Uchumi unakua, takwimu hazidanganyi

Uchumi unakua, takwimu hazidanganyi

Lipi kwako ni kipaumbele, kukufanya usilale njaa au kuruhusiwa kuandamana..???
Mwl Nyerere aliwahi kusema hivi , nanukuu , " HATA KAMA TUTACHAGUA ASIYEAMINI MUNGU , TUTAFUTA NAMNA YA KUMUAPISHA , NA NI LAZIMA AAPE KWAMBA ATAILINDA NA KUITETEA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA " mwisho wa kunukuu .

Kuisigina katiba kwa kisingizio chochote kile ni upuuzi wa kiwango cha juu sana na ni kosa lisilosameheka milele , hapa duniani na ahera .
 
Wakosoaji hawakosi la kupindisha kama kwa mganga wa kienyeji kuishiwa na wimbo
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Pesa ikiwa chache inflation rate lazima ipungue vice versa kwa hiyo uchumi haujakua isipokuwa umeganda kama sio kupungua
You have a quiet nice point, bei itapandaje wakati pesa mtaani hakuna, uchumi bado ni janga nchini, maisha ni magumu kipindi hichi, watu wa mlo mmoja nchini wameongezeka tena kwa asmilia kubwa mno...
 
Mnayosema uchumi umeshrink na inflation imepungua nashindwa kuelewa hebu tufananishe hali hii na Zimbwabwe ambapo uchumi wake umeporomoka with hyperinflations! swali la kujiuliza kwa nini vitu havipandi bei? kwa nini shs haiporomoki? serikali inapata wapi pesa? najiuliza tu
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kukua kwa uchumi tunaangalia pia purchase power kwa watu, huwezi sema uchumi unakua wakati purchasing power ya watu inapungua. Bado tuna safari ndefu
 
unakuwa?
Waziri mkuu aliulizwa juzi bungeni akasema hajui, mpaka akae na wadau na watafiti, leo hii mmeshakaa nao tayari? BOT wametoa takwimu zinazoonyesha economic activity kupungua
Dsm ndio kitovu cha biashara TZ, uchumi ukikua au kusinyaa impact yake inaanza kuonekana kwa wazi zaidi Dar, na ukiangalia hapa watu wengi wameachishwa kazi kwenye makampui ya usfirishaji, mawakala wa forodha, fastjet nao wamepunguza wafanyakazi, mahoteli yanafungwa, baa zinafungwa n.k ku refelect kuwa uchumi umeshuka
Na justification inayotolewa na Magufuli na wanaomuunga mkono kuhusu hili ni kuwa biashara nyingi zilikuwa kutokana na ukwepaji kodi na ubadhirifu wa fedha za umma hivyo Magufuli alipoingia akaondoa hivo vitu lazima uchumi utasinyaa

Leo unakuja kutuambia kuwa uchumi unapanda? kwa hiyo hizo fedha haramu mlizoondoa kwenye mzunguko zimechangia uchumi kukua zaidi? Yaani unapunguza fedha kwenye mzunguko halafu uchumi ukue??? theory ya wapi hii?

Sasa nyie mnawafanya watanzania maboya kwa kuwaambia uchumi unakuwa? na hayo mazao ya wakulima kupanda bei sijui takwimu umezitoa wapi maana watu wanauza nyanya ndoo 700, wenngine wanazilisha mifugo, mbaazi nazo zimepungua bei
Mbona mnawatukana wakulima aisee?? a

rais amesema anapambana na matajiri matokeo yake masikini ndio wanaoishia kuachishwa kazi na kushindwa kutunza familia...........Anyway most of them they deserve it

Napata hasira kumjibu mtu anayepotosha mambo kukidhi matakwa binafsi....nakujibu machache...Dar ni kitovu cha uchumi kwa uzalishaji upi zaidi ya makusanyo ya kodi nchi nzima kisha zikapata matumizi hapo? Dar ni sehemu ni kitovu cha matumizi mabaya ya pesa za umma na ndiyo kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi nitakueleza mpaka uelewe...

