UNLESS YOU ARE A "PROPER-GAMBA" DONT USE PROPAGANDA!!! Kwa kifupi Nape Moses Nnauye, ushindi wa Arusha ni beacon muhimu sana tunapoelekea kwenye chaguzi kubwa zijazo. Matokeo ya uchaguzi huu wa chini ni salamu kwa watu hawa muhimu na sababu kwenye mabano:Kwanza, Mwenyekiti Taifa - kwa kutokutoa pole kwa wafiwa arusha wakati wa mlipuko wa bomu katka mkutano wa CHADEMA. Alikubali kushiriki dirty politics. Kumbuka wananchi wa Arusha hata kama ni CCM wanaumia ndani kwa ndani. Pili, kwa Mwigulu Lameck Nchemba -kwamba CCM inaelekea shimoni kwa kauli zake zisizojenga. Yeye anafikiri ni wakati wote propaganda hufanya kazi. Nafikiri ni wakati wa kubadili tabia kama hawezi avae kondomu ya mdomo. Tatu, Moses Nape Nnauye, Abdulrahman Kinana na Wiliam Lukuvi - Kwamba watanzania wa leo siyo wa Enzi zile na pia kupigiwa makofi na meza bungeni haimaniishi kuwa usemacho kimekuwa na mashiko saaaana! Watanzania wanaona na kuchekecha kila kinachotokea. CCM inajizika yenyewe mchana kweupe. Nne kwa Makamnda wa juu jeshi la polisi -kwamba wananchi wakiamua hakuna linaloshindikana. Wacheze fair play na popote duniani serikali nyingi zimeanguka kwa wanajeshi, polisi na usalama kuingia katika siasa. Mimi naamini kesho kutwa Said Mwema akistaafu utasikia anagombea ubunge huko Hai au Moshi Mjini. Na mwisho, matokeo haya yanamuumbua moja kwa moja Anna Semamba Makinda Spika wetu-Kwamba Tanzania ni jadi yetu kushirikiana katika misiba na majanga. Kitendo cha kuendelea na mikutano ya bunge ili kukifurahisha chama chake kiliwaumiza wananchi wengi. Lusinde kule Arumeru alitukana jukwaani wananchi wakamshangilia lakini mioyoni wakaumia na wakafanya kweli kwenye sanduku la kura. Wananchi kila sehemu wana misiba mioyoni. Wataitoa tu kwa kuwatandika kwenye sanduku la kura!!! Tafakari!!! WAO WANA DOLA SISI TUNA MUNGU..........!