EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
- Thread starter
- #21
Hivi ile kashfa ya ubinafisishaji wa hili shirika iliishia wapi?
Sijui hata iliishia wapi. Kulikuwa na kamati za kuchunguza nyngi tuu.Mojawapo ni kamati ya bunge iliyokuwa chini ya Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini-CCM); Esther Bulaya na Angellah Kairuki (Viti Maalum-CCM), Mbunge wa Viti Maalum CUF, Amina Mwidau; David Kafulila (Kigoma Kusini-NCCR-Mageuzi); Hebert Mtangi (Muheza-CCM) na John Mnyika (Ubungo-Chadema). Kamati hiyo ilipewa siku 14 iwe imekamilisha uchunguzi huo na kutoa majibu.
Pia Takukuru nao walikuwa wanachunguza. Pinda nae aliunda tume ya kuchunguza. Jiji nalo lilikuwa na tume yake ya kuchunguza. CAG nae alikuwa anachunguza pia. Ina maana kweli hakuna hata kamati moja ambayo imekuja na matokeo?
Agosti 13, 2011 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) Keptein mstaafu George Mkuchika, alitekeleza agizo la waziri mkuu na kumpa CAG barua ya kufanya ukaguzi wa UDA ndani ya mwezi, lakini sasa ni zaidi ya miezi mitano matokeo hayajatoka.
Hata hivyo akihojiwa na gazeti la Mwananchi mwanzoni mwa mwezi huu CAG alisema kuwa KPMG iliyopewa jukumu la kuchunguza mchakato wa uuzwaji wa Hisa za UDA, imekamilisha ripoti yake itakayoikabidhiwa kwa CAG wakati wowote kuanzia sasa. CAG,alisema kuwa, kwa sasa ripoti hiyo imewasilishwa Makao Makuu ya Kampuni ya KPMG nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya kuihakiki na kuangalia ubora wa ukaguzi wenyewe ndipo waikabidhi kwake aweze kuipitia.