini wala nini,Ila la CHADEMA ni kuwba zaidi,Wabungwe wa kuteuliwa wote kwanini wawe wachaga au kwa namna au moja nyingine wawe na mahusiano ya kindugu,kifamilia na viongozi wa juu wa CHADEMA.

CCM hata Baraz ala Mawaziri kuna uwiano mkubwa kikanda na hakuna kanda ambayo haina mtu anayeiwakilisha
 
Mwanakijiji wewe ni mchokonozi sana kwa mabo ambayo umekaa nayo muda mrefu sana na nilijua utakuja nayo hapa leo tu,ila bado nasimamia pale Wangwe Doctrine...Wangwe ana Hoja na asikilizwe

Sijui ushauri wangu Viongzoi wa CHADEMA wameufuata kwa hisia au vipi?

1.Mnyika Rudi ukamalize Shule na ujiendeleze zaidi na ikiwezekana utafute kazi nyingine ya Proffesional yako ili mpate pesa za Kampeni..

Hii siyo kwako na uwaambie na wenzako mfanye hivyo,Mmshauri na Mwenyekiti wenu wa taifa Atuambie kamaa shule amemaliza au vipi?

Gembe this is too cheap for you my man. What have you got to do with Mnyika`s education? We elimu yako ni ipi? sijui elimu yake ndugu Mnyika..lakini ni wapi kigezo cha uongozi ni degree? si CCM mlikataa hiki kigezo cha elimu....perhaps kwa ajili ya kuwaccomodate wakina Makamba?

Hapana CCM ni wanafiki...CUF leo ina supporters Zenji..mnawaita wadini..maana kwa hoja hamuwawezi...yaani aise baadhi ya wana CCM wanapoteza mwelikeo. Mimi ni independent...Let me see who can do the job best!
 
Kule kwenye mjadala wa Wangwe na Chadema, nilikanywa ni marufuku kumtaja mtu jina kuna watu walikuwa wakimuhisi Mpaka kielewe ni mtu wa chama fulani, mimi kuna member anayeshabikia Chadema akaniambia kuwa kuna sheria za JF ukimtaja mtu utafungiwa na sheria msumeno,

lakini katika mjadala huo huo watu wakataja kuwa HOLLO ni CHENGE na Cheyo hakuna aliesema kuwa sheria zimevunjwa na wala warning haikutolewa na mamoderators,

punde si punde nikatumiwa warning tatu na moderator kuwa nimewatukana watu wa Singida, nimetafuta tusi sijaliona na nimeuliza kwa uwazi wapi nimetukana sijapata jibu toka kwa Moderators hadi leo hii siku ya tatu,

Alianza kutishwa Mtanzania akalegea nikabaki mimi, mara naambiwa nimeongopa niombe radhi na ujumbe huo umeletwa na majina kama manne,

Ukaletwa ushahidi kukazia kauli yangu kuwa nilichosema ni sahihi na huyu mwanachama niliyesema kuwa kasema uongo, ikathibitishwa amewahi kuongopa zaidi ya mara mbili ndani ya forum hii, wenyewe walikuwa wakidai ni MwanaJF mahiri lazima aombwe radhi lakini bila ya wao kuyafanyia utafiti maneno yangu, vitu hivi zinanipa mashaka makubwa sana kama hakuna fursa sawa kwa wote, na hakuna mtu alisema kuwa nilituhumiwa kuwa muongo na sasa imedhihiri kuwa kauli yangu ilikuwa na ukweli mkubwa na nikasema nina mashahidi wengi ila namba moja awe Zitto KABWE.

hapa kuna double standard kama demokrasia ya kuandika tu tunakuwa intamidated jee kina Wangwe kwenye vikao vya siri walikuwa katika hali ngumu sana, ni rahisi kusema kunataka demokrasia au tunapropagate lakini uwazi wa kujadili hapa unafisadiwa mkipata madaraka itakuwaje?

Mimi siwaogopi wala siogopi kutishwa eti kufungiwa
uzuri Technologia hii yamambo ya kutumia ma protocols ya internet kidogo jamaa yangu hapa chumbani anayafamu.

Sasa mimi bado nawaomba wawakemee wote wanaotaja ID za watu hapa .Bila hivyo ule msamaha ni Batili na nitaendelea kutaja ID za watu kama ni vinginevyo .Wala kunifungia tutafungiana wengi hapa hadi PC nazo tutazifunga hapa.
 
mmmmh hii isue ya ukabila na udini kuna mtu aliwahi izungumza hapa tena sanaa mlimcrash sana tu.KUmbe mmeona madhara yake ni makubwa sana.
Kama Chadema wabunge wote wa kuteuliwa ni wachagga hii ni hatari sana.Kwa hiyo CHADEMA ni chama cha wachagga peke yao?hakuna makabila mengine mle ndani ya CHADEMA ambao ni wanachama??
Upande wa CCM kuna kubebana kwa kifisadi ,mtoto wa fisadi atapigiwa pande kila kona imradi awe kwenye system lakini mtoto wa mwanakijiji hata uwe na CV vp huwezi kula maisha vitengo nyeti kwa kuwa huna harufu ya kifisadi.
Kwa upande wa CCM upo ufisadi wa kupigiane mapande,mafisadi ving'ang'anizi wanazidi kupeta tu yaani wale wakubwa.
 
Mwita,
Asante kwa hili. This is just a tip of an iceberg!!! Serikalini mbona hayo aliyosema Kilontsi ni ya kawaida sana? Humu bwana ukijifanya haki haki utakula jeuri yako. You must dance to the tunes of a boss otherwise you are out unceremoniously!!!! Yaani nakwambia the government system is toten left right and center. Unategemea nnini serikalini kama juu kumeoza huku chini ndo kuwe safi. Uozo uozo tu, hakuna haki wala nini!!!!

Hiyo ndo hali halisi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom