Nashukuru katika maelezo yako unakili kuwa serikali ni kikwazo kwa wakulima,ulivyozungumza upo sahihi sasa nataka unisaidie kujibu kwa mkulima mdogo ambae amelima nyanya na mbaazi kwa pesa ya mkopo wa Viccoba halafu bei yake ni sawa na kutoa bure hiyo bidhaa kwa mteja tokana na gharama alizowekeza hapo,anarejeshaje hiyo pesa? Ambayo itamfanya alime tena kwa ajili ya soko la desemba ambalo Unadai ni zuri kuliko la sasa
Hujaelewa ama hujataka kuelewa.Wapi nimekiri kuwa serikali ni kikwazo kwa wakulima? kwenye kilimo cha nyanya serikali inahusikaje ulime lini,kiasi gani na uuze wapi? Kilimo ni biashara,yeyote anayetegemea kuambiwa auze wapi na auze lini biashara haimfai.
Kabla hujakopa jiulize nakwenda kufanyia nini mkopo huu,nitakachozalisha/kununua nitauza wapi? lini nitauza.Hivi Bakhresa,Mengi,Dewji wanaambiwa na Serikali uza huku ,wakati hu na kwa bei hii.
Tuna tatizo la kukariri.Kuna kpindi cha Mwalimu Christopher Mwakaseghe kinendelea kuanzia jana japo anaeneza habari za imani yake kuna eneo anagusa maisha halisi ya maisha ya kiuchumi na wajibu wa maendeleleo ya kila mtu "maana aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo".
Ninakushauri ukifuatilie sehemu kubwa ya mjadala huu yaweza kwisha.
Kwa wanaoona kusaidiwa ni suluhisho ya matatizo yao watasubiri kusaidiwa