Uchaguzi Zanzibar itakuwaje 2010?

Uchaguzi Zanzibar itakuwaje 2010?

Angalia hapa chini


Sijui udhaifu wako umekusudia kwenye masuala yepi...!

Chief,

Nafikiri hapa udhaifu unaozungumziwa ni kwamba, kulinganisha Ali Karume na Gharib Billal, Maalim Seif ana nafasi ya kumshinda Karume. Kauli ya Maalim Seif kusema Ali ni bora kuliko Amani hiyo ni danganya toto yenye kutaka kumjaza Ali ujinga apate kichwa bure. Hivi kweli ni lini kiongozi wa upinzani akapendekeza chama tawala kiteue mgombea mahiri kushindania Urais? Maalim might have been right that he prefers Ali from Amani, but that does not mean that Ali is better qualifies for the presidency
 
Hhohoho.sumile kwanza!!!
Hebu naturudi katika sera za CCM ambazo ndizo zinazokuzuzuweni wenyewe,walipofukuzwa kina maalim Seif na wenzake katika chama cha CCM, Nyerere si alitangaza kufukuzwa kwao kuwa wanakipinga chama ndani ya chama? Na ndio ikawa sababu ya kuwafukuza?Iweje hii leo ALI Amani Karume awe anakwenda kinyume na chama chake kwa kutamka hadharani kuwa kwanza atapigaina uraisi wakati hata bado wakati wake, na la pili ataunda serikali ya shirikisho na wapinzani wake wakati ni kinyume na katiba ya chama? Anaposema atafanya hivyo bado yumo ndani ya chama chenyewe, jee kwa kina maalim ilikuwaje ikawa sumu kwenda kinyume na chama hichohicho? Hapana shaka kwa kuwa hamkuwa na utaratibu wa kustahamili kukosolewa na kupingwa, na hii leo Ali Karume anapinga msimamo wa kutochanganya wali na chooko, na huku mnamtizama macho, si kufru hii kwa CCM ? Amani ameshamaliza wakati wake hana tena nguvu ya kuendelea, naamalize tumpigie fatha,lakini tulitaraji Ali kwakuwa amekiuka msimamo kwa kujitangaza kusimamia uchaguzi tena hii leo,na halafu kutamka hadharani kuwa ataunda kisichoundika kwa kamba ya CCM na huku mnamtazama macho? Au hakamatiki mzitoooo??? Na yeye mfukuzeni basi kwani kakisaliti chama mnamtazama tu mpaka hapo atakapokutieni vidole vya macho.
 
Hebu naturudi katika sera za CCM ambazo ndizo zinazokuzuzuweni wenyewe,walipofukuzwa kina maalim Seif na wenzake katika chama cha CCM, Nyerere si alitangaza kufukuzwa kwao kuwa wanakipinga chama ndani ya chama? Na ndio ikawa sababu ya kuwafukuza?Iweje hii leo ALI Amani Karume awe anakwenda kinyume na chama chake kwa kutamka hadharani kuwa kwanza atapigaina uraisi wakati hata bado wakati wake,
Alichofanya Bw. Ali ni kutangaza nia yake ya kugombea urais wa zenj 2010. Katiba ya CCM haina pingamizi na hilo. Kinachokatazwa ndani ya katiba hiyo ni kuanza kampeni kabla ya muda.

la pili ataunda serikali ya shirikisho na wapinzani wake wakati ni kinyume na katiba ya chama? Anaposema atafanya hivyo bado yumo ndani ya chama chenyewe, jee kwa kina maalim ilikuwaje ikawa sumu kwenda kinyume na chama hichohicho

Kamanda kilichosemwa na Bw. Ali ni ushauri kwa chama chochote ambacho kitakachoshinda uchaguzi basi ni vema kuunda serikali ya mseto. Hii ina maana kama CUF watashinda basi watoe Prez, huku CCM ikitoa waziri kiongozi,na hali hiyo hiyo iwapo CCM itashinda.
 
