UDA yanunua mabasi mapya 30

Mtoa hoja, naomba unifariji iyo picha sio ya mabasi 30 yalioingizwa nchini.Kama ndio yenyewe ntakua sahihi kutumia neno kuingizwa nchini ckusema kununuliwa
 
Si kulikuwa na kashfa uko UDA yaani washa sort out na kuanza agiza magari?
 
Nchi hii ukiwa kiongozi ndo unapata access ya kujikopesha mali za umma. Haka ka nchi kazuri kweli kwa wababaishaji.
 
Mtoa hoja, naomba unifariji iyo picha sio ya mabasi 30 yalioingizwa nchini.Kama ndio yenyewe ntakua sahihi kutumia neno kuingizwa nchini ckusema kununuliwa

lol. Kwa hiyo hajanunuliwa bali yameingizwa tuu nchini?
 
Those were the days......hapa ni karibu na St Alban's Church

UDA.jpg
 
  • Thanks
Reactions: EMT
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KIKAO CHA WABUNGE WA MKOA WA DAR ES SALAAM JUU YA KASHFA YA SHIRIKA LA USAFIRI DAR ES SALAAM (UDA)

Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari kwamba Kamati ya Wabunge wa Dar es salaam inakutana leo 28 Februari 2012 kwa dharura baada ya kupokea taarifa na nyaraka nyingine mpya za tuhuma za ufisadi, ukiukwaji wa sheria, kanuni na maslahi ya wananchi unaoendelea katika Shirika la Usafiri Dar es salaam (UDA) unaofanyika kinyume na maagizo ya mamlaka husika likiwemo Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam.

Wabunge ambao wanaendelea kushiriki mkutano husika ni: Abbas Mtemvu (Mwenyekiti), John Mnyika (Katibu), Halima Mdee, Mussa Zungu, Idd Azzan, Neema Mgaya Hamid, Suzan Lyimo, Zarina Madabida, Faustine Ndugulile, Phillipa Mturano na Eugen Mwaiposa.

Taarifa kuhusu maamuzi na maazimio ya kikao husika na hatua ambazo wabunge wa Dar es Salaam watachukua kuhusu suala husika itatolewa kesho tarehe 29 Februari 2012. Nyaraka ambazo kamati ya wabunge wa Dar es salaam imezipokea ni pamoja na barua ya UDA ya tarehe 26 Januari 2012 yenye kumb. Ref. CBA/Reg/01/UDA ambayo inataka fedha kiasi cha Dola 133,125 zitolewe kutoka kwenye akaunti ya UDA ambayo ilishaagizwa awali fedha zisitoke kinyemela.

Nyaraka nyingine ni Muktasari wa kinachoitwa kikao haramu kinachodaiwa kuwa cha wanahisa wa UDA cha tarehe 13 Februari 2012 ambacho kimefanywa na Meya wa Jiji Didas Masaburi akiwa ni mwenyekiti pamoja na Robert Kisena ambaye ametambulishwa kwenye muktasari huo kama mwenyekiti mtendaji wa UDA na katibu wa bodi ya UDA. Kikao hicho pamoja na mambo mengine kimefanya maamuzi haramu ya kubadili waweka saini katika akaunti ya UDA iliyozuliwa kwa lengo la kuwezesha fedha kutolewa kinyemela na Simon Group.

Meya wa Jiji Didas Masaburi kwa kushirikiana na Simon Group wameshirikiana kwa mara nyingine tena kukiuka maamuzi ya mamlaka mbalimbali pamoja na sheria na kanuni. Izingatiwe kuwa tarehe 9 Januari 2012 Baraza la Madiwani wa Jiji lilipitisha maazimio mbalimbali kuhusu mgogoro unaoendelea katika shirika la UDA. Baraza la Madiwani wa Jiji liliazimia kwamba uchunguzi wa kughushiwa kwa barua iliyomwelekeza Simon Group Limited kulipa awamu ya pili ya malipo kwa kutumia akaunti ya Mwenyekiti wa Bodi ya UDA lipelekwe kwenye vyombo husika kwa ajili ya kubaini ukweli na hatua kauli zichukuliwe dhidi ya aliyeghushi. Aidha, baraza la madiwani liliazimia kuwa uthamini wa hisa uliotumiwa katika kumwuzia hisa Simon Group haukuwa halisi hivyo hisa zote zifanyiwe uthamini upya ili ziuzwe kwa bei inayostahili.

