Uchumi unakua, takwimu hazidanganyi

Uchumi unakua, takwimu hazidanganyi

Sisi wakulima tuliojenga nyumba za makuti tunaishi kwa nguvu za mungu tumelima mazao yamekuwa mengi kuliko soko la ndani tulitaka kuuza nje serikali chini ya Magufuli ikapiga stop mazao yakaanza haribika ndipo serikali inakuja kusema tumefungua mipaka mje mchukue vibali..kwa akili yako mimi mkulima nitapandisha uchumi wa nchi hi kwa mazao yaliyoharibika? Je serikali hawakuona tatizo walipoambiwa mpaka washtukie bidhaa zinaharibika ndo waruhusu?

Hapo umeongea hoja inayoweza kuleta mjadala wenye tija.Ninaomba nikuulize ulilima zao gani au unawakilisha wakulima wa zao lipi? Katika eneo hili wataalam wetu wa uchumi na wa masoko wameonysha udhaifu mkubwa.Bahati mbaya wakulima wetu wengi wanategemea serikali iwasaidie kupata masoko.

Kwa kuwa tumeamua mfumo wa ubepari utawale japo katiba yetu haisemi hivyo na hamna anayelalamika,ukulima ni biashara.Mfanyabiashara lazima ajue atauza wapi hata kabla hajazalisha.Ajiulize nitashindana na nani ? mbinu gani nitatumia kushinda?

Tumeng'ang'ania kulima mazao tulioelekezwa na waliokuwa watawala wetu.Dunia inahitaji zaidi ya mazao hayo; kwa kuwa tulikariri badala ya kuelewa tunaendelea na mazao yaleyale kwa mbinu zilezile.Wapo wachache kati yetu wameanza kushtukia ujinga huu.Fuatilia AMAGRO wanafanya nini na niambie kama wana malalamiko yoyote kuhusu serikali na masoko.Tusiishie kulalamika tutaue matatizo yetu,tujivunie vilivyo vyetu.Mafanikio hayaji kama mvua huhitaji malengo,utekelezaji,uvumilivu na ndipo tufaidi.
 
uchumi unakua kwa wana ccm wezi ila sio kwa watanzani..hz tafiti za mezani pelekeni huko
 
Rais kasema kuwa pesa hakuna kwa sababu watu wamezificha uvunguni, au Rais hakuona hizo takwimu zako?
 
Hapo umeongea hoja inayoweza kuleta mjadala wenye tija.Ninaomba nikuulize ulilima zao gani au unawakilisha wakulima wa zao lipi? Katika eneo hili wataalam wetu wa uchumi na wa masoko wameonysha udhaifu mkubwa.Bahati mbaya wakulima wetu wengi wanategemea serikali iwasaidie kupata masoko.

Kwa kuwa tumeamua mfumo wa ubepari utawale japo katiba yetu haisemi hivyo na hamna anayelalamika,ukulima ni biashara.Mfanyabiashara lazima ajue atauza wapi hata kabla hajazalisha.Ajiulize nitashindana na nani ? mbinu gani nitatumia kushinda?

Tumeng'ang'ania kulima mazao tulioelekezwa na waliokuwa watawala wetu.Dunia inahitaji zaidi ya mazao hayo; kwa kuwa tulikariri badala ya kuelewa tunaendelea na mazao yaleyale kwa mbinu zilezile.Wapo wachache kati yetu wameanza kushtukia ujinga huu.Fuatilia AMAGRO wanafanya nini na niambie kama wana malalamiko yoyote kuhusu serikali na masoko.Tusiishie kulalamika tutaue matatizo yetu,tujivunie vilivyo vyetu.Mafanikio hayaji kama mvua huhitaji malengo,utekelezaji,uvumilivu na ndipo tufaidi.
Mimi nawakilisha wakulima wa nyanya,matikiti,bamia,mbaazi na viazi Mviringo(maarufu kwa chipsi)..kwanza hapo kwenye wakulima kuwa tunaitegemea serikali kutafuta masoko si kweli mbona miaka tunatafuta wenyewe na wachuuzi toka nchi za jirani huwa wanakuja kununua ila serikali ilichofanya wao ndo wanakuwa wananunua mazao kwa mkulima halafu ndo wanakuwa ma agent wa wakulima katika kuwauzia mazao yao kwa hao wafanyabiashara na bei ya kuwauzia serikali ndo wanapanga..matokeo yake wanakopa kulipa ni tatizo vilevile uwezo wa kununua mazao yote wao wenyewe hawana uwezo sababu bidhaa ni nyingi kushinda wahitaji wa ndani sasa kama wangefungua mipaka mbona wakulima tusingelialia na mazao kuharibika..safari hi wameruhusu kwa kutupa vibali tuuze nje ila wakati huo mambo yashaharibika na kutokana na baadhi ya wabunge kupiga kelele
 
Uchumi unaporomoka - sekta ya Usafirishaji ukuaji katika miezi Sita ya kwanza ya Rais wa Awamu ya Tano -7% ( BoT na NBS data )

Kasi ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji imeporomoka kutoka kukua kwa 14.50% robo ya mwisho ya 2015 mpaka kukua kwa 7.9% robo ya kwanza ya 2016, ikiwa ni kuporoka kwa 7% katika kipindi cha miezi 6 tu ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli. Kuporomoka kwa sekta ya usafirishaji itaathiri watu wengi, wakiwemo madereva, matingo, pamoja na mama Ntilie wanaowauzia chakula.

Juzi Wakati wa Ziara ya Kamati ya Bunge Bandarini, Angelina Ngalula (Mwenyekiti wa TATOA - Umoja wa Wamiliki wa Malori ya Usafirishaji Mizigo Nchini) akifafanua Athari za kupungua Kwa Mizigo Katika Bandari ya Dar Kwa Dkt Dalaly Peter Kafumu alisema yafuatayo;

"TATOA (Umoja wa Wamiliki wa Magari ya Kusafirisha Mizigo Nchini) unamiliki Wastani wa Malori 23,000 Kwa sasa. 60% ya Malori Husika Kwa sasa hayafanyi kazi Kabisa Kwa Sababu ya Uhaba wa Mizigo Bandarini.

Kila gari Moja hutumia Wastani wa Lita za Mafuta 2000 kutoka Bandari ya Dar es salaam Kwenda Burundi, Zambia ama DRC. Ambapo Magari yote 23,000 hutumia Lita Milioni 46 Kwa Safari Moja katika Nchi Tatu Hizo, Na Serikali hukusanya Shilingi 650/- Katika Kila Lita Moja ya Mafuta Kama Kodi.

Kwa Msingi Huo Ukifanya Mahesabu Utaona Athari Za kushuka Kwa Mizigo Katika Bandari ya Dar zinavyosambaa Kutoka Bandarini, Kwenda TRA, Kisha Kwa TAFFA (Umoja wa Mawakala wa Mizigo Nchini), kuja kwetu TATOA, Kwenda TASAA (Umoja wa Mawakala wa Meli Nchini) mpaka Kwa ICDs (Umoja wa Wamiliki wa Bandari Kavu Nchini)".

Kauli Hii ya Mama Ngalula Ndiyo Kielelezo Cha dhahiri Kabisa Juu ya Kushuka Kwa kasi Kwa Sekta ya Usafirishaji Nchini.
 
Wana Jamii forum Mimi sio mwana siasa lakini nadhani miezi kadhaa mbele twaweza pata Tanzania mpya. Acha mkuu aendelee kubana tuone mwisho wake
 
Naona hii mada imekuwa tamu. Hata hivyo imekuwa na changamoto za usiasa kama ilivo kawaida. Watu wakikosoa kidogo wanaitwa "wazungusha mikono". Hivi tukubaliane katika kila jambo tutaendelea kweli?. Wengine wakisapoti wanaitwa "buku 7" hivi tutofautiane katika kila kitu tutashirikiana kweli? Tuweke siasa kando na tujikite kwenye hoja, uchumi umekuwa au la? Nami niseme machache kidogo.

