mzee amini usiamini kuna damu mbichi ndani ya CCM safari hii zitaibuka, na hawa wanaojishaua saa hizi hawana lolote. na wanajua wakifanya mchezo mzee madevu atatinga ikulu sasa akili kichwani mwao
Nakandamiza,
Wanasema eti Amani ni mtoto wa mama, si Karume damu. Ndivyo Ali anavyodai kijiweni. Lakini hii ya kuanza kukampeni miaka miwili kabla ni sign of desperation. Hivi Zanzibar hakuna wengine wanaofaa kuongoza mbali ya akina Karume na Mwinyi?
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeshauriwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kama suluhisho pekee la kumaliza misuguano ya kisiasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).
Ushauri huo umetolewa jana na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Ali Abeid Karume, alipozungumza na waandishi wa habari visiwani hapa. Alisema vyama vikuu vilivyopo Zanzibar ni CCM na CUF ambavyo vina nguvu sawa.
Alisema Zanzibar bila ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa, hali ya migororo haitaweza kuepukika, kutokana na kuwa CCM kimejikita zaidi katika Kisiwa cha Unguja na CUF kuwa na ngome yake kisiwani Pemba.
Balozi Karume alisema serikali ya umoja wa kitaifa pia itamaliza mpasuko wa kisiasa uliopo hivi sasa, kwani nchi imeshindwa kuwa na maendeleo kutokana na migogoro ya kisiasa isiyokwisha visiwani.
Watu wengi hawapendi kusema ukweli, lakini ndio ukweli wenyewe .hali ya kisiasa iliyopo katika visiwa vyetu ni ngumu sana, Pemba CUF ina nguvu sana na CCM ina nguvu Unguja, sasa suluhisho la yote haya ni kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alisisitiza mwanadiplomasia huyo.
Akizungumzia hali ya visiwa vya Zanzibar kiuchumi, Balozi Karume alisema ni mbaya kutokana na migogoro isiyokwisha kutokana na muda mwingi kutumika kutatua mizozo ya kisiasa badala ya kuleta maendeleo ya kiuchumi.
Hakuna maendeleo kunapokuwepo mizozo, kwani migogoro inaharibu maendeleo katika nchi, kwa hivyo watu wakubali kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa ndiyo mizozo itakwisha kwani tatizo liko wapi kufanya hivyo? alihoji balozi huyo.
Alisema ushauri wake unaweza kutumiwa katika uchaguzi mkuu ujao wa 2010 ambapo chama kitakachoshinda kinaweza kuunda serikali hiyo, kwa kuwa rais atakuwa aliyepata kura nyingi huku chama kingine kitapewa waziri kiongozi, ili kuweka mambo sawa katika nchi. Kwa kuwa hapa Zanzibar vyama vikubwa ni viwili tu, basi uchaguzi wa 2010 chama chochote kile kitakachoshinda kwa kura nyingi kitoe rais na kingine chenye kura chache kitatoa waziri kiongozi hilo ni jambo zuri sana, alisema.
Alisema utaratibu huo ndio suluhisho na unamaliza kabisa uhasama na chuki zilizojengwa kwa miaka kadhaa, ambapo wananchi wa Kisiwa na Unguja wamekuwa hawasikilizani kisiasa na wananchi wa Kisiwa cha Pemba kutokana na migongano ya kisiasa.
Alisema kwa miaka mingi Zanzibar imekwama kuleta maendeleo makubwa ya kiuchumi kutokana na hali tete iliyopo ya kisiasa, hivyo wananchi wa Unguja na Pemba wakae kufikiria suala la kuimarisha utawala bora na misingi mizuri ya kidemokrasia kwa kushirikiana kwa kuiletea maendeleo nchi yao kabla mambo hayajaharibika zaidi.
Alisema mivutano na migogoro imeanza tangu kuanza kwa uchaguzi wa kwanza katika mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 na hali hiyo imesababishwa na matokeo ya uchaguzi mkuu ambapo baadhi ya wananchi hawajaridhishwa na matokeo ya uchaguzi huo na hali hiyo imekuwa ikijirudia kila unapomaliza uchaguzi mkuu wa Zanzibar.
