Uchaguzi Zanzibar itakuwaje 2010?

Uchaguzi Zanzibar itakuwaje 2010?

'Suala la wizi wa kura kwa chaguzi za visiwani huwa si la kujadiliwa ama kuumiza vichwa sana, kwani linatambulika. Na mpaka kesho sijajua wale jamaa waliokimbia na maboksi ya kura mwaka 2000 na kwenda kubadili matokeo porini wamechukuliwa hatua gani!Tungepata ufumbuzi wa hili suala tata nadhani tungekuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuchambua suala hili. Mlio na taarifa za suala hili tunaziomba.'

IDIMI umenifanya nicheke saaana mkuu. Lile changa la macho tu, kuonyesha jamaa wapo makini na uchanguzi, jamaa ni wao wenyewe na walipanga nao. Watu wale wapo mitaani kama kawaida hawaijui Jela wala Rumande. (kinyume chake wanasifiwa kwa kufanikisha kazi waliyotumwa).

Mbona wale jamaa wapo nje tu wanafaidi matunda ya Mapinduzi. Kaka wa mmoj wa wahusika wale alipata zawadi ya Ukurugenzi katika Idara moja ya SMZ kwa ndugu yake kukimbia na masunduku yale, kama alivyotunukiwa Ukatibu Mkuu - Mh. Omar Yussuf Mzee kwa kupinda matokeo ya uchaguzi ya mwaka 1995 alipotumia elimu yake ya Takwimu kufanya kazi hiyo ( siri haijulikani alitumia software gani)
 
Nani anafaa kugombea urais CUF mwaka 2010?

2008-11-12 12:16:37
Na Mwinyi Sadallah

Wanachama wa chama cha Wananchi (CUF) wameingia katika mjadala mzito wa kujadili mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya chama hicho baada ya Rais Amani Abeid Karume,kumaliza muda wake Oktoba mwaka 2010, huku Katibu mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, tayari akiwa ametangaza msimamo wake kugombea tena nafasi hiyo.

Mwandishi wetu, Mwinyi Sadallah, aliyehojiana na Duni anaelezea msimamo wake na pamoja na msimamo wa Maalim Seif.

Wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), wameigia katika mjadala huo wakati Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ikiwa katika matayalisho ya uchaguzi wa awamu ya nne tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Mjadala huo wa nani anafaa kuingia katika uchaguzi unaoshirikisha vyama vilivyopata usajili wa kudumu umesababisha wanachama ndani ya chama hicho kugawanyika makundi mawili; wale wanaounga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na wale wanaomjadili mwanasiasa machachari wa chama hicho, Juma Duni Haji, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF upande wa Visiwani.

Wanasiasa hao wamekuwa wakizungumzwa na wanachama na kupewa nafasi kubwa ya kuwania kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar mwaka 2010 kutokan na kuwa na mvuto na nguvu kubwa za ushawishi wa kisiasa kwa wapiga kura.

Katika kila pembe na vijiwe vya kahawa Zanzibar, yametawala mazungumzo juu ya wanasiasa haowaandamizi wawili wa CUF ikiwa imebakia miaka miwili kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.

Wapo wanachama wa CUF,wanaosema kutokana na chama kushindwa kufikia malengo ya kukamata dola katika vipindi vitatu vya uchaguzi, ipo haja ya kubadilisha sura za wagombea wake Tanzania Bara na Zanzibar kutokan na wagombea wake, Maalim Seif Sharif Hamad na Professa Ibrahim Haruna Lipumba, kushindwa kufikia malengo ya kukamata madaraka ya nchi tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992.

``Nigependa sana sura mpya za wagombea katika uchaguzi mkuu ujao kwani hatua hiyo ingetusaidia kujenga matumaini mapya ya chama chetu baada ya kukwama kwa serikali ya mseto na kushindwa kukamata dola kwa miaka 15, ``anasema mwanachama wa chama hicho, Mohammed Kombo.