1: Kuna wakatai humu watu pia wanachanganya kati ya pato la taifa (GDP) na mapato ya serikali (gvt revenue). Kuongezeka kwa makusanyo ya mapato ya serikali kila mwezi sio sawa na kuongezeka kwa ukuaji wa uchumi. Mapato haya yanaweza kuongezeka kwa kuwakamua watu zaidi kwa vipato vyao vile vile. Kwahiyo tusijifariji kwamba kwakuwa mapato yanaongezeka then uchumi wetu unakua.

2: Ukuaji wa uchumi unaweza usiwe na athari katika kuboresha maisha ya watu hasa wa tabaka la chini. Kumekuwa na ukuaji mkubwa wa uchumi tanzania lakini ubora wa maisha ya watu haujaimarika kwa kiasi hicho. Hili limeshaelezwa sana kuwa moja ya sababu kubwa kabisa katika hili ni ukuaji wa sekta ambazo sio shirikishi sana. Sekata za usafirishaji, ujenzi, madini na mawasiliano zimekuwa sana lakini sehemu kubwa ya mapato hayo hayaendi kwa watanzania walio wengi kwakuwa zinamilikiwa na kwa kiwango kikubwa na wageni. Hili linatusaidia kuelewa uhusiano uliopo kati ya uj

3: Mfumuko wa bei unatueleza juu ya "stability" za bei za bidhaa na huduma na sio kipimo tosheleza cha ukuaji wa uchumi.

4: Kuna ukuaji wa uchumi halisi (Real economic growth) na ukuaji wa uchumi kabla ya kutoa athari za mfumuko wa bei (Nominal economic growth). Ili tuseme uchumi halisi umekua ni lazima vitu vilivo zalishwa kwa mwaka husika viwe vingi kuliko vilovozalishwa kwa mwaka ulotangulia. Mathalani, kama nchi inazalisha mahindi tu, ili uchumi ukue ni lazima kiwango cha mahindi kilicho zalishwa mwaka huu kiwe kikubwa kuliko cha mwaka jana. Thamani ya mahindi mwaka huu inaweza kuwa kubwa kuliko mwaka jana sio kwasababu mahindi ni mengi bali inaweza kuwa kwasababu bei za mwaka huu zimeongezeka kuliko mwaka jana. Kwahiyo ukuaji halisi (real economic growth) unaweza kuwa mdogo sana.

5: Sasa pato la taifa linaweza kupungua kwasababu viashiria vyake vyingi vimepungua. GDP= matumizi ya watu(kaya) kwa vitu na bidhaa + uwekezaji wa sekta binafsi + matumizi ya serikali + kinachobaki baada ya kuchukua thamani ya vilivo unzwa nje ukitoa vilivo nunuliwa kutoka nje. (GDP = C +I +G +(X-M)). Sasa hapa ukiangalia uwezo wa manunuzi kwa bidhaa na huduma unaofanywa na watu umepungua, Uwekezaji umepungua (rejea benki kusitisha mikopo ambayo ingetumika kuwekeza) matumizi ya serikali yamepungua ila hapo kwenye (X-M) nahisi patakuwa pameongezeka. Je ongezeko la (X-M) linaweza fidia kupungua kwa hizo "variables zingine"? Makampuni na baishara kadhaa zimeelezwa kufungwa, hapo watu wamepoteza ajira, kipato na mwisho wa siku pato la taifa pia linapungua. Wale mnakataa kuwa hili halijatokea tusaidieni na sisi tuelewe hili limekaaje?

6: Wale wanaojikita kwenye hoja ya kuwa tujiulize sisi wenyewe tumefanyaje na sio kuingalia serikali imetusaidiaje kuna vitu vingi wanasahau. Je sera anatengeneza nani? Serikali ilipiga marufuku kuuza ngozi nje, madhara yake ngozi zikaoza watu wakapata hasara na kulalamika, je tusiilamu serikali kwa mazingira hayo?
Wakati Mh JPM anatoa sababu za kutosaini EPA alisema wazi kuwa wakulima wetu hawawezi shindana na wakulima wa nje wanaopata ruzuku kutoka kwenye serikali zao, Je hapo unataka tusiiulize serikali yetu inatusaidiaje nasisi wakulima ili tushindane na wenzetu?

