Uchambuzi wa Sera mpya ya CHADEMA toleo la 2018

Uchambuzi wa Sera mpya ya CHADEMA toleo la 2018

Mtoa mada

Hoja yako juu ya sera mpya za chama haziwezi kutekelezeka na kuwa funzo endapo mapendekezo tajwa hayataanzia ndani ya chama chenyewe hasa ktk kipengele hiki cha mfumo Wa vyama vingi,,, sera hizi kwangu binafs naona kama ni porojo tu ambazo utekelezaji wake ni totally negative, sera zinaweza zikapangwa ña zikawa positive kabsa ila utekelezaji ni jambo jingine mfano je tunajadili pia juu ya kuandaa viongozi wa kutekeleza Haya ambao watakuwa na udhubutu na uzalendo???? Mfano Chama hiki kinahubiri demokrasia na hata nominó yake kwa maana ya title ni democracy centred!! Lkn kwanini watu wanafikia mahali wanahoji juu ya mwenendo Wa demokrasia ndani ya chama hasa juu ya kukaa saña kwa mwenyekiti Wa chama??? Je katiba ya chama inazungumziaje kuhusu uongozi ndani ya chama??? Je mabadiliko ya katiba ya chama ambayo hata ww unayafahamu je yanaakisi vipi na hizi sera??? Je katiba hiyo ni halali??kama ni halali je ni halisi???? Kama ni halisi je inakidhi mahitaji??? Kama inakidhi mahtaji je inafaa???

Maswali yote haya yakijibiwa itakuwa rahisi kwa umma kujadili sera Mpya hizi ila tuelewe kwamba inahitaji muda sana Wa kuuuelimisha umma kwani uaminifu huenda ukawa siyo Sawa kama udhaniavyo!!
 
Unatupotezea wakati, na inaonyesha huna kazi, ama hnitimiza ajira yako.

Ni afadhali ujatueleza wapi tunaweza kupata nakala kwa wale tusioishi Dar.

By the ni vizuri kila mtanzania akawa na copy za sera ya vyama vyote, it helps one yo know the needs of our country. Pia utaona mambo mengi ni sera ya kila mwana siasa, hakuna mwenye monopoly na sera
Sema wewe unapotezewa wakati usiwe msemaji wa wengine. Nilivyomuelewa mleta mada mwishowe ataweka PDF but kwa sasa ataweka by chapter ili wanabodi, ambao wako interested waweze kuchangia. Pia yeye ameweka sera ya CDM kama wewe unayo ya vyama vingine weka hapa.
 
Mtoa mada

Hoja yako juu ya sera mpya za chama haziwezi kutekelezeka na kuwa funzo endapo mapendekezo tajwa hayataanzia ndani ya chama chenyewe hasa ktk kipengele hiki cha mfumo Wa vyama vingi,,, sera hizi kwangu binafs naona kama ni porojo tu ambazo utekelezaji wake ni totally negative, sera zinaweza zikapangwa ña zikawa positive kabsa ila utekelezaji ni jambo jingine mfano je tunajadili pia juu ya kuandaa viongozi wa kutekeleza Haya ambao watakuwa na udhubutu na uzalendo???? Mfano Chama hiki kinahubiri demokrasia na hata nominó yake kwa maana ya title ni democracy centred!! Lkn kwanini watu wanafikia mahali wanahoji juu ya mwenendo Wa demokrasia ndani ya chama hasa juu ya kukaa saña kwa mwenyekiti Wa chama??? Je katiba ya chama inazungumziaje kuhusu uongozi ndani ya chama??? Je mabadiliko ya katiba ya chama ambayo hata ww unayafahamu je yanaakisi vipi na hizi sera??? Je katiba hiyo ni halali??kama ni halali je ni halisi???? Kama ni halisi je inakidhi mahitaji??? Kama inakidhi mahtaji je inafaa???

