UCHAMBUZI: Adhabu waliyopewa wanafunzi wanaoshukiwa kuchoma shule sio sahihi kwa 100%

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Messages
5,113
Points
2,000

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2013
5,113 2,000
Kwa masikitiko makubwa ninaandika mambo haya...

Sote tumesikia na wengine wameona, wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa shule moja ya sekondari huko Mbeya ambao wanadaiwa kuchoma moto mabweni ya shule yao, wakicharazwa viboko hadharani na mkuu wa mkoa wa Mbeya, wakitangaziwa kufukuzwa shule na wazazi wao kutakiwa kulipa gharama za kufidia uharibifu wote huo.

Ni uamuzi uliokosa subira, hekima, busara, utu na haki. Na hapa nitaanisha sababu za msingi kabisa.

Kwanza kabisa ni kuwa adhabu hizo zimewagusa wanafunzi wote zaidi ya 300 pasipo kuzingatia nani amehusika, amehusikaje na nani hakuhusika. Makosa ya wachache au wengi yamewagharimu wote. Na hili sio haki kabisa.

Jambo la pili ni kuwa wanafunzi hao wamehukumiwa pasipo kusikilizwa. Wengi wetu mpaka sasa hatujui nini kiini cha hayo yote kutokea. Habari iliyopo ni kuwa wanafunzi wamechoma moto shule! Nani kawachochea au nini kimewasukuma hilo halisemwi wazi. (Na jambo hilo limefanywa kimakusudi)

Kwa mtitiriko wa hayo mambo mawili hapo juu, tunapata taswira pana kuwa huenda hata uchunguzi wa kina na huru haukufanyika na hautakuja kufanyika ili kufahamu chanzo na wahusika wa tukio. Kilichofanyika ni tuhuma, hukumu na utekelezaji wa hukumu!

Yote tisa, aina ya adhabu na namna adhabu hiyo ilivyotolewa imekwenda kinyume cha misingi ya haki na sheria. Yaani kosa linalodaiwa kufanywa na Mwanafunzi akiwa shuleni hukumu imetolewa moja kwa moja na mkuu wa mkoa na kisha Rais wa nchi! Yuko wapi mwalimu, mwalimu mkuu, bodi ya shule, afisa elimu nk. Sheria inasemaje? Kama kuna jinai kwanini wasishtakiwe mahakamani?

Sehemu kubwa ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita wana umri wa miaka 18 au zaidi. Hivi tulishawahi kujiuliza adhabu ya viboko hadharani inaweza kuwa ni suluhisho la msingi kuweza kumrekebisha mtu mzima au ni namna ya kumvunjia heshima ya utu wake?

Hivi kumfukuza mwanafunzi shule ni njia ya kumwadhibu mwanafunzi aliyekosea au kumharibia maisha yake yote?

Hivi kuwaambia wazazi wote wa hao watoto walipe zaidi ya laki 2, ni jambo sahihi?

ANGALIZO.
Binafsi ninaunga mkono adhabu ya viboko kwa mtoto(sio viboko kwa mtu mzima) lakini adhabu hiyo ifanywe na mtu sahihi(hususani mwalimu au mzazi), kwa namna sahihi, wakati sahihi na mahali sahihi huku ikilenga kumrekebisha mtoto na sio kumkomoa mtoto.
 
Mchizi

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2009
Messages
1,625
Points
2,000

Mchizi

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2009
1,625 2,000
Adhabu ya viboko inathibitisha unyani wa mwafrica, kwamba bila mijeledi haendi. Upuuzi huu hutauona nchi zilizoendelea, na wanafanya vema kielimu, ndio wagunduzi wa vitu mbalimbali, ndio wanaoipeleka mbele dunia kitechnolojia. Sisi pamoja nakuchapana kwetu, hakuna cha maana tulichowahi kuifanyia dunia, akili zetu ndio zimeishia hapo kufikiri mtoto hawezi kwenda bila viboko. Matokeo yake mtoto anaiona shule kama jehanamu, walimu anawaona ni maadui, sasa hata kuelewa anachofundishwa inakuwa tabu. Maana ni hofu tu akiikaribia shule, wakati wenzetu walioendelea wanajua ku deal na wanafunzi watukutu, sisi watu weusi tunaamini kwenye mabavu. Anayedhani kwamba viboko ndio suluhisho aseme hapa kama wanafunzi wanaochapwa wana uwezo mkubwa kielimu kuliko wanafunzi wa nchi zile zilizoendelea ambazo viboko ni marufuku, vinginevyo utaiaminisha dunia kwamba waafrica ni wanyama pori hivyo bila viboko hakuna njia inayoweza kuwarekebisha.
 
