Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Tatizo siyo udini wala nini,Ila la CHADEMA ni kuwba zaidi,Wabungwe wa kuteuliwa wote kwanini wawe wachaga au kwa namna au moja nyingine wawe na mahusiano ya kindugu,kifamilia na viongozi wa juu wa CHADEMA.

CCM hata Baraz ala Mawaziri kuna uwiano mkubwa kikanda na hakuna kanda ambayo haina mtu anayeiwakilisha

Mkoa wa Kigoma kwenye Baraza la Mawaziri hauna waziri kamili.
Mkoa wa Tanga hauna .
 
Hoja hapa ni kuwa Kamati Kuu ya CCM imejaa udini? hilo ndio la kujadiliwa na mengine yana thread zake .
 
Hawa jamaa wanaleta maada ya kidini wanajua itavuta hisia zenu na kuacha kujadili mambo yanayosababisha VITA vingi Afrika.

Enzi za MOI kenya Ukabila haukuwepo Lakini kilipoingia tu chama chenye sura ya ukabila KIKUYU vita ikatokea.Hili ni swala nyeti mno.

CCM hajateuana kama ilivyo CHADEMA ,CCM hawawezi sema aa hii ni sura ya kidini tubadiri uteuzi kwa maana wamefuata katiba yao na wamepiga kura ,CHADEMA ni tofauti kabisa.
Inamaama pale DAR wanaojua kuendesha magari ni wachaga tuuu.
Inamaana nafasi 8 za ukurugenzi kati 4 wawe wachagga
wabunge 6 kati 5 wawe kutoka KILI.
Wafadhili wa chama wawe wachaga tuu
Hakuna hawezi tokea kila sehemu ni wao tu,unapoangalia swala la udini iwekeni Zanzibar as constant yani muwatoe kabisa wala msiwajumlishe na wanaobaki wa bara ndio angalieni uwiano wao,hapo ndipo utajua kuna udini ama la!!!!!!

CHADEMA inakuaje Mtu anajitolea aruke na HELKOPITA harafu adai haya mapesa, sasa naelewa kwanini jamaa alikuwa analazimisha HELKOPITA harafu watu wanakuja kutuambia anajitolea .

Duuuu Wangwe!!! kumbe ndio maana hawataki kukipanua chama maana wanajua wakikipanua chama watapata watu wengi na watatoa mchango wa kutosha na hiyo itawanyima FURSA ya kukisaidia chama harafu wakadai mil 700.kweli huku nikula kuku kwa mrija yani BIASHARA NZURI sana
endelea uone maajabu ya filauni-




Habari za Tanzania Ijumaa Julai 04, 2008

Imetolewa mara ya mwisho: 04.07.2008 0037 EAT
•
Baada ya CHADEMA kumwaga ugali...Wangwe amwaga mboga

Habari Zinazoshabihiana
• CCM yagaragaza tena CHADEMA, NCCR 29.02.2008 [Soma]
• Wangwe kuadabishwa na kamati iliyojadili akina Mengi na Malima 10.02.2007 [Soma]
• Mbunge amkomalia Spika 09.02.2007 [Soma]

*Alalamikia kuchafuliwa, ubaguzi wa kikabila ndani ya chama
*Awapa viongozi siku 14 kumsafisha, vinginevyo mahakamani
*Akana kutoa siri CCM, adai Mbowe ndiye hukutana nao faragha

Na Mwandishi Wetu

MGOGORO wa uongozi unaorindima ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umeingia katika sura mpya baada ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho aliyesimamishwa hivi karibuni, Bw. Chacha Wangwe, kuwapa siku 14 viongozi wa chama hicho kuthibitisha madai yao kwamba anashirikiana na CCM kukihujumu, vinginevyo atawafikisha mahakamani.

Bw. Wangwe ambaye pia ni Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya chama hicho, aliliambia gazeti hili jana kuwa madai ya viongozi hao yamemchafulia jina na heshima kiasiasa aliyoijenga ndani ya chama hicho kwa gharama kubwa.