Dar ilikuwa mji kando ya bahari ambapo malighafi yalikusanywa Tanganyika nzima kisha yakapakizwa kwenye meli nakusafirisha ng'ambo kwaajili ya viwanda vya nchi za kikoloni...kwa hiyo mafisadi walichukua nafasi ya wakoloni wakajiwejea mifumo rasmi ya kuishi Dar kupitia ajira katika taasisi za umma na serikali kuu

Ndiyo maana kodi yote inayokusanywa 80% hutumiwa hapohapo Dar huku kukiwa hakuna hata shamba moja wala viwanda ambavyo uzalishaji wake unachangia pato la taifa kwa mlingano wa budget inayotumika kuwa service hao watumiaji wa Dar...Mh. Rais anavunja hiyo network kwakuhamisha makao makuu kutoka Dar kupeleka Dodoma...sasa Dar mpya itakuwa ya uzalishaji siyo ya wapiga dili wa makusanyo ya kodi...

Dar hiyo hiyo ambapo hakuna uzalishaji lakini kuba service sector iliyojijenga ku service cadre fulani ndipo ambapo wataalamu wote muhimu wanapoishi tena wakilipwa mishahara mikubwa huku wakiwa hawatumii taaluma yao walizozisomea lakini wamegeuka human resource officers ku attend voucher na salaries zao wenyewe...hili bado halijapatiwa ufumbuzi...

Serikali inapoambiwa ipunguze ukubwa siyo tu kupunguza mawaziri bali pia watendaji wizarani, nichukulie mfano wa wizara ya mali asili kuna wafanyakazi zaidi ya 1000 wizarani ninajiuliza kazi yao ni ipi? Hao pekee kuwa attend itamchukua katibu mkuu kutokufanya kazi za kisera na badala yake kusoma mafaili ya hao waliopo wizarani...implications tumeziona wafanya kazi hewa kila idara na wizara za serikali, thanks to electronic soft wares ambazo zimefunua yote haya...

Hii inaonyesha kuwa kuna congestion ya ajabu kwenye public offices huku kwenye grassroot kukiwa hakuna wafanyakazi wenye taaluma ambao wana deal moja kwa moja na production...hii ina implication siyo tu kwenye production lakini pia distribution of income and consumption of produced goods...Dar hakuna ndizi wala mahindi kwa maana ya vegetables na cerials huku consumer wenye purchasing power kubwa wote wako placed Dar wakati hakuna imfrastructure ya kusafirisha hizo produce Dar ili ziwafikie hao wenye sustainable income...

Matokeo ni mahindi kuozea kule Sumbawanga au kuuzwa kwa bei ya kutupwa huku kibaba cha unga Dar kikiwa sawa na bei ya gunia la mahindi Sumbawanga, hao wachumi wetu huwa wana fanya programming gani? Lakini madaktari wangekuwa mpaka vilage level badala ya wizarani, waalimu wangejaa vijijini badala ya Dar tayari hao wana salaries watakuwa consumers wa goods hukohuko rural na ile organogram ambayo huwa ni pyramid inge enhance marketing strategies....

Now look what Dar has done to constrain our economy...Fisadi anajipitishia tender anapata mtaji wa kujenga hotel, bar na supermarket zote hizo Dar then anatengeneza mfumo mwingine rasmi ili aweze kwenda rural lazima kuwe na projects na workshops tena kupitia donor hao wote ndiyo ambao wata service investments zake Dar na huku akiwaletea goods kutoka nje kuwauzia hao waheshimiwa wataalamu ambao wamejazana Dar...

Kibaya zaidi ndiyo hivyo wamekuwa mlango wa capital flight badala ya ku consume goods from our own farmers wana consume zile ambazo zina lower price kutoka nje kwa msaada wa subsidize ili kum out compete mkulima wa developing countries....Watanzania wenzangu shule tulipelekwa na Nyerere tuje kuimiliki nchi yetu siyo kuwa manyampara wa mataifa ya kibeberu....mnaudhi kupitilizaaaa!
 
