SoC03 Usafiri wa mabasi ya mikoani kwa muda stahiki

Stories of Change - 2023 Competition

Safari79

Member
Sep 15, 2022
6
7
Mimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu mwenendo wa usafiri wa mabasi ya mikoni. Kiongozi mmoja akifuta safari za usiku na mwingine akizikirudisha. Mmoja ikichagua mabasi gani yasafiri usiku na mabasi gani yasisafiri usiku nap engine kusiwe hat ana vigezo vya ruhusa ama makatazo hayo.

Lakini kwa nyakati zote bado sijaona maslahi ya huyo msafiri anayepiganiwa katika hiyo safari. Maathalani mmiliki wa usafiri anasema amepatakibali cha kusafiri mapema zaidi, lakini ukiangalia ni aa 11 asubuhi. Swali linakuja, abiria huyu ametizamwa anatoka nyumbani kwake saa ngapi ili kufika stendi saa 11 asubuhi?

Katika hili, lengo ni kupunguza changamoto kwenye kero za usafiri wa abiria ama tunaziongeza kwa sababu hatujajua nani anamsafirisha abiria usiku huo ili kufika stendi, hatujajua usalama wake kwenye mitaa anayopita kabla ya kufika stendi.

Usafiri wa mikoani hautakiwi kuwa kwenye mikono ya wafanya biashara wasio na uwezo. Mathalani, mtu amebarikiwa uwezo na akaamua kununua mabasi mawiili: moja la kwenda na lingine la kurudi safari, mwisho wa siku mwekezaji huyo anasema naye ni mmiliki wa kampuni ya mabasi.

Nafikiri hili si sawa, walau mmiliki wa mabasi awe na uwezo wa kuanzia mabasi 20 ili kupunguza fujo za mababasi kugombania abiria. Ikiwa mmiliki hana uwezo wa kuwa na idadi kubwa ya mabasi basi walau makampuni hayo madogo yakiungani yanaweza kusimama pamoja na kukua pamoja.

Umri wa madereva wa safari za usiku walau awe na umri kuanzia miaka 40 kwasababu walau wanauzoefu mkubwa na pengine hawana haraka za maisha kama ilivyo madereva wengi vijana

Rekodi ya maderva itizamwe vizuri ili kuhakikisha dereva hana changamoto kubwa katika historia ya leseni yake kwa kuzingatia idadi ya ajali alizosababisha. Ikiwa dereva atakuwa na rekodi mbaya ya matukio ya kuhatarisha usalama wa abiria hivyo hatapesa nafasi ya kuendesha mabasi ya usiku.

Changamoto ya safari za usiku ni kwamba hakuna wasimamizi wengi barabarani. Hivyo nidhamu ya dereva na umakini wa dereva ni muhimu sana kwa uhakika wa kufika mwisho wa safari salama.

Hali ya basi lenyewe, mamlaka iwe na uhakika wa hali ya basi, mfano walau liwe jipya. Upya wa basi unatoa uhakika wa kufika mwisho wa safari salama. Kwa maana hiyo, kuweka gari kuu kuu nyakati za usiku inaleta changamoto kwa abiria na walinzi wa sheria za usafiri. Katika hili walau basi lisizidi umri wa mwaka mmoja tokea kuanza safari ili kuweza kusafiri nyakati za usiku.

Vilevile kama inawezekana, basi kuwe na mabasi ya mwendo wa haraka kidogo ili walau yatembee kwa kilomita 100 kwa saa badala ya 80 ili kusaidia abiria kuwahi safari zao. Lakini na hili liratibiwe vizuri ili abiria waweze kufika mapema zaidi katika safari zao. Masharti katika hili yanaweza pia kuandaliwa.

Taarifa za wanaokiuka wa sheria za barabara zinapotolewa ziwe na uwazi zaidi walau kwa kumtaja dereva kwa jina ili awe mwenye kijitafakari wakati wa safiri na katika kazi zake. Mwisho wa siku dereva kukimbia nje ya spidi aliyopangiwa isiwe kawaida na isiwe sifa.