Hhohoho.sumile kwanza!!!
Hebu naturudi katika sera za CCM ambazo ndizo zinazokuzuzuweni wenyewe,walipofukuzwa kina maalim Seif na wenzake katika chama cha CCM, Nyerere si alitangaza kufukuzwa kwao kuwa wanakipinga chama ndani ya chama? Na ndio ikawa sababu ya kuwafukuza?Iweje hii leo ALI Amani Karume awe anakwenda kinyume na chama chake kwa kutamka hadharani kuwa kwanza atapigaina uraisi wakati hata bado wakati wake, na la pili ataunda serikali ya shirikisho na wapinzani wake wakati ni kinyume na katiba ya chama? Anaposema atafanya hivyo bado yumo ndani ya chama chenyewe, jee kwa kina maalim ilikuwaje ikawa sumu kwenda kinyume na chama hichohicho? Hapana shaka kwa kuwa hamkuwa na utaratibu wa kustahamili kukosolewa na kupingwa, na hii leo Ali Karume anapinga msimamo wa kutochanganya wali na chooko, na huku mnamtizama macho, si kufru hii kwa CCM ? Amani ameshamaliza wakati wake hana tena nguvu ya kuendelea, naamalize tumpigie fatha,lakini tulitaraji Ali kwakuwa amekiuka msimamo kwa kujitangaza kusimamia uchaguzi tena hii leo,na halafu kutamka hadharani kuwa ataunda kisichoundika kwa kamba ya CCM na huku mnamtazama macho? Au hakamatiki mzitoooo??? Na yeye mfukuzeni basi kwani kakisaliti chama mnamtazama tu mpaka hapo atakapokutieni vidole vya macho.

Huu ni mfano hai wa watu wenye mawazo mgando; CCM ya Mwalimu is far from the current CCM and that of Mkapa.

Dunia sasa iantaka siasa izae wana siasa siyo wanasiasa wazae wanasiasa.

JK akiwa Norway confessed kuwa alijiandaa kuichukua nchi tangu 1995.

Sumaye alitamka through Mtanzania Daima kuwa anautaka urais,lakini pia nguvu za wakati zinatutaka sasa tufanye mambo yetu hadharani,msomi wangu tafsiri Vision,Mission kwa kina siyo kwa level ya org bali ya individuality utaona Balozi Ally Karume Yuko sahihi sana.

Zanzibar ya sasa na CCM ya leo inataka kiongozi wa aina yake,mtu asiyemung'unya maneno ,always straight forward.

Hongera sana Balozi Karume.
 
Maalim Seif anakubaliana na Ali kugombea urais wa Zenj. Hii ni hatua kubwa kwa Bw. Ali katika azma yake ya kuwa Prez Zenj...

What a wonderful endorsement from Senator Lierbman kwenda kwa Sen,MacCain, Maalimu uko juu .

Wakubwa pombe ni starehe za kawaida duniani tena sawia na zingine ambazo nasi twzifanya.

Tumkubali huyu bwana kwani at least kathubutu kutupa nafasi ya kumfahamu kabla.

Mtu kama huyu akipewa tuna haki ya kutathmini 100 days zake in the office.

Nimekukubali Mh.Balozi Karume.
 
akanawe miguu akojowe akalale, zanzibr haiwi rais ng,o.

hatujasahaqu kumuua marhoom asha kwa kuwa alimkataaa.

hatutaki wauwaji.

Tupe data hizo kinaga ubaga hatupendi yalomkuta Salim Ahmed Salim

Si safi kumpakazia mtu sifa ya uuaji wakati huna uthibitisho hapa.

Lete taarifa hizo kinaga ubaga watu tukaubaliane nawe au tukutoe nishai kuwa umedanganya.
 
hayo yalipita ila alimuua na akamtupa maisara.

na ndio kisa cha magereza zanzibar kubadilishwa majina baada ya gereza kuitwa chuo cha mafunzo maana baba yake alikusudia kumuweka ndani.

lakini baada ndio ikawa sababu ya kuwa huko nje mida yote hiyo.

nnakumbuka mzee wake waliwapoza wazee wa yule mtoto kama kesi ya dito
 
hayo yalipita ila alimuua na akamtupa maisara.

na ndio kisa cha magereza zanzibar kubadilishwa majina baada ya gereza kuitwa chuo cha mafunzo maana baba yake alikusudia kumuweka ndani.

lakini baada ndio ikawa sababu ya kuwa huko nje mida yote hiyo.

nnakumbuka mzee wake waliwapoza wazee wa yule mtoto kama kesi ya dito
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo......
 
Bilal, Khatib, Mwinyi, Haroun na Hamad Rashid wapewa nafasi

Na Rashid Mkwinda, Zanzibar

IKIWA imebaki takribani miaka miwili kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2010, vuguvugu la kisiasa limeanza kutanda visiwani hapa, huku baadhi ya wanasiasa wakitajwa kutaka kujitokeza kurithi kiti cha Rais Amani Abeid Karume.