Uchumi unakuwa kwenda chini hakika takwimu hazidanganyi..nchi ya giza hii mmefanya ujinga wa watanzania wengi ndo kipaombele chenu kuwandanganya

Tatizo la kukariri badala ya kuelimika.Tungewachagua wazungusha mikono wangeleta mabadiliko ya kiuchumi na kuudhibiti uchumi wetu kuliko yanayofanywa sasa na JPM? Aliyesema umekuwa hajafanya utafiti sawa, mliofanya utafiti tupeni matokeo ya utafiti wenu.Mlisimamia suala la bei ya sukari kupanda.Tajeni maeneo ambayo bado inauzwa kwa bei mliyosema iko juu sana.Je bei ya vyakula bado pia iko juu sana.

Ni kweli kuna athari kubwa kwa waliokuwa wakifaidi bia za bure,kuhonga fedha,simu za gharama kubwa,magari ya kifahari na kuwajengea nyumba malaya kwa vipato visivyoelezeka vyanzo vyake.Kwa kundi hili uchumi umedorora.Kwa wauza bia mauzo yameshuka ajabu makusanyo ya mapato ya Serikali yanapanda,zinatoka wapi na uchumi umedorora?

Kwa ustahimilivu wa bei za vitu hatuoni hasi wala chanya ya kukua kwa uchumi.Kwa wanaojadili hoja hii kwa kuangalia maslahi ya nchi tujipime tumezalisha nini cha kustahili uchumi wetu kukua? nani mwenye jukumu la kuhakikisha uchumi wetu unakuwa? je ni JPM na wasaidizi wake tu,wana CCM tu au ni jukumu letu sote? Kama ni jukumu letu sote kila mchangiaji akijifanyia tathmini yeye mwenyewe anadhani anastahili kuhoji kukua au kutokua kwa uchumi wetu?

Kila mmoja wetu ajihoji ameifanyia nini Tanzania na JPM kakwamisha wapi juhudi hizo.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kukua kwa uchumi tunaangalia pia purchase power kwa watu, huwezi sema uchumi unakua wakati purchasing power ya watu inapungua. Bado tuna safari ndefu

There is difference between purchacing power and thefty...huwezi kuniambia thief ana purchasing power kubwa...Hizo fake purchacingbpower ndicho ambacho kiliwa blind watu wengi...purchacing power ya mtanzania inaonekana kwenye GDP ukiiangalia ya Tanzania ni ndogo mno ndiyo maana tupo kwenye poorest countries lakini hiyo GDP inachangiwa na watu wachache sana kwa hivyo unapo fanya re-distri ution of wealth na pesa zinapoenda kwa watu wengi in form of service provision kama kitoa bure primary education hakuna ambaye atakuwa na hiyo purchacing power...labda useme Rais angeacha ule ujambazi in favour of the few na kuwaacha majority bila elimu wala madawati hapo utakuwa umeongea otherwise development path in njia mbili con entrate wealth to fewa leaving majority with nothing lakini kiwe na re-investments ili kukuza capital au distribute the wealth to many kwakuwa engage kwenye production na service provision then utaona kwakua GDP ni ndogo lazima hardship ya ku accumulate disposed income itakiwa dhahiri...ile ya kwanza ina advantage na disavantage zake kama ilivyo hii ya pili inategemea yupi yuko impacted zaidi...kwa sasa elites ndiyo ambao wanaumia maana kwa muda mrefu walikuwa kwenye comfort zones...kwa wakulima waliokuwa linked na mfumo wa zamani ambao walikuwa wanapata harufu wataumia lakini majority hawaoni the difference mpaka baadaye mfumo utakapo pata equilibrium yake
 