Kuna haja ya safari za mabasi kuwa huru, kwa mfano basi liruhusiwe kusafiri muda wowote na sio nyakati fulani tu. Mfano mabasi yawe na uwezo wa kuamua kusafiri saa 1 usiku, saa 6 usiku nakadhalika. Na sio kulazimisha kila mmoja kusafiri saa 11 asubuhi. Changamoto kubwa ya usafiri wa mabasi kwa safari ndefu Tanzania hutokana na mbio za kuwahi abiria wa njiani. Unakuta mabasi 15 yanaondoka kwa wakati mmoja stendi.

Nyakazi zingine kuwe na askari wanaosafiri na basi husika kwa safari za usiku kama ilivyo kwa afisa usalama katika usafiri wa anga. Kama ulinzi kwenye ndege unapatikana nafikiri hata kwenye aina zingine za usafiri inawezekana pia.

Kusema mabasi yasisafiri nyakati za usiku kwa sababu za kiusalama sio sawa kwasababu ni kama tunasalimu amri kwa wahalifu.Badala ya kukwepa tatizo tunatakiwa kulishughulikia tatizo, kulitatua na likaisha.

Kusimamisha usafiri kwa muda flani ni kusimamisha uchumi kwa muda huo. Watu wanatakiwa wafanye biashara muda wote na sio kuchaguliwa muda ama kupangiwa muda wa kusafiri.

Kusafiri usiku kuna msaidia abiria kuutumia vizuri muda wake, kwasababu badala ya kushinda kwenye usafiri mida ya mchana, basi anatumia muda wake wa usiku kwa kusafiri na kujipumzisha.

Hivyo kupatiwa dereva makini, usafiri makini kutamhakikishia abiria kusafiri bila ya wasiwasi wakati wa safari yake kuanzia mwanzo wa safari yake hadi mwisho.

Vilevile sababu zote zinazo msababishia dereva w abasi kukimbia sana njiani zitizamwe na zishughulikiwe ili kuongeza hali ya usalama kwa abiria na safari zote za mabasi nchini Tanzania.

Hali ya barabara zetu ziendelee kuboreshwa ili mwisho wa siku lawana zisiwalemee sana madereva wa mabasi. Kuna wakati huwa nashangaa, kama mabasi miaka ya 90 yalikuwa na uwezo wa kufika Mbeya kutoka Dar es Salaam saa 10, leo hii baada ya mabasi kuwa ya kisasa kwanini yafike misho wa safari saa 12 jioni?

Tunavyoendelea kuboresha barabara zetu tuendelee kujifunza jinsi reli yetu ya SGR ilivyo zingatia usalama kwa kukwepa muingiliano na waenda kwa miguu kwenye pundamilia ama njia vivuko vya wanyama, ama njia mbadala za kupishana na watumiaji wengine wa barabara.

Tanzania yetu hii ya leo tunahitahi barabara za mwendokasi, pengine sio kwa kuanza kuzijenga leo lakini zilitakiwa ziwepo tokea juzi. Maana unakuta watu wananunua magari na bahati m,baya wala hawajawahi kuzidi mwendo wa kilometa 160 kwa saa kutokana na changamoto za barabara ama watumiaji wa barabara.

Inawezekana tumechelewa, lakini bado tuna nafasi ya kukimbia badala ya kitembea. Tujitahidi sana katika kufikiria mara mbili mipango ya barabara zetu mara mbili kabla ya kufanya maamuzi ya kuzijenga kwa kuzingatia matumizi ya barabara kwa mika walau 30 ijayo ili kuepuka kujenga leo na kesho tunaboresha tena.

Vyombo vya usafiri vikaguliwe walau mara moja kila mwezi na ikiwezekana siku moja kabla ya safari ili kujaribu kupata uhakika wa usalama wa usafiri na kulinda usalama wa abiria katika basi husika.

Mamlaka za usafiri kama LATRA, Polisi, ziwe na vikao vya mara kwa mara na report za mara kwa mara kuhusiana na mahitaji mapya ya biashara ya usafiri Tanzania.
 
Back
Top Bottom