Uchambuzi wa Sera mpya ya CHADEMA toleo la 2018

mbowe.jpg

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (wa pili kushoto) akiwa na viongozi waandamizi wa chama hicho wakionyesha kitabu cha sera mpya ya chama hicho baada ya kuizindua jijini Dar es Salaam jana. Kuanzia kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Zanziba), Salum Mwalimu, Katibu Mkuu, Dk Vincent Mashinji na Naibu Katibu Mkuu (Bara)
 
Hapa ndio utagundua akili za wanasiasa zimejikita zaidi kuona ni jinsi gani wanagawana madaraka/ulaji/kula.

​
 
Magu huwa anaangalia wapinzani wanataka nn then anatekeleza..i hope atatekeleza na hili..[emoji23]
 
MASHABIKI NA WADAU WA SOKA MANISPAA YA MUSOMA WAMEULALAMIKIA UONGOZI WA CCM MKOA KWA KURUHUSU TAMASHA LA MUZIKI LIFANYIKE KATIKA UWANJA UNAOTUMIWA NA TIMU YA BIASHARA INAYOSHIRIKI LIGI KUU , SERA ZA CHADEMA UKURASA WA 71 ZINAELEZA WAZI KUHUSU UGHARAMIAJI WA UMILIKI WA MIUNDOMBINU

#SeraMbadala

UKURASA WA 71.

UGHARAMIAJI NA UMILIKI WA MIUNDOMBINU

- Kuboresha Mfumo wa Ugharamiaji wa Miundombinu.

- Kuwa na Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Ugharamiaji wa Miundombinu.

- Kuhimiza Mashirika ya Kiserikali Kugharamia Miundombinu.

- Kuhimiza Ushiriki Sekta Binafsi katika mfumo wa Jenga, Endesha na Hamisha.

- Kuwa na Utaratibu wa Kisera na Kisheria Kuwezesha mfumo wa Kugharamia Miundombinu.

HII INA MAANA GANI KWETU:

Chadema inaelewa na kutambua kuwa miradi ya miundombinu inagharimu fedha nyingi na masuala mengi yanayoambatana nayo ambayo inabidi yashughulikiwe na kusimamiwa. Chadema inatambua kuwa ugharamiaji wa miundombinu hauwezi kufanywa na Serikali pekee kwa kuwa kwa kufanya hivyo Serikali itashindwa kugharamia huduma nyingine za kijamii. Hivyo, Chadema itaanzisha mfumo wa Kugharamia miundombinu kwa kutumia sekta binafsi ambao utakuwa wa gharama nafuu.

MALENGO TUNAYOTAKA KUYAFIKIA:

Chadema inaunga mkono mfumo wa ugharamiaji wa miundombinu kwa kutumia kodi, mikopo na misaada kutoka nje ya nchi. Hii itahusisha mfumo wa ugharamiaji kwa pamoja kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.

Chadema itahimiza ushiriki imara wa sekta binafsi katika kuwekeza kwenye miradi ya miundombinu kwa kutumia ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa utaratibu kwamba sekta sekta binafsi inajenga na kuendesha miundombinu na baadae kuhamisha Umiliki wa Serikali.

Chadema itahimiza ushiriki wa Mashirika ya Umma katik ujenzi wa miundombinu.

Chadema itaweka Utaratibu wa kisera na kisheria ili kuwezesha kuwa na mbinu za kugharamia ujenzi wa miundombinu ambao utakuwa na uhakika na dhamana kwa uwekezaji uliofanyika ikiwemo kuweka utaratibu wa kuepuka hasara inayoweza kutokea kutokana na mabadiliko ya kisasa. Utaratibu wa kisera utahakikisha unamlinda mtumiaji wa miundombinu dhidi ya hujuma zozote au kukataliwa kutumia miundombinu husika.

NAMNA WANANCHI WATAKAVYONUFAIKA:

Taifa litakuwa na miundombinu ambayo itasaidia maendeleo ya uchumi.

Kwa kushirikisha sekta binafsi kutakuwa na fursa za uwekezaji katika miundombinu.

Miundombinu itapanua fursa za biashara, kilimo, utalii na shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii.

Serikali itakuwa na fedha za kutosha kugharamia huduma za kijamii.

NA UKURASA WA 25 ZINAELEZA WAZI KUHUSU SEKTA YA MICHEZO.

#SeraMbadala
👇🏿
UKURASA WA 25.

KUFANYA MICHEZO NA UTAMADUNI KIBIASHARA ZAIDI

- Kuwa na kupanua wigo wa Wachezaji wa Kulipwa Duniani.

- Kuhimiza uwekezaji na Utaalamu katika sekta ya Burudani.

- Kuwa na Mazingira rafiki kwa Sekta Binafsi.

HII INA MAANA GANI KWETU:

Chadema inachukulia michezo na utamaduni kama moja ya sekta za kiuchumi zinazokuwa kwa kasi na ambazo zina mchango katika ukuaji wa uchumi na kupanua ajira yenye kipato. Ni sekta inayochangia mapato kupitia matangazo ya biashara kwenye vyombo vya habari na kusaidia kutangaza na kutengeneza watu mashuhuri wanaofahamika kimataifa. Kuhusisha michezo na tamaduni kibiashara ni hatua ambayo itahimiza ushindani na itaboresha ubora wa wanamichezo wetu kimataifa.

MALENGO TUNAYOTAKA KUYAFIKIA

Chadema inaamini katika kuendeleza michezo na utamaduni kutoka kuwa sehemu ya burudani na kuwa fursa za kibiashara. Sekta za soka, filamu na muziki zimefanya vizuri ambapo zipo sekta nyingine zikipata kipaumbele zitaweza kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Chadema itaifanya michezo na utamaduni kuwa ya kitaalamu na kulipwa ili kuwa na tija.

Chadema itatumia teknolojia katika michezo kuongeza mapato.

Kufanya michezo na utamaduni kuwa ya kibiashara zaidi itasaidia kupatikana kwa watu mashuhuri ambao watatumika katika matangazo ya biashara kimataifa na hivyo kuongeza mapato.

Michezo na utamaduni vitaitangaza nchi kimataifa na hivyo kupats fursa za biashara na uwekezaji kwenye sekta za utalii na viwanda.

NAMNA WANANCHI WATAKAVYONUFAIKA:

Michezo na Utamaduni inakuza fahari ya Taifa.
Michezo na Utamaduni inaboresha afya ya mwili na akili kwa watu.

Muchezo na utamaduni ni chanzo cha mapato kwa mtu binafsi na kwa Serikali.

Michezo na Utamaduni inahimza watu kujifunza.

Michezo na Utamaduni inapanua fursa za ajira na biashara.

#SeraMbadala
 
Hii ni njema sana.Huyu Jiwe yeye anafungia NGOs na kusema "matajiri kwenye awamu ya tano wataishi kama mashetani.",mimi ninauwezo wa kumfanya tajiri kitu choxhote".

Lakin Chadema wataweka nia ya dhati kushirikiana na mashirika ya binafsi ili kuboresha maendeleo ya Watanzania.
 
Tarehe 25/9/2018 Chama kikuu mbadala nchini Tanzania Chadema kimezindua sera yake mpya inayotoa mwelekeo ama dira sahihi ya taifa letu kuelekea 2020.

Katika sera hiyo yameangaziw mengi, na muhimu zaidi ni mambo 12 yanayotawala mnasaba wa sera yenyewe, nimeisoma, ninaendelea kuisoma, na nitahakikisha wote tunaisoma kwa undani na kwa kila neno.

Nakukuu andiko la Bwana Edward Kinabo kama sehemu ya kusherehesha mjadala huu wa uchambuzi....

"Dhumuni kuu la mfumo wa vyama vingi vya siasa si kushindania madaraka tu, maana madaraka yanaweza hata kushindaniwa ndani ya mfumo wa chama kimoja. Kusudi la msingi na la muhimu zaidi la mfumo wa vyama vingi vya siasa, ni kushindanisha sera mbadala za vyama kwa faida ya kuchochea maendeleo ya nchi.

Kwa nchi zilizokomaa kidemokrasia, chama kilicho madarakani huzipokea sera bora kutoka vyama pinzani kwa furaha na kuzifanyia kazi kwa manufaa ya nchi. Lakini kwa nchi zilizopungukiwa utashi wa kidemokrasia, Chama kilicho madarakani huishia kupinga, kukashifu na kukejeli sera bora kutoka vyama pinzani.

Fikru finyu hudhani kuwa sera za vyama zipo kwaajili ya kuombea kura tu katika chaguzi. Na kwa hiyo hujenga chuki zisizo na msingi bila kujali ubora wa sera hizo kwa manufaa ya wananchi.

Simple minded politicians think of next election, but great leaders think of next generations. "Wanasiasa wenye fikra finyu huwazia uchaguzi ujao, lakini viongozi bora hufikiria mustakabali wa vizazi vijavyo"

Ni kwa jinsi hii, vyama makini na vyenye uongozi bora vitaendelea kujipambanua kwa siasa za sera zaidi, huku vyama uchwara vikijikita kwenye siasa za propaganda, fitina, chuki, ubaguzi na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani wao.

Naungana na Watanzania wote katika kuipongeza Chadema kwa kuzindua sera mbadala kuhusu maendeleo ya nchi.
Huu ni uzalendo wa kupigiwa mfano. Hizi ni sera zetu sote bila kujali tofauti za vyama.

Hongera kwa uongozi makini chini ya Ndugu Freeman Aikaeli Mbowe.

Tupambanishe sera na sio mabavu".

Uzi huu naomba Mods uwe maalumu kwaajili ya Uchambuzi wa sera hii kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho,

Nitaanzia kwenye utangulizi kabisa, na kila siku nitakuwa naelezea kwa kina kila sera ilivyoeleza...

Ninaomba tuanze na Dibaji ya Sera hii...

View attachment 878563

View attachment 881420View attachment 880612
sawa sawa maana hii kitu nimeikosa
 
MASHABIKI NA WADAU WA SOKA MANISPAA YA MUSOMA WAMEULALAMIKIA UONGOZI WA CCM MKOA KWA KURUHUSU TAMASHA LA MUZIKI LIFANYIKE KATIKA UWANJA UNAOTUMIWA NA TIMU YA BIASHARA INAYOSHIRIKI LIGI KUU , SERA ZA CHADEMA UKURASA WA 71 ZINAELEZA WAZI KUHUSU UGHARAMIAJI WA UMILIKI WA MIUNDOMBINU

#SeraMbadala

UKURASA WA 71.

UGHARAMIAJI NA UMILIKI WA MIUNDOMBINU

- Kuboresha Mfumo wa Ugharamiaji wa Miundombinu.

- Kuwa na Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika Ugharamiaji wa Miundombinu.

- Kuhimiza Mashirika ya Kiserikali Kugharamia Miundombinu.

- Kuhimiza Ushiriki Sekta Binafsi katika mfumo wa Jenga, Endesha na Hamisha.

- Kuwa na Utaratibu wa Kisera na Kisheria Kuwezesha mfumo wa Kugharamia Miundombinu.

HII INA MAANA GANI KWETU:

Chadema inaelewa na kutambua kuwa miradi ya miundombinu inagharimu fedha nyingi na masuala mengi yanayoambatana nayo ambayo inabidi yashughulikiwe na kusimamiwa. Chadema inatambua kuwa ugharamiaji wa miundombinu hauwezi kufanywa na Serikali pekee kwa kuwa kwa kufanya hivyo Serikali itashindwa kugharamia huduma nyingine za kijamii. Hivyo, Chadema itaanzisha mfumo wa Kugharamia miundombinu kwa kutumia sekta binafsi ambao utakuwa wa gharama nafuu.

MALENGO TUNAYOTAKA KUYAFIKIA:

Chadema inaunga mkono mfumo wa ugharamiaji wa miundombinu kwa kutumia kodi, mikopo na misaada kutoka nje ya nchi. Hii itahusisha mfumo wa ugharamiaji kwa pamoja kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.

Chadema itahimiza ushiriki imara wa sekta binafsi katika kuwekeza kwenye miradi ya miundombinu kwa kutumia ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa utaratibu kwamba sekta sekta binafsi inajenga na kuendesha miundombinu na baadae kuhamisha Umiliki wa Serikali.

Chadema itahimiza ushiriki wa Mashirika ya Umma katik ujenzi wa miundombinu.

Chadema itaweka Utaratibu wa kisera na kisheria ili kuwezesha kuwa na mbinu za kugharamia ujenzi wa miundombinu ambao utakuwa na uhakika na dhamana kwa uwekezaji uliofanyika ikiwemo kuweka utaratibu wa kuepuka hasara inayoweza kutokea kutokana na mabadiliko ya kisasa. Utaratibu wa kisera utahakikisha unamlinda mtumiaji wa miundombinu dhidi ya hujuma zozote au kukataliwa kutumia miundombinu husika.

NAMNA WANANCHI WATAKAVYONUFAIKA:

Taifa litakuwa na miundombinu ambayo itasaidia maendeleo ya uchumi.

Kwa kushirikisha sekta binafsi kutakuwa na fursa za uwekezaji katika miundombinu.

Miundombinu itapanua fursa za biashara, kilimo, utalii na shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii.

Serikali itakuwa na fedha za kutosha kugharamia huduma za kijamii.

NA UKURASA WA 25 ZINAELEZA WAZI KUHUSU SEKTA YA MICHEZO.

#SeraMbadala
👇🏿
UKURASA WA 25.

KUFANYA MICHEZO NA UTAMADUNI KIBIASHARA ZAIDI

- Kuwa na kupanua wigo wa Wachezaji wa Kulipwa Duniani.

- Kuhimiza uwekezaji na Utaalamu katika sekta ya Burudani.

- Kuwa na Mazingira rafiki kwa Sekta Binafsi.

HII INA MAANA GANI KWETU:

Chadema inachukulia michezo na utamaduni kama moja ya sekta za kiuchumi zinazokuwa kwa kasi na ambazo zina mchango katika ukuaji wa uchumi na kupanua ajira yenye kipato. Ni sekta inayochangia mapato kupitia matangazo ya biashara kwenye vyombo vya habari na kusaidia kutangaza na kutengeneza watu mashuhuri wanaofahamika kimataifa. Kuhusisha michezo na tamaduni kibiashara ni hatua ambayo itahimiza ushindani na itaboresha ubora wa wanamichezo wetu kimataifa.

MALENGO TUNAYOTAKA KUYAFIKIA

Chadema inaamini katika kuendeleza michezo na utamaduni kutoka kuwa sehemu ya burudani na kuwa fursa za kibiashara. Sekta za soka, filamu na muziki zimefanya vizuri ambapo zipo sekta nyingine zikipata kipaumbele zitaweza kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Chadema itaifanya michezo na utamaduni kuwa ya kitaalamu na kulipwa ili kuwa na tija.

Chadema itatumia teknolojia katika michezo kuongeza mapato.

Kufanya michezo na utamaduni kuwa ya kibiashara zaidi itasaidia kupatikana kwa watu mashuhuri ambao watatumika katika matangazo ya biashara kimataifa na hivyo kuongeza mapato.

Michezo na utamaduni vitaitangaza nchi kimataifa na hivyo kupats fursa za biashara na uwekezaji kwenye sekta za utalii na viwanda.

NAMNA WANANCHI WATAKAVYONUFAIKA:

Michezo na Utamaduni inakuza fahari ya Taifa.
Michezo na Utamaduni inaboresha afya ya mwili na akili kwa watu.

Muchezo na utamaduni ni chanzo cha mapato kwa mtu binafsi na kwa Serikali.

Michezo na Utamaduni inahimza watu kujifunza.

Michezo na Utamaduni inapanua fursa za ajira na biashara.

#SeraMbadala

Tupatie Link tupakue tusone wenyewe tujue mbivu na mbichi
 
Back
Top Bottom