Uchambuzi wa Sera mpya ya CHADEMA toleo la 2018

Uchambuzi wa Sera mpya ya CHADEMA toleo la 2018

Sidhani kama uko saw na sidhani kama upo TZ! Hivi Chadema tumezindua nini siku chache zilizopita!?
 
Ni ajabu sana kuwa na chama kinachojiita cha siasa alafu kutwa kinangoja matukio kama chombo cha habari, viongozi wake wamekaa kushadadia udaku mitamdaoni
Jamani embu mje mueleze sera zenu mbadala kuhusu Huduma za kijamii
Sera yenu ya mambo ya nje
Ulinzi na Usalama
Sisi tulio na kiu yakuona haya mambo mnatuboa sana kwakweli maana kila siku nyie na udaku udaku na nyie sasa nnashindwa kutofautisha kati ya chama chenu na magazeti ya udaku
Tumechoka kutekwa
Hatuna uhakika wa usalama wetu,hatuna uhakika wa kuamka tukiwa vitandani mwetu
Sera ni UPUUZI kabisa kama sina uhakika wa usalama wangu!
 
...tahadhari! kwa wana jf...kuna misukule imejitokeza humu jf inaleta Uzi za kipuuzi kama Uhu..kuwen makin .
Sawa nnajua ndio zenu vijana wa ufipa kila jambo mnalijua na mkiulizwa mayusi ndio fimbo yenu ila siku yaja mtabakia na matusi hayo
 
Ni ajabu sana kuwa na chama kinachojiita cha siasa alafu kutwa kinangoja matukio kama chombo cha habari, viongozi wake wamekaa kushadadia udaku mitamdaoni
Jamani embu mje mueleze sera zenu mbadala kuhusu Huduma za kijamii
Sera yenu ya mambo ya nje
Ulinzi na Usalama
Sisi tulio na kiu yakuona haya mambo mnatuboa sana kwakweli maana kila siku nyie na udaku udaku na nyie sasa nnashindwa kutofautisha kati ya chama chenu na magazeti ya udaku
Chadema Hivi Majuzi Wamezindua Sera Mbadala. Zipo, Tafuta Nakala Yako.
 
Tarehe 25/9/2018 Chama kikuu mbadala nchini Tanzania Chadema kimezindua sera yake mpya inayotoa mwelekeo ama dira sahihi ya taifa letu kuelekea 2020.

Katika sera hiyo yameangaziw mengi, na muhimu zaidi ni mambo 12 yanayotawala mnasaba wa sera yenyewe, nimeisoma, ninaendelea kuisoma, na nitahakikisha wote tunaisoma kwa undani na kwa kila neno.

Nakukuu andiko la Bwana Edward Kinabo kama sehemu ya kusherehesha mjadala huu wa uchambuzi....

"Dhumuni kuu la mfumo wa vyama vingi vya siasa si kushindania madaraka tu, maana madaraka yanaweza hata kushindaniwa ndani ya mfumo wa chama kimoja. Kusudi la msingi na la muhimu zaidi la mfumo wa vyama vingi vya siasa, ni kushindanisha sera mbadala za vyama kwa faida ya kuchochea maendeleo ya nchi.

Kwa nchi zilizokomaa kidemokrasia, chama kilicho madarakani huzipokea sera bora kutoka vyama pinzani kwa furaha na kuzifanyia kazi kwa manufaa ya nchi. Lakini kwa nchi zilizopungukiwa utashi wa kidemokrasia, Chama kilicho madarakani huishia kupinga, kukashifu na kukejeli sera bora kutoka vyama pinzani.

Fikru finyu hudhani kuwa sera za vyama zipo kwaajili ya kuombea kura tu katika chaguzi. Na kwa hiyo hujenga chuki zisizo na msingi bila kujali ubora wa sera hizo kwa manufaa ya wananchi.

Simple minded politicians think of next election, but great leaders think of next generations. "Wanasiasa wenye fikra finyu huwazia uchaguzi ujao, lakini viongozi bora hufikiria mustakabali wa vizazi vijavyo"

Ni kwa jinsi hii, vyama makini na vyenye uongozi bora vitaendelea kujipambanua kwa siasa za sera zaidi, huku vyama uchwara vikijikita kwenye siasa za propaganda, fitina, chuki, ubaguzi na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani wao.

Naungana na Watanzania wote katika kuipongeza Chadema kwa kuzindua sera mbadala kuhusu maendeleo ya nchi.
Huu ni uzalendo wa kupigiwa mfano. Hizi ni sera zetu sote bila kujali tofauti za vyama.

Hongera kwa uongozi makini chini ya Ndugu Freeman Aikaeli Mbowe.

Tupambanishe sera na sio mabavu".

Uzi huu naomba Mods uwe maalumu kwaajili ya Uchambuzi wa sera hii kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho,

Nitaanzia kwenye utangulizi kabisa, na kila siku nitakuwa naelezea kwa kina kila sera ilivyoeleza...

Ninaomba tuanze na Dibaji ya Sera hii...

View attachment 878563

View attachment 881420View attachment 880612
Hali yako kamanda,
Nawezaje kupata kopi ya hiko ktabu cha sera? Kopi laini au ngumu
 
Back
Top Bottom