Uchumba wa muda mrefu umenichosha

Uchumba wa muda mrefu umenichosha

Umetumika sana yani tangu sijamaliza Olevel hadi leo na mimi natafuta mke we bado unapigwa mechi za kirafiki tu? Hujafika miaka 45 kweli?
 
Kumbe umeolewa shida yako ni kwenda kuwaringishia watu kanisani?🤣🤣🤣🤣
Yes, kimila dada ameshaolewa ila yeye anataka akapige picha.

Jamaa anamcheki tu, mtu anakaa nae, anahudumiwa na kasema mpaka familia yake inahudumiwa, ila haoni thamani yake analilia ndoa ya picha picha za kupost.

Kunz wenzie wana hizo za kanisani, hawapati huduma nzuri.
 
Binafsi niko kwenye uchumba tangu mwaka 2014. Ninahudumiwa kila kitu.

Kuanzia kula, kuvaa, matembezi na hata mitoko mbalimbali. Tatizo nikimgusia suala la ndoa, anasema tujipange kwanza.

Tujipange mwaka wa 11 huu? Na hata mtoto hatujazaa? Kuna dalili ya ndoa kweli hapa? Nimechunguza kila mahala, kiukweli hana mtoto wala mwanamke mwingine, ila kwanini uchumba umekuwa mrefu hivi?

Wenzangu mlioolewa mlifanyaje mpaka ndoa zenu zikafungwa mapema? Naombeni mbinu mlizotumia ili na mimi niweze kuzitumia katika mahusiano yangu.

Mbarikiwe na muwe na asubuhi njema.
Nusratt Mohamed.
Kuna jambo ulilolikosea nataka nikueleze binti.

Mila takribani za makabila yote zinaulinda uchumba kwa nguvu zote haziruhusu wachumba kukaribiana na kufanya mapenzi.

Vijana wa kileo mila hizi muhimu sana huzipuuza, hutaka kutest mitambo pamoja na kuchunguzana tabia za mchumba, sasa hii ni mbaya.

Uthamani wa mwanamke ni uanamke wake, hakuna zaidi ya hicho.

Ukijiexpose uanamke wako kwa mtu, kabla ya kufunga ndoa ile presha ya kumfanya mchumba wa kiume awe na haraka ya kuoa hushuka, tena huanza kumuona huyo mchumba ni wa kawaida na kuanza kuangalia vipaumbele vingine vya kimaisha na kufanya jambo hilo aliahirishe.

Mila za kibantu, uchumba ukishashikwa na mahari ikatolewa, huwa hakuna muda wa kusubirishwa.

Mahari ikishatolewa, ndoa huandikiswa kanisani, kwa Dc ama kwa shehe na kupangiwa siku ya kufungwa na kuanza kutangazwa rasmi.

Kosa mlikwisha kulifanya, ulishauvunja uchumba mara tu uliporuhusu kulala na mchumba wako kabla ya ndoa.

Hapo ulishageuzwa ni mtumwa wake wa ngono kwa kifungo cha laghai za uchumba na kwa maoni yako unajiona kama huna pa kuvukia na ukikiuka utakuwa umedhulumu, no!

Cha kufanya, mfosi jamaa achukue jukumu la kufunga ndoa haraka, akikuletea ngebe zake za aina yoyote kuendelea kukusubirisha, mkatalie wazi na kumweleza kuwa muda uliompatia wa kumsubiri umetosha na sasa dhamira yako unatamani kuishi maisha ya pamoja ndani ya ndoa yenye majukumu na malengo.

Asipoafikiana, itakuwa ni kisicho ridhiki hakiliki, angalia ustaarabu mwingine.

Hivyo vitu anavyokupatia visikufunge na dhamira yako sahihi ya kuolewa, vitu hutafutwa.

Kuishi kwingi ni kuona mengi mama, kuna issue nilishuhudia jamaa alichumbia na kulipia mahari kabisa, akawa anatembea na huyo mchumba wake na kadri siku zilivyokwenda jamaa akawa haoneshi utayari wa kuoa, ndipo msichana akafosi ndoa.

Siku ya ndoa jamaa akaingia mitini bila kujali gharama za maandalizi ya harusi hiyo kwa pande zote mbili.

Kishika uchumba ama kutolewa mahari hakilazimishi ndoa kufungwa, saazingine ni viini macho na mitego ya wakware, jitathimini mama, chukua hatua.
 
Back
Top Bottom