Alisema wananchi wa Unguja na Pemba ni wamoja kidamu, kwani wanaingiliana sana katika uzawa, hivyo si busara kupoteza muda kwa malumbano, hali ambayo inaweza kurekebishwa kwa mazungumzo ya pamoja kati ya pande mbili zinazovutana.
Tuwe na utamaduni wa kupunguza malumbano na kujenga taifa lenye umoja na mshikamano, hatuwezi kuepuka serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itatoa nafasi kwa wananchi wa vyama vyote, alisisitiza Karume.
Hata hivyo, alieleza kufurahishwa na mazungumzo yanayoendelea kati ya vyama vya CCM na CUF ambapo alitaka kuwekwa bayana zaidi, ili kila upande uweze kuyapanua mazungumzo hayo ya kutafuta muafaka wa kisiasa Zanzibar.
Kauli ya Balozi Karume ni miongoni mwa maoni ya wasomi na wataalamu wa fani mbali mbali yaliyowahi kutolewa nchini Tanzania ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar kuwa ndilo suluhisho pekee la mgogoro wa kisiasa visiwani hapa.
Ali Karume hivi karibuni ametangaza azima yake ya kuingia katika kinyanganyiro cha kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar ifikapo mwaka 2010, ambapo itakuwa ni mara ya pili kugombea nafasi hiyo, katika uchaguzi wa mwaka 2005 alijaza fomu za kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mi nawashangaa sana hawa watoto si watangaz tu ta ni kingdom.Jamaa hawezi kupata kabisa anajisumbua tu huyo ndio mana kaanza mapema ili watu wamjue but hamna kitu pale bora hata huyo FatmaMtu mwenyewe anavyoongea tu unamuona kabisa kwamba ameshindwa hata kabla hajaanza hiyo safari yenyewe. Tena wanatakiwa wamrudishe haraka sana nyumbani maana inaonekana hata kazi yenywe ya udiplomasia haiwezi kwa jinsi anavyobwabwaja!
Kwa mujibu wa gazeti la Majira la hivi majuzi Balozi Karume
ametuonya Wazanzibari wenzake tusifanye kosa la kumpa nchi "dereva wa teksi" aendeshe; tumpe "msomi" kama yeye. Huu ni wasia mwema kwani hata Mtume Muhammad (SAW) amesema. "Muislamu hang'atwi na nyoka mara mbili ndani ya shimo moja". Kukubali kung'atwa mara tatu utakuwauzembe uliokithiri.
Kwa maoni ya mheshimiwa, Wazanzibari "hawawezi kumkataa". Huu nao
ni ukweli usiopingika. Mathalan katika kura ya maoni Balozi wetu
atajaaliwa kupata kura tisa na mpinzani wake apate 42, atakayechaguliwa kuwa mgombea ni yeye. Kama mlango wa mbele umekomewa wa nyuma si upo? Vile vile katika uchaguzi utakaofuata Janjaweed (Janjawire) kwa Kiunguja, polisi na majeshi ya vita watahakikisha ushindi wa kishindo unapatikana. Baada ya hapo mgombea wetu ataapishwa haraka na ving'ora vitaingia mjini kutukumbusha kwamba aliyeingia madarakani ni A.K. wa tatu (AK III) mfano wa (George VI) n.k. siyo A.K.wa kwanza wala wa pili. Mchezo utaishia hapo ila kwa wale watakaothubutu huhoji.
Kweli kabisa mheshimiwa anaposema akitetea azma yake kugombea urais
wa Zanzibar mwaka 2010, kwamba hawana hoja wanaosema si vyema yeye
kugombea nafasi hiyo kwa vile kuna Karume wawili tayari wamemtangulia. Ni sahihi kabisa mfano wake kwamba Singapore nayo imetawaliwa na marais kadha kutoka familia moja. Analotunyima mheshimiwa wetu ni kutwambia kwamba katika miaka ambayo wana familia wa Lee Kuan Yew wameitawala Singapore nchi hiyo imejitoa kwenye kundi la nchi maskini na kujiingiza kwenye ulimwengu wa kitajiri na leo Singapore ni ngome ya uchumi mwema na demokrasia. Laiti kama mafanikio kama hayo au yanayokaribiana na hayo hata kwa mbali yangekuwa yamepatikana nchini mwetu, basi Wazanzibari kwa ujumla wetu tungeimba, "Marhaban, nawaje kina Karume, hata kama ishirini "
Kuhusu usomi tuchukue fursa hii kumkumbusha Balozi Karume kwamba
shahada za uzamili zimejaa vururu nchini mwetu, na wachumi wanatwambia bidhaa ikijaa sokoni thamani hupungua. Kama lengo ni ria, kama inavyoonesha basi ushauri wetu kwa Mheshimiwa Balozi ni huu: Jiunge na Chuo Kikuu Wazi uchukue masomo ya shahada ya juu zaidi na halahala usije shindwa njiani. Baadaye ukumbuke kwamba "Chema," chambilecho Waswahili, "chajiuza, kibaya chajitembeza". Wasomi wa kweli hawana haja ya kutamba hadharani. Wenyewe tunawafahamu.
Mwishowe mheshimiwa aniruhusu niulize tangu lini kukauka kwa wino
kwenye kadi ya uanachama kukawa sifa mojawapo ya uongozi ndani ya CCM?
Abdullah Masoud
Usishangae FM huyo jamaa sikumbuki hata mara ya mwisho kuishi tz hata kwa miezi mitatu ni lini mana katoka ujerumani kapelekwa italy na kabla ya hapo sikmbuki alikuwa nchi gani ila wakati umefika wa hawa mabalozi wa nchi kavu kupewa nchi hawa nao wanahitaji kutumikia nchi wakiwa nje sio akina karume kila muda ukiisha badala ya kurudi home anapelekwa nchi nyingine WHY?kWANINIIIIIINow wait a minute, haya ni maneno ya kutamkwa na mwananchi anayetaka kuwa rais wetu huko visiwani? Unajua hiii ndio faida ya secretive affirmative Act, ambayo bongo tumekuwa nayo kwa muda mrefu, yaani kuona kuwa pia kuna viongozi toka visiwani kwenye sekta zetu mbali mbali za taifa na sio wa bara tu! I mean yes kwa sababu huwezi kuniambia kuwa huyu ni balozi wetu tena wa Italy, among all the countries duniani!
Huyu si ndiye mwenye mke anaitwa Huda something na ambao wote hulewa na kulala popote, halafu anataka urais? Kwanza amekuwaje hata akafikia ubalozi? Huko foreign kuna wananchi wangapi wenye uwezo wamewekwa pemebeni? Anyway ni uamuzi wenu huko visiwani yaaani nimenawa mikono!
Yaaani kweli huyu utamuweka meza moja na kina Manongi, Mama Taji, Mama Mulamula, Francis, Komando, ambao wamesota huko foreign na hawana nchi mpaka leo?
Hao akina Karume mabalozi wapo wangapi?kutumikia nchi wakiwa nje sio akina karume kila muda ukiisha badala ya kurudi home anapelekwa nchi nyingine WHY?kWANINIIIIII
Maalim Seif kama mwanasiasa yuko tayari kuona mgombea mwenye udhaifu kama Ali anagombea, kuliko mtu kama Bilal.
SIKU chache baada ya Balozi wa Tanzania nchini Italia, Ali Karume, kutangaza azma yake ya kutaka kugombea urais wa Zanzibar mwaka 2010, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad amesema, balozi huyo ana uwezo kuliko kaka yake ambaye ni Rais wa sasa wa Zanzibar.
Katibu huyo wa CUF aliliambia gazeti hili katika mahojiano maalum wiki hii kuwa; "Ali ana unafuu mkubwa walau anaweza kukubalika. Ameanza kutambua matatizo yaliyopo Zanzibar, hii kidogo inanipa faraja kwamba kuna mtu anayeweza kutambua matatizo yaliyopo ndani ya nchi, alisema Maalim Seif.
Kweli huyu bwana kajaa kejeli tupu. Anawadhalilisha madereva tax kuwa hawakusoma au vipi. Je, amesahau kuwa Marehemu baba yake aliukwaa urais wakati alikuwa "KULI TU WA BANDARINI?". Kweli Nyani haoni KUNDULE.