Wiki iliyopita katika kikao chake, mjini Dodoma, Kamati Kuu ya CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake, Bw. Freeman Mbowe, ilimsimamisha uongozi Bw. Wangwe kwa tuhuma mbalimbali ikiwamo kutoa siri za chama hicho kwa viongozi wa CCM.

Bw. Wangwe alituhumiwa pia kukashifu chama hicho, viongozi na watendaji wake, bila kutofautisha kashfa na ukosoaji wa kisiasa na kiutendaji, kwa kutumia wanachama waliochukuliwa hatua za kinidhamu na vikao halali vya chama hicho.

Tuhuma zingine ni pamoja na kuwatuhumu viongozi wenzake wa juu na watendaji wake kwa kuwahusisha na ukabila na kuvujisha siri za vikao halali vya chama kwa watu wenye lengo la kukihujumu chama hicho.

Akizungumza katika ofisi za gazeti hili Dar es Salaam jana, Bw. Wangwe alipinga madai hayo na kueleza kuwa hayana msingi na kwamba katika kipindi chote, ameipigania CHADEMA kwa nguvu zake zote na gharama kubwa, bila kuogopa mazingira magumu kwenye harakati hizo.

Alisema akiwa kiongozi wa chama hicho wilayani Tarime, alinyakua jimbo hilo na halmashauri ya wilaya hiyo huku 'wapiganaji' wenzake wakijeruhiwa kwa vipigo, kupata vilema vya maisha, kupoteza ajira na hata maisha.

Kutokana na harakati hizo, waliwezesha kupatikana asilimia 64 ya kura za jimbo hilo ambazo zilichangia ushindi wa CHADEMA na kuiwezesha kupata ruzuku ya sh. milioni 66 kila mwezi na viti maalumu sita bungeni vya chama hicho.

Alisema jitihada zake zilimfanya mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Mbowe kuibuka na kura nyingi kumzidi mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wilayani humo, kwenye uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2005.

Akizungumzia uhusiano wake na Dkt. Amani Kabourou ambaye alikihama chama hicho na kwenda CCM, alisema ni wa siku nyingi hata kabla ya kujiunga na CCM na uhusiano huo haufungamani kwa namna yoyote ile na masuala ya kisiasa kama inavyodaiwa na viongozi wa CHADEMA.

"Dkt. Kabourou nashirikiana naye siku nyingi tangu aliporudi kutoka Marekani, naheshimu uamuzi wake wa kwenda CCM na huo ni uamuzi wake mwenyewe, tangu aende CCM sijakutana naye bali Juni 7 mwaka huu, nilikwenda kwake kuhani msiba wa mama yake mzazi tukiwa na Bibi Maulida Anna Komu," alisema Bw. Wangwe.

Bw. Wangwe alishangaa suala hilo kuhusishwa na hujuma dhidi ya chama hicho na kuzidi kufafanua Katiba ya CHADEMA haina kipengele kinachozuia mwanachama kuwa na uhusiano na wanachama wa vyama vingine, bali tofauti iliyopo ni hoja.

Alimshambulia Mwenyekiti wa Chama hicho, Bw. Mbowe kwa maelezo kuwa amekuwa karibu zaidi na viongozi wengi wa CCM na wakati mwingine wanakutana faragha, lakini kama mwanachama ana uhuru wa kufanya hivyo na hakuna anayempinga kwa hilo.

"Dkt. Slaa (Wilbroad), mkewe ni kada wa CCM aliyekubuhu ni Diwani wa kuchaguliwa wanakaa pamoja, simu, nyaraka zote, wageni wote wanaokuja mama anasikiliza, hawanitendei haki mimi kwa hili," alisema Bw. Wangwe.

Alisema kuengulia kwake ni mkakati ulioandaliwa muda mrefu kumng'oa kwenye nafasi hiyo, kutokana na dhamira yake ya kutaka kufanyika mageuzi ya kweli ndani ya chama hicho.

"Nilisema uongozi uliopo tutaupumzisha, kwani umeshindwa kupeleka chama mbele," alisema Mbunge huyo machachari na kusisitiza kuwa ajenda ya kumsimamisha uongozi haikuwa kwenye mkutano wa Dodoma ila kilichokuwapo ni kuwasilishwa Ripoti ya Tume ya Mzirai, iliyoundwa kuchunguza tuhuma mbalimbali ndani ya chama hicho, lakini suala hilo likaibuliwa.

Alibainisha kuwa tofauti iliyojitokeza kati yake na Bw. Mbowe, ni suala la mgawanyo wa ruzuku kati ya makao makuu kwa upande mmoja na wilaya kwa upande mwingine, jambo alilosema kwa muda mrefu amekuwa akipigia debe chama hicho kujijenga kuanzia chini kwenda juu, jambo linalokinzana na msimamo wa mwenyekiti wake.

"Ninachopigania ni mfumo wa 'bottom up' (kuanzia chini kwenda juu) fedha zipelekwe kwenye vitovu vya mapambano zikajenge chama kwenye maeneo ambayo hakipo, lakini wenzangu wanataka mfumo wa 'up bottom' (juu kwenda chini).

Alisema gharama za kuendesha chama wilayani ni ndogo, kwani endapo kila mwezi zitapelekwa sh. 100,000 zitatosha kulipa pango la ofisi linaloweza kugharimu kati ya sh. 25,000 hadi 30,000 na sh. 70,000 zikabaki kwa matumizi mengine ya ofisi. Mbali na fedha hizo, alishauri pia kutolewa sh. 100,000 nyingine kwa ajili ya kulipa wasimamizi wa ofisi hizo.

"Yeye (Bw. Mbowe) anataka fedha zitumike kwa helikopta, sisemi kwamba helikopta ni kitu kibaya, lakini tuangalie katika mruko tulipata watu wangapi? Lazima tuwe na majimbo, wanachama na matawi ya kutosha, hata kama CCM itatuzidi nguvu, basi angalau tupate majimbo 150, hata ruzuku itapanda.

Alipinga kile alichokiita madeni hewa wanayojilipa viongozi wakuu wa chama hicho kwa madai ya kukikopesha chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, ambapo alisema Bw. Mbowe alidai kuikopesha CHADEMA sh. milioni 500, Bw. Philemon Ndesamburo sh. milioni 100 na Bibi Grace Kiwelu sh. milioni 100

"Nilipochaguliwa umakamu niligundua udhaifu huu, mfano kuhitilafiana wakati Baraza Kuu linatoa ratiba ya uchaguzi wa ndani ngazi zote...baadhi uchaguzi hautafanyika kwa sababu hakuna fedha zilizotolewa.

"Tutapataje chama chenye uhai kama hakuna fredha za kuwaewezesha wanachama kugombea? Sheria ya vyama inasema wazi, kuwa Msajili wa Vyama atafuta chama kisipochaguana kwa kuzingatia taratibu zilizopo. Kwa mwendo huu tutazamie mamluki bila uchaguzi," alisema.

Alidai kuwa hadi sasa, Bw. Mbowe ameshajilipa sh. 218,330,543.

Kuhusu ubaguzi wa kikabila, alikariri taarifa ya Tume ya Mzirai iliyobaini kuwa ubaguzi huo upo ikisema katika uongozi wa juu wa chama hicho, wakurugenzi, wenye watu wanane, wanne ni kutoka Kaskazini (Wachagga).


Alisisitiza nia yake ya kupinga kusimamishwa kwa kutumia vikao vya juu vya chama hicho ikiwa ni pamoja na Baraza Kuu, Mkutano Mkuu na hata kulifikisha suala hilo kwa wanachama kama vikao hivyo vitashindwa.
 
Hivi ni wapi mimi nimesema CCM kuna udini? Angalia hoja ya kwanza Mgagagigikoko don't project what you think of me na kufikiri nimesema kitu ambacho sijasema.

spin??!!!mwanzo kabisa wa thread ulisema ccm isiguswe??? cleverly insisting that udini umo??? sasa unasema hujasema baada ya kujua umejicontradict! kwa hili umechemka big time mzee mwanakijiji.
 
Dini haielezi utofauti wao, nafikiri kwa kuwa asilimia zaidi ya 90 ni waumini wa dhehebu jipya linaloitwa mafisadi. Hivyo tusiogope uislamu au ukristo wao, isipokuwa imani yao isiyotetereka juu ya ufisadi ambayo kwao ni dini takatifu kabisa.

bila kusahau dini ya uchawi!
 
Hoja hapa ni kuwa Kamati Kuu ya CCM imejaa udini? hilo ndio la kujadiliwa na mengine yana thread zake .
Kamati KUu ya CCM haijajaa UDINI labda useme imejaa waislam

UDINI
Udini ni khali ambyo inatokea kwa watu kuanza kubaguana na mwingine kwa kutumia Dini kwa lengo na madhumuni flani.Suala la Wananchama wa CCCM kuchagua Viongozi wao kwa kuangalia uwezo wao tu ni jukumu lao la msingi na ikumbukwe kuwa kamati kuu ya CCM inatoka pande mbali mbali ya Tanzania ni si rahisi kumwambia au kupanga kila mkoa uchague Mwislam.Hii imetokea tu na wala siyo kwamba RAis alipanga kuchagua waislam.Kwa hoja hii hakuna UDINI katika kamati kuu ya CCM na Mzee Mwanakijiji naomba uhitimishe hili.na wajumbe wa CCM ni wa KUCHAGULIWA.

UKABILA
Ukabila ni Tabia ya watu kutumia Kigezo ya ukabila kupeana madaraka kwa kufuata imani yao waliyo nayo ya UDINI,Udini ni Imani kabisa ya kuamini kwamba bila mtu mwenye kabila letu mambo hayataenda.Suala la Wangwe kusema kuna Ukabila CHADEMA ni suala amblo ni la kweli,Iweje Wabunge wote wa kuteuliwa wawe wachaga au wanatoka kadna ya Kaskazini.Kumbuka hawa ni KUTEULIWA.

Dhana ya KUTEULIWA na KUCHAGULIWA
Kuchagua mtu anaweza kuchaguliwa kwa kuangalia uwezo wake au pi akutokana na mambo ambayo yanaweza kuamuliwa na jamii aliyopo ,na inawezekana kwa ukabila,dini na jambo lingine ambalo litaamuliwa na wapiga kula hao na sehemu wanyotoka.Kuteuliwa huwa kunafanywa na mtu mmoja au wengi ili wanangalia Vigezo vilivyopo na mazingira waliyopo,Mfano CHADEMA waliangalia Vigezo vya ukabila na ukaribu wao na wateuliwa ila kuweza kurahisisha utendaji wao wa kazi,na hii inawezekana ilichangiwa na wazazi wao au wakwe zao kuchangia kiasi flani cha Pesa katika Kampeni,ambalo ni kweli na halina chembe ya ubishi.

HITIMISHO
Tusitumie Wangwe Doctrine kuhalalisha mambo ambayo hayana ukweli,Ukishindwa kwa hoja uslite vioja,ona tayari mlishaanza kuleta Vioja.Mpaka Kieleweke jenga hoja Nzuri ili kuweza kuweka uzito katika nia yenu.Kuanza kuonge ambao ambayo hamkuyaweka katika Ripoti yenu kwa umma hapa kwa kumpataka MAtope Wangwe Mnakosea
 


Nona hii topic inakoelekea sio kuzuri sana na matokeo yake kwa wananchi wastaarabu itakuwa ni kujiuliza swali moja gumu kuwa ni nini nia na madhumuni ya kuanzishwa kwa hii topic?