Maswali yote haya yakijibiwa itakuwa rahisi kwa umma kujadili sera Mpya hizi ila tuelewe kwamba inahitaji muda sana Wa kuuuelimisha umma kwani uaminifu huenda ukawa siyo Sawa kama udhaniavyo!!
Sera hazina maana kama kiongozi mkuu ni mungumtu. Sera yeyote ya kisiasa kama hailengi kukuza demokrasia ni upuuzi mtupu
 
Nimewasikia baadhi ya viongozi wa CHADEMA walipata nafasi ya kuieleza hiyo Sera lakini hakuna hata mmoja alibainisha UMASKINI ni nini, hata katika mazingira ya Tanzania, na mikakati iliyoanishwa ya kuondokana na UMASKINI huo.

Isitoshe dibaji imesheheni yale yale tunayoyasikia mara kwa mara kutoka kwa viongozi wa CHADEMA - Tume Huru ya Uchaguzi.

Hivyo mleta mada aweke hapa hiyo Sera (soft copy) tuipitie kwa kina.
Duuh hivi leo hii kuna mtanzania asiyejua maana ya umasikini? Assume wewe ni afisa maendeleo unaenda kijijini kwenye mkutano mkuu wa kijiji unawauliza wanakijiji "mnajua maana ya umasikini? [emoji23] [emoji23] [emoji13] [emoji13]
 
Umasikini ndio mtaji wa chadema ila masikini nao wameanza kuistukia janja yao
 
Mwenye nakala ya sera ya chadema toleo la 2018 atuwekee hapa wana JF tusome na kuitafakari. Sera iliyopita ilikuwa ya hovyo yenye kuchochea unyonyaji na dhuluma kwa wanyonge.
Habari hiyo haina mvuto, Sera wataziuzia wapi WAKATI hawataki kushiriki kwenye chaguzi!!!::Mbowe na genge lake wameshapoteza uelekeo
 
Tarehe 25/9/2018 Chama kikuu mbadala nchini Tanzania Chadema kimezindua sera yake mpya inayotoa mwelekeo ama dira sahihi ya taifa letu kuelekea 2020.

Katika sera hiyo yameangaziw mengi, na muhimu zaidi ni mambo 12 yanayotawala mnasaba wa sera yenyewe, nimeisoma, ninaendelea kuisoma, na nitahakikisha wote tunaisoma kwa undani na kwa kila neno.

Nakukuu andiko la Bwana Edward Kinabo kama sehemu ya kusherehesha mjadala huu wa uchambuzi....

"Dhumuni kuu la mfumo wa vyama vingi vya siasa si kushindania madaraka tu, maana madaraka yanaweza hata kushindaniwa ndani ya mfumo wa chama kimoja. Kusudi la msingi na la muhimu zaidi la mfumo wa vyama vingi vya siasa, ni kushindanisha sera mbadala za vyama kwa faida ya kuchochea maendeleo ya nchi.

Kwa nchi zilizokomaa kidemokrasia, chama kilicho madarakani huzipokea sera bora kutoka vyama pinzani kwa furaha na kuzifanyia kazi kwa manufaa ya nchi. Lakini kwa nchi zilizopungukiwa utashi wa kidemokrasia, Chama kilicho madarakani huishia kupinga, kukashifu na kukejeli sera bora kutoka vyama pinzani.

Fikru finyu hudhani kuwa sera za vyama zipo kwaajili ya kuombea kura tu katika chaguzi. Na kwa hiyo hujenga chuki zisizo na msingi bila kujali ubora wa sera hizo kwa manufaa ya wananchi.

Simple minded politicians think of next election, but great leaders think of next generations. "Wanasiasa wenye fikra finyu huwazia uchaguzi ujao, lakini viongozi bora hufikiria mustakabali wa vizazi vijavyo"

Ni kwa jinsi hii, vyama makini na vyenye uongozi bora vitaendelea kujipambanua kwa siasa za sera zaidi, huku vyama uchwara vikijikita kwenye siasa za propaganda, fitina, chuki, ubaguzi na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani wao.

Naungana na Watanzania wote katika kuipongeza Chadema kwa kuzindua sera mbadala kuhusu maendeleo ya nchi.
Huu ni uzalendo wa kupigiwa mfano. Hizi ni sera zetu sote bila kujali tofauti za vyama.

Hongera kwa uongozi makini chini ya Ndugu Freeman Aikaeli Mbowe.

Tupambanishe sera na sio mabavu".