Anasema kushidwa kwa chama kufikia malengo ya kisiasa katika vipindi vitatu vya uchaguzi na kukwama kwa mpango wa mazungumzo ya kuudwa kwa serikali ya mseto kumerejesha nyuma matumani ya makubwa waliyokuwa nayo wanachama ya kujitayarisha kupokea mabadiliko ya kiutawala Visiwani.

Wanachama wanaotetea hoja ya Juma Duni Haji,mwenye asili ya kisiwa cha Unguja, kumrthi Maalim Seif, wanadai kwamba anaweza kufufua hali mpya ya matumaini kwa wanachama kujitayarisha na mabadiliko ya kiutawala kutokana na ushawishi wake mkubwa wa kisiasa na kukubalika kwake kisiwani Unguja, sehemu ambayo ni ngome kubwa ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wanadai kwamba kitendo cha Duni kukubalika kisiwani Unguja, kunaweza kusaidia kuiagusha CCM katika uchaguzi kutokan na kisiwa cha Pemba kuwa tayari ni ngome kubwa ya chama hicho tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi na kufanikiwa kunyakuwa majimbo yote 18 ya uchaguzi.

``Hakuna anayeweza kupigana vita vya kisiasa vya kuwania urais na Maalim Seif na kupata ushindi kwa vile bado wanachama wengi tuna imani na Maalim Seif, mizengwe ya uchaguzi ndiyo kikwazo kinachomfanya kushindwa kufikia malengo ya kisiasa,`` anasema mwanachama mwingine wa CUF, Said Masoud.

Mjadala huo unaendelea kupanuka kutokana na baadhi ya wanachama kutetea hatua ya wagombea wa zamani kug`atuka ili kutoa nafasi ya kuimarisha demokrasia ili kuleta matumaini mapya ya kisiasa ndani ya chama hicho.

Hata hivyo, Duni anapingana kabisa na wale wote wanaotaka ajitose katika mbio hizo za urais wa Zanzibar.

``Kama kuna wanachama wanataka nigombee nafasi ya urais mwaka 2010 basi watu hao hawanitakii mema kwa sababu bado tuna viongozi wenye uwezo mkubwa na kitendo hicho kinalenga kunichonganisha na viongozi wezangu,``anasema Duni wakati akijibu swali aliloulizwa na Nipashe.

Duni anasema kama kweli kuna wanachama wa CUF wanamtaka agombee nafasi hiyo wajitokeze hadharani na yupo tayari kuwapokea kwa vile nyumbani kwake wanapafahamu na ofisini badala ya kutoa maoni yao nje ya utaratibu wa chama hicho.

``Kuzungumzia msimamo wao nje ya utaratibu wa chama ni sawa na kutafuta kunichoganisha na viongozi wenzangu,`` anasisitiza mwanasiasa huyo.

Hata hivyo Duni anasema kimsingi viongozi ambao wamekuwa wakisimamishwa kuwania nafasi hiyo Tanzania Bara na Zanzibar bado wana uwezo mkubwa na mvuto wa kisiasa kwa wapiga kura,lakini tatizo kubwa wamekuwa wakishindwa kufikia malengo ya kisiasa kutokana na ZEC kuonyesha upendeleo wa kuiibeba CCM katika chaguzi zote tatu.

Anaeleza kwamba kama kweli wanachama hao wana nia njema na yeye, wagemfuata kueleza nia yao na siyo kuzungumzia mitaani ingawa mfumo wa demokrasia unamruhusu kila mwanachama kuwa huru kutoa maoni yake bila ya woga.

Duni anasema kwamba chama cha CUF kina nguvu kubwa za kisiasa nchini, isipokuwa kimekuwa kikinyimwa haki yake kutokan na uchaguzi kutawaliwa na mizengwe tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini na kutaka mfumo mzima wa kusimamia uchaguzi kuangaliwa upya upande wa Zanzibar.