CC haijawahi kuwa na udini hata siku moja, hakuna one decision ya CC ambayo inaweza kuwa translated as ni kutokana na udini ndani ya CC, as opposed na some decisions on the otherside, ambazo ndio hasa chanzo cha mallalamiko yanayojaribiwa kufunikwa na hii topic,

Wananchi we know better, kama kuna matatizo ndani ya chama yatatuliwe na kile chama, badala ya kujaribu kukwepa kwa kutumia mifano hewa, sisi wananchi wa Tanzania tuna akili sana kuliko this kind of nasty politics, JF hatuhusiki in one way or another na matatizo ya ndani yanayojitokeza kwenye baadhi ya vyama vyetu vya siasa vya upinzani, sasa nashangaa all the effort kuja hapa na kujaribu kwa ahli na mali kama kina Lowassa kujisafisha kwa some of their leaders,

tunabaki tunajiuliza kuna nini hasa huko? Why all this? na why JF? Kuna mtu au chama kinatuchukulia for granted nini? sasa tunapouliza maswali genuine hawaamini maana tumezoea kuwabeba tu?

Wakuu huko msijaribu kutuchanganya, we know better than this please just clean your act huko ili mje hapa clean sio kujaribu kuja kujisafisha hapa, sisi hapa hatuna peremende! na tumesema mara nyingi tayari kuwa tunajua ukweli wa hii ishu ulipo ila tunawastahi tu, sasa msianze kutuchukulia for granted just clean your act huko!
 
Watu hapa wanajaribu kuspin tuu lakini ukweli unajulikana . Kama tunataka kutumia standard tulizotumia Chadema basi standard hizo hizo zitumike CCM pia. Huu ni ujinga wa hali ya juu, Mimi naipinga hoja ya kusema watu wanapewa vyeo Chadema kutokana na kuwa ni wachaga , kwanza nataka mniambie tunazungumza Wachaga wa sehemu gani ? Kwani kwa kusema Wachaga tuu aitoshi ni too vague jamani . Hivi mnajua historia ya hilo kabila mnalolizungumzia ? Mfano Wachaga wamachame na wakibosho mnajua ya kuwa hawapatani kabisa na mnajua ni mwiko kabisa kuoana ? Mnajua chuki zilizojengeka na ambazo zimerithishwa kwa vizazi mbali mbali ? Sasa mtu anaposema wachaga wanasaidiana hiyo haitoshi , inabidi mtu atuambie ni wachaga wa sehemu gani ?

Nazungumza hivi kwa sababu naona watu hawajui wanazungumza nini hapa , wanafikiri wachaga ni kama makabila mengine yenye lugha moja na hakuna tofauti kati yao . Swali ni kuwa kama hawa watu hawasikilizani kwa lugha na kuna chuki kubwa kati yao watawezaje kupatiana hizo favor mnazozisema ?
 
Mwankijiji, mgaya ,Mkandara

Ule msamaha niliomba kule naufuta rasimi ulikua batili ,ni halali kutaja ID za watu na kama ninyi ni waungwana inabidi mniombe msamaha.

Kunifungia kama ule mkwara wenu mnaopenda kuupiga hautofanya kazi labda tu niamue mwenyewe.
Asanteni.
NB.Ila mkandara aliniambia kistaarabu si ki mkwara
 
Kila chama huwa kina utaratibu wake wa kupata viongozi ama kwa kuwateua au kuwachagua/kupigiwa kura.

Hoja ya Kuhani ni nzito hasa kuhusu madai kwamba wabunge wa CHADEMA wa viti maalum walikuwa "hand picked". Swali, je ni kweli kuna kitu kama hicho? Najua hapa JF tuna viongozi wa CHADEMA na wanaweza kutupatia utaratibu ambao hutumika kuchagua/kuteua wabunge wa viti maalum ama kama kuna document yoyote ambayo imeainisha namna ya kuwapata hao wabunge nadhani ni vyema iwekwe hapa ili kumaliza hizi hoja za udini na ukabila ambazo zinatupotezea muda. Ni hoja za kisiasa zaidi zinazolenga kwenye maslahi binafsi na mwana siasa anayetumia hoja hiyo namuona ni kama ameishiwa hoja au anatapata ili kupata support.

Wangwe ni mwana-CHADEMA alitakiwa atuambie wazi kwamba hao viongozi ambao yeye amewataja kwamba wanatoka kabila moja, je walipatikana vipi? Waliteuliwa ama walichaguliwa. Hata kama ni uteuzi lazima huwa kuna ushindani and from huo ushindani ndipo mmoja kati walioshindanishwa huteuliwa kuchukua nafasi kwa consensus ya wajumbe walioshiriki kwenye mchakato huo.

Nitumie mfano wa CCM ambao mchakato wa uteuzi/uchaguzi uko documented na wengi tunaufahamu.

Uchaguzi wa NEC uko wazi kwamba kila mkoa lazima uwe na mwakilishi mmoja, then makundi hutoa wawakilishi ambapo kuna wanawake, kapu la Bara na Visiwani, vijana na wazazi. What if wagombea wanaowakilisha makundi ikatokea kwamba wengi walioshinda wametoka dini moja/mkoa mmoja, je, unaweza kudai kwamba CCM ina ukabila/udini?

Nije kwenye uchaguzi wa wabunge viti maalum, utaratibu ni ule ule kwamba kila mkoa unapewa nafasi moja, then kuna makundi kama NGOs, RAAWU, Walemavu, Vijana, na kapu la UWT. Swali hapa ni kwamba suppose kwenye hayo makundi kukawa na wanawake wengi ambao wanatoka mkoa mmoja/kabila moja lakini wanawakilisha makundi tofauti, je utadai kwamba hicho chama ni cha kikabila au cha kidini?

Tusiangalie huyu mtu katoka mkoa/kabila/dini gani, bali tuangalie alipatikana vipi mpaka akaingia huko. Si ajabu hao wamama wa CHADEMA walichaguliwa/teuliwa kihalali na vikao halali vya chama chao.

Nije kwenye hoja ya “hand picking”, pamoja na kwamba CCM ina maelezo ya namna mtu anaweza kuchaguliwa/teuliwa kwenye nafasi fulani. Huwa kuna tatizo la big shots wa CCM kumkataa ama kumtaka mgombea fulani na hivyo hao big shots wakisema NO hata ufanye nini huwezi kuingia kwenye anga zao, je hiyo siyo hand picking? Pamoja na taratibu zilizo wazi kabisa ambazo zimekuwa documented, hakuna chama kina ZENGWE kama CCM na ndiyo maana kila uchaguzi lazima watu huwa wanalia na mizengwe ambayo hutumika kuwaondoa wagombea ambao hawatakiwi (refer barua ya Butiku kwa Mkapa na mizengwe/rushwa ilivyotumika kumpata JK kama mgombea).

Uteuzi wa mgombea Ubunge kwenye majimbo, hata kama mtu anaweza kuongoza kwenye kura za maoni, lakini utashangaa jina lake halirudi na sababu ambazo CC wanazijua wao wenyewe. Inawezekana vipi mtu aliyeongoza kura za maoni kutoka kwa wanachama akapigwa panga na kikao cha wajumbe wachache? Ina maana wao wana nguvu kuliko wapiga kura wa jimboni ambao ndiyo wanachama wanaomtaka mwakilishi wao? Je, huyo mbunge anawakilisha wapiga kura wake ama anawakilisha CC? No wonder wabunge wakifika Bungeni badala ya kuwakilisha maoni ya wapiga kura wao huishia kutetea maslahi ya mafisadi. Kuna baadhi ya wagombea ambao huwa wanakuwa hand picked kwa Baraka za vikao halali vya chama na hasa CC. Talk of hand picking candidates? Basi CCM wanaweza kuwa wanaongoza na tena kwa kivuli cha vikao halali vya Chama kwa vigezo vyao ambavyo ni siri yao. Mzee Tinga Tinga anaweza kuwa na maelezo sahihi juu ya hilo, ama Elisa Mollel alipogombea NEC-Arusha.

Bottom line katika hoja ya Mwanakijiji ni kwamba je hao waliochaguliwa/teuliwa walichaguliwa/teuliwa kihalali kwa kufuata utaratibu wa Chama chao? Kama jibu ni NDIYO basi hoja ya ukabila/udini haipo.

