Uchaguzi ujao utakuwa mwepesi sana kwa CCM tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe hapa nchini

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,338
9,766
Ndugu zangu watanzania,

Uchaguzi ujao Ni uchaguzi ambao CCM inakwenda ikiwa na ushindi mkononi, uchaguzi ambao CCM inakwenda ikiwa na Matokeo ya ushindi wa kishindo, Hii Ni kutokana na kazi kubwa Sana iliyofanywa na serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia katika utekelezaji wa ilani ya CCM.

CCM inakwenda katika uchaguzi huo ikiwa na uungwaji mkono na kibali na baraka kutoka makundi yote kutokana na utendaji kazi wa serikali yake uliyogusa makundi yote pasipo kumwacha mtu nyuma au kundi lolote lile,Inakwenda katika uchaguzi huo ikiwa imejibu maswali yote na kero zote kubwa kwa kuzipatia majibu ya kuridhisha.

CCM inakwenda katika uchaguzi huo ikiwa imejiwekea Rekodi mpya ya maendeleo katika secta zote kuanzia Elimu ambapo Sasa Ni bure Hadi kidato Cha sita, huku ikiwa imeongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu kufikia biliioni 654 kiasi kilichopelekea wanafunzi wote wenye sifa kupata mikopo bila shida ya aina yoyote pamoja na kuongeza fedha za kujikimu kufikia elfu kumi kwa siku Jambo lililoibua shangwe kubwa Sana hapa nchini.

CCM inakwenda katika uchaguzi huo ikiwa imejihakikishia kura za Ndio kwa wakulima baada ya kuwafuta machozi na kuwaheshimisha kwa kukifanya kilimo ni biashara na hivyo kuwafanya kunufaika na jasho lao,huku mabillioni ya Ruzuku takribani billioni Mia moja hamsini yakiwa yametolewa na serikali ya CCM zilizo pelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu.

CCM inakwenda katika uchaguzi huo ikiwa inaungwa mkono na wafanyabiashara wote hapa nchini baada ya kuwa mazingira ya biashara yameboreshwa kwa kuweka Sera nzuri na kuwa na maafikiano mazuri na yenye Afya na tija katika ukadiriaji wa Kodi ,Sasa biashara zinafunguliwa kila Kona ya nchi hii badala ya kufungwa,Sasa TRA na maafisa wake wanatenda haki na kuwatendea haki wafanyabiashara na hivyo kujenga Hali ya kuaminiana katika ulipaji wa Kodi,Hali iliyopelekea kupanda kwa mapato kufikia Trioni mbili kwa Mwezi.

Ni uchaguzi utakao kuwa mwepesi Sana kwa CCM kupita na kuweza kushinda,inakwenda kuzoa Kura kwa kishindo Sana katika nafasi zote,Ni historia mpya inakwenda kuandika hapa nchini katika uchaguzi huo.

Kazi Iendeleee mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu

0742-676627
 
Mtakoma 2025. Lile fisadi la msoga lilisikika likisema labda mambo yaharibike saaana! Hiiiiiii bangosha!
Uwe na adabu wewe, Hakuna chama chenye uwezo wa kuitikisa CCM,Hakipo chama hicho na Wala hakitatokea,Vyama vya upinzani vilivyopo Ni vikundi vya usaka tonge
 
Ndugu zangu watanzania,

Uchaguzi ujao Ni uchaguzi ambao CCM inakwenda ikiwa na ushindi mkononi, uchaguzi ambao CCM inakwenda ikiwa na Matokeo ya ushindi wa kishindo, Hii Ni kutokana na kazi kubwa Sana iliyofanywa na serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia katika utekelezaji wa ilani ya CCM.
Uchaguzi 2025 utayeyuka ikiwa CCM watakaza shingo na kukataa Katiba mpya na TUME HURU ya UCHAGUZI.

Nashauri wadau wakuchangie kupitia namba hizo Ili upoze njaa, maana Hali ni Tete!!
 
Uchaguzi 2025 utayeyuka ikiwa CCM watakaza shingo na kukataa Katiba mpya na TUME HURU ya UCHAGUZI.

Nashauri wadau wakuchangie kupitia namba hizo Ili upoze njaa, maana Hali ni Tete!!
Atakaye kimbia uchaguzi au kushiriki uchaguzi Wala hataizuia CCM kushika Dola maana watanzania Wana Imani kubwa Sana na ccm
 
Ndugu zangu watanzania,

Uchaguzi ujao Ni uchaguzi ambao CCM inakwenda ikiwa na ushindi mkononi, uchaguzi ambao CCM inakwenda ikiwa na Matokeo ya ushindi wa kishindo, Hii Ni kutokana na kazi kubwa Sana iliyofanywa na serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia katika utekelezaji wa ilani ya CCM.

Hakuna uchaguzi Tanzania, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Machafuko au mapinduzi tu ndio njia ya kuitoa CCM madarakani, maana hakuna mtu anayejitambua ataenda kupoteza muda kwenye box la kura lisiloheshimika.
 
Kwa hiyo mmepanga kuiba kura zote kwa kishindo.
 
Atakaye kimbia uchaguzi au kushiriki uchaguzi Wala hataizuia CCM kushika Dola maana watanzania Wana Imani kubwa Sana na ccm
Unajua nguvu ya umma?

Nguvu ya Dola inatokana na umma, nadhani unaweza jua kati ya Umma na Dola nani boss.
 
Ndugu zangu watanzania,

Uchaguzi ujao Ni uchaguzi ambao CCM inakwenda ikiwa na ushindi mkononi, uchaguzi ambao CCM inakwenda ikiwa na Matokeo ya ushindi wa kishindo, Hii Ni kutokana na kazi kubwa Sana iliyofanywa na serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia katika utekelezaji wa ilani ya CCM.
Unatuchosha na huu upuuzi wako. Kama itashinda,hofu ya nini Sasa? Sio ndio Raha yako.
Kwa nini uweweseke?
 
Unatuchosha na huu upuuzi wako. Kama itashinda,hofu ya nini Sasa? Sio ndio Raha yako.
Kwa nini uweweseke?
Ni furaha ya watanzania kuona CCM inashinda kwa kishindo kwa kuwa wanakuwa na Imani kuwa ushindi wa CCm ni ushindi wa Taifa na kuwa katika mikono salama, ushindi wa CCm Ni usalama wa Rasilimali zetu
 
Hakuna uchaguzi Tanzania, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Machafuko au mapinduzi tu ndio njia ya kuitoa CCM madarakani, maana hakuna mtu anayejitambua ataenda kupoteza muda kwenye box la kura lisiloheshimika.
Tindo rafiki yangu naomba nikwambie kuwa hakuna wa kuleta machafuko nchii hii Wala kuingia Barabarani kuipinga serikali hii shupavu ya CCM,Kama huamini maneno yangu Basi anzisha wewe hayo maandamano na uwe mstari wa mbele, au kamuulize lisu kilichomkuta 2020 ambapo Hadi wewe ulimsaliti kwa kukataa kuingia Barabarani na kubaki umejificha chumbani kwako
 
Back
Top Bottom