THE LOST

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Messages
577
Points
1,000

THE LOST

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2017
577 1,000
mkuu Tanzania tunapitia katika jaribu kuu... Mtu mmoja anasimama na kusema sheria ilikosewa kweli? halafu kuna watanzania wanashangilia na kumuunga mkono! binafsi nashindwa kuwaelewa wanaotetea fimbo nyingi kwa wanafunzi wanataka ama ni binadamu wa namna gani.. miaka ya nyuma adhabu ya viboko mashuleni ilikuwa kali na ya kikatili sana lakini tujiulize migomo na matukio ya shule kuchomwa moto yalikuwa mangapi? miaka ya nyuma haukuweza kupita miez 6 bila tukio la moto kuteketeza shule licha ya kuwepo kwa adhabu kali kipindi hiko... now elimu imekuwa so democracy na adhabu za viboko zimepungua ndo maana matukio hayo si tu yamepungua bali hata nidhamu ya wanafunzi imeongezeka tofauti na miaka ya 90s to early 2000s ambapo wanafunzi kuchoma moto shule was a normal issues. Watu wanadai mara oooh watoto wa siku hizi hawana nidhamu kwa sababu hawachapwi viboko serious! hivi kati ya watoto wa sasa hivi na kipindi cha nyuma wapi wenye nidhamu? kipindi kipi shule zilikuwa makundi ya wavuta bangi? kati ya sasa na zamani?
 
babukijana

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2009
Messages
6,206
Points
2,000

babukijana

JF-Expert Member
Joined Jul 21, 2009
6,206 2,000
bado natafakari kitendo cha kufukuza watoto shule kama kina tija kwa taifa...
300,kwa kosa la mpuuzi mmoja au wawili tu.
Wangewakabidhi hao JKT nzovwe au kwa bwana magereza na heka zao kadhaa za kulima,kupalilia na kuvuna na kupeleka mazao sokoni huku wenzao wakisoma.wakimaliza hapo watajua warudi elimu ya watu wazima au waende mtaani.
 
THE LOST

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Messages
577
Points
1,000

THE LOST

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2017
577 1,000
nchi imekuwa vuluvulu hapa naona kabisa kama taifa tumepotoka, wanafunzi hawafukuzwi kwa makosa ya wengine... watu wanamtetea rais wanashindwa kuelewa maana ya EFA na haki ya mtoto.. hapa dunia lazima ituchore tu...
 
sokowelehk

Senior Member
Joined
Sep 16, 2018
Messages
141
Points
250

sokowelehk

Senior Member
Joined Sep 16, 2018
141 250
Nafikili adhabu waliopewa hao wanafunzi haitoshi, ikiwezekana wangekatwa mikono ili wanafunzi wengine wajifunze kupitia jambo hili. Hao haki za binadam nao wakileta fyoko timuaaa kule. Pumbavu saana.
 
Onjwaria

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
928
Points
1,000

Onjwaria

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
928 1,000
Wakuu kuna mtu mmoja alitamba kuwa alivunja vioo vya madirisha......sijui wapi ila alikuja kutengeneza majuzi baada ya miaka 40 na usher. Maamuzi ya juzi tuyatafakari upya. Tuelewe kuwa miamvuli ya kukusanya kundi la watu regardless ni Watoto au ni watu wazima matukio hayakosekani. Leo hii hata ukiwachukua MDC au MRC wote ukawaweka Shule saikolojia yao itakuwa tofauti na jinsi walivyo hivi sasa. Matendo yao yatashangaza kitaswira na ukija kuwachunguza utakuta ni tofauti kabisa kimaadili.
Hili tukio la wanafunzi linaweza kupatiwa ufumbuzi na siyo sababu mtu kumiliki simu ndiyo awe na hatia. Nijuavyo kwa level ya advance simu ni msaada mkubwa kabisa pale ambapo unakuta Mwalimu pengine wa somo Fulani aamekosekana. Tujaribu kufanya uchunguzi na kubaini waliohusika. Kufanya upelelezi kwa wanafunzi ni rahisi sana kuliko kumpeleleza jambazi. Tutoe nafasi walimu wafanye hiyo kazi na ninaamini walimu nao wanahusika kwa asilimia Fulani. Tupunguze jazba
 
Mateja M.G Yango

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Messages
605
Points
1,000

Mateja M.G Yango

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2013
605 1,000
kuna notion ipo kwa sasa among Tanzanians ya kuonyesha kila jambo linalofanywa na uongozi ni bovu.

Kwangu mimi sioni shida mkuu wa mkoa kuwachapa hao wayoto, sababu baada ya simu zao kukamatwa ndio wakachoma moto mabweni mawili ili warudishiwe simu zao.

Watoto wote kulipa laki mbili ndio warudi kuendelea na shule ni sawa pia, namna hiyo ni funzo, watakiwa na uchungu wa matendo ya ajabu maisha yao yote, wazazi always watakuwa karibu kuangalia mienendo ya watoto.
 
ZALEMDA

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Messages
588
Points
500

ZALEMDA

JF-Expert Member
Joined Aug 15, 2017
588 500
Kwa masikitiko makubwa ninaandika mambo haya...

Sote tumesikia na wengine wameona, wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa shule moja ya sekondari huko Mbeya ambao wanadaiwa kuchoma moto mabweni ya shule yao, wakicharazwa viboko hadharani na mkuu wa mkoa wa Mbeya, wakitangaziwa kufukuzwa shule na wazazi wao kutakiwa kulipa gharama za kufidia uharibifu wote huo.

Ni uamuzi uliokosa subira, hekima, busara, utu na haki. Na hapa nitaanisha sababu za msingi kabisa.

Kwanza kabisa ni kuwa adhabu hizo zimewagusa wanafunzi wote zaidi ya 300 pasipo kuzingatia nani amehusika, amehusikaje na nani hakuhusika. Makosa ya wachache au wengi yamewagharimu wote. Na hili sio haki kabisa.

Jambo la pili ni kuwa wanafunzi hao wamehukumiwa pasipo kusikilizwa. Wengi wetu mpaka sasa hatujui nini kiini cha hayo yote kutokea. Habari iliyopo ni kuwa wanafunzi wamechoma moto shule! Nani kawachochea au nini kimewasukuma hilo halisemwi wazi. (Na jambo hilo limefanywa kimakusudi)

Kwa mtitiriko wa hayo mambo mawili hapo juu, tunapata taswira pana kuwa huenda hata uchunguzi wa kina na huru haukufanyika na hautakuja kufanyika ili kufahamu chanzo na wahusika wa tukio. Kilichofanyika ni tuhuma, hukumu na utekelezaji wa hukumu!

Yote tisa, aina ya adhabu na namna adhabu hiyo ilivyotolewa imekwenda kinyume cha misingi ya haki na sheria. Yaani kosa linalodaiwa kufanywa na Mwanafunzi akiwa shuleni hukumu imetolewa moja kwa moja na mkuu wa mkoa na kisha Rais wa nchi! Yuko wapi mwalimu, mwalimu mkuu, bodi ya shule, afisa elimu nk. Sheria inasemaje? Kama kuna jinai kwanini wasishtakiwe mahakamani?

Sehemu kubwa ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita wana umri wa miaka 18 au zaidi. Hivi tulishawahi kujiuliza adhabu ya viboko hadharani inaweza kuwa ni suluhisho la msingi kuweza kumrekebisha mtu mzima au ni namna ya kumvunjia heshima ya utu wake?

Hivi kumfukuza mwanafunzi shule ni njia ya kumwadhibu mwanafunzi aliyekosea au kumharibia maisha yake yote?

Hivi kuwaambia wazazi wote wa hao watoto walipe zaidi ya laki 2, ni jambo sahihi?

ANGALIZO.
Binafsi ninaunga mkono adhabu ya viboko kwa mtoto(sio viboko kwa mtu mzima) lakini adhabu hiyo ifanywe na mtu sahihi(hususani mwalimu au mzazi), kwa namna sahihi, wakati sahihi na mahali sahihi huku ikilenga kumrekebisha mtoto na sio kumkomoa mtoto.