Anaeleza kuwa wakati umefika kwa CCM kujifundisha kueshimu misingi ya demokrasia kwa kuangalia mchakato wa uchaguzi wa Marekani wa Novemba 4 ulivyofanyika bila ya kuwepo mizengwe wala askari wenye silaha katika vituo vya wapiga kura, kinyume na chaguzi za ndani ya nchi ambazo utawaliwa na vurugu.

Anasema kitendo kilichofanywa na Wamarekani kumchagua rais mwenye asili ya Afrika ni mfano wa kuigwa katika siasa za Zanzibar na kuondokana siasa za ubaguzi za uafrika na uarabu kwa vile Wazanzibari wote ni wamoja kama alivyosema Rais Mteule wa Marekani, Barack Obama kuwa ``Wamarekani wote wanahaki sawa mbele ya uongozi wake``.

``Katika maisha yangu ya kisiasa sijawahi kusema mwisho wa utawala wa mtu mweusi umefika Zanzibar katika uchaguzi wa mwaka 1995 hivyo naamini ilikuwa ni propagada za CCM kama yupo mtu mwenye ushahidi nipo tayari kutoa zawadi ya shilingi milioni moja kama atathibitisha madai hayo,`` anasema Duni, ambaye amewahi kushitakiwa kwa kesi ya uhaini na kukaa kizuizini kwa miaka mitatu na katika gereza lenye ulinzi mkali la Kilimani, wakati wa utawala wa Rais mstaafu wa awamu ya tano, Dk. Salimin Amour Juma.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, amewahakikishia wanachama wake kuwa atapambana kiume mpaka mwisho wa tone la damu yake kuhakikisha anachaguliwa rais wa Zanzibar na anaingia `Ikulu`.

``Nitagombea urais tena kwa vile uwezo ninao nanimekuwa nikishinda katika kila uchaguzi isipokuwa sipewi haki yangu,``alisema Maalim Seif mwishoni mwa wiki mjini Zanzibar.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Kizimkazi. Mkoa wa Kusini Unguja, Hamad aliwataka wananchi wa Zanzibar kuwa na subira na kutokata tama kwani siku moja itafika na atakuwa rais wa Zanzibar .

``Naamini ipo siku (One day yes) kuwa nitaingia Ikulu Zanzibar.

Sitorudi nyuma na nitaendeleza mapambano bila ya kuchoka wala kuvunjika moyo,`` alisema Seif ambaye tayari amechukua fomu ya kutetea nafasi yake ya ukatibu mkuu wa chama hicho.

Maalim Seif kwa mara ya kwanza alisimama kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar na kutingisha visiwa vya Unguja na Pemba mwaka 1995, lakini aliangushwa kwa ushihidi wa asilimia 50.2 na aliyekuwa Rais wa Zanzibar wakati ule, Dk Salimin Amour Juma na yeye (Maalim Seif) kupata asilimia 49.8, matokeo yaliyozua utata na kuzua mpasuko wa kisiasa Visiwani unaoendelea hadi leo.

Maalim Seif anasema Zanzibar inahitaji mabadiliko makubwa ya kiutawala ili kuleta mabadiliko ya uchumi kwa wananchi wanaoendelea kuishi katika hali ya umaskini na ufukara, ikiwa miaka karibu 45 tokea Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

``Utawala uliopo madarakani umeshindwa kuweka misingi mizuri ya uchumi pamoja na kutumia rasilimali ya bahari na ardhi kuleta maendeleo na kupunguza umaskini ulioota mizizi``anasema maalim Seif.

kwa mujibu wa matokeo ya Tume ya uchaguzi kiiwango cha ushindi dhidi ya wagombea wa CCM kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 kimeongezeaka kutoka ushindi wa asilimia 50.2 hadi asilimia 53.2 mwaka 2005 wakati Maalim Seif matokeo ya uchaguzi kinaonyesha matokeo ya kura zake kwa mujibu wa tume ya uchaguzi yamekuwa yamekuwa yakishuka kutoka asilimia 49.8 mwaka 1995 hadi asilimia 46.1 mwaka 2005.