Hoja inayobaki ni MIZENGWE na sidhani kama kuna chama kinaweza kukwepa lawama ya MIZENGWE kutokana na set up ya vikao vya vyama vya siasa vya Tanzania na mfumo mzima wa uteuzi/uchaguzi wa wagombea ambao kwa kiasi kikubwa maamuzi ya mwisho huachwa kwa watu wachache (Kamati Kuu, Baraza Kuu, or whatever the name). Matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona leo na kukimbilia kwenye hoja za udini na ukabila na huku kiini ambacho ni mizengwe tukikiacha bila kukiongelea ama kukirekebisha. Siku tukiondokana na mizengwe ndipo ambapo tutaweza kuwapata watu kwa vigezo vinavyotakiwa.

Leo hii ndani ya CC hakuna mtu anaweza kukemea ufisadi kwa kuwa mafisadi wenyewe wako humo ndani na ni mabingwa wa mizengwe na ukicheza nao wanaweza kukutoa vile vile na ukabaki unapiga kelele za kuchezewa rafu wakati refa anaendelea kupeta na ukileta za kuleta unapigwa na red card na ndiyo mwisho wa mchezo. Ndiyo maana CCM wamekuwa wagumu sana kukubali hoja ya mgombea binafsi kwa kuwa wana uhakika watu makini watakimbia CCM na kuamua kugombea kivyao na kama wanakubalika na wananchi hakuna namna ya kuwashinda zaidi ya kuendelea kuwatisha na vikao vya CC na NEC ili kuwanyamazisha. Same applies hata huko kwenye hivyo vyama vingine.
 
Watu hapa wanajaribu kuspin tuu lakini ukweli unajulikana . Kama tunataka kutumia standard tulizotumia Chadema basi standard hizo hizo zitumike CCM pia. Huu ni ujinga wa hali ya juu, Mimi naipinga hoja ya kusema watu wanapewa vyeo Chadema kutokana na kuwa ni wachaga , kwanza nataka mniambie tunazungumza Wachaga wa sehemu gani ? Kwani kwa kusema Wachaga tuu aitoshi ni too vague jamani . Hivi mnajua historia ya hilo kabila mnalolizungumzia ? Mfano Wachaga wamachame na wakibosho mnajua ya kuwa hawapatani kabisa na mnajua ni mwiko kabisa kuoana ? Mnajua chuki zilizojengeka na ambazo zimerithishwa kwa vizazi mbali mbali ? Sasa mtu anaposema wachaga wanasaidiana hiyo haitoshi , inabidi mtu atuambie ni wachaga wa sehemu gani ?

Nazungumza hivi kwa sababu naona watu hawajui wanazungumza nini hapa , wanafikiri wachaga ni kama makabila mengine yenye lugha moja na hakuna tofauti kati yao . Swali ni kuwa kama hawa watu hawasikilizani kwa lugha na kuna chuki kubwa kati yao watawezaje kupatiana hizo favor mnazozisema ?


PROBABILIty ya kupata viongozi eiza wote ni waiislamu ama wote ni wakristu ni 1
maana waisislamu /wakristu wanaishi mikoa yote 26 yani 26/26=1. ktk chama

Probability yakupata kiongozi mchaga ni 1/26=0.0385.Katika chama ni
Under condition hii kila kabila linarudi ktk mkoa wake.
 
kama wahusika walioorodheshwa kwenye katiba walikaa wakapendekeza majina kwa kutumia vigezo halali, coincidentally wakitoke wanawake, wanaume, waislamu, wakristu, au makabila fulani. mimi sioni ubaya wowote.

Ikumbukwe kwamba chama cha siasa (vya upinzani) huanza na wazo la mtu mmoja, anakusanya watu, then ndio wanajaribu kukisambaza Tanzania nzima.
Uwezekano wa kukusanyana watu wanaofahamiana ni mkubwa sana, pia lazima watakuwamo ndugu na jamaa.