Mwanafunzi wa sekondari awe ni above 18 ni mtoto tu!!adhabu nyengine inatolewa ili iwe fundisho kwa wengine
 
Coaster2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2018
Messages
1,510
Points
2,000

Coaster2015

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2018
1,510 2,000
Wakuu kuna mtu mmoja alitamba kuwa alivunja vioo vya madirisha......sijui wapi ila alikuja kutengeneza majuzi baada ya miaka 40 na usher. Maamuzi ya juzi tuyatafakari upya. Tuelewe kuwa miamvuli ya kukusanya kundi la watu regardless ni Watoto au ni watu wazima matukio hayakosekani. Leo hii hata ukiwachukua MDC au MRC wote ukawaweka Shule saikolojia yao itakuwa tofauti na jinsi walivyo hivi sasa. Matendo yao yatashangaza kitaswira na ukija kuwachunguza utakuta ni tofauti kabisa kimaadili.
Hili tukio la wanafunzi linaweza kupatiwa ufumbuzi na siyo sababu mtu kumiliki simu ndiyo awe na hatia. Nijuavyo kwa level ya advance simu ni msaada mkubwa kabisa pale ambapo unakuta Mwalimu pengine wa somo Fulani aamekosekana. Tujaribu kufanya uchunguzi na kubaini waliohusika. Kufanya upelelezi kwa wanafunzi ni rahisi sana kuliko kumpeleleza jambazi. Tutoe nafasi walimu wafanye hiyo kazi na ninaamini walimu nao wanahusika kwa asilimia Fulani. Tupunguze jazba
Viongozi wa serikali hii stupid sana, juzi tuliambiwa walimu wa shule hiyo waliwatishia wanafunzi kwamba wasingetaja waliohusika na tukio la kuchoma moto bweni wangefukuzwa wote na wakaweza kuwataja wanafunzi waliohusika na kuchoma moto bweni, sasa uamuzi wa rc kuwafukuza wanafunzi wote ni ujuha kwa sababu kuna watoto wa watu pale hawahusiki na unawataka walipe, kwa nini wasichukue hela za serikali ambazo huwa wanazitumia kuhonga viongozi wa upinzani ili wahamie ccm na kusababisha gharama za kurudia uchaguzi wakazitumie kujenga hayo mabweni mawili ?!!, magufuli mwenyewe anakiri aliwahi kuvunja madirisha na milango kwenye shule aliyosomea na hakufukuzwa.
 
ighaghe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2013
Messages
1,413
Points
2,000

ighaghe

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2013
1,413 2,000
Adhabu ya viboko inathibitisha unyani wa mwafrica, kwamba bila mijeledi haendi. Upuuzi huu hutauona nchi zilizoendelea, na wanafanya vema kielimu, ndio wagunduzi wa vitu mbalimbali, ndio wanaoipeleka mbele dunia kitechnolojia. Sisi pamoja nakuchapana kwetu, hakuna cha maana tulichowahi kuifanyia dunia, akili zetu ndio zimeishia hapo kufikiri mtoto hawezi kwenda bila viboko. Matokeo yake mtoto anaiona shule kama jehanamu, walimu anawaona ni maadui, sasa hata kuelewa anachofundishwa inakuwa tabu. Maana ni hofu tu akiikaribia shule, wakati wenzetu walioendelea wanajua ku deal na wanafunzi watukutu, sisi watu weusi tunaamini kwenye mabavu. Anayedhani kwamba viboko ndio suluhisho aseme hapa kama wanafunzi wanaochapwa wana uwezo mkubwa kielimu kuliko wanafunzi wa nchi zile zilizoendelea ambazo viboko ni marufuku, vinginevyo utaiaminisha dunia kwamba waafrica ni wanyama pori hivyo bila viboko hakuna njia inayoweza kuwarekebisha.
Ila mkuu, kuna watoto watukutu jamani, Yaani kama hakuna kinachomtisha ili apunguze utukutu utakuta kuna mambo ya ajabu sana yamefanyika. Sijajua wenzetu wamefaulu vipi kudeal na vizazi vyao bila fimbo.
 
Forum statistics

Threads 1,379,949
Members 525,639
Posts 33,761,999
Top