Wakuu ama kwa hakika usije ukathubutu kushindana na Aliyejaaliwa na Maulana , unaweza kujikuta unatembea umbali mrefu kwa miguu baada ya kuishiwa nauli.
Chadema ni mpango wa Mungu mwenyewe ambao bila ya shaka HAKUNA MWANADAMU YEYOTE ALIYEUMBWA KWA UDONGO ataweza kuishikia chini , hiki chama kiacheni tu jamani , kimeshindikana ! Hivi wanatumia njia zipi hawa watu jamani ? kitabu kimetoka juzi lakini kinasomwa , kinafuatiliwa na kuzingatiwa utadhani ni filamu ya Sultan ! ama kweli Chadema inapendwa mno !
Ufuatiliaji huu wa sera hizi mbadala ambao kiukweli siku ya kuzinduliwa kwake hazikupewa promo yoyote ya maana ni ishara ya wananchi wa Tanzania kuchoshwa na umasikini , njaa na mateso wanayoyapata , kuchoshwa kwa wananchi na porojo za takwimu feki za viongozi kuhusu uchumi wa nchi , maendeleo , afya na elimu , wananchi wanaziangalia sera za chadema kama Mkombozi wao , na kiukweli hakukuwa na namna yoyote ile zaidi ya kuzuia siasa za majukwaa ili kuokoa jahazi .
View attachment 883997View attachment 883998View attachment 883999