Assessment yako imeishia njiani na hivyo kufanya madai yako ya uchumi kukua kuwa ni sawa na debe tupu. Maelezo yako yamezungumzia tu upande wa serikali na ongezeko la mapato yake, hivyo basi uchumi wa serikali inawezekana kama takwimu zako ziko sahihi umekuwa. Uchumi tunaouzungmzia ni uchumi wa taifa, na kwa sababu spending power ya walaji na watumiaji, yaani watu baki ya serikali, imeshuka mno madai ya uchumi kukua ni mambo ya mizaha na propaganda za awamu ya tano.
Uchumi unakuaje wakati hautengenezi ajira mpya, uzalishaji umeshuka, bei za bidhaa zimepanda, mishahara iko pale pale au imepungua na kwa ujumla watu hawana fedha na hivyo hawamudu kufanya matumizi?
Tutumie akili jamani, ni aibu hii kutetea mambo ya hovyo kiasi hiki.
 
Tatizo la kukariri badala ya kuelimika.Tungewachagua wazungusha mikono wangeleta mabadiliko ya kiuchumi na kuudhibiti uchumi wetu kuliko yanayofanywa sasa na JPM? Aliyesema umekuwa hajafanya utafiti sawa, mliofanya utafiti tupeni matokeo ya utafiti wenu.Mlisimamia suala la bei ya sukari kupanda.Tajeni maeneo ambayo bado inauzwa kwa bei mliyosema iko juu sana.Je bei ya vyakula bado pia iko juu sana.

Ni kweli kuna athari kubwa kwa waliokuwa wakifaidi bia za bure,kuhonga fedha,simu za gharama kubwa,magari ya kifahari na kuwajengea nyumba malaya kwa vipato visivyoelezeka vyanzo vyake.Kwa kundi hili uchumi umedorora.Kwa wauza bia mauzo yameshuka ajabu makusanyo ya mapato ya Serikali yanapanda,zinatoka wapi na uchumi umedorora?

Kwa ustahimilivu wa bei za vitu hatuoni hasi wala chanya ya kukua kwa uchumi.Kwa wanaojadili hoja hii kwa kuangalia maslahi ya nchi tujipime tumezalisha nini cha kustahili uchumi wetu kukua? nani mwenye jukumu la kuhakikisha uchumi wetu unakuwa? je ni JPM na wasaidizi wake tu,wana CCM tu au ni jukumu letu sote? Kama ni jukumu letu sote kila mchangiaji akijifanyia tathmini yeye mwenyewe anadhani anastahili kuhoji kukua au kutokua kwa uchumi wetu?

Kila mmoja wetu ajihoji ameifanyia nini Tanzania na JPM kakwamisha wapi juhudi hizo.
Kumbe watanzania wananunua sukari kwa bei elekezi ya 1800/2200? Huwezi kusema ni jukumu letu sote kuukuza uchumi kama anayeongoza nchi na wasaidizi wake hawana mipango madhubuti na hawaonyeshi dalili za kuukuza uchumi wenyewe..labda wewe mwenzetu unaishi peponi siyo TZ hi,maana naweza kuwa namjibu mtu ambae yupo Denmark anabeba box
 
Katika siku za karibuni kumetokea ukosoaji mkubwa hasa kuhusu hali ya uchumi wa Nchi yetu, baadhi ya wakosoaji wakidai hali ya uchumi ni mbaya na kwamba mtaani hakuna fedha jambo ambalo lilimfanya Mhe. Rais atolee majibu hoja hii na kusema bayana kuwa wanaosema kuwa hakuna hela mifukoni ni wale ambao walikuwa wakipata fedha zao kwa njia zisizo halali.

Kauli hiyo ya Mhe Rais inakubalika na watafiti na inapewa nguvu na takwimu za mapato kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani ya Nchi. Uchunguzi unaonesha kuwa sera na staili ya uongozi wa Rais Magufuli hasa katika nyanja ya Uchumi imewavutia wawekezaji na wageni kutoka nje.

