UCHAMBUZI: Adhabu waliyopewa wanafunzi wanaoshukiwa kuchoma shule sio sahihi kwa 100%

Kwa masikitiko makubwa ninaandika mambo haya...

Sote tumesikia na wengine wameona, wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa shule moja ya sekondari huko Mbeya ambao wanadaiwa kuchoma moto mabweni ya shule yao, wakicharazwa viboko hadharani na mkuu wa mkoa wa Mbeya, wakitangaziwa kufukuzwa shule na wazazi wao kutakiwa kulipa gharama za kufidia uharibifu wote huo.

Ni uamuzi uliokosa subira, hekima, busara, utu na haki. Na hapa nitaanisha sababu za msingi kabisa.

Kwanza kabisa ni kuwa adhabu hizo zimewagusa wanafunzi wote zaidi ya 300 pasipo kuzingatia nani amehusika, amehusikaje na nani hakuhusika. Makosa ya wachache au wengi yamewagharimu wote. Na hili sio haki kabisa.

Jambo la pili ni kuwa wanafunzi hao wamehukumiwa pasipo kusikilizwa. Wengi wetu mpaka sasa hatujui nini kiini cha hayo yote kutokea. Habari iliyopo ni kuwa wanafunzi wamechoma moto shule! Nani kawachochea au nini kimewasukuma hilo halisemwi wazi. (Na jambo hilo limefanywa kimakusudi)

Kwa mtitiriko wa hayo mambo mawili hapo juu, tunapata taswira pana kuwa huenda hata uchunguzi wa kina na huru haukufanyika na hautakuja kufanyika ili kufahamu chanzo na wahusika wa tukio. Kilichofanyika ni tuhuma, hukumu na utekelezaji wa hukumu!

Yote tisa, aina ya adhabu na namna adhabu hiyo ilivyotolewa imekwenda kinyume cha misingi ya haki na sheria. Yaani kosa linalodaiwa kufanywa na Mwanafunzi akiwa shuleni hukumu imetolewa moja kwa moja na mkuu wa mkoa na kisha Rais wa nchi! Yuko wapi mwalimu, mwalimu mkuu, bodi ya shule, afisa elimu nk. Sheria inasemaje? Kama kuna jinai kwanini wasishtakiwe mahakamani?

Sehemu kubwa ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita wana umri wa miaka 18 au zaidi. Hivi tulishawahi kujiuliza adhabu ya viboko hadharani inaweza kuwa ni suluhisho la msingi kuweza kumrekebisha mtu mzima au ni namna ya kumvunjia heshima ya utu wake?

Hivi kumfukuza mwanafunzi shule ni njia ya kumwadhibu mwanafunzi aliyekosea au kumharibia maisha yake yote?

Hivi kuwaambia wazazi wote wa hao watoto walipe zaidi ya laki 2, ni jambo sahihi?

ANGALIZO.
Binafsi ninaunga mkono adhabu ya viboko kwa mtoto(sio viboko kwa mtu mzima) lakini adhabu hiyo ifanywe na mtu sahihi(hususani mwalimu au mzazi), kwa namna sahihi, wakati sahihi na mahali sahihi huku ikilenga kumrekebisha mtoto na sio kumkomoa mtoto.
Kiongozi naomba nikushukuru kwa andiko lako,lakini tambua kuwa mkuu wa mkoa wa mbeya hana taaluma ya uongozi hivyooo anajiendea tu.(alikuwa assistant lecturer) yeye kama mkuu wa mkoa angeweza ku-handle suala kwa utulivu bila kugharimu maisha ya watoto na athari zingine za ki-saikolojia (kielimu) huyu bwana ana chembechembe za usanii...anafanya ili aonekane,jambo ambalo ni baya kwa kiongozi.watu kama hawa wanadumaza taifa
 
Umewafukuza watoto shule kwa kosa la kuchoma moto shule. Mafisadi waambiwa kutubu. Huyu mtu hayupo sawa kichwani.
 
Nafikili adhabu waliopewa hao wanafunzi haitoshi, ikiwezekana wangekatwa mikono ili wanafunzi wengine wajifunze kupitia jambo hili. Hao haki za binadam nao wakileta fyoko timuaaa kule. Pumbavu saana.
Nafsi yako yenyewe inakusunta. Umeandika kinafiki tu.
 
Nafikili adhabu waliopewa hao wanafunzi haitoshi, ikiwezekana wangekatwa mikono ili wanafunzi wengine wajifunze kupitia jambo hili. Hao haki za binadam nao wakileta fyoko timuaaa kule. Pumbavu saana.
Mwanao angekuwa mmoja wao mimi ninge sema kata vichwa kabisa nini mikono wewe iwe kama uarabuni sio kuiga nusu nusu nusu tuingie mazima.Jino kwa jina.
 
Kiongozi naomba nikushukuru kwa andiko lako,lakini tambua kuwa mkuu wa mkoa wa mbeya hana taaluma ya uongozi hivyooo anajiendea tu.(alikuwa assistant lecturer) yeye kama mkuu wa mkoa angeweza ku-handle suala kwa utulivu bila kugharimu maisha ya watoto na athari zingine za ki-saikolojia (kielimu) huyu bwana ana chembechembe za usanii...anafanya ili aonekane,jambo ambalo ni baya kwa kiongozi.watu kama hawa wanadumaza taifa
Uki wafukuza shule huwa wanatafuta kazi ya kufanya.Halafu baadae tunaombwa kuisaidia Polisi kwa upumbavu wa mpumbavu mmoja polisi wetu wanapata kazi ya ziada.
 
Back
Top Bottom