Uchumi unakua, takwimu hazidanganyi

Uchumi unakua, takwimu hazidanganyi

Kwa hiyo nyumbani kwa baba na mama yako kama ulikuta uwezo wako ni kujenga nyumba ya miti na makuti huwezi kufanya zaidi yao.Uchumi wa nchi uanategemea uwezo wa kila mmoja wetu,jukumu la kukuza uchumi wa kila mmoja wetu ni la kila mmoja wetu.Tuelezane humu jukwaani wapi JPM analikoroga kuhusu uchumi wetu ashauriwe tusitegemee ushauri wa wageni tutakuwa siyo wajinga bali wapumbavu.Hakuna mzungu mwenye akili timamu atakayetupa maarifa ya kushindana naye au kumshinda.
Sisi wakulima tuliojenga nyumba za makuti tunaishi kwa nguvu za mungu tumelima mazao yamekuwa mengi kuliko soko la ndani tulitaka kuuza nje serikali chini ya Magufuli ikapiga stop mazao yakaanza haribika ndipo serikali inakuja kusema tumefungua mipaka mje mchukue vibali..kwa akili yako mimi mkulima nitapandisha uchumi wa nchi hi kwa mazao yaliyoharibika? Je serikali hawakuona tatizo walipoambiwa mpaka washtukie bidhaa zinaharibika ndo waruhusu?
 
Hizo "histograms" umechora mwenyewe kwenye "excel" maana taharifa zinatofautiana na za BoT
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mbona hii maneno yako inakinzana na taarifa ya BOT; y akwamba uchumi wetu una-shrink.

Anybody out there labda sijui kimombo; shrink = kukua? Nilidhani taarifa za BOT ndiyo sahihi au zenu ninyi wanasiasa?

Hapa anaongelea UCHUMI wa wana SIASA
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Katika siku za karibuni kumetokea ukosoaji mkubwa hasa kuhusu hali ya uchumi wa Nchi yetu, baadhi ya wakosoaji wakidai hali ya uchumi ni mbaya na kwamba mtaani hakuna fedha jambo ambalo lilimfanya Mhe. Rais atolee majibu hoja hii na kusema bayana kuwa wanaosema kuwa hakuna hela mifukoni ni wale ambao walikuwa wakipata fedha zao kwa njia zisizo halali.

Kauli hiyo ya Mhe Rais inakubalika na watafiti na inapewa nguvu na takwimu za mapato kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani ya Nchi. Uchunguzi unaonesha kuwa sera na staili ya uongozi wa Rais Magufuli hasa katika nyanja ya Uchumi imewavutia wawekezaji na wageni kutoka nje.

Uchambuzi unaitaja sekta ya Utalii ambayo inaiingizia Serikali takribani 25% ya fedha za kigeni, pamoja na upotoshaji mkubwa wa wakosoaji baada ya imposition ya VAT, bado kuna ongezeko la asilimia 11 ya watalii kuanzia Julai mwaka huu.

Lakini si tu kwa Utalii, bali mapato ya Nchi kwa ujumla wake yameendelea kuongezeka na hivyo kuipa Serikali fursa ya kuwekeza na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Infalation imepungua kufikia asilimia 4.9 na inashuka zaidi, maana yake ni kuwa bei za bidhaa muhimu zinazidi kushuka na bei ya mazao ya wakulima zinapanda.

Ni kama vile ujenzi wa Reli ya Kati ni utani wa kusimulia, lakini tunategemea kuiona Tanzania yenye uwezo mkubwa sana katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano ambayo itategemewa na nchi za maziwa makuu na Afrika ya Kati.

Bomba la Mafuta kutoka Uganda ni mradi ambao wakosoaji wanajaribu kuufanya uonekane kama ni upanuzi wa jengo la machinga complex, wanaficha ukweli wa nafasi ya bomba hilo katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania na maendeleo ya watu wake.

Wakosoaji, wanabeza Ununuzi wa Ndege tatu kwa ajili ya Shirika letu, tena kwa hoja dhaifu tu kuwa zimenunuliwa cash, kwanini zisinunuliwe kwa mkopo, tununue kwa mkopo ili tulipe riba maradufu. Ndege zinawasili na watanzania watanufaika na kuona matunda ya kura zao kwa Magufuli.

Kimsingi yako mengi yanayohusiana na uchumi wetu, isipokuwa TANZANIA yetu wapo WASEMAJI na WAKOSOAJI wazuri ila tunao WATENDAJI na WACHAPAKAZI wachache ambao tunajitahidi kuwavunja moyo ili mambo yasiende.

Mhe Rais wangu, Hongera kwa kazi kubwa unayoifanya kwa maslahi ya Nchi yetu na ustawi wa watu wake.
View attachment 399299
Ulitakiwa kasema, UCHUMI LABDA UTAKUA, Kutokana na sababu ulizo zitoa. Otherwise, ulichosema sikweli. BOT imesema uchumi umeshuka na serekali imeliambia bunge, haijui kama uchumi umeshuka.
 
Ili tujadiliane kwa tija na kuelewana vizuri chagua lugha moja ya mawasiliano,iwe Kiwahili au kiingereza tuendeleze mjadala.Uwezo wa kununua chanzo chake kiwe thabiti na kieleweke,JPM na maamuzi yake kaathiri kipi kilichofanyika kwa haki na kwa kufuata sheria zetu ili ashauriwe.

Ni narejea kauli yangu tuna tatizo kubwa la watu kukariri na siyo kuelewa.Marekani ambayo wengi wamwkaririshwa na kuaminiishwa kuwa ni kitovu cha demokrasia na misingi sahihi ya uchumi je tunaweza kuambiana hapa jukwaani mgawanyo wa raslimali zao ukoje.Kundi gai la wamarekani linamiliki sehemu kubwa ya uchumi wao? Huu upuuzi tunaousikia kuhusu mauaji wanayofanyiaa chanzo chake nini? Marekani hakuna cha bure kwa hiyo tungetarajia kuwe na amani kubwa.Kuna mgombea mmoja analenga kujenga ukuta kuzuwia wahamiaji haramu tuambizane chanzo ni nini?

Waliotukaririsha mmojha wapo anaitwa Maslow aliorodhesha mahitaji ya binadamu katika muundo wa ngazi,hadi ngazi ya kwanza kabisa ya mahitaji ya msingi yaani malaz,mavazi na chakula ndipo tunaweza kutafuta ngazi ya pili,wengine ya tatu wengine ya nne hadi kilele cha tamaa ya binadamu.Ni imani yangu kuwa watanzania wengi ngazi ya kwanza hatujaimaliza,na hawa ndiyo wapiga kura wengi.Kwa mtumishi anayejua matakwa ya mwajiri wake atatimiza matakwa ya mwajiri wake kwanza.Kuhusiana na uchumi wetu je JPM anatimiza au anapuuza matakwa ya walio wengi Tanzania.Nina uhakika matakwa ya watawala wetu anayavuruga kisawasaw,matakwa ya vibaraka wao anayvuruga kisawasawa na hawa wana uwezo mkubwa wa kura za mitandaoni,je kura zinazoamua nani atutawale zinapatikana humu mitandaoni?

Tuelezane ukweli uchumi unakuwa eneo lipi,unashuka eneo lipi tufanye nini kutatua kwa manufaa ya wengi.Fedha za bia zimepungua lakini fedha za ujenzi wa miundombinu zinapatikana kwa walio ofisini OC haionekani lakini mishahara haikosekani.

Kwa Wakulima bado kuna tatizo mazao mengi wanazalisha hayauziki,je ni jukumu la rais tu kutatua au kuwashauri wakulima wafanye nini.Humu jamii forum hatuna watu wanaoweza kuwashauri wakulima walime nini,walime lini,wauze wapi badala ya kulima na kuzalisha kwa wingi ndipo waulize soko.Kama tupo humu ambao hatuoni kuwa kuwa huu ni wajibu wetu kwa nchi yetu je tumeelimika au tumejaza vyeti vya kutafutia ajira.

Nitatoa mfano mmoja unaoonyesha kiwango cha ujinga wetu na bado tunasubiri serikali itatue.Tanzania inazalisha machungwa kuliko Kenya lakini Kenya inasafirisha machungwa mengi nje ya Kenya kuliko Tanzania,machungwa hayo yananunuliwa Tanzania (Muheza inaongoza) tujiulize je ni jukumu la Serikali kuhakikisha fursa hii hatuwaachi wakenya?

Mnisamehe yawezekana akili yangu ni mbovu maana inaamini kuwa wengi wetu tumekariri hatujaelimika tunasubiri baba afanye kila kitu sisi tle tu.Ninahesabu kuwa ukiwa ni miongoni mwa akina baba hao una hasara kubwa.

Mimi bahati mbaya siyo mswahili wala mwingereza sasa nisaidie nichague luga ipi...pili kukariri ni moja wapo ya kuelewa jambo tatizo unapokariri alafu ukashindwa kutafsiri baada ya kukariri...
Baada ya kuacha utoto wa hapo juu then kasome maelezo yangu then nipinge moja baada ya lingine kwa hoja mbadala ama kwa ujumla...

Ila kama siyo umegafilika naona kama vile tupo page moja ebu kanisome tena
Shikamoo!
 
Hizo "histograms" umechora mwenyewe kwenye "excel" maana taharifa zinatofautiana na za BoT

Nimecheka mpaka basi...JF kuna raha saa nyingine...

But...si bora hiyozo zake kuliko hizo za wachumi ambao wanatumia takwimu za Dar?

Ebu kamuulize mchumi yeyote farm gate price ya mahindi kilo 100 ni TZS ngapi? Akikwambia mimi narudi kusoma darasa lakwanza maana hunda nilikariri tu sikuelewa...sasa kama mazao huko kwenye viwanda (mashambani) hayana specifications wao hizo graph wanachoraga kwa takwimu zipi?

Uchumi wa nchi yetu haukidhi kusomwa kwa takwimu za kinataifa kwakua bado upo informal na haufanywi kwa pesa (peasant) upo zaidi in batter na in kind kuupima kwa vigezo vya IMF na world bank ni kujitakia kuudumaza na kutoutambua matakwa yake ni yapi..

Hii hali haitaondoka mpaka wachumi wetu wakubali kuwa njia wanazotumia kuupima zipo kwenye vitabu lakini bila kuwekea context hawatakaa kuleta takwimu zinazo reflect what is on the ground...Ndiyo maana hata tamplate za budget zina sigara, bia, soda etc vitu vilivyotumiwa tangu mkoloni..mihogo, kuku wa kienyeji, ng'ombe, pombe za kienyeji, huoni vitumbua, mitumba, maandazi and the like ambavyo walipa kodi wakubwa ndiyo biashara yao...lakini ebu jiulize pombe ya kienyeji na bia ipi ina nyweka sana huku nchini, tumbaku na sigara ipi ina vutwa sana...yaani specification zetu hazi reflect uhalisia ni copy paste ya chumi zenye viwanda ambavyo huku kwetu havipo...
 
Hatuna tatizo na ukuaji wa uchumi, tatizo letu ni kuchezewa kwa katiba
Huwa Machadema hamuelewekagi huwa mnataka nini hasa. Kazi kubadili gia angani tu! Kwa hiyo ajenda ya ufisadi nayo ilikuwa gia ya kutafuta cheap popularity! Ha ha ha ha ha! Hamna jipya.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
You know nothing about economics pal, i can't waste my time arguing witcha!!
Thank you Prof help me know for I want to know, I am passionate to know that I may use my knowledge to serve my country...
 
Huwa Machadema hamuelewekagi huwa mnataka nini hasa. Kazi kubadili gia angani tu! Kwa hiyo ajenda ya ufisadi nayo ilikuwa gia ya kutafuta cheap popularity! Ha ha ha ha ha! Hamna jipya.

Hapo umetuonea tupo wa aina mbili CHADEMA version ya wazalendo na ile version ya ufisadi...ile ya wazalendo ndiyo tuliwawezesha nyie muepuke mafisadi mtuletee mzalendo...tuombe radhi!
 
BOT na NBS ndio wanatakiwa kutoa takwimu za ukuaji wa uchumi. Kama takwimu zako hazijatoka uko ni batili.
Na NBS na BOT wamesema uchumi unaporomoka.
 
Democrasia mumeiua Tanzania sasa ni kwa nini basi uchumi unakwenda chini?
Mlidhani watu hawachoki na siasa za ccm tu?
Sasa hivi watu karibu tutaacha hata kusikiliza tv na radio kwa ajili ya kuepuka sauti za wakina Makonda.
 
Wachumi wapo walichokisema kimesikiwa. Kati ya vitu ambavyo siasa haina nafasi ni Uchumi. Uchumi pamoja na kwamba ni takwimu hata mtu ambaye hajenda shule anaweza kujua kuwa hali ni nzuri au ni mbaya. Ninachoweza kusema ni kuwa kiasi cha mzunguko wa fedha ni kidogo mno kiasi kwamba baadhi ya biashara zimefungwa. Ukweli ni kuwa hali si shwari hata kidogo.
 
BOT na NBS ndio wanatakiwa kutoa takwimu za ukuaji wa uchumi. Kama takwimu zako hazijatoka uko ni batili.
Na NBS na BOT wamesema uchumi unaporomoka.
Hiyo chart [emoji409] imetoka NBS, muwe mnasoma sio kuangalia juu juu, angalia chini ya chart,
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Huwa Machadema hamuelewekagi huwa mnataka nini hasa. Kazi kubadili gia angani tu! Kwa hiyo ajenda ya ufisadi nayo ilikuwa gia ya kutafuta cheap popularity! Ha ha ha ha ha! Hamna jipya.
Wewe kila siku nakwambia toa maoni yako kwa kujitegemea, acha kusubiri wanaume watoe maoni yao ndiyo uwanukuu, jifunze kuheshimu maoni ya wanaume
 
Back
Top Bottom