Uchumi umekua, wananchi wana/wataendelea kuwa maskini," Aina gani hii ya uchumi isiyo na tija kwa mwananchi?

Mbogi

JF-Expert Member
Oct 10, 2021
681
825
Katika taarifa ya ripoti ya utafiti wa REPOA unasomeka kwamba uchumi wa nchi yetu unakua kwa kasi lakini nao umaskini wa wananchi unaongezeka kwa kasi.

Hoja yangu ni kwamba huu uchumi usio na manufaa kwa wananchi unatengenezwa na nani na kwa manufaa ya nani?

Niombe msaada wa elimu kwa wataalam wa uchumi lakini pia na mifano ya nchi zinazopiga/ zilizopiga hatua zikiwa na aina hii ya uchumi.

Kwetu tusio na elimu ya uchumi hatuoni matumaini wala ahueni ya maisha kwa kusikia ripoti hii.

Serikali inawezaje kuona na kufurahia aina hii ya uchumi huku wimbi kubwa la wananchi wakisalia ktk dimbwi kubwa la umaskini namna hii?
 
On now. Kama wewe una mku.................... Ba l Sa. .m
A
Aiseeeee jalibu kukwepa hiyo laana. Ni laaaaaana tosha
 
Maana yake uchumi unakua miongoni mwa watu wachache pekee! (Wapiga dili, mafisadi, wanasiasa, wala rushwa, wageni, nk)

Wananchi wa kawaida wataendelea kuteseka iwapo tutaendelea kuwakumbatia hawa wahuni wa ccm.
 
Maana yake uchumi unakua miongoni mwa watu wachache pekee! (Wapiga dili, mafisadi, wanasiasa, wala rushwa, wageni, nk)

Wananchi wa kawaida wataendelea kuteseka iwapo tutaendelea kuwakumbatia hawa wahuni wa ccm.
Duu! Hapa naanza kukuelewa. Sasa kama ndivyo hivi kuna haja gani ya wananchi kuendelea kuchagua serikali isiyojali uchumi wa wananchi walio wengi.
 
Back
Top Bottom