Uchumi unakua, takwimu hazidanganyi

Yaani tatizo kubwa la nchi hii ni maCCM. Sasa cheki huyu ameokoteza maneno ya kisiasa na kuja kutuaminisha hapa kwamba uchumi unakua pasi kutumia data hata moja kuthibitisha maelezo yake. Yaani wenyewe bado wanaamini kwamba kizazi cha sasa ni sawa na kile walichokuwa wanakiburuza enzi za mamlaka mikoani (1972).
 
Mbona hii maneno yako inakinzana na taarifa ya BOT; y akwamba uchumi wetu una-shrink.

Anybody out there labda sijui kimombo; shrink = kukua? Nilidhani taarifa za BOT ndiyo sahihi au zenu ninyi wanasiasa?
Leo unakubaliana na BOT. Kipindi cha Nyuma ulikuwa unabishana na takwimu za BOT.
Sasa ueleweke vipi?
 
HEBU TUMPE MUDA MAGUFULI AFANYE MAMBO YAKE ILI TUNEEMEKE WOTE,MUDA MCHACHE SANA BADO ANAPANGA JINSI YA KUTEKELEZA NA MENGINE KATEKELEZA TAYARI.
MAGUFULI JUU JUU JUU ZAIDI
 
Hizi blaa blaa zote ni fine,but if they don't end up to increased bread on the table,it's useless.Mzee ambaye hajapata pension yake,mfanyabiashara ambaye anafirisika kwa kuwa walaji hawana fedha na mkulima ambaya bei ya mazao yake ni ndogo kwa kuwa soko la nje limefungwa hawezi kukuelewa kabisa.To him or her you are a day dreamer.
Katika siku za karibuni kumetokea ukosoaji mkubwa hasa kuhusu hali ya uchumi wa Nchi yetu, baadhi ya wakosoaji wakidai hali ya uchumi ni mbaya na kwamba mtaani hakuna fedha jambo ambalo lilimfanya Mhe. Rais atolee majibu hoja hii na kusema bayana kuwa wanaosema kuwa hakuna hela mifukoni ni wale ambao walikuwa wakipata fedha zao kwa njia zisizo halali.

Kauli hiyo ya Mhe Rais inakubalika na watafiti na inapewa nguvu na takwimu za mapato kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani ya Nchi. Uchunguzi unaonesha kuwa sera na staili ya uongozi wa Rais Magufuli hasa katika nyanja ya Uchumi imewavutia wawekezaji na wageni kutoka nje.

Uchambuzi unaitaja sekta ya Utalii ambayo inaiingizia Serikali takribani 25% ya fedha za kigeni, pamoja na upotoshaji mkubwa wa wakosoaji baada ya imposition ya VAT, bado kuna ongezeko la asilimia 11 ya watalii kuanzia Julai mwaka huu.

Lakini si tu kwa Utalii, bali mapato ya Nchi kwa ujumla wake yameendelea kuongezeka na hivyo kuipa Serikali fursa ya kuwekeza na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Infalation imepungua kufikia asilimia 4.9 na inashuka zaidi, maana yake ni kuwa bei za bidhaa muhimu zinazidi kushuka na bei ya mazao ya wakulima zinapanda.

Ni kama vile ujenzi wa Reli ya Kati ni utani wa kusimulia, lakini tunategemea kuiona Tanzania yenye uwezo mkubwa sana katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano ambayo itategemewa na nchi za maziwa makuu na Afrika ya Kati.

Bomba la Mafuta kutoka Uganda ni mradi ambao wakosoaji wanajaribu kuufanya uonekane kama ni upanuzi wa jengo la machinga complex, wanaficha ukweli wa nafasi ya bomba hilo katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania na maendeleo ya watu wake.

Wakosoaji, wanabeza Ununuzi wa Ndege tatu kwa ajili ya Shirika letu, tena kwa hoja dhaifu tu kuwa zimenunuliwa cash, kwanini zisinunuliwe kwa mkopo, tununue kwa mkopo ili tulipe riba maradufu. Ndege zinawasili na watanzania watanufaika na kuona matunda ya kura zao kwa Magufuli.

Kimsingi yako mengi yanayohusiana na uchumi wetu, isipokuwa TANZANIA yetu wapo WASEMAJI na WAKOSOAJI wazuri ila tunao WATENDAJI na WACHAPAKAZI wachache ambao tunajitahidi kuwavunja moyo ili mambo yasiende.

Mhe Rais wangu, Hongera kwa kazi kubwa unayoifanya kwa maslahi ya Nchi yetu na ustawi wa watu wake.
View attachment 399299
 
Kukaribisha Demokrasia ni kuchelewesha maendeleo ya wananchi. tujiulize je watanzania wanahitaji nini?? Demokrasia au wanahitaji kuona kuna elimu bora? huduma za afya bora? huduma za usafiri bora? huduma za maji bora? Demokrasia ije baada ya hivyo vyote kupatikana

Unajua demokrasia au unabwabwaja tu, au unadhani demokrasia ni kufanya uchaguzi tu? rudi shule ukasome uraia
 
Ndiyo matatizo yenu hayo. Wewe hata hujaisoma na hujui mini kimeandilwa humo ndani. Mimi mishaisoma muda sasa, Hanna kitu Kama hicho.

Nina wasiwasi na uelewa wako. Report imeelezea kila kitu.
Uchumi umeporomoka na siku sio nyingi wananchi watanza kulia na kusaga meno.
 
mmmh huyu Tandale one mbona haileleweki?....BoT wanasema uchumi umedorora yyeye anasema umekuwa!!!!!....kivipi??!!!
 
Hatuna tatizo na ukuaji wa uchumi, tatizo letu ni kuchezewa kwa katiba
Kila siku hamkosi sababu. Tumepiga kelele kuhusi uchumi weeee, uchumi unaenda vizuri sasa tunarukia katiba. Kwa nini tusiwe na msimamo kuhusu kitu kimoja na tuendelee kushauriana na serikali namna bora zaidi ya kuboresha uchumi. Katiba imefanyaje sasa ?? Inahusianaje na uchumi kukua au kutokua? ? Tusiwe wajinga makamanda
 
Back
Top Bottom