Ni kwanini uchumba huwa unaweza kudumu muda mrefu kuliko ndoa?

sepema

JF-Expert Member
Jun 13, 2019
591
1,000
Salaam wakuu, Naomba niende Kwenye mada.

Jamaa yangu kaishi na mchumba wake kwa miaka10 bila ndoa(2012-2022). Waliishi pamoja maisha mazuri japo vimgogoro vya hapa na pale vilikuepo.

Sasa tatizo limeanzia baada ya wawili hao kuamua kufunga pingu za maisha mnamo February mwaka huu. Ndoa imekuwa na sarakasi nyingi Jambo lililopelekea wawili hao kutengana na kila mtu kuishi maisha yake.

Stori yake imenikumbusha rafiki yangu mwingine aliyekutana na madhira kama hayo. Nimejiuliza naomba mnisaidie wakuu, ni kwanini uchumba huwa unaweza udumu muda mrefu kuliko ndoa?

1653377110258.png
 
ndio maana maboss wengi hawataki kumwajiri mtu,wanakuweka kibarua tu.

ukiishaajiriwa unaanza maseke maana una security mbali mbali,kama ndoa.
mfano ndoa za kikristo unafanya vitimbi ukijua kuachika si rahisi,kitu ambacho ni kosa,hamtakiwi mfungwe na nira ya ndoa bali upendo kati yenu.
 
Kwenye uchumba ni kama wanakuwa field kwa hyo ukikosea tu umefeli ndo maana uchumba unadumu.
Na pia kwenye ndoa ndo sawa na kazini so mtu anajiachia apendavyo.
 
Mkiwa wachumba Kila mmoja anakuwa na hamu na mwenzake Kwa sababu ya umbali, na Kila mmoja huwa anataka kumuaminisha mwenzake Kwamba yeye ni Bora kuliko wanaume/wanawake wote Ndio maana utaona kwenye uchumba kama Kuna mseleleko Fulani, halafu pia wanawake wakiachika kwenye uchumba kwao huwa wanaona ni risk zaidi kuliko kuachika kwenye ndoa hivyo hujikuta wanakuwa wanyenyekevu japo Kwa kuigiza
 
Salaam wakuu, Naomba niende Kwenye mada.

Jamaa yangu kaishi na mchumba wake kwa miaka10 bila ndoa(2012-2022). Waliishi pamoja maisha mazuri japo vimgogoro vya hapa na pale vilikuepo.

Sasa tatizo limeanzia baada ya wawili hao kuamua kufunga pingu za maisha mnamo February mwaka huu. Ndoa imekuwa na sarakasi nyingi Jambo lililopelekea wawili hao kutengana na kila mtu kuishi maisha yake.

Stori yake imenikumbusha rafiki yangu mwingine aliyekutana na madhira kama hayo. Nimejiuliza naomba mnisaidie wakuu, ni kwanini uchumba huwa unaweza udumu muda mrefu kuliko ndoa?
NI kwa sababu ndoa zinadumu muda mfupi kuliko uchumba
 
Mahusiano.....ndoa....uchumba...havinaga formula maalum...hakuna aliyebobea hayo maeneo.....kila mtu atakupa sababu yake
 
Commitment
Commitment
Commitment

Kila kitu taarifa ukitoka uage ukichelewa uage kama upo bungeni vile.
 
Wanasiasa wakati wa Kampeni huwa wanyenyekevu sana.

Tukishawapatia Kura zetu ndipo huanzisha Jeuri. Mara hamieni Burundi, Mara kama hukupata Mkopo wewe ni Mkenya, Mara baki na M*v yako nyumbani..
 
Siku hizi watu hawana upendo wamejaa usanii. Kwahiyo kwenye ndoa usanii hugundulika kirahisi kuliko kwenye uchumba
 
Salaam wakuu, Naomba niende Kwenye mada.

Jamaa yangu kaishi na mchumba wake kwa miaka10 bila ndoa(2012-2022). Waliishi pamoja maisha mazuri japo vimgogoro vya hapa na pale vilikuepo.

Sasa tatizo limeanzia baada ya wawili hao kuamua kufunga pingu za maisha mnamo February mwaka huu. Ndoa imekuwa na sarakasi nyingi Jambo lililopelekea wawili hao kutengana na kila mtu kuishi maisha yake.

Stori yake imenikumbusha rafiki yangu mwingine aliyekutana na madhira kama hayo. Nimejiuliza naomba mnisaidie wakuu, ni kwanini uchumba huwa unaweza udumu muda mrefu kuliko ndoa?
Shetani yupo kazini na kitu asichopenda ni ndoa yenye amani .. maombi pekee ndio siraha plus upendo na hekima.
 
Kufunga NDOA wakati mnaiishi tayari ni kumkebehi Mungu!!

NDOA zilifungwa kea mabikira pekee na Kama bikra haipo Basi binti anauawa kwa uzinzi au anarudishwa kwao enzi hizo!!

Siku hizi NDOA zinafungwa na wazinzi watupu KWA KIGEZO wametubu!mzinzi au kijana alieipoteza bikra yake hapaswi kupongezwa kwa sherehe ya ndoa!!!

Bali waishi tu Hivyo Hivyo hata mahari hawapaswi kutoa au kupokea maana wameshachakaa!!

Ndoa hazidumu coz ni laana kutoka KWA MUNGU kwa wazinzi kufungishwa NDOA!!

Ndio màana hazidumu!!
 
Ooohoooo!

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom