Watu kama nyinyi mlio kwenye nchi ya fursa, mnapojaribu kuona mazingira yenu huko ni kama huku nyumbani mnatia hasira sana.
Wewe umeona hata waraka waliondikiwa mababa, lakini wajitia upofu.
Huoni hata watu wanavyolalamika mitaaani?
Huoni majira yetu yalivyoacha desturi yake? Mabadiliko hayo huyaoni?
Hujui kwamba zaidi ya 75% ya watanzania tunategemea majira haya kwa kilimo?
Huoni ukame unavyolikumba taifa letu mpaka watumishi wanaomba maombi yasikome kwa ajili ya haya.
Watu kama nyinyi mlitakiwa muuonje huu uhalisia ili kuujua vizuri, japo haiwezekani, msidhihaki wengine.
Ni bahati kwako nchi ilishatumia rasilimali nyingi kukufanya uone, lakini umekataa kuona.
Unadhulumu wengine.