Kabila la wachaga lina shida moja ya kwamba lazima mtu ujulikane tu kwamba wewe ni mchaga, popote uendapo, na inakuwa badge yako.
Personalities za wachaga ziko too strong for the liking of Watanzania (speaking from experience)
 
Mzee mwana kijiji umekosa busara, mbona baraza la mawaziri hausemi?? wakati watu wa dini nyingine wako kwa asilimia hiyo hiyo????, kama alivyosema Macho_ M , mzee anataka kuturudisha nyuma, ambacho kinachotakiwa kuangaliwa ni uwezo na siyo kinginecho siye wote ni watanzania, anayeangalia kwa mlengo wa dini ,ukabila hatufai kabisaaaa
 
Kama kweli kuna ukabila na chama hiki ni cha kichaga kwa nini mwaka 1995 chama hiki kilishinda jimbo moja tuu la ubunge huko Kilimanjaro ?

Ni dhahiri watu ambao wanaona ni sawa kumtetea Wangwe kutokana na sababu wanazozijua wao , watu hao hao wanampinga Mwanakijiji na kumlabel ni mdini . Kwa nini tunakuwa na double standard katika ishu moja ? Jee ni kweli ya kuwa kuna watu wengi wa dini fulani kwenye halmshauri kuu ya CCM ? Na kama jibu ni ndiyo , jee ni sahihi kutumia Wangwe's Doctrine ?
 
Mzee mwana kijiji umekosa busara, mbona baraza la mawaziri hausemi?? wakati watu wa dini nyingine wako kwa asilimia hiyo hiyo????, kama alivyosema Macho_ M , mzee anataka kuturudisha nyuma, ambacho kinachotakiwa kuangaliwa ni uwezo na siyo kinginecho siye wote ni watanzania, anayeangalia kwa mlengo wa dini ,ukabila hatufai kabisaaaa


Ukabila ni KIMEO hata mkijifanya kutouungalia lakini wananchi wanauoona na kuusema ,kenya nao walijidai hivyohivyo kujifanya hawauoni ukabila kilichotokea ilikuwa htari tupu.

mfano ZIMBAMBWE kama kungekua na chama vhenye sura ya kikabila VITA ingekuwa ilishapigwa siku nyingi ,hali ya ZIM ni mbaya kuliko ilivyokua RWANDA,BURUNDI na KENYA survival ya ZIM ni kwamba hakuna ukabila.

PAnapofuka moshi jua chini kunamoto ,haya ya funika twende hatutoyapa nafasi.
 
Hongera mwanakijiji kwa kuanzisha hii mada.
Naona imepata wachangiaji kwa kasi ya ajabu sana.
Ama kweli dini ni sensitive issue.
Sasa na sie tunaosali kwa askofu kakobe nafasi yetu kwenye CC ya CCM sijui ni ipi hasa???
Oooh Gosh, nimesahau ndugu zangu makarasinga!!
Ohh god, nimeidhihaki dini yangu niliyoachiwa na babu yangu Ng'wana malundi.
Oooh God, nimegundua sunni ndio wametawala katika CC ya CCM, tuangalie na Shia vilevile. Oooh Yes, what about Ahamadiya? Kadiani??
I might be wrong though!!!
 
Hongera mwanakijiji kwa kuanzisha hii mada.
Naona imepata wachangiaji kwa kasi ya ajabu sana.
Ama kweli dini ni sensitive issue.
Sasa na sie tunaosali kwa askofu kakobe nafasi yetu kwenye CC ya CCM sijui ni ipi hasa???
Oooh Gosh, nimesahau ndugu zangu makarasinga!!
Ohh god, nimeidhihaki dini yangu niliyoachiwa na babu yangu Ng'wana malundi.
Oooh God, nimegundua sunni ndio wametawala katika CC ya CCM, tuangalie na Shia vilevile. Oooh Yes, what about Ahamadiya? Kadiani??
I might be wrong though!!!

u get the point of the discussion. Na hapa JF pia udini utaingia, mama yangu mzazi! Dini gani ina wafuasi wengi JF? kidding!!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom