Uchumi unakua, takwimu hazidanganyi

Uchumi unakua, takwimu hazidanganyi

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Posts
1,644
Reaction score
709
Katika siku za karibuni kumetokea ukosoaji mkubwa hasa kuhusu hali ya uchumi wa Nchi yetu, baadhi ya wakosoaji wakidai hali ya uchumi ni mbaya na kwamba mtaani hakuna fedha jambo ambalo lilimfanya Mhe. Rais atolee majibu hoja hii na kusema bayana kuwa wanaosema kuwa hakuna hela mifukoni ni wale ambao walikuwa wakipata fedha zao kwa njia zisizo halali.

Kauli hiyo ya Mhe Rais inakubalika na watafiti na inapewa nguvu na takwimu za mapato kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani ya Nchi. Uchunguzi unaonesha kuwa sera na staili ya uongozi wa Rais Magufuli hasa katika nyanja ya Uchumi imewavutia wawekezaji na wageni kutoka nje.

Uchambuzi unaitaja sekta ya Utalii ambayo inaiingizia Serikali takribani 25% ya fedha za kigeni, pamoja na upotoshaji mkubwa wa wakosoaji baada ya imposition ya VAT, bado kuna ongezeko la asilimia 11 ya watalii kuanzia Julai mwaka huu.

Lakini si tu kwa Utalii, bali mapato ya Nchi kwa ujumla wake yameendelea kuongezeka na hivyo kuipa Serikali fursa ya kuwekeza na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Infalation imepungua kufikia asilimia 4.9 na inashuka zaidi, maana yake ni kuwa bei za bidhaa muhimu zinazidi kushuka na bei ya mazao ya wakulima zinapanda.

Ni kama vile ujenzi wa Reli ya Kati ni utani wa kusimulia, lakini tunategemea kuiona Tanzania yenye uwezo mkubwa sana katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano ambayo itategemewa na nchi za maziwa makuu na Afrika ya Kati.

Bomba la Mafuta kutoka Uganda ni mradi ambao wakosoaji wanajaribu kuufanya uonekane kama ni upanuzi wa jengo la machinga complex, wanaficha ukweli wa nafasi ya bomba hilo katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania na maendeleo ya watu wake.

Wakosoaji, wanabeza Ununuzi wa Ndege tatu kwa ajili ya Shirika letu, tena kwa hoja dhaifu tu kuwa zimenunuliwa cash, kwanini zisinunuliwe kwa mkopo, tununue kwa mkopo ili tulipe riba maradufu. Ndege zinawasili na watanzania watanufaika na kuona matunda ya kura zao kwa Magufuli.

Kimsingi yako mengi yanayohusiana na uchumi wetu, isipokuwa TANZANIA yetu wapo WASEMAJI na WAKOSOAJI wazuri ila tunao WATENDAJI na WACHAPAKAZI wachache ambao tunajitahidi kuwavunja moyo ili mambo yasiende.

Mhe Rais wangu, Hongera kwa kazi kubwa unayoifanya kwa maslahi ya Nchi yetu na ustawi wa watu wake.
Inflation.PNG
 
unakuwa?
Waziri mkuu aliulizwa juzi bungeni akasema hajui, mpaka akae na wadau na watafiti, leo hii mmeshakaa nao tayari? BOT wametoa takwimu zinazoonyesha economic activity kupungua

Dsm ndio kitovu cha biashara TZ, uchumi ukikua au kusinyaa impact yake inaanza kuonekana kwa wazi zaidi Dar, na ukiangalia hapa watu wengi wameachishwa kazi kwenye makampui ya usfirishaji, mawakala wa forodha, fastjet nao wamepunguza wafanyakazi, mahoteli yanafungwa, baa zinafungwa n.k ku refelect kuwa uchumi umeshuka

Na justification inayotolewa na Magufuli na wanaomuunga mkono kuhusu hili ni kuwa biashara nyingi zilikuwa kutokana na ukwepaji kodi na ubadhirifu wa fedha za umma hivyo Magufuli alipoingia akaondoa hivo vitu lazima uchumi utasinyaa

Leo unakuja kutuambia kuwa uchumi unapanda? kwa hiyo hizo fedha haramu mlizoondoa kwenye mzunguko zimechangia uchumi kukua zaidi? Yaani unapunguza fedha kwenye mzunguko halafu uchumi ukue??? theory ya wapi hii?

Sasa nyie mnawafanya watanzania maboya kwa kuwaambia uchumi unakuwa? na hayo mazao ya wakulima kupanda bei sijui takwimu umezitoa wapi maana watu wanauza nyanya ndoo 700, wenngine wanazilisha mifugo, mbaazi nazo zimepungua bei....Mbona mnawatukana wakulima aisee?? a

Rais amesema anapambana na matajiri matokeo yake masikini ndio wanaoishia kuachishwa kazi na kushindwa kutunza familia...........Anyway most of them they deserve it
 
Mbona hii maneno yako inakinzana na taarifa ya BOT; y akwamba uchumi wetu una-shrink.

