UCHAMBUZI: Adhabu waliyopewa wanafunzi wanaoshukiwa kuchoma shule sio sahihi kwa 100%

Kwa masikitiko makubwa ninaandika mambo haya...

Sote tumesikia na wengine wameona, wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa shule moja ya sekondari huko Mbeya ambao wanadaiwa kuchoma moto mabweni ya shule yao, wakicharazwa viboko hadharani na mkuu wa mkoa wa Mbeya, wakitangaziwa kufukuzwa shule na wazazi wao kutakiwa kulipa gharama za kufidia uharibifu wote huo.

Ni uamuzi uliokosa subira, hekima, busara, utu na haki. Na hapa nitaanisha sababu za msingi kabisa.

Kwanza kabisa ni kuwa adhabu hizo zimewagusa wanafunzi wote zaidi ya 300 pasipo kuzingatia nani amehusika, amehusikaje na nani hakuhusika. Makosa ya wachache au wengi yamewagharimu wote. Na hili sio haki kabisa.

Jambo la pili ni kuwa wanafunzi hao wamehukumiwa pasipo kusikilizwa. Wengi wetu mpaka sasa hatujui nini kiini cha hayo yote kutokea. Habari iliyopo ni kuwa wanafunzi wamechoma moto shule! Nani kawachochea au nini kimewasukuma hilo halisemwi wazi. (Na jambo hilo limefanywa kimakusudi)

Kwa mtitiriko wa hayo mambo mawili hapo juu, tunapata taswira pana kuwa huenda hata uchunguzi wa kina na huru haukufanyika na hautakuja kufanyika ili kufahamu chanzo na wahusika wa tukio. Kilichofanyika ni tuhuma, hukumu na utekelezaji wa hukumu!

Yote tisa, aina ya adhabu na namna adhabu hiyo ilivyotolewa imekwenda kinyume cha misingi ya haki na sheria. Yaani kosa linalodaiwa kufanywa na Mwanafunzi akiwa shuleni hukumu imetolewa moja kwa moja na mkuu wa mkoa na kisha Rais wa nchi! Yuko wapi mwalimu, mwalimu mkuu, bodi ya shule, afisa elimu nk. Sheria inasemaje? Kama kuna jinai kwanini wasishtakiwe mahakamani?

Sehemu kubwa ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita wana umri wa miaka 18 au zaidi. Hivi tulishawahi kujiuliza adhabu ya viboko hadharani inaweza kuwa ni suluhisho la msingi kuweza kumrekebisha mtu mzima au ni namna ya kumvunjia heshima ya utu wake?

Hivi kumfukuza mwanafunzi shule ni njia ya kumwadhibu mwanafunzi aliyekosea au kumharibia maisha yake yote?

Hivi kuwaambia wazazi wote wa hao watoto walipe zaidi ya laki 2, ni jambo sahihi?

ANGALIZO.
Binafsi ninaunga mkono adhabu ya viboko kwa mtoto(sio viboko kwa mtu mzima) lakini adhabu hiyo ifanywe na mtu sahihi(hususani mwalimu au mzazi), kwa namna sahihi, wakati sahihi na mahali sahihi huku ikilenga kumrekebisha mtoto na sio kumkomoa mtoto.
Exactly the point, there are rules to be followed in administering any form of punishement. We don't just act as political ragtags....
 
Kwa maoni yangu, Bodi ya Shule, RC hata na Rais wamewaonea huruma vijana hawa na ndio maana wakawapa adhabu "ndogo" ya kuchapwa viboko, wazazi wao kulipa gharama za uharibifu na kufukuzwa shule. Wewe unahisi unawapenda na kuwatetea ndio unataka kuwaangamiza. Eti wapelekwe mahakamani. Kwa taarifa yako, adhabu ya kuchoma moto jengo inaenda hadi KIFUNGO CHA MAISHA!

Naona unaamini sana kwenye Collective Punishment kama walivyokuwa wakoloni.
 
Watoto watukutu lazima waadhibiwe, je ungesemaje kama wangefunga mabweni na kuchoma wenzao kama Shaulitanga Moshi??
Unachoma shule tena Formsix unategemea nini, una akili kweli simu ni bora kuliko elimu yako, utasomea wapi??
Wafukuzwe wazazi washiriki kujenga hayo mabweni!!
Tusitetee ujinga tutatengeneza taifa la watu wa ajabu sana!!
Hata hoja hamjailewa mnakimbilia kukosoa, hivi ninyi watu mna matatizo gani humo vichwani mwemu. Mbona ameeleweka vizuri tu, kwamba watoto watukutu lazima wapewe adhabu lakini lazima taratibu na sheria zifuatwe. Hapa napo ni pagumu kuelewa ???
 
Hata hoja hamjailewa mnakimbilia kukosoa, hivi ninyi watu mna matatizo gani humo vichwani mwemu. Mbona ameeleweka vizuri tu, kwamba watoto watukutu lazima wapewe adhabu lakini lazima taratibu na sheria zifuatwe. Hapa napo ni pagumu kuelewa ???
Hata sisi hatujasema sheria isifuatwe. Na kwa taarifa yako utaratibu wote wa kufuatwa tunaujua.
 
