KERO Serikali imeshindwa kudhibiti adhabu za Viboko shuleni?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kumekuwepo na malalamiko mengi juu ya utitiri wa adhabu za viboko shuleni.
Watoto wanaogopa kwenda shuleni kisa adhabu za viboko ni kali na pia namna ya utoaji wa adhabu hiyo umepelekea wanafunzi kuacha shule, ulemavu pamoja na alama zisizifutika yaani makovu ya kudumu.

Upigaji aua utiajia wa adhabu hii umekiuka Sheria ya viboko shuleni. Kwamba mwanafunzi anapaswa apewe adhabu ya viboko na Mwalimu Mkuu au mwalimu wa nidhamu ya hata mwalimu mwingine awaye yote.

Katika kutoa adhabu hiyo lazima mazingira ya makosa yapewe kipaumbele, aina ya kosa na mtenda kosa ana umri gani!

Adhabu ya viboko haipaswi kuzidi viboko vinne (4) kisheria na Kila anayepokea adhabu hiyo anapaswa kirekodiwa katika daftari, ikijumuisha idadi ya viboko na mwalimu aliyotoa adhabu hiyo.

Vile vile utoaji wa adhabu hii unapaswa kuzingatia jinsia na siyo kupiga piga tu kwani kunaweza kusababisha athari kwa wanafunzi kulingana na maumbile yao na umri wao.

Kutoka na hili nipende kutoa rai kwa walimu hasa katika Shule ya Msingi Bwagula na Shule ya Sekondari Tunamkumbuka zote za Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera kwa ukiukwaji wa sheria za viboko shuleni.

Nipende kutoa duku duku langu kwa jamii na Kwa serikali hasa kupitia Afisa Elimu na madawati ya jinsia mashuleni kutatua KERO hizo amabazo zinasababisha, utoro, ulemavu na ukiukwaji wa haki za binadamu.
 
Kama wazazi wenyewe ndio huyu mwandishi kwanini walimu msiachane na kuchapa hayo matoto yao yakajifie mbele na wazazi wao ?
 
Utafiti wa kisayansi umethibitisha kuwa elimu bora BILA viboko inawezekana,futilia mbali hii barbaric copral punishment kwa wanafunzi wetu,Mkwawa CNE mpooooo mnamkumbuka yule jambazi principal aliyeanzisha adhabu hii kwa waalimu watarajiwa?,ilipigwa push back akarudishwa kwa Moshi ndani ya sanduku,salute kwa generation ile kwa push back ile
 
Back
Top Bottom