Hali hiyo, imekuja huku hatima ya muafaka baina ya vyama hivyo ikiwa bado haijapatiwa ufumbuzi ambapo pia kumekuwa na mvutano wa kisiasa nchini, unaojadili suala la Zanzibar ni nchi au si nchi.

Rais Karume ambaye anatarajia kumaliza kipindi chake cha miaka kumi mwaka 2010 ametajwa kushindwa kutekeleza kiu ya Wazanzibari na kudaiwa kujenga matabaka na ubaguzi wa itikadi za kisiasa katika maendeleo ya wananchi wa visiwa hivyo, sawa na mtangulizi wake, Dkt. Salmin Amour.

Kwa mujibu wa taarifa zilizozagaa visiwani hapa ni kwamba wanaotajwa kujitosa kurithi nafasi hiyo, ni Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Bw. Muhammed Seif Khatib, Bw. Haroun Ali Suleiman na Dkt. Hussein Ali Mwinyi na kwamba kati yao, huenda mmoja anaweza kuchaguliwa kurithi nafasi ya Rais Karume.

Aidha, mtazamo huo wa urithi umeelekezwa pia katika CUF ambapo imedaiwa kuwa mtu pekee anayeweza kukabiliana na wawaniaji wa CCM, ni kiongozi wa upinzani bungeni, Bw. Hamad Rashid Mohamed, ambapo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, imedaiwa kuwa hawezi tena kuwania urais wa Zanzibar.

Wakizungumza na gazeti hili juu ya kuwapo mchakato huo, baadhi ya wakazi visiwani hapa, walisema kumalizika kwa muda wa uongozi wa Rais Karume kutahitimisha mtazamo hasi wa Wazanzibari, ambao walitarajia mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi.

Walisema kutobadilika kwa mtazamo wa kisiasa kumesababisha nchi wafadhili kususia kutoa msaada kutokana na historia ya kukiuka demokrasia ya mfumo wa vyama vingi visiwani, ambao ulisababisha baadhi ya wananchi kuuawa na wengine kukimbia makazi yao na kuwa wakimbizi nje.

"Historia iko wazi, hakuna nchi yoyote inayoweza kutufadhili watu wa visiwani, baadhi ya watu waliuawa, wengine walipata vilema vya maisha na hata kuhama makazi yao, hii yote ni kutokana na kutokuwapo kwa demokrasia," alisema mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni.

Naye Bibi Hamida Hassan Mohammed (28) mkazi wa Bububu, alisema mabadiliko ya uongozi ndani ya visiwa hivi, yatasaidia kuimarika kwa uchumi na kwamba utawala uliopo unawatenga baadhi ya watu kutokana na itikadi za kisiasa.

"Sisi sote tu wahitaji wa huduma za kijamii, lakini kumekuwa na ubaguzi katika huduma hizo, wapo watu wanaohudumiwa kulingana na vyama vyao, wengine wanatengwa...hili si jambo jema kwa wananchi, bora yawepo mabadiliko," alisema Bibi Mohamed.

Kwa upande wake, mkazi wa Mkanyageni aliyejitambulisha kuwa mfuasi wa CUF, alisema fursa ya Maalim Seif kuchuana na damu changa kama vile za akina Dkt. Mwinyi zinaweza kumfanya amalizike kisiasa, hivyo ni vyema akamwachia Bw. Rashid ambaye ameonesha kuwa upeo wake unaweza kukidhi mabadiliko yajayo.

"Si kwamba tunambeza Maalim Seif la, bali atabaki kuwa na heshima yake kutokana na uvumilivu aliouonesha kwa kupokwa (kuporwa) ushindi mara zote alizowania kiti cha urais hapa visiwani," alisema.

Alisema Maalimu Seif alionesha uvumilivu wa hali ya juu kutokana na mtafaruku wa kisiasa visiwani humo na kwamba bila uvumilivu wake, visiwa hivyo visingeweza kukalika na kuongeza kuwa heshima yake italindwa na kuheshimiwa kwa hekima na busara zake.

My take:

Wote hawafai Zanzibar inataka mtu ngangari type ya Komandoo Salmin Amour ambae kwa sasa hakuna.

Dr Mwinyi has an advantage ya usomi na ni sober but soft soft approach yake kwa siasa za Znz atashindwa.