Pia, Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es salaam liliazimia kuwa Simon Group asitambuliwe kama mwanahisa mkuu katika shirika la UDA na hivyo baraza liliazimia kuwa iteuliwe bodi ya muda itayosimamia utekelezaji wa mkataba kati ya UDA na Simon Group.

Baraza lilimteua Mheshimiwa Eugen Mwaiposa kuwa mjumbe wa bodi hiyo akiwakilisha Halmashauri ya Jiji; hata hivyo Meya Dr Didas Masaburi kinyume na maazimio ya mkutano wa tarehe 9 Januari 2012 wa Jiji, ameshiriki kikao kinyemela kikao cha bodi ya UDA cha tarehe 13 Februari 2012 na kufanya maamuzi haramu ya kubadili wawekasaini wa akaunti ili fedha kuweza kuhamishwa.

Itakumbukwa kwamba wakati wa mkutano wanne wa Bunge tarehe 4 Agosti 2011 Wabunge wa Dar es salaam tulikutana na kutoa tamko la kueleza kusikitishwa na tuhuma za ufisadi, ukiukwaji wa sheria, kanuni na maslahi ya wananchi katika mchakato wa ubinafsishaji wa Shirika la Usafiri Dar es salaam (UDA).

Wabunge wa Mkoa wa Dar es salaam tulirejea ufafanuzi ambao Waziri Mkuu Mizengo Pinda alioutoa bungeni tarehe 4 Agosti 2011 wakati wa kipindi cha maswali kwa mujibu wa Kanuni za Bunge kifungu cha 38 (4) ya kuelekeza vyombo vya dola hususan Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) , Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na
Ofisi ya Upepelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma husika. Wabunge wa Jiji la Dar es salaam tulieleza kwamba tayari kutoa ushahidi kwa vyombo hivyo pamoja na kushirikiana na serikali kwa ujumla wake ili kuwezesha hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa haraka kuhusu tuhuma hizo kwa lengo la kulinda mali za umma na pia kutetea maslahi ya wakazi wa jiji letu wanaohangaika na adha ya usafiri.

Pamoja na kuagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi, wabunge wa Jiji la Dar es Salaam tulitoa mwito kwa Serikali kuagiza kusitishwa mara moja kwa mkataba batili na maamuzi haramu yaliyofanyika ya kukabidhi hisa, mali na uendeshaji wa kampuni ya UDA kwa Kampuni ya Simon Group Limited ili katika kipindi hiki cha uchunguzi masuala yote ya kampuni hiyo yaratibiwe na bodi huru itayoundwa na kusimamiwa na Shirika la Hodhi ya Mali za Mashirika ya Umma (CHC) kwa mujibu wa sheria zinazohusika.

Wabunge wa Jiji la Dar es Salaam kwa nafasi yetu kama wajumbe wa Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam tulisisitiza kuufahamisha umma wa wakazi wa mkoa wetu na watanzania kwa ujumla kwamba maamuzi yote yaliyofanywa na Mstahiki Meya Didas Massaburi yanayotajwa kuridhiwa na vikao vya jiji ni batili kwa kuwa yamefanyika kwenye vikao visivyokuwa halali bila kuzingatia sheria, kanuni na maslahi ya wananchi wa Dar es Salaam. Izingatiwe kuwa tarehe 10 Juni 2011 Meya Massaburi kwa kushirikiana na kaimu Mkurugenzi wa Jiji walishiriki kikao batili kilichoitwa mkutano maalum wa wanahisa wa UDA na kufanya maamuzi haramu ya kukabidhi Shirika na mali zake kwa kampuni ya Simon Group. Wabunge wa Jiji la Dar es salaam tuliunga mkono kuvunjwa kwa bodi iliyokuwepo ya UDA na hatua za haraka za kunusuru hisa na mali za UDA hata hivyo, hatua za kuvunja kwa bodi hiyo hazikupaswa kuambatana na na kukiuka sheria na kanuni kwa kuhamisha umiliki huo.

