Uchaguzi una kushinda na kushindwa...

Uchaguzi una kushinda na kushindwa...

Poleni CCm jifunzeni siasa za kistaarabu, vinginevyo mtazidi kupoteza zaidi kwani mnaonekana kama wahuni fulani hivi.
 
attachment.php

Hodi hodi naingia jamvini, malenga mnipokee
Ujumbe wangu kumpelekea, meneja uchaguzi CCM
Umfikie aliko, akiomboleza chama chake kushindwa uchaguzi
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Uchaguzi ndivyo ulivyo, kuna mshindi na mshindwa
CCM mlijiamini, tena mno kupita kiasi
Badala ya kutangaza sera, mkawatumia wajeshi
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Mkawatisha wananchi, kwa mitutu na mabomu
Hofu kuu ilitanda, Jiji la Arusha likazizima
Wakazi wakakimbizwa, vijana kukamatwa
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Ikawadia siku ya uchaguzi, wakapiga wachache mno
Ukweli ukabainika, wengi waliopiga ni wana-CCM
Wana-CCM hao wakaamua, CHADEMA kuichagua
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Kumbe mlipowapiga CHADEMA, wana-CCM nao walichoka
Ahadi kedekede mlitoa, chache sana mlitimiza
Hali ikawa mbaya, vijana kukosa ajira
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Mkatangaza mikopo, kwa akinamama na vijana
Kumbe mliwaandaa, maswahiba zenu kuwapa
Wananchi wakabaini, mkenge kuingizwa
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Tamati najongea, malenga nahitimisha
Najua hamu bado mnayo, shairi hili kulisoma
Japokuwa vina halina, bado laitwa shairi
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Natumai mmejifunza, wananchi kutowadharau
Mabomu kutowapiga, bure bilashi kuwaua
Mnapovunja haki zao, mwawatakia nini
Usiomboleze sana Mwigulu, uchaguzi ndivyo ulivyo

Moderators, hamkunielewa maana yangu, labda kwa kuwa sikuwaomba. Lengo langu lilikuwa kuanzisha uzi wa kudumu, ambao ungetumika kuelezea hisia zetu kisiasa kupitia mashairi. Nilisahau kutoa mwongozo kwamba kila ambaye angejibu, alipaswa kutoa shairi, hata kwa ubeti mmoja. Lazima tuijenge na kuisheshimu lugha yetu Kiswahili.

Je, mnaweza kuirudisha post yangu kwenye uzi wake?
 
Nguruvi3,
Kwa kiasi fulani nakubaliana nawe kwamba low turn out might be in favour of chadema lakini kuna maangalizo muhimu:Kwanza, as we speak, sehemu nyingi in the electorate (kama mikoa, sio miji) ni aidha green column au too close to call; na kwa dynamics zilivyo, katika maeneo mengi, a low turn out itakuwa ni ushindi kwa ccm kuliko chadema, na hii itachangiwa na hoja yangu ya pili kwamba ccm is in a better position kuhakikishia wapiga kura wao ulinzi hivyo kuwahamasisha wajitokeze kwa wingi 2015; unless chadema nao kupitia mfumo wao mpya wa ulinzi they manage to gain that trust ya umma, otherwise low turn out katika most of the voting areas itakuwa ni ushindi kwa ccm in my humble view;

Chadema wanaweza to put up a good fight at the ballot box iwapo watafanya haya matatu kwa pamoja tena kwa UFANISI wa hali ya juu: Kwanza, kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura; Pili, Kuhakikishia wapiga kura wao usalama (aidha kupitia polisi au utaratibu utakaokubalika) kwa siku kadhaa kabla ya uchaguzi lakini muhimu zaidi, siku ya uchaguzi wanapotoka kwenye makazi yao kwenda kupiga kura na kurudi; na tatu ndio lije suala la kulinda masanduku ya kura; Vinginevyo bila ya kuhakikishia wapiga kura wao usalama, low turn out will prevail na wengi wa hawa itakuwa ni wale watakao hisi usalama wao upo, na wengi ya hawa watakuwa ni wana ccm, hence kuipa ccm ushindi kwa low turn out advantage;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Yes, Mchambuzi ni kweli ulichokisema.
Low turn out katika chaguzi zilizopita si kwasababu ya wananchi kutohamasika bali kulikuwa na mbinu ambazo CCM na tume ya uchaguzi ilikuwa inafanya.Mathalani matumizi makubwa ya kununua shahada za wapiga kura.