On flip side its time kwa Maalim Seif kumuachia Mh Juma Duni Haji the guy has potential na anaweza kuwa bridge nzuri ya ufa wa upemba na uunguja, especially kwa kuwa anatokea kaskazini Unguja
 
Bilal, Khatib, Mwinyi, Haroun na Hamad Rashid wapewa nafasi

Na Rashid Mkwinda, Zanzibar



My take:

Wote hawafai Zanzibar inataka mtu ngangari type ya Komandoo Salmin Amour ambae kwa sasa hakuna.

Dr Mwinyi has an advantage ya usomi na ni sober but soft soft approach yake kwa siasa za Znz atashindwa.

On flip side its time kwa Maalim Seif kumuachia Mh Juma Duni Haji the guy has potential na anaweza kuwa bridge nzuri ya ufa wa upemba na uunguja, especially kwa kuwa anatokea kaskazini Unguja
Jamaa wakaskazini hawana nafasi msimu ujao, na mbegu hiyo alipandikiza Komandoo
 
Bilal, Khatib, Mwinyi, Haroun na Hamad Rashid wapewa nafasi

Na Rashid Mkwinda, Zanzibar



My take:

Wote hawafai. On flip side its time kwa Maalim Seif kumuachia Mh Juma Duni Haji the guy has potential na anaweza kuwa bridge nzuri ya ufa wa upemba na uunguja, especially kwa kuwa anatokea kaskazini Unguja

Naye pia siyo rasmi. Kutoka Kaskazini siyo hoja.
 
Tumekwisha liongea laupande wa visiwani sasa tukirudi hapa kwetu Tanganyika Tunamtizamo gani kwanza kuna CCM na Mgobea pili kwa upande wa upinzania wananchi wameamka vya kutosha na hali inavyokwenda na matendo ya viongozi wao sasa jee ikiwa cham cha upizani kitachukuwa URASIS CCM itakuwa tayari kuwachia au yatafanyika mauwaji kama ya navyofanyika visiwani?
 
Urais 2010 waitikisa Zanzibar

na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Tanzania Daima~Sauti ya watu

KILE kilichotokea wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2000, kinaelekea kujirudia tena baada ya kuwepo kwa baadhi ya matukio yanayoshabihiana na yaliyotokea wakati huo.

Wakati mwaka 2000, aliyekuwa rais za Zanzibar, Dk. Salmin Amour alijaribu bila mafanikio kung’ang’ania madarakani, tukio kama hilo limeanza dalili za kujirudia tena baada ya kundi la wazee wa CCM kumtaka Rais wa sasa Zanzibar, Amani Abeid Karume, kubadili katiba ili agombee tena urais kwa kipindi cha tatu.

Hali hiyo ilidhihirika kuwepo baada ya kundi la wazee katika kampeni za kujenga wagombea kueleza msimamo wa kutetea ushauri wa kutaka katiba ifanyiwe marekebisho, ili imuwezeshe Rais Karume kugombea tena nafasi hiyo mwaka 2010 baada ya kumaliza muhula wa pili wa urais wake.

Hata hivyo, katika kile kinachoonekana kuwa umakini wa kusoma alama za nyakati, Rais Karume tayari amekwishatoa tamko kuhusu nia hiyo ya wazee kuwa hana mpango wa kuwania tena urais baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka kumi.

Rais Karume alikaririwa wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti kuwa, kuna wazee walimfuata na kumshauri kuangalia uwezekano wa kubadili katiba, ili agombee tena nafasi hiyo, lakini aliwajibu kuwa hilo haliwezekani, kwa kuwa ndani ya CCM wapo watu wengi wenye uwezo wa kushika nafasi hiyo.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa baadhi ya mashabiki wa Rais Karume, idadi ya wana CCM wanaotajwa kujiandaa kumrithi atakapomaliza kipindi chake mwaka 2010 sasa wamefikia 10, wakiwemo wanasiasa wakongwe na vijana, ambao wamekuwa wakipanda ngazi za uongozi haraka haraka.

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumapili, umebaini kuwepo kwa makundi yanayoendesha kampeni za kujenga wanasiasa wanaotaka wawe viongozi wa visiwa hivyo mwaka 2010, ambao baadhi yao wamehamia Tanzania Bara baada ya ngome ya Zanzibar kugawanyika kwa kiwango kikubwa.

Uchunguzi umebaini kuwa kundi linaloonekana kuwa na nguvu hasi sasa na ambalo limekwishaonyesha nia ya wazi na ya dhati ya kutaka kuingia ikulu ya nchi hiyo baada ya kuondoka kwa Rais Karume ni lile linalomuunga mkono Waziri Kiongozi mstaafu, Dk. Mohamed Gharib Bilal.

Kundi hili ndilo linalotajwa kuwa lina baraka za Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour Juma, mwenye maskani yake eneo la Migombani, mjini hapa.

Hata hivyo, kundi hili limeanza kupata upinzani kutoka kwa wanasiasa wengine wanaowania nafasi hiyo baada ya kuwepo kwa dalili za wazi za Dk. Bilal kutengwa au kubaguliwa na baadhi ya wanasiasa waliopo sasa madarakani, kiasi kwamba baadhi ya makada wa CCM wamekuwa wakiogopa kusalimiana naye au kukaa naye karibu.

Uchunguzi zaidi wa gazeti hili umebaini kuwa Dk. Bilal amekuwa akijikuta katika wakati mgumu, hasa anapohudhuria mikusanyiko mbalimbali ya sherehe za kitaifa, ambapo amekuwa akishindwa kusalimiana vizuri na watu wanaotajwa kutaka kuwania urais, kwa kuhofia kuonekana kwamba wanamuunga mkono au wanaunga mkono kundi fulani.

Hali hiyo ilidhihirika wazi wakati wa Baraza la Idd el Fitr lililofanyika Jumatano, baada ya baadhi ya viongozi (majina yao tunayo) kulazimika kumkwepa Dk. Bilal kwa kuhofia kuonekana kuwa wanamuunga mkono kiongozi huyo anayeonekana kuwa na nguvu na ushawishi mkubwa miongoni mwa wana CCM.

“Zanzibar tuna siasa za unafiki mkubwa, leo hii watu wanapita nyuma ya mgongo wa Dk. Bilal kwa kuhofia kuhusishwa na makundi ya watu wanaotaka kuwania urais,” alisema mwanasiasa mmoja wa siku nyingi aliyeomba asitajwe gazetini.

Hata hivyo, alisema ni jambo la kushangaza kuwa wale wanaomkwepa hadharani Dk. Bilal ndio hao hao wanaohudhuria vikao vya kampeni vya baadhi ya wagombea vinavyofanyika nyakati za usiku katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.

Mbali na Dk. Bilal, kundi jingine linaloonekana kuanza mikakati ya kuhakikisha linaweka mtu wake katika nafasi hiyo mwaka 2010, ni lile linalotajwa kuwa la makada wa CCM wanaomuunga mkono mwanasiasa machachari wa visiwani hapa, Ali Juma Shamuhuna, ambaye ni Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar.

Shamuhuna anaokena kuwa na nguvu zaidi kwa sasa baada ya kuonyesha msimamo wake ambao umekuwa ukitofautiana na viongozi wenzake wengi ndani ya chama chake, kuhusu masuala yanayoihusu Zanzibar.

Mbali na vigogo hao, makundi mengine yanayotajwa kuhaha kujipanga kwa ajili ya mwaka 2010 ni lile linalomuunga mkono Waziri Kiongozi wa sasa, Shamsi Vuai Nahodha.

Wanasiasa wengine wanaotajwa kuwa na makundi yaliyo katika jitihada za kuwania nafasi hiyo ni Waziri wa Ulinzi, Dk. Hussein Mwinyi (aliyechaguliwa Mbunge wa Kwahani baada ya kuliacha la Mkuranga, (Tanzania Bara), na Kamishna wa Umoja wa Afrika (AU) mjini New York, Amina Salum Ali.

Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Zanzibar, Dk. Mwinyihaji Makame, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mohammed Aboud Mohammed, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Zanzibar, Haroun Ali Suleiman, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Ali Abeid Amani Karume, ambaye ndiye pekee aliyetangaza wazi nia ya kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao.

Baadhi ya makada wa CCM waliozungumza na gazeti hili, walieleza kuwa nafasi ya urais wa Zanzibar isipochukuliwa kwa umakini inaweza kuigawa tena CCM kama ilivyokuwa mwaka 2000 baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kumteua Karume kugombea nafasi hiyo badala ya Dk. Bilal, aliyepewa alama nyingi dhidi ya Karume aliyepata alama chache katika mikutano ya uteuzi.

