Uchumba wa muda mrefu umenichosha

Uchumba wa muda mrefu umenichosha

Binafsi niko kwenye uchumba tangu mwaka 2014.
Ninahudumiwa kila kitu.
Kuanzia kula, kuvaa, matembezi na hata mitoko mbalimbali.
Tatizo nikimgusia suala la ndoa, anasema tujipange kwanza.

Tujipange mwaka wa 11 huu? Na hata mtoto hatujazaa?
Kuna dalili ya ndoa kweli hapa?
Nimechunguza kila mahala, kiukweli hana mtoto wala mwanamke mwingine, ila kwanini uchumba umekuwa mrefu hivi?

Wenzangu mlioolewa mlifanyaje mpaka ndoa zenu zikafungwa mapema?
Naombeni mbinu mlizotumia ili na mimi niweze kuzitumia katika mahusiano yangu.

Mbarikiwe na muwe na asubuhi njema.
Nusratt Mohamed.
11 years? Umeolewa bila documentation na hujui
Be serious mwambie unalipeleka kwa wazazi else hamna future
 
Hahitaji mtoto mpaka tujipange.
Tunaishi maisha mazuri tu.
Kua kama dada zangu niliozaliwa nao... Mchune hadi upate mtaji wa uhakika alafu fanya biashara unayoiweza kwa nguvu zako zote.

Utafanikiwa kiuchumi hata ukipata watoto wawili utawamudu wasome shule nzuri, wapate kila wanachotaka... Ndoa sio lazima sababu unaweza kuipata ukabaki kujuta kwanini usingeishi maisha yako
 
Hapana. Ninapata huduma zote kama mke na mpaka kuna baadhi ya ndugu zangu anawasomesha. Ni mtu anayeniheshimu sana.
Tunaishi pamoja na huenda hilo ndilo linalomtia jeuri
Mmnh,.
Inanitia ukakasi kidogo,. Ila kama vipi pambana tu hapohapo huenda ukasitirika hujui mipango yake..

Huku nje wenzio wanalalamika ni kugumu
 
Mwanamme ana jukumu la kuanzisha mahusiano, ila Swala la Ndoa ni kazi ya mwanamke kuanzia kuianzisha, kuihudumia na Kuhakikisha haivunjiki.

Jaribu kuwaza tu kwamba mwenza wako anakosa nn ambacho mpaka aingie kwenye ndoa ndo atakipata?? Ukishapata jawabu anzia hapo!!

Ila Ukiona hauolewi ujue uzembe ni wa kwako, na kwa namna ulivyoandika hapo kama ni kweli basi ndoa utaendelea kuisikia kwenye Vyombo vya habari.

Njoo PM na Elfu tano niache kazi yangu ya kubonda makalai nikusaidie kujitambua.
 
Binafsi niko kwenye uchumba tangu mwaka 2014.
Ninahudumiwa kila kitu.
Kuanzia kula, kuvaa, matembezi na hata mitoko mbalimbali.
Tatizo nikimgusia suala la ndoa, anasema tujipange kwanza.

Tujipange mwaka wa 11 huu? Na hata mtoto hatujazaa?
Kuna dalili ya ndoa kweli hapa?
Nimechunguza kila mahala, kiukweli hana mtoto wala mwanamke mwingine, ila kwanini uchumba umekuwa mrefu hivi?

Wenzangu mlioolewa mlifanyaje mpaka ndoa zenu zikafungwa mapema?
Naombeni mbinu mlizotumia ili na mimi niweze kuzitumia katika mahusiano yangu.

Mbarikiwe na muwe na asubuhi njema.
Nusratt Mohamed.
Nusratt Ukiwa Muongo Uwe na Kumbukumbu 👉Ninapitia msongo mkali wa mawazo baada ya kusimamishwa kazi kisa vyeti feki. Naomba ushauri niweze kujikwamua
 
Kua kama dada zangu niliozaliwa nao... Mchune hadi upate mtaji wa uhakika alafu fanya biashara unayoiweza kwa nguvu zako zote.

Utafanikiwa kiuchumi hata ukipata watoto wawili utawamudu wasome shule nzuri, wapate kila wanachotaka... Ndoa sio lazima sababu unaweza kuipata ukabaki kujuta kwanini usingeishi maisha yako
Kanifungulia duka kubwa la jumla.
Na yeye ni mwalimu wa sekondari.
Sio kama mimi ni tegemezi, hapana.
Ninajimudu mahitaji yangu.
Na huoni kama nikimbebea mimba ndio nitakuwa nimejifukuzisha?
 
Back
Top Bottom