UCHAMBUZI: Adhabu waliyopewa wanafunzi wanaoshukiwa kuchoma shule sio sahihi kwa 100%

Mkuu hakuna cha kushangaza hapo, kama watu wazima waliweza kupanga kumshambulia mbunge kwenye makazi ya wabunge, na vyombo vya dola havijachukua hatua yoyote, ni kipi cha kushangaza kwa hao watoto kuchoma bweni?
Point.
 
Mi nafikiri adhabu hii ingekuwa nzuri zaidi .....hapo ni kama wamesamehewa
tapatalk_1570265222638.jpeg
 
Adhabu ya viboko inathibitisha unyani wa mwafrica, kwamba bila mijeledi haendi. Upuuzi huu hutauona nchi zilizoendelea, na wanafanya vema kielimu, ndio wagunduzi wa vitu mbalimbali, ndio wanaoipeleka mbele dunia kitechnolojia. Sisi pamoja nakuchapana kwetu, hakuna cha maana tulichowahi kuifanyia dunia, akili zetu ndio zimeishia hapo kufikiri mtoto hawezi kwenda bila viboko. Matokeo yake mtoto anaiona shule kama jehanamu, walimu anawaona ni maadui, sasa hata kuelewa anachofundishwa inakuwa tabu. Maana ni hofu tu akiikaribia shule, wakati wenzetu walioendelea wanajua ku deal na wanafunzi watukutu, sisi watu weusi tunaamini kwenye mabavu. Anayedhani kwamba viboko ndio suluhisho aseme hapa kama wanafunzi wanaochapwa wana uwezo mkubwa kielimu kuliko wanafunzi wa nchi zile zilizoendelea ambazo viboko ni marufuku, vinginevyo utaiaminisha dunia kwamba waafrica ni wanyama pori hivyo bila viboko hakuna njia inayoweza kuwarekebisha.
Hao unaosema wameendelea na hawachapani viboko ndio walikuja uku kwetu walipoona hatuelewi mpaka tupigwe viboko ndio waliamua iwe hivyo kwaiyo ili sisi tuendelee viboko lazima
 
Kwa hiyo unasema mwafrica si binadamu wa kawaida ni lazima achapwe viboko?
 
Mwaka 1998 kwenye michezo ya UMISETA wilaya ya Sumbawanga mjini, kulikuwepo na dabi ya muda mrefu kati ya KANTALAMBA NA MAZWI, dabi hii ilikua ni zaidi ya vita kwakua zilikua ni shule hasimu nje na ndani ya uwanja.

Vijana wa Mazwi wakakodi Basi la Sumri kuwaleta uwanjani (Mandela), Basi lile dereva akalizungusha uwanjani kabla ya wachezaji na vijana wa Mazwi kushuka. katika mzunguko ule vijana wa Mazwi wakawaonyesha alama ya dole la kati wanafunzi wa KANTALAMBA, subra ikawashinda wakalipopoa gari lile kwa mawe polisi wakaingilia kati mechi ikavunjika,l.

Asubuhi ya siku iliyofuata vijana wa KANTALAMBA wakapanga njama kulivamia gari lile likiwa katika safari likiwa na abiria 65 toka Sumbawanga kuelekea mbeya. Wakalishambulia kwa mawe na kuvunja vioo, bahati nzuri madhara hayakua makubwa ukiachia mbali mvajeruhi madogo ya kukatwa na vioo pamoja na mawe yaliyomjeruhi dereva na baadhi ya abiria.

Ni hayo tu.
 
Subiri muda kidogo tu, utasikia serikali ya CCM yennye huruma imewasamehe warudi shuleni haraka. Kila tatizo ni mtego na fursa kwa CCM.
Kwa masikitiko makubwa ninaandika mambo haya...

Sote tumesikia na wengine wameona, wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa shule moja ya sekondari huko Mbeya ambao wanadaiwa kuchoma moto mabweni ya shule yao, wakicharazwa viboko hadharani na mkuu wa mkoa wa Mbeya, wakitangaziwa kufukuzwa shule na wazazi wao kutakiwa kulipa gharama za kufidia uharibifu wote huo.