Makada hao walieleza kuwa vitendo vilivyotokea vya kuzungumzia matabaka na asili za watu watokao Pemba, Ngazija, Tumbatu, Makunduchi na kwingineko, ni mambo yaliyokumbatiwa na watu kama silaha ya kisiasa katika harakati za kutafuta kuwa wagombea wa chama hicho mwaka 2010.

Walidai pia kuwa, hata hatua ya kusambazaji vikaratasi vinavyomkashifu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri (Muungano), Muhammed Seif Khatib, kuwa ni mwanzo wa kuipeleka CCM kubaya na ni kwenda kinyume cha misingi ya waasisi wa chama hicho.

Akizungumzia kuhusu kampeni za kuwania nafasi hiyo kuanza kujitokeza mapema, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhani Ferouz, alisema chama hicho kinaongozwa na kanuni, hivyo mwanachama yeyote anayezikiuka atachukuliwa hatua wakati utakapofika.

Alisema chama kinafuatilia matukio yanayohusisha wanachama wake na wakati wa uchukuaji fomu wote watakaobainika kufanya kampeni kinyume na maadili, watajadiliwa na kushughulikiwa kulingana na taratibu zilivyo.

Wakati huo huo, taarifa nyingine kutoka Zanzibar zinaeleza kuwa askari wastaafu wa vikozi vya SMZ wanaodai kupunjwa mafao yao wametishia kufichua siri jinsi walivyotumika katika uchaguzi mkuu wa 2000 na 2005 Zanzibar.

Wakizungumza jana na gazeti hili, walisema wanatoa wiki mbili mapendekezo ya mafao yao mapya kuwa yamezingatiwa na Wizara ya Fedha na Uchumi ya Zanzibar.

“Hapa kinachoonekana hawathamini mchango wetu, tumetumika sana kwenye uchaguzi na tunajua mambo mengi, hiki ni choyo cha watendaji wa Wizara ya Fedha”, alisema ofisa mmoja mstaafu ambaye alifikia cheo cha juu katika Kikosi cha KMKM.

Wastaafu hao walisema kwamba inashangaza kuona watendaji wa Wizara ya Fedha wamekuwa na kinyongo na mafao yao wakati baadhi yao wameajiriwa hivi karibuni wakiwa wanamiliki mali nyingi, yakiwamo majumba na magari.

Mapema wiki iliyopita, Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Hassan Haji Wambi, alisema mapendekezo ya mafao ya askari hao wastaafu yamekwama baada ya kutokea mgongano wa kisheria kati ya sheria ya Tume ya Uajiri namba 7 ya mwaka 2007 na sheria ya fedha ya mwaka 2005.
 
Huyo Jaji Mkuu wa zanzibar bado yupo ofisini kama jaji Mkuu au amestafu. Kama bado yupo ofisini ni hatari sana, Jaji Mkuu na kada wa chama cha siasa. hii ni bongo tu.
 
Huyo Jaji Mkuu wa zanzibar bado yupo ofisini kama jaji Mkuu au amestafu. Kama bado yupo ofisini ni hatari sana, Jaji Mkuu na kada wa chama cha siasa. hii ni bongo tu.

Mh. U can be a good analyst. Nakushukuru umegundua chumvi za mwandishi. Yeye mwenyewe Jaji hajasema hivyo. Ni mtu makini na hata haonekani kujishughulisha na mambo ya siasa, ingawa mimi najua kuwa ni mshabiki na mpenzi wa Chama fullani. Chukulia ya mwandishi (hasa wa Tanzania Daima) kama ndio hizo chumvi zao.
 
Kibunango
Sasa hawa Tume ya uchaguzi ya CCM watapendelea CCM au watapendelea Upinzani?
Naona unaporoja tu nadhani Wazanzibari imefika wakati sasa wakudai uhuru wao kutoka Tanganyika mumetawaliwa kwa muda mrefu.
 
Kibunango
Sasa hawa Tume ya uchaguzi ya CCM watapendelea CCM au watapendelea Upinzani?
Naona unaporoja tu nadhani Wazanzibari imefika wakati sasa wakudai uhuru wao kutoka Tanganyika mumetawaliwa kwa muda mrefu.
Kamanda hapo juu sijakuelewa...
 
kwa kweli kumekucha


sasa tunaangalia kwa makini mrithi wa nafasi hio na nani ambae ataeweza kukabiliana na hali halisi ya sasa
 
Back
Top Bottom