Uchambuzi unaitaja sekta ya Utalii ambayo inaiingizia Serikali takribani 25% ya fedha za kigeni, pamoja na upotoshaji mkubwa wa wakosoaji baada ya imposition ya VAT, bado kuna ongezeko la asilimia 11 ya watalii kuanzia Julai mwaka huu.

Lakini si tu kwa Utalii, bali mapato ya Nchi kwa ujumla wake yameendelea kuongezeka na hivyo kuipa Serikali fursa ya kuwekeza na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Infalation imepungua kufikia asilimia 4.9 na inashuka zaidi, maana yake ni kuwa bei za bidhaa muhimu zinazidi kushuka na bei ya mazao ya wakulima zinapanda.

Ni kama vile ujenzi wa Reli ya Kati ni utani wa kusimulia, lakini tunategemea kuiona Tanzania yenye uwezo mkubwa sana katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano ambayo itategemewa na nchi za maziwa makuu na Afrika ya Kati.

Bomba la Mafuta kutoka Uganda ni mradi ambao wakosoaji wanajaribu kuufanya uonekane kama ni upanuzi wa jengo la machinga complex, wanaficha ukweli wa nafasi ya bomba hilo katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania na maendeleo ya watu wake.

Wakosoaji, wanabeza Ununuzi wa Ndege tatu kwa ajili ya Shirika letu, tena kwa hoja dhaifu tu kuwa zimenunuliwa cash, kwanini zisinunuliwe kwa mkopo, tununue kwa mkopo ili tulipe riba maradufu. Ndege zinawasili na watanzania watanufaika na kuona matunda ya kura zao kwa Magufuli.

Kimsingi yako mengi yanayohusiana na uchumi wetu, isipokuwa TANZANIA yetu wapo WASEMAJI na WAKOSOAJI wazuri ila tunao WATENDAJI na WACHAPAKAZI wachache ambao tunajitahidi kuwavunja moyo ili mambo yasiende.

Mhe Rais wangu, Hongera kwa kazi kubwa unayoifanya kwa maslahi ya Nchi yetu na ustawi wa watu wake.
View attachment 399299
Usipende kusema wakosoaji, hakuna akosoae bila kuwa na ukweli. Kuambiwa sikukosolewa, unafikiri angefanyaje Rais ilikupambana na pesa chafu matokeo ya mapambano hayo ulitegemea uchumi kupanda juu au kushuka. Kwa vyovyote uchumi ulikuwa ushuke lazima, jambo baya ni kufukuza wateja ndilo litachelewesha kupandisha uchumi, Serikali ndy chanzo kikuu cha kusisimua uchumi inatakiwa sasa ianze kutoa pesa za miradi. Wafanyakazi ndy walikuwa wakiwaibia wateja sivema kufukuza na wateja kauli zilizokuwa zinatoka na zinazoendelea kutoka ndy adui mkubwa wa uchumi kukua.
 
Napata hasira kumjibu mtu anayepotosha mambo kukidhi matakwa binafsi....nakujibu machache...Dar ni kitovu cha uchumi kwa uzalishaji upi zaidi ya makusanyo ya kodi nchi nzima kisha zikapata matumizi hapo? Dar ni sehemu ni kitovu cha matumizi mabaya ya pesa za umma na ndiyo kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi nitakueleza mpaka uelewe...

Dar ilikuwa mji kando ya bahari ambapo malighafi yalikusanywa Tanganyika nzima kisha yakapakizwa kwenye meli nakusafirisha ng'ambo kwaajili ya viwanda vya nchi za kikoloni...kwa hiyo mafisadi walichukua nafasi ya wakoloni wakajiwejea mifumo rasmi ya kuishi Dar kupitia ajira katika taasisi za umma na serikali kuu

Ndiyo maana kodi yote inayokusanywa 80% hutumiwa hapohapo Dar huku kukiwa hakuna hata shamba moja wala viwanda ambavyo uzalishaji wake unachangia pato la taifa kwa mlingano wa budget inayotumika kuwa service hao watumiaji wa Dar...Mh. Rais anavunja hiyo network kwakuhamisha makao makuu kutoka Dar kupeleka Dodoma...sasa Dar mpya itakuwa ya uzalishaji siyo ya wapiga dili wa makusanyo ya kodi...

