Uchambuzi wa Sera mpya ya CHADEMA toleo la 2018

Uchambuzi wa Sera mpya ya CHADEMA toleo la 2018

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,026
Reaction score
20,513
Tarehe 25/9/2018 Chama kikuu mbadala nchini Tanzania Chadema kimezindua sera yake mpya inayotoa mwelekeo ama dira sahihi ya taifa letu kuelekea 2020.

Katika sera hiyo yameangaziw mengi, na muhimu zaidi ni mambo 12 yanayotawala mnasaba wa sera yenyewe, nimeisoma, ninaendelea kuisoma, na nitahakikisha wote tunaisoma kwa undani na kwa kila neno.

Nakukuu andiko la Bwana Edward Kinabo kama sehemu ya kusherehesha mjadala huu wa uchambuzi....

"Dhumuni kuu la mfumo wa vyama vingi vya siasa si kushindania madaraka tu, maana madaraka yanaweza hata kushindaniwa ndani ya mfumo wa chama kimoja. Kusudi la msingi na la muhimu zaidi la mfumo wa vyama vingi vya siasa, ni kushindanisha sera mbadala za vyama kwa faida ya kuchochea maendeleo ya nchi.

Kwa nchi zilizokomaa kidemokrasia, chama kilicho madarakani huzipokea sera bora kutoka vyama pinzani kwa furaha na kuzifanyia kazi kwa manufaa ya nchi. Lakini kwa nchi zilizopungukiwa utashi wa kidemokrasia, Chama kilicho madarakani huishia kupinga, kukashifu na kukejeli sera bora kutoka vyama pinzani.

Fikru finyu hudhani kuwa sera za vyama zipo kwaajili ya kuombea kura tu katika chaguzi. Na kwa hiyo hujenga chuki zisizo na msingi bila kujali ubora wa sera hizo kwa manufaa ya wananchi.

Simple minded politicians think of next election, but great leaders think of next generations. "Wanasiasa wenye fikra finyu huwazia uchaguzi ujao, lakini viongozi bora hufikiria mustakabali wa vizazi vijavyo"

Ni kwa jinsi hii, vyama makini na vyenye uongozi bora vitaendelea kujipambanua kwa siasa za sera zaidi, huku vyama uchwara vikijikita kwenye siasa za propaganda, fitina, chuki, ubaguzi na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani wao.

Naungana na Watanzania wote katika kuipongeza Chadema kwa kuzindua sera mbadala kuhusu maendeleo ya nchi.
Huu ni uzalendo wa kupigiwa mfano. Hizi ni sera zetu sote bila kujali tofauti za vyama.

Hongera kwa uongozi makini chini ya Ndugu Freeman Aikaeli Mbowe.

Tupambanishe sera na sio mabavu".

Uzi huu naomba Mods uwe maalumu kwaajili ya Uchambuzi wa sera hii kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho,

Nitaanzia kwenye utangulizi kabisa, na kila siku nitakuwa naelezea kwa kina kila sera ilivyoeleza...

Ninaomba tuanze na Dibaji ya Sera hii...

IMG_20180925_172835_520.jpg

IMG_20180929_145335.jpg
Screenshot_20180928-194021.png
 
Tarehe 25/9/2018 Chama kikuu mbadala nchini Tanzania Chadema kimezindua sera yake mpya inayotoa mwelekeo ama dira sahihi ya taifa letu kuelekea 2020.

Katika sera hiyo yameangaziw mengi, na muhimu zaidi ni mambo 12 yanayotawala mnasaba wa sera yenyewe, nimeisoma, ninaendelea kuisoma, na nitahakikisha wote tunaisoma kwa undani na kwa kila neno.

Uzi huu naomba Mods uwe maalumu kwaajili ya Uchambuzi wa sera hii kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho,

Nitaanzia kwenye utangulizi kabisa, na kila siku nitakuwa naelezea kwa kina kila sera ilivyoeleza...

Ninaomba tuanze na Dibaji ya Sera hii...

View attachment 878563
Ili kuwe na uchambuzi wa haki na usawa (balanced discourse) na wenye tija... Asidanganywe mtu, asionewe MTu; basi, tupia humu sera yote kamili ili tujadili tukiwa na uelewa mmoja baada ya kuisoma
 
Tarehe 25/9/2018 Chama kikuu mbadala nchini Tanzania Chadema kimezindua sera yake mpya inayotoa mwelekeo ama dira sahihi ya taifa letu kuelekea 2020.

Katika sera hiyo yameangaziw mengi, na muhimu zaidi ni mambo 12 yanayotawala mnasaba wa sera yenyewe, nimeisoma, ninaendelea kuisoma, na nitahakikisha wote tunaisoma kwa undani na kwa kila neno.

Uzi huu naomba Mods uwe maalumu kwaajili ya Uchambuzi wa sera hii kuanzia ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho,

Nitaanzia kwenye utangulizi kabisa, na kila siku nitakuwa naelezea kwa kina kila sera ilivyoeleza...

Ninaomba tuanze na Dibaji ya Sera hii...

View attachment 878563
Bravo. Jericho.
Ccm wanajiita masikini wanyonge wajamaa, wakati viongozi wao ni mabepari hizo habari chadema hawatakikusisikia,

Wenzetu ccm sifa ya kuwa kiongozi in umasikini,

Eti sasa chini ya mwenyekiti wao mpya wana Sera ya waliokuwa wanaishi kama malaika waishi kama mashetani.

Chadema wanasema kila MTU ataishi kama malaika
 
Ile ya mwanzo imeisha kilimo kwanza sasa tuna Raisi mpya na nchi ya viwanda
Rais ni yuleyule mnabadilisha maneno tu siyo mtazamo sababu mtazamo unatokana na fikra za anayewaongoza.
 
Mimi toka nishuhudie madawa ya kulevya yakiuzwa na mabaunsa wa club billicanas nikasema sitakuja kuamini CHAMA kinachoongozwa na mmiliki wa club hio.never!
 
Naamini hii sera inatakiwa iwe hapa katika PDF format ili tuweze kuisambaza kwa watanzania walio wengi. Wazo hili linazingatia ukweli kuwa walengwa wengi watakaoweza kuisoma hii sera kwa uelewa wana nyenzo zinazotakiwa kuisomea kwenye digital devices. Pia wazo hili lipo sawia na mwelekeo wa CHADEMA kuwa tunatakiwa kuwaza katika mfumo wa kisasa kuliko ku-deal na mambo PHYSICAL.
 
Wemeandaa sera ili waseme serikali inaendeshwa bila sera,it's to late kama waliacha kukemea mafisadi wakapokea mafisadi hapo wanaada wananchi wakushikiwa akili na akina mbowe like.
Kwa nini uwawekee mambo unayofikiria wewe, kwa nini tusiichambue kwanza tukiona haiendani na mahitaji ya Taifa hili si tunaachana nao tunaendelea na ile ya kijani.
 
Back
Top Bottom