Ahasnateni.
 
Nimepitia post nyingi sana,zinazo jadili hali halisi ya uchumi nchini mwetu hivi sasa.
Takwimu zote zinaonyesha kushuka kwa uchumi,na maoni ya wengi wamesema hali ya maisha imekuwa ngumu.
Nimeona nijihakikishie mwenyewe kwa kupitia mijadala mingine humu,mfano kilimo na ufugaji.
Ktk kilimo na ufugani napo pana changamoto zifuatazo kiufupi.
-bidhaa zimekuwa nyingi sana na bei kushuka kwa kukosa wanunuzi. Nimeingia kwa kina ktk hii habari,nimegundua ya kuwa serikali imezuia kuuza bidhaa nje ya nchi hadi kibali.
Kwa hiyo uuzaji wa bidhaa nje kwa wingi umethibitiwa,bei imeshuka,wananchi wa kipato cha chini wanakidhi bei. Wafanya biashara wameathirika kwa kupata faida kidogo kulinganisha na hapo awali.
- Nimepitia tena ktk mifugo,mayai trei ilikuwa 8000 na sasa imefika hadi5000.
NAOMBA MNIELEWESHE UCHUMI UKISHUKA NA BIDHAA HUSHUKA BEI? AU HIZO TAKWIMU WAMEKOKOTOA VIPI.
Natanguliza shukran
 
Kwa mpumbavu demokrasia haina maana ,yeye anafikiri demokrasia ni kwenda kupiga kura!!
 
Mimi nawakilisha wakulima wa nyanya,matikiti,bamia,mbaazi na viazi Mviringo(maarufu kwa chipsi)..kwanza hapo kwenye wakulima kuwa tunaitegemea serikali kutafuta masoko si kweli mbona miaka tunatafuta wenyewe na wachuuzi toka nchi za jirani huwa wanakuja kununua ila serikali ilichofanya wao ndo wanakuwa wananunua mazao kwa mkulima halafu ndo wanakuwa ma agent wa wakulima katika kuwauzia mazao yao kwa hao wafanyabiashara na bei ya kuwauzia serikali ndo wanapanga..matokeo yake wanakopa kulipa ni tatizo vilevile uwezo wa kununua mazao yote wao wenyewe hawana uwezo sababu bidhaa ni nyingi kushinda wahitaji wa ndani sasa kama wangefungua mipaka mbona wakulima tusingelialia na mazao kuharibika..safari hi wameruhusu kwa kutupa vibali tuuze nje ila wakati huo mambo yashaharibika na kutokana na baadhi ya wabunge kupiga kelele

Umetoa hoja nzuri ila kwa nadharia zaidi.Kwa mazao uliyotaja yaani nyanya,matikiti,bamia,mbaazi na viazi mviringo.Nitachangia hali halisi isipokuwa kwa mazao mawili mbaazi na viazi mviringo ambayo sina uhakika mkamiliofu wa changamoto zake.

Kwa nyanya,matikiti na Bamia yana changamoto na fursa zinazofanana sokoni.Nina uzoefu wa kulima zao la nyanya kwa zaidi ya miaka 30.Nimeanza kulima nikiwa sina mtaji kabisa.Ninawafahamu kwa sura na majina wakulima halisi na waliofaidi kwa zao hili.

Mazao haya yanawaumiza sana wakulima wanapolima bila kujiuliza nilime lini.Kwa waliopo Mkoa wa Mbeya,Tanga na Morogoro watakuthibitishia kuwa historia inaonyesha kuwa kwa kawaida nyanya inayouzwa kuanzia mwezi Disemba kuishia Mei ina uhakika wa soko.

Kwa mwenye mtaji mdogo ni gharama kubwa kuzalisha nyanya itakayovunwa miezi hiyo kwa Mikoa hiyo.Gharama kubwa zipo kwenye umwagiliaji na udhibiti wa wadudu.Kwa bahati mbaya sana Serikali( na siyo wanasiasa bali wataalam) wameonyesha udhaifu mkubwa katika udhibititi wa viatilifu.

Nyanya kipimo kinachouzwa kati ya Sh. 500-1500 kwa sasa kiliuzwa Sh. 25000 kwa mikoa hiyo kwa muda ninaokutajia.Jiandae kufuatilia bei ya nyanya itakuwaje kuanzia Disemba-Mei kwa mikoa niliyokutajia halafu nipe mrejesho.

Niliyoyasema kwenye nyanya yapo kwenye matikiti na bamia.Kwa Mkoa wa Tanga kabla ya mwezi wa saba mwaka huu debe moja la bamia liliuzwa na mkulima kwa bei ya Sh.10,000/= na 15,000/=, sasa hivi limeteremka hadi kufikia Sh.5,000/=wa debe.Kama upo Mkoa wa Tanga jiandae kupanda bamia utakazovuna kuanzia mwezi Januari hadi Machi kisha tupe mrejesho wa bei.

Kwa mazao niliyoyataja sina uhakika kama serikali imehusika kupanga bei au kuzuwia masoko.Kama kuna kiongozi yeyote amefanya hivyo hakushauriwa vizuri na ni upuuzi kuzuwia mazao usiyowapa msaada wowote wazalishaji wala hulipi fidia endapo soko linashuka chini ya gharama za mzalishaji.Hatujaandaa kuongeza thamani ya mazao hasa jamii ya mbogamboga hivyo hatuna sababu ya kuzuwia yasiuzwe popote.

Kwa mkulima makini na Serikali ikidhamiria kuhimiza kilimo bila kutumia nguvu kubwa bali mahitaji ya soko yaamue iruhus na ihamasishe uuzaji wa mahindi mabichi.Kwa sasa yanalipa kuliko kusubiri yakauke.Wazalishaji wakiwa wengi bei ya mahindi mabichi sokoni itatelemka na mahindi mengi yataachwa yakauke,hatutakuwa na njaa.

Kwa Serikali ninashauri mambo mawili kwenye kilimo waruhusu mkulima azalishe nini na auze anapotaka bila kumzuwia.Kuna vyombo vinatetewa ili vinunue mazao ya wakulima havina uwezo wa mbinu,masoko ,mitaji wala uadilifu wa kuachwa vifanye kazi hiyo vyenyewe,acha vishidane na wanunuzi wengine.Njia ya pili kama ya kwanza haifai serikali itoe ruzuku kwenye pembejeo zote za kilimo na kufidia bei inapokuwa chini ya gharama za uzalishaji.Ndivyo wanavyofanya wanaotudanya wanaoshawishi soko huru kwenye nchi zao.
 
Nashukuru katika maelezo yako unakili kuwa serikali ni kikwazo kwa wakulima,ulivyozungumza upo sahihi sasa nataka unisaidie kujibu kwa mkulima mdogo ambae amelima nyanya na mbaazi kwa pesa ya mkopo wa Viccoba halafu bei yake ni sawa na kutoa bure hiyo bidhaa kwa mteja tokana na gharama alizowekeza hapo,anarejeshaje hiyo pesa? Ambayo itamfanya alime tena kwa ajili ya soko la desemba ambalo Unadai ni zuri kuliko la sasa
 
Juliana Shonza, Gazeti kubwa kama Citizen ni kijarida cha mtaani?

Issue siyo ya makamanda, vipi wegine tusiokuwa makamanda? Wanasiasa pigeni siasa zenu, mambo ya kitaaluma waachineni wenyewe.

Suala langu kubwa ni maneno yenu wanasiasa kama TandaleOne; analeta za kwake na magazeti ama Citizen with quote from BOT officials wanasema uchumi unapungua. Tumuani nani.....
 
kuna faida gani uchumi kukua halafu wananchi wanateseka.hizi ndo sifa kama za wakenya kujisifia uchumi uko juu wakati majority wanateseka na umaskini huko kibera na mathare
wanainch wanateseka... ni kweli lakin mateso yanapungua ukilinganisha na zamani.
sasa wanainch wanapeleka watoto wao shule bila kulipa ada.

sasa umeme unawafikia hadi vijijini, nikiri kijijini kwetu sikuwahi kufikiri kama kutakuwa na umeme. lakin leo hii naandika hapa umeme umefika miez 2 iliyopita. na ile solar tulomwekea mama tunampango wa kuong'oa. maana umeme ni wa uhakika.

sasa wanainch wanapata huduma za afya kijijini, sikutegemea kama kwetu pale tutapata zahanati, lakin mwaka jana imefunguliwa na akina mama wanajifungua pale bila shida.

huduma za simu, naongea na mama yangu kila mara bila shida. zamani mpaka aende parokiani mjini ndo uongee naye sijui kwa redio nk.

usafiri ndo usiseme.. akitaka kwenda mjini anaita boda boda analipa 3000 anafika mjini, zamani pikipiki ilikuwa ya padre tu na bwanashamba wa wilaya.

maji safi ndo usiseme.. bomba lishawekwa bado kufungulia maji tu. na hata hivo walisubiri umeme waweze ku pump maji kwenye tank. soon yata flow.
secondary ipo mita 200 kutoka nyumbani, mimi nilisoma secondary km 7 toka nyumbani. hata hivo nafasi zilikuwa chache nilichaguliwa mmoja tu kati ya wanafunzi 54 tuliomaliza darasa la saba.. back in 1996. leo hii shule ya msingi zaidi ya nusu wanahamia secondary. na secondary hiyo hiyo ishatoa more than 20 graduates. thanks to LOWASA kwa kusimamia vema ujenz wa secondary hizi.

yapo mengi mengi mengi...... na sio kijijini kwetu tu, hata vijiji jirani wameendelea hata zaidi ya kijiji chetu.

sikatai unaposema bado wanateseka, kwa sababu tunahita hayo waliyoyaleta yawe bora zaidi. lakin ukweli tuseme maisha yamekuwa bora ukilinganisha na miaka 15 iliyopita. kwa reference ya kijijini kwangu.
 
Unajua demokrasia au unabwabwaja tu, au unadhani demokrasia ni kufanya uchaguzi tu? rudi shule ukasome uraia
Kwani watanzania wanahitaji nini?? Demokrasia au Elimu bora, huduma za afya ,maji na uchumi bora?? au kwako demokrasia ni kuandamana na kupinga kila kitu. Ufahamu wako kuhusu nin I watanzania wanahitaji bado mdogo rudi kawasome watanzania wanahitaji nini
 
Vyote hivyo havina maana kama utakuwa umefungwa kifikra.
Fikra haziwezi kufunguka kama jamii haiwezi kupata elimu bora na kuboresha afya kwa ajili ya ufikiri peveu. Watu wenye njaa hawwezi kufikiri sawa zaidi zaidi watakuwa watwana na bendera fuata upepo ilimradi tu wapewe mlo wao
 
Una haki ya mawazo yako kama vile mimi nilivyo na haki na mawazo yangu.
Ukipata vyote vilivyotajwa kama umefungwa kifikra haisaidii.
 
Kwani watanzania wanahitaji nini?? Demokrasia au Elimu bora, huduma za afya ,maji na uchumi bora?? au kwako demokrasia ni kuandamana na kupinga kila kitu. Ufahamu wako kuhusu nin I watanzania wanahitaji bado mdogo rudi kawasome watanzania wanahitaji nini

Demokrasia ni ushirikishwaji watu katika kufanya maamuzi, siyo unakurupuka huko unafanya mambo ambayo kichwa chako kinakutuma. Bila ushirikishwaji watu hata hayo mambo unayotaja hayatafanyika kwa kuwa hutajua vipaumbele vya watu. Demokrasi ni neno pana sana na haliishii tu shule dawa na hayo mambo madogo uliyotaja
 
Back
Top Bottom