Maamuzi hayo yalifanyika bila kuheshimu maelekezo ya barua ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya tarehe 28 Februari 2011 yenye kumbu. Na CAB. 185/295/01/27 ambayo iliagiza kusitisha mara moja mchakato wa kuuza hisa ambazo hazijagawiwa barua ambayo nakala yake iliwasilishwa kwa mkurugenzi wa Jiji na Meneja Mkuu wa UDA pamoja na Wizara zingine zinazohusika. Wabunge wa Dar es salaam wanaendelea na kikao cha kupitia nyaraka zote na kufanya maamuzi ya hatua za kuchukua na taarifa juu ya hatua hizo itatolewa kwa umma baada ya kumalizika kwa mkutano unaoendelea.

Izingatiwe kwamba mkutano alioufanya Meya Massaburi ulitanguliwa na kikao batili cha bodi ya wakurugenzi wa UDA chini ya uenyekiti wa Iddi Simba cha tarehe 28 January 2011 kilichofanya maamuzi haramu ya kuuza hisa zisizogawiwa (unallotted shares) kwa kampuni ya Simon Group Limited bila kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maslahi
ya wananchi wa Dar es Salaam.

Vikao hivyo vya kamati ya uongozi pamoja na baraza la madiwani viliitishwa kinyemela wakati wabunge tukiwa kwenye bunge la bajeti Dodoma bila kuwashirikisha wabunge kwa ukamilifu wetu ambao ni wawakilishi wa wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam.

Katika tamko la tarehe 4 Agosti 2012 tulieleza kuwa mikutano maalum iliyoitishwa kuhalalisha maamuzi haramu yaliyofanywa na Meya Massaburi kuhusu UDA yaani kikao cha kamati ya fedha na uongozi ya tarehe 29 Juni 2011 na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji tarehe 20 Julai 2011 ilikuwa batili kwa notisi kutolewa bila kuzingatia kanuni na maamuzi kufanyika bila mikutano kuwa na akidi. Kwa mujibu wa Kanuni za kudumu za Mikutano na Shughuli za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (Zilizotungwa chini ya Kifungu cha 42 cha Sheria ya Serikali za Mitaa-Mamlaka za Miji ) na. 8 ya mwaka 1982) kifungu 8(2) na 52 akidi katika mikutano maalum ni theluthi mbili ya wajumbe hivyo vikao vyote vilivyofanyika ni batili na maamuzi yote yaliyofikiwa ni haramu.

Hivyo, wabunge wa Mkoa wa Dar es salaam tulitaka Meya Massaburi, Mkurugenzi wa Jiji Bakari Kingobi (aliyekuwepo wakati huo) na watendaji wote wa jiji la Dar es salaam waliohusika wasimamishwe mara moja katika kipindi chote cha uchunguzi na kuchukuliwa hatua stahili baada ya uchunguzi huo kwa mujibu wa sheria, kanuni na maslahi ya umma. Aidha, tulitaka hatua kali zaidi za kisheria zichukuliwe kwa mwenyekiti wa bodi ya UDA, wajumbe wote wa bodi na watendaji wote wa UDA waliohusika na kashfa hiyo.

Wabunge wa Dar es salaam tulitoa tamko tarehe 4 Agosti 2011 la kuitaka Serikali izingatie kwamba pamoja na udhaifu kwenye uongozi wa Jiji la Dar es salaam matatizo ya UDA yamechangiwa pia na Ofisi ya Msajili wa Hazina na CHC kutokuwa makini katika hatua zote kwa kushirikiana na CHC katika masuala ya ubinafsisaji wa UDA. Hivyo, tuliitaka Serikali ichukue hatua kwa watendaji wote wa Wizara ya Fedha waliosababisha taifa kuingia katika hasara, mali za umma za UDA kupotea na wananchi wa Dar es salaam kuendelea kupata matatizo ya usafiri.