Anybody out there labda sijui kimombo; shrink = kukua? Nilidhani taarifa za BOT ndiyo sahihi au zenu ninyi wanasiasa?
 
Wewe ndio umefanya uo utafiti?
Ili kukwepa lawama ni vema ukaweka chanzo cha hiyo tafiti b4 hatujakutukana.
 
Hatuna tatizo na ukuaji wa uchumi, tatizo letu ni kuchezewa kwa katiba
Kukaribisha Demokrasia ni kuchelewesha maendeleo ya wananchi. tujiulize je watanzania wanahitaji nini?? Demokrasia au wanahitaji kuona kuna elimu bora? huduma za afya bora? huduma za usafiri bora? huduma za maji bora? Demokrasia ije baada ya hivyo vyote kupatikana
 
kuna faida gani uchumi kukua halafu wananchi wanateseka.hizi ndo sifa kama za wakenya kujisifia uchumi uko juu wakati majority wanateseka na umaskini huko kibera na mathare
 
Wewe ndio umefanya uo utafiti?
Ili kukwepa lawama ni vema ukaweka chanzo cha hiyo tafiti b4 hatujakutukana.
Mliacha lini kunitukana..?
Nadhani itakuwa ni muendelezo wa jambo ambalo mmezaliwa duniani kulitimiza.
 
unakuwa?
Waziri mkuu aliulizwa juzi bungeni akasema hajui, mpaka akae na wadau na watafiti, leo hii mmeshakaa nao tayari
Kabla ya Utafiti, circumstancial evidence zinazosaidiwa na takwimu halali zinatosha kujua muelekeo wa uchumi wetu.
 
Katika siku za karibuni kumetokea ukosoaji mkubwa hasa kuhusu hali ya uchumi wa Nchi yetu, baadhi ya wakosoaji wakidai hali ya uchumi ni mbaya na kwamba mtaani hakuna fedha jambo ambalo lilimfanya Mhe Rais atolee majibu hoja hii na kusema bayana kuwa wanaosema kuwa hakuna hela mifukoni ni wale ambao walikuwa wakipata fedha zao kwa njia zisizo halali.

Kauli hiyo ya Mhe Rais inakubalika na watafiti na inapewa nguvu na takwimu za mapato kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani ya Nchi.

Uchunguzi unaonesha kuwa sera na staili ya uongozi wa Rais Magufuli hasa katika nyanja ya Uchumi imewavutia wawekezaji na wageni kutoka nje.

Uchambuzi unaitaja sekta ya Utalii ambayo inaiingizia Serikali takribani 25% ya fedha za kigeni, pamoja na upotoshaji mkubwa wa wakosoaji baada ya imposition ya VAT, bado kuna ongezeko la asilimia 11 ya watalii kuanzia Julai mwaka huu.

Lakini si tu kwa Utalii, bali mapato ya Nchi kwa ujumla wake yameendelea kuongezeka na hivyo kuipa Serikali fursa ya kuwekeza na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Infalation imepungua kufikia asilimia 4.9 na inashuka zaidi, maana yake ni kuwa bei za bidhaa muhimu zinazidi kushuka na bei ya mazao ya wakulima zinapanda.

Ni kama vile ujenzi wa Reli ya Kati ni utani wa kusimulia, lakini tunategemea kuiona Tanzania yenye uwezo mkubwa sana katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano ambayo itategemewa na nchi za maziwa makuu na Afrika ya Kati.

Bomba la Mafuta kutoka Uganda ni mradi ambao wakosoaji wanajaribu kuufanya uonekane kama ni upanuzi wa jengo la machinga complex, wanaficha ukweli wa nafasi ya bomba hilo katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania na maendeleo ya watu wake.

Wakosoaji, wanabeza Ununuzi wa Ndege tatu kwa ajili ya Shirika letu, tena kwa hoja dhaifu tu kuwa zimenunuliwa cash, kwanini zisinunuliwe kwa mkopo, tununue kwa mkopo ili tulipe riba maradufu. Ndege zinawasili na watanzania watanufaika na kuona matunda ya kura zao kwa Magufuli.

Kimsingi yako mengi yanayohusiana na uchumi wetu, isipokuwa TANZANIA yetu wapo WASEMAJI na WAKOSOAJI wazuri ila tunao WATENDAJI na WACHAPAKAZI wachache ambao tunajitahidi kuwavunja moyo ili mambo yasiende.

Mhe Rais wangu, Hongera kwa kazi kubwa unayoifanya kwa maslahi ya Nchi yetu na ustawi wa watu wake.
View attachment 399299
Ko tukwamini wewe au benki kuu yaan central bank m kua mkwel bana
 
Uchumi unakuwa kwenda chini hakika takwimu hazidanganyi..nchi ya giza hii mmefanya ujinga wa watanzania wengi ndo kipaombele chenu kuwandanganya
 
Back
Top Bottom