Uchaguzi Zanzibar itakuwaje 2010?

MR PM HATIMAE ALIPEWA LAKINI KWA HIYO HILI USITARAJIE AKAWA RAIS MTARAJIWA......RAIS UCHAGULIWA NA CCM TUSUBIRI WATATUPA HUYU CHAPOMBE AU Swala TANO DK...M//////I
 
mzee amini usiamini kuna damu mbichi ndani ya CCM safari hii zitaibuka, na hawa wanaojishaua saa hizi hawana lolote. na wanajua wakifanya mchezo mzee madevu atatinga ikulu sasa akili kichwani mwao

Mtu wa Pwani ; Siasa za Zenj 2010 ndizo zitakazoamua rais ajaye wa muungano,Karume yuko sahihi maana kama mnakumbuka MWAKA 2000 aliwaomba wazee wa ccm-Zenj wasimsahau na ujio wake wa 2005 ni dalili za kusisitiza kuwa yuaja.

Ninamkubali kuwa ni mtu jasiri,muungwana na mwanasiasa, hizi si zama za kuoneana haya wala kujificha ktk dhamiri zetu, ni vema tukawa wawazi na wakweli mapema ili tuwape umma nafasi ya kutuchambua kabla ya siku ya maamuzi kutufikia.
We were taken by suprise kila mara huko nyuma,this time no,watu waseme mapema hadharani nia zao nasi tuwanange kwa haki pasipo kuoneana haya na wala chuki,wao nao wajieleze na watujibu kinaga ubaga na kututolea mashaka juu yao na hatimaye tujiridhishe kuwa huyu ndiye.

Bravo Amb.Karume umeonyesha njia kuelekea demokrasia ya kweli na kwa dhati nasema shame on you all ambao mnataka kutuletea viongozi ktk mabano,this time no- TRANSPARENCY FROM THE BEGINNING TO THE END.
 

Jasusi mmeanza ku plant maneno vinywani mwa watu sasa,kama kuna truth hiyo kijiweni tupen details, Amani ni wa pili kuzaliwa baada ya yule wa kwanza kufariki akiwa mdogo hivyo Ally ni wa tatu waungwana.

Wakuu tungependa ninyi mtuongoze kwa facts na msiingie ktk malumbano ya kishabiki kiasi hiki.

Keshatamka anayofikiria huko mbeleni wakuu,wengine wajitokeze sasa wasijifiche ,si dhambi kuutaka urais jamani sasa siri ya nini ? Semeni tu kama mnao watu nao waambieni wajitokeze,vivyo hivyo kwa vyama vingine huko Zenj navyo vifanye hivyo mapema .Ni haki ya jamii kuwatambua mapema.

Ni hayo tu
 

Source:Tanzania Daima
 
Karume kusema juu ya Serikali ya mseto kwa uwazi namna hii kwa mara ya kwanza naona kapata akili na kumzidi hata JK ambaye anacheza tu na maongezi ya sirini . Kwenye Karume nimemkubali .
 
Kwa mujibu wa gazeti la Majira la hivi majuzi Balozi Karume
ametuonya Wazanzibari wenzake tusifanye kosa la kumpa nchi "dereva wa teksi" aendeshe; tumpe "msomi" kama yeye. Huu ni wasia mwema kwani hata Mtume Muhammad (SAW) amesema. "Muislamu hang'atwi na nyoka mara mbili ndani ya shimo moja". Kukubali kung'atwa mara tatu utakuwauzembe uliokithiri.

Kwa maoni ya mheshimiwa, Wazanzibari "hawawezi kumkataa". Huu nao
ni ukweli usiopingika. Mathalan katika kura ya maoni Balozi wetu
atajaaliwa kupata kura tisa na mpinzani wake apate 42, atakayechaguliwa kuwa mgombea ni yeye. Kama mlango wa mbele umekomewa wa nyuma si upo? Vile vile katika uchaguzi utakaofuata Janjaweed (Janjawire) kwa Kiunguja, polisi na majeshi ya vita watahakikisha ushindi wa kishindo unapatikana. Baada ya hapo mgombea wetu ataapishwa haraka na ving'ora vitaingia mjini kutukumbusha kwamba aliyeingia madarakani ni A.K. wa tatu (AK III) mfano wa (George VI) n.k. siyo A.K.wa kwanza wala wa pili. Mchezo utaishia hapo ila kwa wale watakaothubutu huhoji.

Kweli kabisa mheshimiwa anaposema akitetea azma yake kugombea urais
wa Zanzibar mwaka 2010, kwamba hawana hoja wanaosema si vyema yeye
kugombea nafasi hiyo kwa vile kuna Karume wawili tayari wamemtangulia. Ni sahihi kabisa mfano wake kwamba Singapore nayo imetawaliwa na marais kadha kutoka familia moja. Analotunyima mheshimiwa wetu ni kutwambia kwamba katika miaka ambayo wana familia wa Lee Kuan Yew wameitawala Singapore nchi hiyo imejitoa kwenye kundi la nchi maskini na kujiingiza kwenye ulimwengu wa kitajiri na leo Singapore ni ngome ya uchumi mwema na demokrasia. Laiti kama mafanikio kama hayo au yanayokaribiana na hayo hata kwa mbali yangekuwa yamepatikana nchini mwetu, basi Wazanzibari kwa ujumla wetu tungeimba, "Marhaban, nawaje kina Karume, hata kama ishirini…"

Kuhusu usomi tuchukue fursa hii kumkumbusha Balozi Karume kwamba
shahada za uzamili zimejaa vururu nchini mwetu, na wachumi wanatwambia bidhaa ikijaa sokoni thamani hupungua. Kama lengo ni ria, kama inavyoonesha basi ushauri wetu kwa Mheshimiwa Balozi ni huu: Jiunge na Chuo Kikuu Wazi uchukue masomo ya shahada ya juu zaidi na halahala usije shindwa njiani. Baadaye ukumbuke kwamba "Chema," chambilecho Waswahili, "chajiuza, kibaya chajitembeza". Wasomi wa kweli hawana haja ya kutamba hadharani. Wenyewe tunawafahamu.

Mwishowe mheshimiwa aniruhusu niulize tangu lini kukauka kwa wino
kwenye kadi ya uanachama kukawa sifa mojawapo ya uongozi ndani ya CCM?

Abdullah Masoud
 
Jamani hivi Zanzibar ni nchi ya mamwinyi au karume family ndio imezaliwa kwaajili ya kuongoza Zanzibar? hoja sio kuomba kugombea hoja kwanini wawe wao tu kila siku
 
akanawe miguu akojowe akalale, zanzibr haiwi rais ng,o.

hatujasahaqu kumuua marhoom asha kwa kuwa alimkataaa.

hatutaki wauwaji.
 
Mtu mwenyewe anavyoongea tu unamuona kabisa kwamba ameshindwa hata kabla hajaanza hiyo safari yenyewe. Tena wanatakiwa wamrudishe haraka sana nyumbani maana inaonekana hata kazi yenywe ya udiplomasia haiwezi kwa jinsi anavyobwabwaja!
Mi nawashangaa sana hawa watoto si watangaz tu ta ni kingdom.Jamaa hawezi kupata kabisa anajisumbua tu huyo ndio mana kaanza mapema ili watu wamjue but hamna kitu pale bora hata huyo Fatma
 

Masou,

Thats classic...
 
Usishangae FM huyo jamaa sikumbuki hata mara ya mwisho kuishi tz hata kwa miezi mitatu ni lini mana katoka ujerumani kapelekwa italy na kabla ya hapo sikmbuki alikuwa nchi gani ila wakati umefika wa hawa mabalozi wa nchi kavu kupewa nchi hawa nao wanahitaji kutumikia nchi wakiwa nje sio akina karume kila muda ukiisha badala ya kurudi home anapelekwa nchi nyingine WHY?kWANINIIIIII
 
Ali aliua mtu ama ni mimi sijaelewa ?Je sasa kuna sheria mpya inakuja can we ask for an inquest ?
 
Maalim Seif anakubaliana na Ali kugombea urais wa Zenj. Hii ni hatua kubwa kwa Bw. Ali katika azma yake ya kuwa Prez Zenj...
 
Maalim Seif kama mwanasiasa yuko tayari kuona mgombea mwenye udhaifu kama Ali anagombea, kuliko mtu kama Bilal.
 
Maalim Seif kama mwanasiasa yuko tayari kuona mgombea mwenye udhaifu kama Ali anagombea, kuliko mtu kama Bilal.

Angalia hapa chini

Sijui udhaifu wako umekusudia kwenye masuala yepi...!
 
Hivi naomba mwanga!

Ni sababu ipi inaifanya SMZ kuwa na Coalition? Wanahofia nini?

Au ni ubabe?

Mwenye uzoefu na siasa za Visiwani -naomba mwanga!
 
mimi huwaambia hivi :

bahati haina kwao popote inathibiti;

ilipo kwangu upeo nasubiri siifati ;

moyo nimesema nao isipokuja sijuti ;

-----------------------------------

sihusudu wapatao ingawa mimi sipati;

sihusudu wenye vyao siihimizi bahati;

toka kale hadi leo mambo hwenda kwa wakati;
 
Kweli huyu bwana kajaa kejeli tupu. Anawadhalilisha madereva tax kuwa hawakusoma au vipi. Je, amesahau kuwa Marehemu baba yake aliukwaa urais wakati alikuwa "KULI TU WA BANDARINI?". Kweli Nyani haoni KUNDULE.
 
Kweli huyu bwana kajaa kejeli tupu. Anawadhalilisha madereva tax kuwa hawakusoma au vipi. Je, amesahau kuwa Marehemu baba yake aliukwaa urais wakati alikuwa "KULI TU WA BANDARINI?". Kweli Nyani haoni KUNDULE.

Hilo linajulikana, una jipya lipi ambalo unahisi litaweza kutomfanya Ali kugombea Uprez Zenj?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…