Pili, hili la Arusha nadhani ni special case ndio maana nikasema kura ilikuwa ya hasira ku-prove CCM wrong kwa kauli za viongozi, kutojali n.k. Ujasiri huo walikuwa nao wanachama wa CDM ambao ni victims.
Wale wa CCM wakaoga na ndicho kilichopelekea hiyo low turn out.
Mbinu ya CCM ya kutumia vyombo vya dola na kushabikia maafa ilikuwa mbovu sana.

Nadhani lazima Chadema wawe na daftari la wapiga kura wao, wahakikishe siku ya kupiga kura wanakwenda na kuwa na follow up ya kuhakikisha hakuna ununuzi wa shahada za wapiga kura.
Walinde kura zao katika vituo na muhimu zaidi watumie watu wao katika maeneo yao na wala si makapi kutoka CCM.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3, Mchambuzi,

..sasa ni maeneo mangapi watakuwa na hasira/usongo wa kwenda kupiga kura against CCM au CDM??

..je, kundi gani kati ya vijana, wazee, na wanawake, liko more likely kupiga kura ya hasira dhidi ya CCM,CDM,au chama chochote kile?

..mimi nadhani mwelekeo wa siasa za sasa hivi, kila chama kinajaribu kutafuta kura za hasira dhidi ya mwenzake. CCM wanadai wenzao ni wamwagaji wa damu hivyo wasichaguliwe. CDM nao wanadai wenzao ni mafisadi, na hameshindwa kutatua kero za wananchi.
 
Last edited by a moderator:
Nape kasahau kusema pia dalili ya mvua ni mawingu! Yaliyotokea Arusha ni dalili ya kuendelea kushinndwa kwa chama dola
 
Nguruvi3, Mchambuzi,

..sasa ni maeneo mangapi watakuwa na hasira/usongo wa kwenda kupiga kura against CCM au CDM??

..je, kundi gani kati ya vijana, wazee, na wanawake, liko more likely kupiga kura ya hasira dhidi ya CCM,CDM,au chama chochote kile?

..mimi nadhani mwelekeo wa siasa za sasa hivi, kila chama kinajaribu kutafuta kura za hasira dhidi ya mwenzake. CCM wanadai wenzao ni wamwagaji wa damu hivyo wasichaguliwe. CDM nao wanadai wenzao ni mafisadi, na hameshindwa kutatua kero za wananchi.
Mkuu JokaKuu, nianzie kujadili hoja zako kuanzia ulipomalizia.

Hili la kutuhumiana CCM wana wakati mgumu sana. Tuhuma zao kuwa Chadema wanataka kumwaga damu haziingii akilini mwa wananchi. Watu wanajiuliza ni kwa kutumia njia gani hawa watu wanataka kumwaga damu.

Kinyume chake wananchi wanaona wazi jinsi CCM inavyobebwa na Polisi na jinsi Polisi wanavyotumika kuwanyanyasa wapinzani. Nimesema hapo awali kuwa huu mkakati wa CCM kutumia vyombo vya dola ni mbovu sana.
Wapinzania wanaonekana kama mayatima na wanapata sympathy kirahisi sana.

Kuhusu kundi gani litapiga kura ya hasira, nadhani unaona jinsi vijana walivyokumbatia mabadilliko.
Zamani siasa ilikuwa jambo la wazee na akina mama, siku hizi ni suala la vijana na hao wazee hata kushiriki wanaogopa kwasababu wanaona kama wakati umeshawapita.

Kundi hili la vijana ndilo pia kundi linaloathirika sana na mabomu ya machozi, virungu na kutiwa ndani bila sababu.
Mfano, Arusha wamekamata wapiga picha na yoyote mwenye Camera ili mradi tu.
Ukiangalia wapiga kura waliokataa kutishwa 70% ni vijana ambao likely walinyanyaswa na Polisi

Likitokea jambo watu wa mwanzo kuathirika ni kundi la vijana.
Ndilo kundi lenye hasira na mfumo mzima wa siasa, uchumi,uonevu na sasa unyimwaji wa haki za kushiriki katika mambo ya kisiasam,lipo more likely kupiga kura ya hasira kwa CCM ambayo imepoteza sehemu kubwa ya kundi hili.

Kwa upande wa kura ya huruma, CCM wanategemea akina mama watu wazima na si vijana kwa mazoea tu kuwa uwepo wa amani ni matokeo ya utawala na kwamba yanayotokea hayakuwepo siku za nyuma. Ni kundi linaloishi kwa historia na hisia na halipendi mabadiliko.

Kundi la wanaume wenye umri kupindukia ujana linaegemea sana upande wa wapinzani.
Sababu kubwa ni hasira kutokana na mambo yanavyokwenda hasa katika rushwa, ukosefu wa maadili n.k yanayotokana na CCM na serikali yake. Ni kundi la wastaafu au wastaafu watarajiwa ambalo linaona limemenyeka na sasa watu wanakula tena kwa gharama kubwa za vijana wao. Ni kundi linalohisi kuwa uzalendo haukulisaidia kimaisha na hivyo lipo likely kupiga kura against CCM.

Ushahidi kuwa CCM ipo matatani ni kuzingatia kuwa kila chaguzi wana loose ground na wapinzani wana gain ground. Na angalia nani wapo behind the oppositions' success.

Habari za siri kuvuja kutoka ndani ya CCM au serikali ni kutokana na uwepo wa makundi mawili niliyotaja.
Wengi wao ni wanachama wa CCM kwa mafao lakini wana sympathy kubwa sana na opposition kama nilivyoeleza.

Maeneo gani yatakayokuwa na hasira na CCM, hili lipo wazi sasa. Arusha CCM wameshasalim amri na kura za chuki zitaendelea. Kilimanjaro chuki imeshaingia katika wilaya tiifu za Mwanga na Same na CCM ipo neck in neck na wapinzani.

Mwanza kuna kura za chuki, Igunga, Morogoro mjini, Mbeya, Tarime na Bukoba.Hayo ni maeneo ambayo wagombea wa CCM wanaweza kushindwa kwa kura ya chuki bila kujali ni wazuri na weledi kiasi gani.

Utashangaa kama nikikuambia kuwa Mtwara mjini imeshaondoka mikononi mwa CCM na sasa ni swing constituent, Singida ni hotbed kwa CCM na kuna ondoka chini ya umiliki wa CCM.Tukio la Mwangosi linaiweka Njombe kama toss up constituent

Kwa Dar CCM wapo salama Ilala na Kigamboni. Kinondoni sasa ni toss up.
Kwa Tanga jimbo la kwanza kufanya uasi dhidi ya CCM litakuwa Muheza mjini na ushawishi wa Muheza kwa mkoa wa Tanga hasa Tanga mjini ni mkubwa sana.

Uwezekano wa Lushoto kupoteza jimbo moja kati ya mawili ni mkubwa sana kuliko ilivyowahi kuwa huko nyuma
CCM bado ni salama Korogwe na Handeni.

Kwa haraka haraka, Kigoma, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Mara, Bukoba, Mbeya, Iringa yameshaondoka CCM.
Morogoro, Mtwara mjini na Masasi, Singida, Igunga,Muheza, Lushoto, Same, Mwanga, Kindondoni, Njombe haya ni toss up na likely kutumia kura ya adhabu dhidi ya CCM.

CCM wanabaki salama Ruvuma, Lindi, Dodoma, Pwani, Simiyu, Morogoro vijijini, Katavi, Shinyanga.
 
Mkuu JokaKuu, nianzie kujadili hoja zako kuanzia ulipomalizia.

Hili la kutuhumiana CCM wana wakati mgumu sana. Tuhuma zao kuwa Chadema wanataka kumwaga damu haziingii akilini mwa wananchi. Watu wanajiuliza ni kwa kutumia njia gani hawa watu wanataka kumwaga damu.

Kinyume chake wananchi wanaona wazi jinsi CCM inavyobebwa na Polisi na jinsi Polisi wanavyotumika kuwanyanyasa wapinzani. Nimesema hapo awali kuwa huu mkakati wa CCM kutumia vyombo vya dola ni mbovu sana. Wapinzania wanaonekana kama mayatima na wanapata sympathy kirahisi sana.

Kuhusu kundi gani litapiga kura ya hasira, nadhani unaona jinsi vijana walivyokumbatia mabadilliko.
Zamani siasa ilikuwa jambo la wazee na akina mama, siku hizi ni suala la vijana na hao wazee hata kushiriki wanaogopa kwasababu wanaona kama wakati umeshawapita.

Kundi hili la vijana ndilo pia kundi linaloathirika sana na mabomu ya machozi, virungu na kutiwa ndani bila sababu.
Mfano, Arusha wamekamata wapiga picha na yoyote mwenye Camera ili mradi tu. Ukiangalia wapiga kura waliokataa kutishwa 70% ni vijana ambao likely walinyanyaswa na Polisi

Likitokea jambo watu wa mwanzo kuathirika ni kundi la vijana. Ndilo kundi lenye hasira na mfumo mzima wa siasa, uchumi,uonevu na sasa unyimwaji wa haki za kushiriki katika mambo ya kisiasa.
Kundi la vijana lipo more likely kupiga kura ya hasira kwa CCM na CCM imepoteza sehemu kubwa ya kundi hili.

Kwa upande wa kura ya huruma, CCM wanategemea akina mama watu wazima na si vijana kwa mazoea tu kuwa uwepo wa amani ni matokeo ya utawala na kwamba yanayotokea hayakuwepo siku za nyuma.
Ni kundi linaloishi kwa historia na hisia na halipendi mabadiliko.

Kundi la wanaume wenye umri kupindukia ujana linaegemea sana upande wa wapinzani.
Sababu kubwa ni hasira kutokana na mambo yanavyokwenda hasa katika rushwa, ukosefu wa maadili n.k yanayotokana na CCM na serikali yake. Ni kundi la wastaafu au wastaafu watarajiwa ambalo linaona limemenyeka na sasa watu wanakula tena kwa gharama kubwa za vijana wao. Ni kundi linalohisi kuwa uzalendo haukulisaidia kimaisha na hivyo lipo likely kupiga kura against CCM.

Ushahidi kuwa CCM ipo matatani ni kuzingatia kuwa kila chaguzi wana loose ground na wapinzani wana gain ground. Na angalia nani wapo behind the opposition success.
Habari za siri kuvuja kutoka ndani ya CCM au serikali ni kutokana na uwepo wa makundi mawili niliyotaja.
Wengi wao ni wanachama wa CCM kwa mafao lakini wana sympathy kubwa sana na opposition kama nilivyoeleza.

Maeneo gani yatakayokuwa na hasira na CCM, hili lipo wazi sasa. Arusha CCM wameshasalim amri na kura za chuki zitaendelea. Kilimanjaro chuki imeshaingia katika wilaya tiifu za Mwanga na Same na CCM ipo neck in neck na wapinzani. Mwanza kuna kura za chuki, Igunga, Morogoro mjini, Mbeya, Tarime na Bukoba.
Hayo ni maeneo ambayo wagombea wa CCM wanaweza kushindwa kwa kura ya chuki bila kujali ni wazuri na weledi kiasi gani.

Utashangaa kama nikikuambia kuwa Mtwara mjini imeshaondoka mikononi mwa CCM na sasa ni swing constituent, Singida ni hotbed kwa CCM na kuna ondoka chini ya umiliki wa CCM.
Tukio la Mwangosi linaiweka Njombe kama toss up constituent

Kwa Dar CCM wapo salama Ilala na Kigamboni. Kindondoni sasa ni toss up.
Kwa Tanga jimbo la kwanza kufanya uasi dhidi ya CCM Llitakuwa Muheza mjini na ushawishi wa Muheza kwa mkoa wa Tanga hasa Tanga mjini ni mkubwa sana.
Uwezekano wa Lushoto kupoteza jimbo moja ni mkubwa sana kuliko ilivyowahi kuwa huko nyuma
CCM bado ni salama Korogwe na Handeni.

Kwa haraka haraka, Kigoma, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Mara, Bukoba, Mbeya, Iringa yameshaondoka CCM.
Morogoro, Mtwara mjini na Masasi, Singida, Igunga,Muheza, Lushoto, Same, Mwanga, Kindondoni, Njombe haya ni toss up na likely kutumia kura ya adhabu dhidi ya CCM.

CCM wanabaki salama Ruvuma, Lindi, Dodoma, Pwani, Simiyu, Morogoro vijijini, Katavi, Shinyanga.
mkuu hii post usisahau kuiweka kule kwenye jamvi kubwa.
 
Sasa kama majibu ni haya hayo mengineyanini? Utayafungulia ukifunguaeeee....
Sawa kwani umeanza wewe? Tunaye Kibajaj then wamekuja kina Nkamia nk nk... Ndivyo mlivyo.

Mkuu kuna kitu gani usichoelewa? Mimi kama muumini nataekeleza nguzo ya dini yangu; huu sio wakati muafaka kwangu kujibishana na vichaa na waganga njaa; Ibada kwangu mbele siabubu mtu wala chama; mfungo ukisha tutakesha kama kawaida; hakuna hata mmoja kati yenu nyie waganga njaa anayeniumiza kichwa wala kunikosesha usingizi. Mimi sio muajiriwa wa CCM wala sitegemei riziki yangu kutoka huko.
 
Foum Jnr,

..huko CCM karibia kila kiongozi ni liability.

..sijui kama ulisoma ile post ya Mwingulu Nchemba akizungumzia red brigade vs green guard.

..kwa kweli inashtusha, kama siyo kusikitisha, kwamba imefika mahali CCM ina mtu wa hovyo kama Mwigulu Nchemba ktk nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.

..sasa kama CCM imefika hapo, hivi kweli unategemea wanaweza kujitathmini?

cc: NasDaz, chama, Jasusi, Mchambuzi, HAMY-D

JokaKuu,

Awali ya yote nianze kwa kupingana na wewe kuwa ndani ya CCM kila mtu ni liable kwa matendo yanayo endelea.

Kumbuka huu msemo, "kila mtu awajibike kwa vitendo vyake mwenyewe", huu msemo unaingia mpaka ndani ya CCM.

Wana CCM sio miungu, ni watu, na hakuna mtu aliye kamilika, kama kutatokea mapungufu yoyote, tuna utaratibu wa ndani ya chama wa namna ya kurekebisha na kuwajibisha.

Ukiona kuna mtu ndani ya CCM ana chukiwa na wapinzani, ujue huyo ni mwiba kwa wapinzani hao.

CHADEMA wamekuwa vinara wa siasa majitaka, katika hali kama hiyo wanapaswa wapate mtu anaeweza kuwadhibiti na siasa za aina hiyo, Mwigulu is a right person for such job.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi,

..hata mimi nimeshangazwa na hii low turn out.

..labda wananchi waliogopa vurugu.

..sasa ktk mazingira hayo inaelekea it came down to upande gani walikuwa na USONGO zaidi wa kupiga kura.

..kitu kingine ni campaign tactics za Mwigulu na Nape. Je, watu viongozi hawa wanakisaidia chama au la??

cc: NasDaz, chama, Nguruvi3
Mkuu JokaKuu,
Hili la turn out ni jambo la kutisha kiasi cha kushindwa kutotoa picha halisi ya Arusha!! Kwa maoni yangu, suala hili limewasaidia zaidi CHADEMA kuliko CCM kutokana na aina ya wapenzi/wanachama/mashabiki wa CHADEMA ilionao as compared to CCM!!! Hawa wa CHADEMA ni kama watu waliobadili dini au kumjua mungu siku za karibuni; hivyo huwa ni watu wa kufanya ibada kwelikweli kuliko waumini wa siku nyingi, ambao ni wana-CCM au natural born believers kama tulivyo wengi wetu.....umekuta baba na mama anaamini hiki, basi nawe unaamini hiko hiko....more often than not; this starts on not what you really believe but what others believe! Hapa hakuna msisimko!!

Lakini vile vile, akili ya kawaida inanishawishi kuamini kwamba ni rahisi watu kujitoa muhanga kuondoa utawala madarakani kuliko kuhakikisha unabaki madarakani! So, kwavile wana-CHADEMA wana-fight kuindoa CCM madarakani basi ni rahisi sana wao kufanya chochote kwenda kupiga kura; with the hope of expected changes as compared to wana-CCM ambao hakuna jipya wasilofahamu kuhusu CCM yao!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kuna kitu gani usichoelewa? Mimi kama muumini nataekeleza nguzo ya dini yangu; huu sio wakati muafaka kwangu kujibishana na vichaa na waganga njaa; Ibada kwangu mbele siabubu mtu wala chama; mfungo ukisha tutakesha kama kawaida; hakuna hata mmoja kati yenu nyie waganga njaa anayeniumiza kichwa wala kunikosesha usingizi. Mimi sio muajiriwa wa CCM wala sitegemei riziki yangu kutoka huko.

Nisichokielewa ni pale unapojipinga mwenyewe.
Eleweka kwanza ndipo nikuelewe.
 
Waziri wa Mawasiliano ambaye ni mgeni rasmi wa kutoa zawadi za stories of change amesema yeye ni member wa Jamii Forums

Amesema tofauti na wengine yeye ana ngozi ngumu ya kustahimili matusi. Na wakati mwingine huwa anayasoma kabla ya kulala.

Possibly Nape anatumia ID ambayo haijulikani so kuweni makini mnapotukana watu.

Nafuatilia youtube

View attachment 2420687
This is true, Nape ni mwenzetu humu, tupo naye kwa ID yake ya nape mnauye, ila pia yupo yupo!.
Mwenye ngozi ngumu ni hapa JF ni Pascal Mayalla wengine ngozi ya u-bwbw
Naomba kuthibitisha ana ngozi ngumu!.
P
 
Naona leo Paschal Mayala ameamua kufufua nyuzi za Nape maana nimekuta notification za kutosha kumbe content ni moja
 
Back
Top Bottom