Wabunge wa Dar es salaam tulitaka mali zilizobaki za kampuni ya UDA hususani magari, majengo na viwanja kufanyiwa tathmini upya na ya haraka ili kuunganisha mchakato wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) ambao uko chini ya ofisi ya Waziri Mkuu ili kuwa na mfumo thabiti zaidi na mamlaka itakayosimamia vizuri zaidi mfumo wa usafiri wa umma (mass transit) katika mkoa wa Dar es salaam ili kuongeza ufanisi, kupunguza adha ya usafiri kwa wananchi na kuchangia katika kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

Wabunge wa mkoa wa Dar es salaam tunawaomba wakazi wa mkoa wetu na wananchi kwa ujumla kuendelea kutuunga mkono katika hatua zote tunazochukuwa kuhusu suala la UDA na mali nyingine za jiji la Dar es salaam kama sehemu ya wajibu tuliotumwa wa kuwawakilisha na kuisamamia serikali.

Taarifa imesambazwa na John Mnyika Katibu wa Wabunge leo tarehe 28 Februari 2012 saa 8:37 mchana wakati mkutano ukiendelea.

Source: wavuti.com  - Blogu
 
Wabunge wa Dar-es-Salaam wataonekana ni vituko. Kama wana umoja wa hivyo; kwanini wasipeleke Bungeni mswada wa mabadiliko ya sheria ilyounda UDA na DART ili kuunda mamlaka mpya ya Usafiri wa Umma - mwenyewe napenda iitwe DAR METRO
 
wabunge wa dar-es-salaam wataonekana ni vituko. Kama wana umoja wa hivyo; kwanini wasipeleke bungeni mswada wa mabadiliko ya sheria ilyounda uda na dart ili kuunda mamlaka mpya ya usafiri wa umma - mwenyewe napenda iitwe dar metro

huenda na wao wana maslahi yao kama ya huyo makalio
 
Mwekezaji UDA amwaga mabasi mengine 15. Mpango ni kumwaga mabasi 300 ya abiria ifikapo Machi mwakani. Aliongeza kuwa kati ya mabasi hayo kutakuwa na mabasi ya wanawake, mabasi ya wanafunzi, mabasi ya binafsi, mabasi ya mikoani na mabasi yatakayosafiri barani Afrika. Kuhusu mabasi ya wanafunzi, alisema yatakuwa matano kila barabara kuu jijini Dar es Salaam na yatafanya kazi hiyo tu. Kuhusu mabasi ya binafsi (Executive class), alisema yatakuwa na nauli ya juu lakini yatatoa huduma kama vile televisheni, vinywaji, magazeti na kiyoyozi.


Akizungumzia mradi wa mabasi yaendayo kasi (Dart) alisema kuwa wanatarajia kushinda zabuni ya kuuendesha kwa kuwa kampuni hiyo haina mshindani katika usafirishaji nchini. “Kwa sasa Dart inajengwa barabara ya Morogoro na barabara itakamilika mwaka 2014. Kwa sasa tutaendesha mradi huo kabla Dart haijaanza na kwa barabara nyingine baada ya hapo. Kwa kuwa sasa UDA haina mpinzani katika sekta ya usafirishaji nchini, naamini tutashinda zabuni ya kuendesha,” alisema. Aliongeza kuwa mradi huo unatarajia kutoa ajira kwa zaidi ya Watanzania 1,500.

656057487.JPG


Viongozi wa Kampuni ya Simon Group na wengine Wakielekea kuzindua mabasi15 waliyowekeza UDA.

582957490.JPG


819024342.JPG


Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Simon Group,Robert Kisena (wa pili kulia) Wawekezaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA akipokea mfano wa funguo kutoka kwa Meneja wa Biashara wa TATA Afrika Holding Tanzania Ltd,Srinivas Nemalapuri (wa pili kushoto) kulia ni Mkurugenzi wa Simon Group, Leonard Rubuye na kushoto Kaimu Meneja Biashara,Sarvan Keshri. ikiwa ishara makabidhiano ya mabasi 15 katika awamu ya kwanza, hafla hiyo ilifanyika kwenye Ofisi za UDA Dar es Salaam.

796109719.JPG


Mwenyekiti Mtendaji wa Simon Group,Robert Kisena (wa nne kushoto) akiwaongoza viongozi wengine ndani ya Basi la UDA.

Source: wavuti.com - wavuti
 
Back
Top Bottom