Hata sisi hatujasema sheria isifuatwe. Na kwa taarifa yako utaratibu wote wa kufuatwa tunaujua.
Hujui kitu, Hufahamu kitu: Ungekuwa unafahamu walau chembe usingeongea kama nyapara wa kikoloni kufurahia Collective Punishment vis-a-vis Punishment Before Trial. A simple objectivity and you will clearly see how wrong the Government is.

Mnanikumbusha yaleyale ya Raisi Mwinyi na Warioba kuteka Raisi wa UDSM na kumpeleka bandarini kisa mgomo wa wanafunzi wa chuo.

Najua huwezi kuelewa kwasababu huu unyama (Barbarism) and (Brutality) ni sehemu ya tamaduni zenu: Deeply embedded in your ways of reason and purview of the world.
 
Mkuu wa mkoa ni mzazi na mwenyekiti wa usalama, kuchoma shule sio jambo la masihara
 
Hata hoja hamjailewa mnakimbilia kukosoa, hivi ninyi watu mna matatizo gani humo vichwani mwemu. Mbona ameeleweka vizuri tu, kwamba watoto watukutu lazima wapewe adhabu lakini lazima taratibu na sheria zifuatwe. Hapa napo ni pagumu kuelewa ???
Taratibu za sheria zipi. Sheria zenyewe zakucopy na kupest kutoka kwa mkoloni.
Madogo ile azabu ni ndogo sana. Nafikiri wote watupwe jena mienzi sita kwanza wakitoka huko wapate akili
 
Hujui kitu, Hufahamu kitu: Ungekuwa unafahamu walau chembe usingeongea kama nyapara wa kikoloni kufurahia Collective Punishment vis-a-vis Punishment Before Trial. A simple objectivity and you will clearly see how wrong the Government is.

Mnanikumbusha yaleyale ya Raisi Mwinyi na Warioba kuteka Raisi wa UDSM na kumpeleka bandarini kisa mgomo wa wanafunzi wa chuo.

Najua huwezi kuelewa kwasababu huu unyama (Barbarism) and (Brutality) ni sehemu ya tamaduni zenu: Deeply embedded in your ways of reason and purview of the world.
Pumba pumba na kiingereza chako cha chekechea
 
Kwa sehemu nakubalina na hoja zako na zingine sikubaliani nazo

Naomba nijibu hoja zako Kama ifuatavyo Aya y mwisho kabisa nakubalina nayo na Sina tatizo katika Hilo

Ila Aya 3 kabla ya Aya ya mwisho naomba nizijibu


Kuhusu kutoa adhabu ya viboko kwa wanafunzi wa kidato Cha tano na sita ambao wewe umewaita watu wazima kulingana na miongozo na taratibu za shule ilimradi tu unasoma unawajika kutii na Kama usipo tii adhabu itakufata tu bila kujali umri wako


Pili umekua na hoja kuhusu kufukuza shule Kama sehemu ya adhabu hili liko wazi kabisa kwa watu/wanafunzi ambao wao watakua na makosa ya jinia sheria inatoa ruhusa kwa mkuu wa shule kwa kushilikiana na bodi ya shule kuwafukuza shule wanafunzi hao ambao wamekutwa na makosa ya jinia


MWISHO

mkuu wa mkoa kutoa adhabu yeye mwenyewe kwa kuwatandika viboko wanafunzi si sawa hata kidogo Kuna mamlaka zenye kutakiwa kufanya hayo ambazo ni mkuu wa shule
Pamoja na walimu wake
Hizo taratibu mnazijua nyie. Tushawachapa viboko. Tuchawasimamisha masomo kwa muda na wakirudi warudi na hizo 200k .
Kama hamjatizika nendeni kunakofaa kutafuta haki mkazitafute
 
Haya ni natokeo yakuendekeza uzembe mashuleni. Kufutwa kwa viboko ni kosa kubwa sana mashuleni.
 
Adhabu ya viboko inathibitisha unyani wa mwafrica, kwamba bila mijeledi haendi. Upuuzi huu hutauona nchi zilizoendelea, na wanafanya vema kielimu, ndio wagunduzi wa vitu mbalimbali, ndio wanaoipeleka mbele dunia kitechnolojia. Sisi pamoja nakuchapana kwetu, hakuna cha maana tulichowahi kuifanyia dunia, akili zetu ndio zimeishia hapo kufikiri mtoto hawezi kwenda bila viboko. Matokeo yake mtoto anaiona shule kama jehanamu, walimu anawaona ni maadui, sasa hata kuelewa anachofundishwa inakuwa tabu. Maana ni hofu tu akiikaribia shule, wakati wenzetu walioendelea wanajua ku deal na wanafunzi watukutu, sisi watu weusi tunaamini kwenye mabavu. Anayedhani kwamba viboko ndio suluhisho aseme hapa kama wanafunzi wanaochapwa wana uwezo mkubwa kielimu kuliko wanafunzi wa nchi zile zilizoendelea ambazo viboko ni marufuku, vinginevyo utaiaminisha dunia kwamba waafrica ni wanyama pori hivyo bila viboko hakuna njia inayoweza kuwarekebisha.
Maamuzi yaliyofanywa nia sahihi kabisa kama kulikuwa na tatizo lilitakiwa kuripotiwa katika mamlaka husika kwa hatua zaidi sio kuchoma mabweni ambayo hayana hatia kwa matatizo yao.
Big up Rais. Kiukweli huyu ndo Rais.
 
Back
Top Bottom