Uzi huu naomba Mods uwe maalumu kwaajili ya Uchambuzi wa sera hii kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho,

Nitaanzia kwenye utangulizi kabisa, na kila siku nitakuwa naelezea kwa kina kila sera ilivyoeleza...

Ninaomba tuanze na Dibaji ya Sera hii...

View attachment 878563

View attachment 881420View attachment 880612
CDM mlishapoteza uhalali wa kuongoza nchi Mara mlipoachana na dhana ya kupiga vita ufisadi ili kumfurahisha Lowasa. Hata Sera yenu hakuna pahala ilipoongelea moja kwa moja kupambana na UFISADI NCHINI
 
Nahitaji pdf format tyu nijielimishe ili nipate msingi wa kusimamia nacho uelewa nacho
 
Nahitaji pdf format tyu nijielimishe ili nipate msingi wa kusimamia nacho uelewa nacho

We are living in a digital age. I am a bit surprised, by the fact that it is a week since these revived policies were released but no newspapers are publishing them including CHADEMA's own, no online release of these documents, no effort is being made to elaborate them by the gurus, etc.

Hata hii PDF version tu inakuwa kazi kuipata!!!!

Ushauri wangu kwa CHADEMA, wazisambaze kwenye kila tawi la chama, pia waandae wataalam watakaotafuta vipindi kwenye TV kuziongelea na kuziibua kwenye mijadala mbalimbali ya kisera.
 
Unamtofautishaje Nyerere na uenyekiti wa CCM wakati yeye ni mmoja kati ya waanzilishi na mtumikiaji wa nafasi hiyo.
labda anamaanisha tofauti hii
IMG-20180927-WA0001.jpg
 
Asante! Huna dola,hutegemei kuunda serikali sio leo wala kesho.
Huu ndio ulevi unaopelekea wengine wetu tuwachukie. Neno hilo nalitumia kwa tabu sana kwa mtu ambaye ni mTanzania mwenzangu. Lakini sina neno zuri zaidi ya hilo kuelezea 'attitude' yenu hiyo isiyofaa.
 
[QUOTE="bernardp, post: 2857

Ushauri wangu kwa CHADEMA, wazisambaze kwenye kila tawi la chama, pia waandae wataalam watakaotafuta vipindi kwenye TV kuziongelea na kuziibua kwenye mijadala mbalimbali ya kisera.[/QUOTE]

Can't put it any better than this. Na huko kwenye matawi na vijijini, viongozi wawe na uelewa mzuri wa kueleza kushawishi na kutetea sera hizo. Isiwe tu ni kusambaza na kukaa kimya.
 
Wakuu ama kwa hakika usije ukathubutu kushindana na Aliyejaaliwa na Maulana , unaweza kujikuta unatembea umbali mrefu kwa miguu baada ya kuishiwa nauli.

Chadema ni mpango wa Mungu mwenyewe ambao bila ya shaka HAKUNA MWANADAMU YEYOTE ALIYEUMBWA KWA UDONGO ataweza kuishikia chini , hiki chama kiacheni tu jamani , kimeshindikana ! Hivi wanatumia njia zipi hawa watu jamani ? kitabu kimetoka juzi lakini kinasomwa , kinafuatiliwa na kuzingatiwa utadhani ni filamu ya Sultan ! ama kweli Chadema inapendwa mno !

Ufuatiliaji huu wa sera hizi mbadala ambao kiukweli siku ya kuzinduliwa kwake hazikupewa promo yoyote ya maana ni ishara ya wananchi wa Tanzania kuchoshwa na umasikini , njaa na mateso wanayoyapata , kuchoshwa kwa wananchi na porojo za takwimu feki za viongozi kuhusu uchumi wa nchi , maendeleo , afya na elimu , wananchi wanaziangalia sera za chadema kama Mkombozi wao , na kiukweli hakukuwa na namna yoyote ile zaidi ya kuzuia siasa za majukwaa ili kuokoa jahazi .

Instagram media - BoYfceTgv4X.jpg
Instagram media - BoZCTa2g5jC.jpg
Instagram media - BoZav3OBEdB.jpg
 
Back
Top Bottom