Ni uamuzi uliokosa subira, hekima, busara, utu na haki. Na hapa nitaanisha sababu za msingi kabisa.

Kwanza kabisa ni kuwa adhabu hizo zimewagusa wanafunzi wote zaidi ya 300 pasipo kuzingatia nani amehusika, amehusikaje na nani hakuhusika. Makosa ya wachache au wengi yamewagharimu wote. Na hili sio haki kabisa.

Jambo la pili ni kuwa wanafunzi hao wamehukumiwa pasipo kusikilizwa. Wengi wetu mpaka sasa hatujui nini kiini cha hayo yote kutokea. Habari iliyopo ni kuwa wanafunzi wamechoma moto shule! Nani kawachochea au nini kimewasukuma hilo halisemwi wazi. (Na jambo hilo limefanywa kimakusudi)

Kwa mtitiriko wa hayo mambo mawili hapo juu, tunapata taswira pana kuwa huenda hata uchunguzi wa kina na huru haukufanyika na hautakuja kufanyika ili kufahamu chanzo na wahusika wa tukio. Kilichofanyika ni tuhuma, hukumu na utekelezaji wa hukumu!

Yote tisa, aina ya adhabu na namna adhabu hiyo ilivyotolewa imekwenda kinyume cha misingi ya haki na sheria. Yaani kosa linalodaiwa kufanywa na Mwanafunzi akiwa shuleni hukumu imetolewa moja kwa moja na mkuu wa mkoa na kisha Rais wa nchi! Yuko wapi mwalimu, mwalimu mkuu, bodi ya shule, afisa elimu nk. Sheria inasemaje? Kama kuna jinai kwanini wasishtakiwe mahakamani?

Sehemu kubwa ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita wana umri wa miaka 18 au zaidi. Hivi tulishawahi kujiuliza adhabu ya viboko hadharani inaweza kuwa ni suluhisho la msingi kuweza kumrekebisha mtu mzima au ni namna ya kumvunjia heshima ya utu wake?

Hivi kumfukuza mwanafunzi shule ni njia ya kumwadhibu mwanafunzi aliyekosea au kumharibia maisha yake yote?

Hivi kuwaambia wazazi wote wa hao watoto walipe zaidi ya laki 2, ni jambo sahihi?

ANGALIZO.
Binafsi ninaunga mkono adhabu ya viboko kwa mtoto(sio viboko kwa mtu mzima) lakini adhabu hiyo ifanywe na mtu sahihi(hususani mwalimu au mzazi), kwa namna sahihi, wakati sahihi na mahali sahihi huku ikilenga kumrekebisha mtoto na sio kumkomoa mtoto.
 
Nafikili adhabu waliopewa hao wanafunzi haitoshi, ikiwezekana wangekatwa mikono ili wanafunzi wengine wajifunze kupitia jambo hili. Hao haki za binadam nao wakileta fyoko timuaaa kule. Pumbavu saana.

Kata mikono waliokwapua trillion1.5

CAG ALISEMA HAZIJULIKANI ZILIPOENDA (Nyaraka za matumizi hazikuoneshwa / hazipo)

1.5 trillion tunajenga mabweni mangapi?
 
Lijamaa halijawahi kuchapa mtoto siku ile akaona ajaribu siku ile,nadhani aliona raha hivo watumishi mnafuata hii awamu nahisi hata mawaziri wataanza kula viboko vya mr magogoni
 
Ha!ha!ha!umenikumbusha mbaliiii,nahisi we know each other 😁😂😀😁
Km mtu wa nzovwe tunajuana,mboga zao zile hasa saladi wanaita nshaiba sana nilikua nazipenda halafu mtaani hazipo basi ilikua sarakasi tu.bahati hawajawahi kunishika
 
bado natafakari kitendo cha kufukuza watoto shule kama kina tija kwa taifa...
Revenue collection scheme. Kila mtoto anapaswa kurudi shule na 200,000/- ila hao 14 wanaotuhumiwa kama vinara, watapeleka 500,000 kila mmoja kabla ya tarehe 18 Oct. Rais keshacement haya maagizo
 
Kwa masikitiko makubwa ninaandika mambo haya...

Sote tumesikia na wengine wameona, wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa shule moja ya sekondari huko Mbeya ambao wanadaiwa kuchoma moto mabweni ya shule yao, wakicharazwa viboko hadharani na mkuu wa mkoa wa Mbeya, wakitangaziwa kufukuzwa shule na wazazi wao kutakiwa kulipa gharama za kufidia uharibifu wote huo.

Ni uamuzi uliokosa subira, hekima, busara, utu na haki. Na hapa nitaanisha sababu za msingi kabisa.

Kwanza kabisa ni kuwa adhabu hizo zimewagusa wanafunzi wote zaidi ya 300 pasipo kuzingatia nani amehusika, amehusikaje na nani hakuhusika. Makosa ya wachache au wengi yamewagharimu wote. Na hili sio haki kabisa.

Jambo la pili ni kuwa wanafunzi hao wamehukumiwa pasipo kusikilizwa. Wengi wetu mpaka sasa hatujui nini kiini cha hayo yote kutokea. Habari iliyopo ni kuwa wanafunzi wamechoma moto shule! Nani kawachochea au nini kimewasukuma hilo halisemwi wazi. (Na jambo hilo limefanywa kimakusudi)

Kwa mtitiriko wa hayo mambo mawili hapo juu, tunapata taswira pana kuwa huenda hata uchunguzi wa kina na huru haukufanyika na hautakuja kufanyika ili kufahamu chanzo na wahusika wa tukio. Kilichofanyika ni tuhuma, hukumu na utekelezaji wa hukumu!

Yote tisa, aina ya adhabu na namna adhabu hiyo ilivyotolewa imekwenda kinyume cha misingi ya haki na sheria. Yaani kosa linalodaiwa kufanywa na Mwanafunzi akiwa shuleni hukumu imetolewa moja kwa moja na mkuu wa mkoa na kisha Rais wa nchi! Yuko wapi mwalimu, mwalimu mkuu, bodi ya shule, afisa elimu nk. Sheria inasemaje? Kama kuna jinai kwanini wasishtakiwe mahakamani?

Sehemu kubwa ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita wana umri wa miaka 18 au zaidi. Hivi tulishawahi kujiuliza adhabu ya viboko hadharani inaweza kuwa ni suluhisho la msingi kuweza kumrekebisha mtu mzima au ni namna ya kumvunjia heshima ya utu wake?

Hivi kumfukuza mwanafunzi shule ni njia ya kumwadhibu mwanafunzi aliyekosea au kumharibia maisha yake yote?

Hivi kuwaambia wazazi wote wa hao watoto walipe zaidi ya laki 2, ni jambo sahihi?

ANGALIZO.
Binafsi ninaunga mkono adhabu ya viboko kwa mtoto(sio viboko kwa mtu mzima) lakini adhabu hiyo ifanywe na mtu sahihi(hususani mwalimu au mzazi), kwa namna sahihi, wakati sahihi na mahali sahihi huku ikilenga kumrekebisha mtoto na sio kumkomoa mtoto.
Kwa sehemu nakubalina na hoja zako na zingine sikubaliani nazo

Naomba nijibu hoja zako Kama ifuatavyo Aya y mwisho kabisa nakubalina nayo na Sina tatizo katika Hilo

Ila Aya 3 kabla ya Aya ya mwisho naomba nizijibu

Kuhusu kutoa adhabu ya viboko kwa wanafunzi wa kidato Cha tano na sita ambao wewe umewaita watu wazima kulingana na miongozo na taratibu za shule ilimradi tu unasoma unawajika kutii na Kama usipo tii adhabu itakufata tu bila kujali umri wako

Pili umekua na hoja kuhusu kufukuza shule Kama sehemu ya adhabu hili liko wazi kabisa kwa watu/wanafunzi ambao wao watakua na makosa ya jinia sheria inatoa ruhusa kwa mkuu wa shule kwa kushilikiana na bodi ya shule kuwafukuza shule wanafunzi hao ambao wamekutwa na makosa ya jinia

MWISHO

mkuu wa mkoa kutoa adhabu yeye mwenyewe kwa kuwatandika viboko wanafunzi si sawa hata kidogo Kuna mamlaka zenye kutakiwa kufanya hayo ambazo ni mkuu wa shule
Pamoja na walimu wake
 
Kwa masikitiko makubwa ninaandika mambo haya...