Dar hiyo hiyo ambapo hakuna uzalishaji lakini kuba service sector iliyojijenga ku service cadre fulani ndipo ambapo wataalamu wote muhimu wanapoishi tena wakilipwa mishahara mikubwa huku wakiwa hawatumii taaluma yao walizozisomea lakini wamegeuka human resource officers ku attend voucher na salaries zao wenyewe...hili bado halijapatiwa ufumbuzi...

Serikali inapoambiwa ipunguze ukubwa siyo tu kupunguza mawaziri bali pia watendaji wizarani, nichukulie mfano wa wizara ya mali asili kuna wafanyakazi zaidi ya 1000 wizarani ninajiuliza kazi yao ni ipi? Hao pekee kuwa attend itamchukua katibu mkuu kutokufanya kazi za kisera na badala yake kusoma mafaili ya hao waliopo wizarani...implications tumeziona wafanya kazi hewa kila idara na wizara za serikali, thanks to electronic soft wares ambazo zimefunua yote haya...

Hii inaonyesha kuwa kuna congestion ya ajabu kwenye public offices huku kwenye grassroot kukiwa hakuna wafanyakazi wenye taaluma ambao wana deal moja kwa moja na production...hii ina implication siyo tu kwenye production lakini pia distribution of income and consumption of produced goods...Dar hakuna ndizi wala mahindi kwa maana ya vegetables na cerials huku consumer wenye purchasing power kubwa wote wako placed Dar wakati hakuna imfrastructure ya kusafirisha hizo produce Dar ili ziwafikie hao wenye sustainable income...

Matokeo ni mahindi kuozea kule Sumbawanga au kuuzwa kwa bei ya kutupwa huku kibaba cha unga Dar kikiwa sawa na bei ya gunia la mahindi Sumbawanga, hao wachumi wetu huwa wana fanya programming gani? Lakini madaktari wangekuwa mpaka vilage level badala ya wizarani, waalimu wangejaa vijijini badala ya Dar tayari hao wana salaries watakuwa consumers wa goods hukohuko rural na ile organogram ambayo huwa ni pyramid inge enhance marketing strategies....

Now look what Dar has done to constrain our economy...Fisadi anajipitishia tender anapata mtaji wa kujenga hotel, bar na supermarket zote hizo Dar then anatengeneza mfumo mwingine rasmi ili aweze kwenda rural lazima kuwe na projects na workshops tena kupitia donor hao wote ndiyo ambao wata service investments zake Dar na huku akiwaletea goods kutoka nje kuwauzia hao waheshimiwa wataalamu ambao wamejazana Dar...

Kibaya zaidi ndiyo hivyo wamekuwa mlango wa capital flight badala ya ku consume goods from our own farmers wana consume zile ambazo zina lower price kutoka nje kwa msaada wa subsidize ili kum out compete mkulima wa developing countries....Watanzania wenzangu shule tulipelekwa na Nyerere tuje kuimiliki nchi yetu siyo kuwa manyampara wa mataifa ya kibeberu....mnaudhi kupitilizaaaa!
You know nothing about economics pal, i can't waste my time arguing witcha!!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
There is difference between purchacing power and thefty...huwezi kuniambia thief ana purchasing power kubwa...Hizo fake purchacingbpower ndicho ambacho kiliwa blind watu wengi...purchacing power ya mtanzania inaonekana kwenye GDP ukiiangalia ya Tanzania ni ndogo mno ndiyo maana tupo kwenye poorest countries lakini hiyo GDP inachangiwa na watu wachache sana kwa hivyo unapo fanya re-distri ution of wealth na pesa zinapoenda kwa watu wengi in form of service provision kama kitoa bure primary education hakuna ambaye atakuwa na hiyo purchacing power...labda useme Rais angeacha ule ujambazi in favour of the few na kuwaacha majority bila elimu wala madawati hapo utakuwa umeongea otherwise development path in njia mbili con entrate wealth to fewa leaving majority with nothing lakini kiwe na re-investments ili kukuza capital au distribute the wealth to many kwakuwa engage kwenye production na service provision then utaona kwakua GDP ni ndogo lazima hardship ya ku accumulate disposed income itakiwa dhahiri...ile ya kwanza ina advantage na disavantage zake kama ilivyo hii ya pili inategemea yupi yuko impacted zaidi...kwa sasa elites ndiyo ambao wanaumia maana kwa muda mrefu walikuwa kwenye comfort zones...kwa wakulima waliokuwa linked na mfumo wa zamani ambao walikuwa wanapata harufu wataumia lakini majority hawaoni the difference mpaka baadaye mfumo utakapo pata equilibrium yake

Ili tujadiliane kwa tija na kuelewana vizuri chagua lugha moja ya mawasiliano,iwe Kiwahili au kiingereza tuendeleze mjadala.Uwezo wa kununua chanzo chake kiwe thabiti na kieleweke,JPM na maamuzi yake kaathiri kipi kilichofanyika kwa haki na kwa kufuata sheria zetu ili ashauriwe.

Ni narejea kauli yangu tuna tatizo kubwa la watu kukariri na siyo kuelewa.Marekani ambayo wengi wamwkaririshwa na kuaminiishwa kuwa ni kitovu cha demokrasia na misingi sahihi ya uchumi je tunaweza kuambiana hapa jukwaani mgawanyo wa raslimali zao ukoje.Kundi gai la wamarekani linamiliki sehemu kubwa ya uchumi wao? Huu upuuzi tunaousikia kuhusu mauaji wanayofanyiaa chanzo chake nini? Marekani hakuna cha bure kwa hiyo tungetarajia kuwe na amani kubwa.Kuna mgombea mmoja analenga kujenga ukuta kuzuwia wahamiaji haramu tuambizane chanzo ni nini?

Waliotukaririsha mmojha wapo anaitwa Maslow aliorodhesha mahitaji ya binadamu katika muundo wa ngazi,hadi ngazi ya kwanza kabisa ya mahitaji ya msingi yaani malaz,mavazi na chakula ndipo tunaweza kutafuta ngazi ya pili,wengine ya tatu wengine ya nne hadi kilele cha tamaa ya binadamu.Ni imani yangu kuwa watanzania wengi ngazi ya kwanza hatujaimaliza,na hawa ndiyo wapiga kura wengi.Kwa mtumishi anayejua matakwa ya mwajiri wake atatimiza matakwa ya mwajiri wake kwanza.Kuhusiana na uchumi wetu je JPM anatimiza au anapuuza matakwa ya walio wengi Tanzania.Nina uhakika matakwa ya watawala wetu anayavuruga kisawasaw,matakwa ya vibaraka wao anayvuruga kisawasawa na hawa wana uwezo mkubwa wa kura za mitandaoni,je kura zinazoamua nani atutawale zinapatikana humu mitandaoni?

Tuelezane ukweli uchumi unakuwa eneo lipi,unashuka eneo lipi tufanye nini kutatua kwa manufaa ya wengi.Fedha za bia zimepungua lakini fedha za ujenzi wa miundombinu zinapatikana kwa walio ofisini OC haionekani lakini mishahara haikosekani.

Kwa Wakulima bado kuna tatizo mazao mengi wanazalisha hayauziki,je ni jukumu la rais tu kutatua au kuwashauri wakulima wafanye nini.Humu jamii forum hatuna watu wanaoweza kuwashauri wakulima walime nini,walime lini,wauze wapi badala ya kulima na kuzalisha kwa wingi ndipo waulize soko.Kama tupo humu ambao hatuoni kuwa kuwa huu ni wajibu wetu kwa nchi yetu je tumeelimika au tumejaza vyeti vya kutafutia ajira.

Nitatoa mfano mmoja unaoonyesha kiwango cha ujinga wetu na bado tunasubiri serikali itatue.Tanzania inazalisha machungwa kuliko Kenya lakini Kenya inasafirisha machungwa mengi nje ya Kenya kuliko Tanzania,machungwa hayo yananunuliwa Tanzania (Muheza inaongoza) tujiulize je ni jukumu la Serikali kuhakikisha fursa hii hatuwaachi wakenya?

Mnisamehe yawezekana akili yangu ni mbovu maana inaamini kuwa wengi wetu tumekariri hatujaelimika tunasubiri baba afanye kila kitu sisi tle tu.Ninahesabu kuwa ukiwa ni miongoni mwa akina baba hao una hasara kubwa.
 
Kukaribisha Demokrasia ni kuchelewesha maendeleo ya wananchi. tujiulize je watanzania wanahitaji nini?? Demokrasia au wanahitaji kuona kuna elimu bora? huduma za afya bora? huduma za usafiri bora? huduma za maji bora? Demokrasia ije baada ya hivyo vyote kupatikana
Vyote hivyo havina maana kama utakuwa umefungwa kifikra.
 
Kumbe watanzania wananunua sukari kwa bei elekezi ya 1800/2200? Huwezi kusema ni jukumu letu sote kuukuza uchumi kama anayeongoza nchi na wasaidizi wake hawana mipango madhubuti na hawaonyeshi dalili za kuukuza uchumi wenyewe..labda wewe mwenzetu unaishi peponi siyo TZ hi,maana naweza kuwa namjibu mtu ambae yupo Denmark anabeba box

Kwa hiyo nyumbani kwa baba na mama yako kama ulikuta uwezo wako ni kujenga nyumba ya miti na makuti huwezi kufanya zaidi yao.Uchumi wa nchi uanategemea uwezo wa kila mmoja wetu,jukumu la kukuza uchumi wa kila mmoja wetu ni la kila mmoja wetu.Tuelezane humu jukwaani wapi JPM analikoroga kuhusu uchumi wetu ashauriwe tusitegemee ushauri wa wageni tutakuwa siyo wajinga bali wapumbavu.Hakuna mzungu mwenye akili timamu atakayetupa maarifa ya kushindana naye au kumshinda.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Usipende kusema wakosoaji, hakuna akosoae bila kuwa na ukweli. Kuambiwa sikukosolewa, unafikiri angefanyaje Rais ilikupambana na pesa chafu matokeo ya mapambano hayo ulitegemea uchumi kupanda juu au kushuka. Kwa vyovyote uchumi ulikuwa ushuke lazima, jambo baya ni kufukuza wateja ndilo litachelewesha kupandisha uchumi, Serikali ndy chanzo kikuu cha kusisimua uchumi inatakiwa sasa ianze kutoa pesa za miradi. Wafanyakazi ndy walikuwa wakiwaibia wateja sivema kufukuza na wateja kauli zilizokuwa zinatoka na zinazoendelea kutoka ndy adui mkubwa wa uchumi kukua.

Nisamehe ndugu yangu kwa ujumbe ninaokupa sasa ni ukweli utakaokuudhi.Ni upuuzi kutegemea serikali itoe fedha kwa watu wake ili maendeleo yaje.Ni ndoto za Abunuwas hazijawahi kufanikiwa poipote duniani.Tunahitaji maarifa ya kila mmoja wetu,serikali iandae mazingira rafiki tu.Moja ya kasoro kubwa ianyoendelea kufanywa na Serikali kwenye uchumi ni kuwagawia watu(maskini/fukara) fedha za bure hazitawasaidia ila zitawapumbaza.Huo ndiyo ukweli mchungu.
 
Back
Top Bottom