Hata hivyo wachambuzi wa siasa za Zanzibar wanasema kwamba chama cha CUF hakitokuwa na kazi kubwa katika kutafuta mgombea wake wa urais kutokana na wanachama wake kutawaliwa na sera ya kumpenda mtu,lakini watakuwa na wakati mgumu wa kuwaunganisha wanachama wake baada ya muafaka kukwama kwa mara ya tatu.

Wachabuzi hao wa masuala ya siasa wanasema Maalim Seif bado anayo nafasi kubwa ya kusimama kwa mara ya nne kutetea nafasi ya urais wa Zanzibar bila ya kupingwa na mwanacham yoyote kutokana na idadi kubwa ya wanachama hasa kutoka kisiwani pemba kuwa bado wanaiimani naye na kuamini kushindwa kwake katika uchaguzi kumetokana na mizengwe ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar(ZEC).

Hata hivyo wanasema iwapo wananchi wa Zanzibar wagekuwa wanachagua viongozi kutokana na kupima sera za wagombea basi CUF wagekuwa katika mazingira magumu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kutokana na serikali ya CCM kuamua kuwekeza miradi mikubwa ya maendeleo katika ngome ya CUF kisiwani Pemba hasa mradi wa umeme kutoka gridi ya Taifa mkoani Tanga unaotarajia kukamilika mwaka 2010.

SOURCE: Nipashe


Nani anafaa kugombea urais CUF mwaka 2010?
 
Ibrahim Lipumba kwa sababu Seif Shariff Hamad ameshajaribu mara tatu (1995, 2000, 2005) bila mafanikio ingawaje mimi naamini alishinda miaka yote hiyo lakini CCM waliiba kura na pia kupeleka wapiga kura toka bara ili wakaongeze idadi ya wapiga kura wa CCM. Pia ningependa kuona Dr Slaa ndiye mgombea wa Urais 2010 toka CHADEMA.
 
Sio siri mtu wa ushindi wa kishindo urais Zanzibar 2010 ni Juma Duni Haji na waziri wake kiongozi ni Ali Emer muhamad. Nimepata bati ya kuzungumza nao wote wawili katika mazungumzo rfasmi hivyo nawafahamu fika.
Wote wana uwezo wa uongozi ili Maalim seif ana siasa za jazba na chuki, Juma Duni ana sisa za taratibu, na utulivu lakini ni makini kweli kweli.

Maalim Seif anautaka urais wa Zanzibar kwa jazba, nguvu na usongo akiamini urais wa Zanzibar ni kama kitumbua chake alichopokwa kabla hakijaafika mdomoni ili hali ana njaa ya kufa mtu.
Juma Duni yeye hana usongo na urais kama heshima na utii kwa wakubwa zake chamani ila ni mtu mwenye akili na uwezo mkubwa wa uongozi bila siasa za jazba chuki wala kinyongo cha kukaa jela miaka mitatu bila kosa.

Nadhani ni kweli siku zote anashinda uchaguzi Maalim ila nani atakubali kumpa urais mtu mshari mwenye kila dalili ya kulipiza kisasi na hata kuuvunja muungano hivyo hata akisimama mara mia hapewi dola ng'o labda adhikr uchi.

Juma Duni anaonyesha ni muungwana na mstaarabu hivyo akisimama atashinda na atakabidhiwa dola.

Tatizo jingine la Maalim Seeifu ni nasaba na sultan aliyepinduliwa, tena kuna tetesi ni mtoto haswa wa Sultan aliyemzaa nje ya ndoa ili kuziba aibu ya uzinifu wa sultan-na adha ya kuwa mwanaharam, ndipo mamaye akaolewa huko aliko olewa lakini mpaka sasa mfadhili mkuu wa Maalim ni Sultan wa Brunei ndiye anayempa kiburi cha kuishi hotelini hapa bara kwa siku zote, sijui sasa. Sultani wa Brunei ni ukoo -ule ule wa Sultani wa Oman na ndio unaomgharimia Sultan wa mwisho aliyepinduliwa Zanzibar, Sultan Jamsed kuishi London mpaka sasa. Kwa vile Maalim ni ukoo huo, anahofiwa ataurudisha usultani na kuyakana mapinduzi ya Zanzibar yaliyouwa ndugu zake na labda ndio maana jamaa ana hasira na usongo.
Juma Duni yeye Mbantu hahatarishi usalama wa kurudisha usultani.
Tatizo kubwa la baadhi ya washabikiwa CUF ni mafanatik wa siasa za jino kwa jino huwaelezi kitu wao wanaangalia sura na sharubu sio uwezo wa mtu.
 
Ibrahim Lipumba kwa sababu Seif Shariff Hamad ameshajaribu mara tatu (1995, 2000, 2005) bila mafanikio ingawaje mimi naamini alishinda miaka yote hiyo lakini CCM waliiba kura na pia kupeleka wapiga kura toka bara ili wakaongeze idadi ya wapiga kura wa CCM. Pia ningependa kuona Dr Slaa ndiye mgombea wa Urais 2010 toka CHADEMA.

Aaa..BAK haya sio mambo. Lipumba akagombee urais wa Zanzibar!?.
Dr. Wibroad Silaha ni makini na anauwezo ila hana mvuto wa kipresident
 
Seif anafaa kugombea urais kwa sababu alishinda mara zote tatu. Duni na CUF wanafahamu kuwa, Duni anataka kutumiwa kuivuruga CUF, lakini itakuwa hadithi ile ile seif atashinda, cuf watashinda CCM itatawala. watachapwa viboko utakuja muafaka mwingine utakaa miaka minne unaharibiwa, uchaguzi tena na tena na tena na tena
 
Ibrahim Lipumba kwa sababu Seif Shariff Hamad ameshajaribu mara tatu (1995, 2000, 2005) bila mafanikio ingawaje mimi naamini alishinda miaka yote hiyo lakini CCM waliiba kura na pia kupeleka wapiga kura toka bara ili wakaongeze idadi ya wapiga kura wa CCM. Pia ningependa kuona Dr Slaa ndiye mgombea wa Urais 2010 toka CHADEMA.

Samahani I'm very sorry. Headline ni tofauti na contents. Moderator naomba rekebisha hiyo ili isomeke ni urais wa Zanzibar ili mjajada utokane na mada kuu ya ABT,
 
Kifupi kwa nini CUF wasitumie mfumo wa kura za Uchaguzi ndani ya chama chao kwa kuwasimamisha wagombea wawili Sharif Hamad na Duni kisha wanachama wa chama hicho Visiwani wamchague nani ataongoza mapambano yao ktk uchaguzi mkuu..

Muhimu zaidi watazame nani mgombea wa CCM visiwani kuweza kumpa mtu ambaye wako legue moja kwa sababu hadi sasa hivi Watanzania tunawachagua viongozi wetu kwa sura na jina ya nasaba yake..
Kwa mfano Mtoto wa Mwinyi akigombea Urais Zanzibar ni nani anaweza kusimama naye sambamba!
Jambo jingine kwa sababu kuna muafaka kati ya Chadema na CUF ni vizuri sana kama vyama hivi vitakubaliana kuhusu mgombea wa kila jimbo visiwani na bara mapema kabla ya uchaguzi mkuu kwani kuna majimbo ambayo CUF imeyashika vizuri bara ktk ngazi za Diwani lakini wanapwaya ktk Ubunge, vile vile Chadema wanapeta baadhi ya sehemu ktk ngazi fulani lakini pia hawana ubavu baadhi ya sehemu...

