Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,101
- 2,344
Maswali muhimu kujiuliza na utakayoyatumia kama msingi wa majadiliano katika mada hii:
1. Kikatiba Mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama anaweza kukasimu mamlaka yake ya kutoa amri au maelekezo kwa majeshi yetu ya Ulinzi na usalama kwa mtu mwingine ili kufanya operation yoyote ya kijeshi?
2. Mkuu wa mkoa wa DSM Ndugu Albert Chalamila, alipata wapi mamlaka ya kuliagiza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kufanya usafi mitaani siku ya tarehe 23 na 24/01/2024?
3. Kama aliagizwa na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan, Je huyu Rais hajakiuka na kuvunja katiba?
4. Na kama ni maamuzi ya RC Albert Chalamila mwenyewe bila ridhaa ya mkuu wa nchi, huyu mkuu wa mkoa bado anafanya nini ofisini mpaka sasa maana katika hili ni wazi kuwa huyu kiongozi ni "mjinga" hajui majukumu yake na katika hili amevuka mipaka ya mamlaka yake?
=====================
All in all, unaweza kutazama na kusikiliza uchambuzi maridadi kabisa wa kukujengea ufahamu juu ya jambo hili ktk video hiyo hapo☝️☝️☝️juu.
Katika video hiyo kwanza utaona upogo wa tamko la RC Chalamila na pia utajifunza kitu kuwa, hawa watawala wetu wako ktk hatua za mwisho za anguko lao kwa sababu wako desperate kulinda madaraka yao kwa gharama yoyote hata kama ni kuuza akili na ufahamu wao!