Uchumba wa muda mrefu umenichosha

Uchumba wa muda mrefu umenichosha

Binafsi niko kwenye uchumba tangu mwaka 2014. Ninahudumiwa kila kitu.

Kuanzia kula, kuvaa, matembezi na hata mitoko mbalimbali. Tatizo nikimgusia suala la ndoa, anasema tujipange kwanza.

Tujipange mwaka wa 11 huu? Na hata mtoto hatujazaa? Kuna dalili ya ndoa kweli hapa? Nimechunguza kila mahala, kiukweli hana mtoto wala mwanamke mwingine, ila kwanini uchumba umekuwa mrefu hivi?

Wenzangu mlioolewa mlifanyaje mpaka ndoa zenu zikafungwa mapema? Naombeni mbinu mlizotumia ili na mimi niweze kuzitumia katika mahusiano yangu.

Mbarikiwe na muwe na asubuhi njema.
Nusratt Mohamed.

Hamna kitu hapo, utakutwa na menopause bure na jamaa atakamata kifaa cha 22yrs old maisha yanaendelea, akili kumkichwa!
 
Hapana. Ninapata huduma zote kama mke na mpaka kuna baadhi ya ndugu zangu anawasomesha. Ni mtu anayeniheshimu sana.
Tunaishi pamoja na huenda hilo ndilo linalomtia jeuri
Sasa kama hivyo vyote unapata na una title ya mke wewe shida yako ni nini?? Ndoa itakusaidia nini hapo??

Kwamba akikuoa kuna vitu vitaongezeka zaidi ya hivyo??
 
Hapana. Ninapata huduma zote kama mke na mpaka kuna baadhi ya ndugu zangu anawasomesha. Ni mtu anayeniheshimu sana.
Tunaishi pamoja na huenda hilo ndilo linalomtia jeuri

Kuna mahali umesema ulipunguzwa kazi na jiwe kwa vyeti feki na maisha magumu sana na una 42y hapa hautupangi kweli?
 
Binafsi niko kwenye uchumba tangu mwaka 2014. Ninahudumiwa kila kitu.

Kuanzia kula, kuvaa, matembezi na hata mitoko mbalimbali. Tatizo nikimgusia suala la ndoa, anasema tujipange kwanza.

Tujipange mwaka wa 11 huu? Na hata mtoto hatujazaa? Kuna dalili ya ndoa kweli hapa? Nimechunguza kila mahala, kiukweli hana mtoto wala mwanamke mwingine, ila kwanini uchumba umekuwa mrefu hivi?

Wenzangu mlioolewa mlifanyaje mpaka ndoa zenu zikafungwa mapema? Naombeni mbinu mlizotumia ili na mimi niweze kuzitumia katika mahusiano yangu.

Mbarikiwe na muwe na asubuhi njema.
Nusratt Mohamed.
 
mlifanyaje mpaka ndoa zenu zikafungwa mapema?
mkalishe kikao mwambie nachohitaji mpe mwaka mzima kwamba ndani ya mwaka huu natarajia hili na umwambie mwaka ukiisha tu halijatokea ntaona sio riziki yangu nitaaga mashindano mwambie kwa utu na utulivu ila kwa kumaanisha na huo mwaka ukiisha achana nae si wako huyo akirudi kuomba mrudiane mwambie apeleke washenga home yani wewe uitwe home uulizwe tupokee posa au tusipokee pale ndo msamaha wako. haya kaa humo ushauri kama huu canada tunawatoza laki nne za kibongo
 
Asante sana, nitafanya hivo
 
Kua kama dada zangu niliozaliwa nao... Mchune hadi upate mtaji wa uhakika alafu fanya biashara unayoiweza kwa nguvu zako zote.

Utafanikiwa kiuchumi hata ukipata watoto wawili utawamudu wasome shule nzuri, wapate kila wanachotaka... Ndoa sio lazima sababu unaweza kuipata ukabaki kujuta kwanini usingeishi maisha yako
Huyu ni muislam ndoa kwake ni heshima na inamuepusha na zinaa ndio maana anauliza maswali km hayo
 
Back
Top Bottom