Nguvu ya pamoja kati ya Chadema na CUF nadhani inatosha sana kuwavuta wananchi hasa kwa kuzingatia kwamba maelewano kati yao yatakuwa yameondoa dosari kubwa za vyama hivi kulingana na siasa chafu zinazoendeshwa na chama tawala - Udini na Ukabila...
Nina mashaka makubwa kama swala hili litawezekana kwa sababu hizo hizo za Udini na Ukabila kwani ktk mazungumzo mengi niliyoyaona hapa na hasa ktk maswala yanayohusu Zanzibar nimeona mawazo ya wananchama wengi wa Chadema wakichukulia swala la Zanzibar kama vile haliwahusu na pengine Wapemba (CUF) wajikate na kuvunja Muungano kwani hatuwahitaji...

Mtanisamehe wakubwa lakini panapo ukweli ni lazima niuzungumze....
Wapambe wa Chadema wanapeleka very wrong message kwa wananchi, iwe bara ama visiwani na kusema kweli ktk kijiwe hiki nimeona hitalafu nyingi sana zinazotokana na wanachama wa Chadema..They are selfish na wanafikira kuwa wao ndio wanaojenga Taifa zima!
 
Could it be too late moderators wamelala?. Maana saa hizi ni usiku mkubwa Bongo. Ama AbT ulimanisha nini?. Kutokana na makala inazungumzia uchaguzi wa Zanzibar. Usiporekebisha headline watu wataendelea kuchangia uchaguzi wa bara.
 
Pasco,
Watu tunaelewa kuwa ni uchaguzi wa Zanzibar, wengine tumeongezea tu baadhi ya hoja zetu lakini swala bado linasimama kuwa chaguzi ni mgombea wa Urais Visiwani kwa tiketi ya chama cha CUF.
Kama kuna Muafaka kati ya Chadema na CUF kuna kila sababu ya kupendekeza jina ama majina ya wagombea pande zote mbili iwe Visiwani ama Bara..
 
We believe allah will guide from those who have cruelity plan agaist us
 
Maalim Seif ana siasa za jazba na chuki,

Maalim Seif anautaka urais wa Zanzibar kwa jazba, nguvu na usongo akiamini urais wa Zanzibar ni kama kitumbua chake alichopokwa kabla hakijaafika mdomoni ili hali ana njaa ya kufa mtu. Nadhani ni kweli siku zote anashinda uchaguzi Maalim ila nani atakubali kumpa urais mtu mshari mwenye kila dalili ya kulipiza kisasi na hata kuuvunja muungano hivyo hata akisimama mara mia hapewi dola ng'o labda adhikr ....

Tatizo jingine la Maalim Seeifu ni nasaba na sultan aliyepinduliwa,mpaka sasa mfadhili mkuu wa Maalim ni Sultan wa Brunei ndiye anayempa kiburi cha kuishi hotelini hapa bara kwa siku zote, sijui sasa. Sultani wa Brunei ni ukoo -ule ule wa Sultani wa Oman na ndio unaomgharimia Sultan wa mwisho aliyepinduliwa Zanzibar, Sultan Jamsed kuishi London mpaka sasa. Kwa vile Maalim ni ukoo huo, anahofiwa ataurudisha usultani na kuyakana mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyouwa ndugu zake na labda ndio maana jamaa ana hasira na usongo.

Tatizo kubwa la baadhi ya washabikiwa CUF ni mafanatik wa siasa za jino kwa jino huwaelezi kitu wao wanaangalia sura na sharubu sio uwezo wa mtu.
Natafakari tuu haya yanayotokea Zanzibar na hiki nilichoandika mwaka 2008!.

Pasco


 
Natafakari tuu haya yanayotokea Zanzibar na hiki nilichoandika mwaka 2008!.

Pasco



TAFAKARI SANA MAANA HAPO ULIPOANDIKA KWA CHUKI NA JAZIBA ; LEO NI 2015 BADO UNGALI NA AKILI MGANDO AU UNATAKA KULETA CHUKI .


WACHENI KUWAADHIBU WAZANZIBARI WAPIGA KURA AU UMETUMWA NA PENGO????


 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom