Uchaguzi Zanzibar itakuwaje 2010?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,187
670
kati ya hawa ni yupi anategemewa kuwa rais 2010????????

1. mohammed ghariib bilal
2. ali juma shamhuna
3. salim ahmed salim
4. ali ameir mohammed
5. shamsi vuai nahodha
 
Salim Ahmed Salim atagombea kweli? Yule ni matawi ya juu zaidi naona. Wengine wote sawa na Hussein Mwinyi ana chance kubwa.
 
nnakusudia kwa CCM kalamu.

mie nnategemea kwa kumaliza mzozo wa zanzibar ni CCM kumsimamisha Salim, kwanza itaondosha yale malalamiko kuwa Rais wa zanzibar lazima awe muunguja, pili Salim kimtazamo ni moderates na zanzibar inahitaji mtu kama huyu ktk kuleta utengamano wa kisiasa au mwaonaje waungwana?
 
mtoto wa mwinyi hana mvuto kwa wazanzibari waliowengi, huo ndio ukweli kwa hiyo sitegemei hata yeye mwenyewe kama atachukua fomu
 
Mtumwitu,
Salim atakubalika kwa Wa-CCM wa Zanzibar? Si huyu wao wanamwona eti Hizbu?
 
Vigogo Zanzibar wajipanga
na Mwandishi WetuVIGOGO wanaojiandaa kurithi nafasi ya Urais wa Zanzibar mwaka 2010, wameanza kupigana vikumbo kuchukua fomu za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitia Mkoa wa Mjini Magharibi.
Vigogo hao kwa muda mrefu wamekuwa katika harakati za kujiimarisha kisiasa na wamefanikiwa kujipenyeza katika mikoa mbali mbali ya Unguja na Pemba na kujijengea ngome.

Hata hivyo hadi sasa ngome pekee inayopewa nafasi kubwa ya kutoa mgombea huyo ni ile ambayo iko chini ya himaya ya Rais mstaafu, Dk. Salmin Amour, ambayo ndiyo inayoonekana kuwa na nguvu zaidi kisiasa kwa upande wa Zanzibar.

Kuanzia wiki iliyopita, vigogo hao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi katika ofisi za CCM Mkoa wa Mjini Magharibi, Amani Mjini Unguja, kuchukua fomu huku wengine wakisafirisha wapambe na wengine kuingia kwa kutegeana.

Wanasiasa wakongwe waliojitokeza hadi sasa kuchukua fomu ni Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Idd Pandu Hassan, mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Kiongozi mstaafu, Dk. Mohammed Gharib Bilal, na Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamuhuna.

Hata hivyo, kundi la vijana ambalo linaonekana kuchukua fomu hizo kwa umakini mkubwa haliko nyuma, lakini idadi kubwa wamo vijana ambao katika uchaguzi uliopita walianguka na kufanikiwa kuingia NEC kulingana na uteuzi wa nafasi zao.

Katika kundi la vijana waliojitokeza hadi sasa ni Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, ambaye amekuwa akitajwa sana kuwa ni miongoni mwa watu walio katika pilika pilika za maandalizi ya kurithi nafasi ya Rais Karume.

Hata hivyo, Shamsi mwenyewe hadi sasa hajatoa msimamo wowote juu ya nia hiyo, licha ya baadhi ya viongozi na wananchi kutoka Mkoa wa Kusini Unguja alikozaliwa, kusema kwamba hii ni zamu yao kushika urais.

Hata hivyo, duru za kisiasa zinasema kwamba mtazamo huo huenda usipewe nafasi katika chama, kwa vile hadi sasa kuna makundi yanadai ni zamu ya Pemba na tayari yameanza kujipanga kupitia kundi la wasomi, ambao wanadaiwa kuungwa mkono na CCM Tanzania Bara.

Kundi hilo linadai kwamba kupata Rais wa Zanzibar kutoka Pemba, ndio utakuwa mwanzo wa kuiteka kambi ya CUF Pemba, ambayo inaonekana kuiumiza kichwa CCM Zanzibar.

Vijana wengine waliochukua fomu hizo hadi sasa ni Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yussuf Himid, ambaye aliibuka katika siasa za CCM mwaka 2000.

Mansour ambaye ni shemeji ya Rais Amani Abeid Karume, pia amekuwa akitajwa kuwa ni miongoni mwa viongozi vijana wanaokubalika kuchukua nafasi za juu, hasa kwa vile anatoka katika mifupa ya wanamapinduzi wa mwaka 1964.

Baba yake Waziri Mansour, Yussuf Himid, ni miongoni mwa watu mashuhuri walioshiriki katika mapinduzi ya mwaka 1964 yaliyoung'oa utawala wa kisultani.

Pia waliochukua fomu hizo hadi jana ni Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar, Machano Othman Said, ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM.

Mjadala mkubwa hadi sasa upo kwa vigogo wawili, Dk. Mohammed Gharib Bilal na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Mohammed Seif Khatib.

Baadhi ya wajumbe wa NEC wanasema Dk. Bilal chama kinamkubali Zanzibar na Bara, lakini kikwazo kikubwa alikuwa Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Rais Benjamin Mkapa, lakini sasa atakuwa msikilizaji tu katika vikao vya maamuzi ya chama.

Katika kinyang'anyiro hicho pia wanatajwa Dk. Hussein Mwinyi, ambaye ni Mbunge wa Kwahani, Unguja, baada ya kuhama Jimbo la Mkuranga, hatua ambayo inaonekana ni maandalizi ya kuchukua nafasi ya juu Zanzibar.

Hata hivyo, hivi karibuni, Rais Karume alikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa Zanzibar kuwa ni mapema kufanya harakati za kugombea urais wakati muda wake ukiwa bado.

Rais Karume aliingia madarakani mwaka 2000, baada ya kuwaangusha washindani wake katika vikao vya chama ambao waliongoza katika kura za maoni Zanzibar.

Na katika mwaka 2005, alipata nafasi ya kuwania kiti hicho, baada ya mpinzani wake, Dk. Mohammed Gharib Bilal, kulazimishwa kujitoa katika usiku wa kuamkia kupiga kura mjini Dodoma.

Uamuzi huo uliotolewa na Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa, unadaiwa ulilenga kujenga umoja ndani ya chama hicho visiwani.


source: http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/5/29/habari4.php

hata mie nnaona wakati wa wapemba kupewa nafasi na nnaamini itaisaidia sana CCM kushinda Pemba na kuondoa Dhana kuwa CCm ni chama cha wabara na wa unguja.

pia CUF wkimsimamisha JUma Duni itaondosha ile dhana kuwa CUF ni Chama cha wapemba tu. nnaomba wazanzibari tubadilike
 
kati ya hawa ni yupi anategemewa kuwa rais 2010????????

1. mohammed ghariib bilal
2. ali juma shamhuna
3. salim ahmed salim
4. ali ameir mohammed
5. shamsi vuai nahodha

Unauliza mgombea kupitia CCM au Rais wa Zanzibar, ama nawe ni miomgoni wa wanaoamini kuwa ni CCM tu wenye haki ya kuongoza iwe kwa kura au mbinde? Your response please kabla hatujaendelea zaidi!
 
Mwanasiasa najua kweli unajua siasa, ujue hii imani ya kuwa chama fulani tuu ndi kitatawala ni kasumba mbaya sana. Hii nchi si ya kifalme japo kweli Hussen Mwinyi anaandaliwa kuwa raisi lakini yanaweza yakajatokea yaliyotokea kwa Moi kwa kutaka kumrithisha Uhuru Kennyata ili kulipa fadhila za baba yake. Ni wazi kuwa kuna uwezekano Dr. Mwiny anaandaliwa kuwa raisi wa visiwani.
 
Kuna baadhi ya watu wametajwa hapa sidhani kama watataka kugombea Urais visiwani tukianzia na Salim na Shein lakini again siasa inabadirika.
Kuhusu Mwinyi, no comments lakini kuna kila dalili kuwa kijana anaandaliwa,(Kupelekwa Znz/wizara ya muungano).
Tuombe uhai tuu 2010 sio mbali.
 
Kuna baadhi ya watu wametajwa hapa sidhani kama watataka kugombea Urais visiwani tukianzia na Salim na Shein lakini again siasa inabadirika.
Kuhusu Mwinyi, no comments lakini kuna kila dalili kuwa kijana anaandaliwa,(Kupelekwa Znz/wizara ya muungano).
Tuombe uhai tuu 2010 sio mbali.

Ni kweli kijana wa Mwinyi anaandaliwa lakini ni kwamba muda wake bado, kuna mtu/watu watapita kwanza halafu ndio yeye !! Itakuwa mapema mno kwake kuwa rais
 
tunazungumzia CCM, tunajua kuwa CUF wapo, ila nguvu zao inaonyesha zimeisha na kwa miaka kumi hadi ishirini hakuna chama kinachoweza kuiondoa CCM madarakani.

mie nnaona mtotoi wa Mwinyi kwa sasa hana mvuto zenji sijui baadae, ila ngoma ipo.

nnahisi kuondosha mushkeli CCM wamuombe Dr Salim agombee zenji au ,nahisi uarabu wake bado utakuwa tatizo?
 
Waungwana najua joto la Uongozi wa Juu Zanzibar.Ndugu zangu napenda kuwaeleza wazi kuwa Dr.Hussein Mwinyi ndio chaguo la wanaCCM wakubwa.Naomba nieleweke nikisema wakubwa!,Najua Dr Bilal anakubalika na wananchi wengi wa kawaida(walio CCM na wapinzani),lakini bado Bilal anaonekana sio mwenzao sana,kumbukeni walivyomuondoa hatua za Mwisho 2000.Urais wa Zanzibar 2010 ni mgumu kuliko bara ambako inaonekana wazi Edward Lowasa hana upinzani mkubwa ndani ya CCM.
 
tunazungumzia CCM, tunajua kuwa CUF wapo, ila nguvu zao inaonyesha zimeisha na kwa miaka kumi hadi ishirini hakuna chama kinachoweza kuiondoa CCM madarakani.

/QUOTE]

Fact or myth? You cannot predict the unpredictable; politics is an unpredictable game, don't accept CCM propaganda uncritically!
 
salim hawezi kugombea urais wa znz....kwani mara zote wazanzibar ndio wamemkwamisha kuchukua nafasi ya URAIS wa mungano..
 
Kwa maoni yangu huyu mzee ndiye next on line, ama sivyo ccm watahitaji kuiba kura na kupiga wananchi ovyo wakati wa uchaguzi, lakini kuna some guarantees kwamba huyu mzee akigombea hakutakuwa na noma, maana anakubalika pia na wananchi wengi wa upinzani,

kutokana na ukweli kwamba jamaaa na kundi lake la Salmin, hawaupendi sana Muuungano, pamoja na kwamba hawauvunji, wataufanyia vitimbi vingi kama vile Salmin alipokuwa madarakani, ikiwa ni pamoja na kuilazimisha serikali ya bara kuwapa umeme bure na kuwalipa mishara wafanyakazi wahuko visiwani as opposed na mkataba mbuzi wa huo muungano!

Na huyu Mzee ndiye pekee so far aliyepewa green light na mkubwa kuendleea na kampeni ingawa wengine walikatazwa kwenye kikao cha mwisho cha kamati kuu ya ccm, kwa kukemewa na Muuungwana mwenyewe!

Lakini still, siasa ina maajabu yake, mtu mwingine mwenye nfasi kubwa ni Shamuhuna, ambaye alikuwa ni chaguo la Muuungwana kuwa makamu wa rais, baada ya kukataliwa kwa Mama Megji, and then kuna Mzee Khatibu waziri wa bara sasa hivi, that is all I knoiw na ninaweza kuwa wrong!

Salim aliapa kuwa hatarudia tena siasa za bongo, baada ya uchaguzi uliopita wa rais kule Chimwanga, siku hizi yuko Abuja!
 
Subirini. Labda wanamtandao wa JK wasifungue branch Zenji! maana watawachafua wote mnaowataja na kumweka wamtakae. Jamaa wanasubira hao ! maana hata miaka 10 wanauwezo wa kusubiri na kujiaanda kuchukua walicho dhamiria.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom