Uchumi jumuishi Tanzania sio rahisi kufikiwa na wananchi wote

Bando la wiki

JF-Expert Member
May 23, 2023
314
875
Naionea sana huruma nchi yangu ya Tanzania hasa wananchi wake ambao majority wanazama kwenye lindi la umaskini mkubwa.

Sababu kubwa ya umaskini kwenye taifa hili, zipo nyingi ila kubwa kupita zote ambayo nitaielezea hapa ni; WIZI, UFISADI NA RUSHWA.

Yaani nchi itakuwa na rasilimali za kutosha kama ilivyo nchi yetu iliyobalikiwa wingi wa rasilimali kama madini, gesi, ardhi, misitu, hifadhi za wanyama, fukwe za bahari na maziwa lakini kwa tamaa za viongozi wetu hizo zawadi zote tulizopewa na Mungu hazitakuja kuwanufaisha watanzania wengi bali kikundi cha watanzania wachache (wanasiasa).

Hapa nchi inatengeneza tatizo lingine nchi hii kila mtu kuwaza kuwa mwanasiasa, ndio maana maprofesa wanaacha kazi ya kunoa wanafunzi wa vyuo wanakimbilia kwenye siasa.

Wizi, rushwa na ufisadi vimetamalaki awamu hii, kila eneo unalogusa unasikia kuna upigaji huko. Kibaya zaidi wanasiasa wa Tanzania wanaolindana, mtu anaiba hapa hawajibishwi anahamishiwa wizara au idara nyingine akaendelee kuiba.

Duuh hii imaitia uchungu sana, yaani mwizi wa Kuku mtaani anawajibishwa ipasavyo lakini mawaziri wezi wa Mabilioni ya maskini wa Tanzania wanaachwa wanakenua meno tu wakipongezena kwa wezi wanaowafanyia watanzania.

Hii sio sawa kwa mamlaka zinazoendelea kuwapa uteuzi watu hao. Shida ni kwamba WIZI, UFISADI NA RUSHWA kwa Tanzania huanzia ofisi ya mkuu hadi kwa mtendaji wa kijiji hivyo hakuna wa kumfunga paka kengele lakini mimi niwatahadharishe wezi na mafisadi wa Tanzania kila jambo huwa lina mwanzo na mwisho wake, lakini mwisho wake huwa unakuja kwa aibu na fedheha kubwa sana.

Kitu kinachoumiza watanzania wengi ni kutokufanyiwa kazi kwa ripoti za CIG huku kila jambo likiwa limeelezwa humo ndani.

Uchumi jumuishi ni ule ukuaji wa uchumi unaotembea (kukua) pamoja na mabadiliko (maendeleo) ya wananchi walio wengi. Sasa uchumi huu hauwezi kufikiwa kwa wote kwa sababu kile kilichopaswa kuwafikia wananchi wengi kunapunguzwa na mafisadi wachache wanajiwekea kwenye hazina zao hasa nje ya nchi ambapo ufisadi wao hauleti impact kwenye uchumi wa nchi bali unafaidisha nchi walikokwenda kuficha pesa (mitaji) hizo.

Ni bora basi mafisadi wa Tanzania, pesa hizo muwekeze nchini hasa viwandani ambapo vijana wengi watapata ajira kuliko kwenda kuficha pesa hizo nchi za nje.

Mafisadi muwe na huruma na maisha ya watanzania, wanashinda juani kuwapigia kura lakini mkishapata nafasi hizo mnageuka miungu watu. Wanawalipia kila kitu hadi umeme, usafiri, maji, semina, malazi n.k lakini mnaona hiyo hisani haitoshi mnaanza kuwaibia hata kile kidogo walichonacho kwa kuwaongezea "Double taxation" yaani mnapandisha kodi, mnaongeza Tozo, mnapandisha ushuru yaani nchi hii ni taflani.

Hata kama nchi hii itakuwa na sera nzuri za uchumi jumuishi na uwekezaji ila kama hakutakuwa na sera nzito za kupambana na wezi na mafisadi nchi hii, bado kama nchi tutakuwa tukipiga Mark time huku nchi ndogo ki uchumi zikitupita na kutushangaza sisi tuliobalikiwa kuwa na rasilimali za kila aina.

Sheria ngumu na zito kama kwenda jela na kuwafilisi mafisadi na wezi wa mali za umma bila kupepesa macho wala kuogopa mtu na cheo chake hata kama alikuwa Rais wa nchi nadhani kunaweza kutupa suluhisho la muda mrefu kwa hiki kizazi cha viongozi tulionao wanaoona njia nzuri ya kuendelea kudumu madarakani ni kuandaa watoto wao kurithi wizi na ufisadi katika vitengo wanavyo vijua wao huko serikalini kama kichaka cha kuchotea pesa za umma.
  • Mwananchi una maoni gani namna ya wananchi wengi nchi hii kufikiwa na keki ya taifa huku tukipunguza umaskini kwa kaya nyingi nchini Tanzania.
  • Na pia ni kwa namna gani kama taifa tushughulike wezi na mafisadi Tanzania maana huyo ndo mchawi wetu.
 
Back
Top Bottom