Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,105
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema mwanafunzi akichelewa kuripoti shule atalimishwa matuta kumi, kauli hii ni amri kwa wakuu wakuu wa shule lakini tujiulize ni amri halali?
Kwanini mwanafunzi anachelewa shule? Ni mwanafunzi wa umri gani atalimishwa matuta kumi? Je hata wanafunzi wa private school ambao wengi ni watoto wa viongozi na wanasiasa wakichelewa watalimishwa matatu kumi au ni agizo kwa watoto wa wakulima pekee?
Ni kwa namna gani kauli hii inamshinikiza mzazi kutimiza wajibu wake? Kama mtoto hajanukuliwa uniform akichelewa shule anastahili adhabu pia?
Kwanini tunaamini watoto ndio wanapaswa kupewa adhabu badala ya wazazi?