Sote tumesikia na wengine wameona, wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa shule moja ya sekondari huko Mbeya ambao wanadaiwa kuchoma moto mabweni ya shule yao, wakicharazwa viboko hadharani na mkuu wa mkoa wa Mbeya, wakitangaziwa kufukuzwa shule na wazazi wao kutakiwa kulipa gharama za kufidia uharibifu wote huo.

Ni uamuzi uliokosa subira, hekima, busara, utu na haki. Na hapa nitaanisha sababu za msingi kabisa.

Kwanza kabisa ni kuwa adhabu hizo zimewagusa wanafunzi wote zaidi ya 300 pasipo kuzingatia nani amehusika, amehusikaje na nani hakuhusika. Makosa ya wachache au wengi yamewagharimu wote. Na hili sio haki kabisa.

Jambo la pili ni kuwa wanafunzi hao wamehukumiwa pasipo kusikilizwa. Wengi wetu mpaka sasa hatujui nini kiini cha hayo yote kutokea. Habari iliyopo ni kuwa wanafunzi wamechoma moto shule! Nani kawachochea au nini kimewasukuma hilo halisemwi wazi. (Na jambo hilo limefanywa kimakusudi)

Kwa mtitiriko wa hayo mambo mawili hapo juu, tunapata taswira pana kuwa huenda hata uchunguzi wa kina na huru haukufanyika na hautakuja kufanyika ili kufahamu chanzo na wahusika wa tukio. Kilichofanyika ni tuhuma, hukumu na utekelezaji wa hukumu!

Yote tisa, aina ya adhabu na namna adhabu hiyo ilivyotolewa imekwenda kinyume cha misingi ya haki na sheria. Yaani kosa linalodaiwa kufanywa na Mwanafunzi akiwa shuleni hukumu imetolewa moja kwa moja na mkuu wa mkoa na kisha Rais wa nchi! Yuko wapi mwalimu, mwalimu mkuu, bodi ya shule, afisa elimu nk. Sheria inasemaje? Kama kuna jinai kwanini wasishtakiwe mahakamani?

Sehemu kubwa ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita wana umri wa miaka 18 au zaidi. Hivi tulishawahi kujiuliza adhabu ya viboko hadharani inaweza kuwa ni suluhisho la msingi kuweza kumrekebisha mtu mzima au ni namna ya kumvunjia heshima ya utu wake?

Hivi kumfukuza mwanafunzi shule ni njia ya kumwadhibu mwanafunzi aliyekosea au kumharibia maisha yake yote?

Hivi kuwaambia wazazi wote wa hao watoto walipe zaidi ya laki 2, ni jambo sahihi?

ANGALIZO.
Binafsi ninaunga mkono adhabu ya viboko kwa mtoto(sio viboko kwa mtu mzima) lakini adhabu hiyo ifanywe na mtu sahihi(hususani mwalimu au mzazi), kwa namna sahihi, wakati sahihi na mahali sahihi huku ikilenga kumrekebisha mtoto na sio kumkomoa mtoto.
Umesema vyema
 
Kwa kuongezea ni kuwa adhabu kwa mtoto itolewe na mtu mwenye uelewa na akili timamu. Na siyo lazima iwe fimbo.

Waafrika ndio waliozoea kutandika watoto lakini ndio wanaoongoza kwa ihalifu na mambo ya hovyo Duniani. Na waafrika kieleimu, kiteknolojia na kiufanisi ndiyo walio hohe hahe. Kama fimbo zingekuwa zinamtengeneza mtu basi Waafrika ndio wangekuwa watu bora kwa kila nyanja Duniani.

Pili, huyu aliyetoa adhabu, nina mashaka kama ana uelewa wa kutosha na akili timamu. Kuna wakati aliwahi kutamka kuwa polisi wakiwakamata vibaka wawaue maana yeye aliwahi kumwua wa kwake. Siamini mtu mwenye akili timamu anaweza kunena hivi.
 
Back
Top Bottom