Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 8,154
- 11,561
Mapungufu madogo madogo na kasoro chache zilizopo, vipo pia kila mahali inapotekelezwa demokrasia ya aina ya Tanzania, mathalani Marekani na kwingineko.
Na kwasababu hiyo uchaguzi huru na wa haki Tz upo, Tume huru ya uchaguzi Tz ipo, Utawala wa Sheria na utawala bora Tz upo, heshima kwa haki za binadamu na makundi maalumu Tz vipo, uhuru wa maoni, habari, vyombo vya habari na mawasilino Tz vipo, uwazi na uwajibikaji Tz upo, bunge na mahakama huru Tz vipo, usawa na haki ya kupata huduma za msingi Tz vipo, ulinzi na usalama wa watu, mali na makazi yao Tz vipo, uhuru wa kuabudu na kuabudiwa Tz upo, uhuru wa kutoa na kupokea sadaka na misaada Tz upo, nakadhalika nakadhali, nakadhalika, nakadhalika.....
Tunaweza kutofautiana kwa kiwango cha kuridhika cha utekelezaji wa Demokrasia hii ya vyama vingi Tanzania na ufanisi wake. Na hiyo ni haki na ni Demokrasia ya maoni, kutofautiana na kukubaliana kutofautiana.
Mathalani, wingine anaweza kusema hakuna kabisa demokrasia, mwingine akasepa ipo kidogo, mwingine akasema ipo sana, na mwingine akasema hana maoni kabisa juu ya Demokrasia Tanzania, nakadhalika, nakadhalika, nakadhalika...
Lakini, ukweli usemwe,
Amani, Utulivu na utangamano miongoni mwa waTanzania ni matokeo na matunda matamu ya utekelezaji wa Demokrasia nchini. Ni muhimu sana hali hii ya ustahimilivu na kuvumiliana kuimarishwa zaidi ndani ya mioyo ya wanasiasa na watanzani wote ile umaja wetu usitetereke.
Maendeleo ya watu na makazi yao, maendeleo ya biashara, utalii, miundombinu ya barabara, anga, maji, reli, afya elimu, michezo na vyote vinavyoonekana na visivyo onekana kisiasa, kiuchumi na kijamii ni zao la Demokrasia ya vyama vingi nchini.
Kwa kiwango kikubwa sana maendeleo yanayonekana hivi sasa yamechochewa pakubwa sana na utekelezaji wa demokrasia ya vyama vingi. Mathalani uwazi, uwajibikaji, ulinzi na usalama serikalini.
Changamoto ndogo ndogo na kasoro chache zilizopo na mara nyingi huonekana nyakati za uchaguzi, zinarekebishika na kutatulika ikiwa tu utashi wa kisiasa na dhamira ya kweli miongoni mwa wanasiasa utawekwa kwenye mizania sawa kwa maneno na matendo, kwa maslahi mapana ya umoja na mshikamano wa Tanzania.
Njia zinazotumiwa na wanasiasa kujaribu kushinikiza marekebisho ya mapungufu na kasoro za kidemokrasia nchini, zinarefusha zaidi kupata majawabu. Ushari wa maneno ya wanasiasa dhidi ya serikali, amri na matakwa ya lazima ya wanasiasa dhidi ya serikali, ubabe na utoto wa wanasiasa dhidi ya serikali, nakadhalika nakadhalika nakadhalika.....
Hakuna ungwana, ustaarbu wala utashi katika kauli na matendo miongoni mwa wanasiasa dhidi ya serikali. Ni kutunishiana misiuli kusiko koma, kutwa kucha ni kiburi na majivuno cha eti chama hiki au kile kina wafuasi wengi kuliko kingine na kwahivyo kina haki zaidi na kinaweza kufanya chochote itakacho.
Hii si sawa.
Huu ni mwanzo wa kuharibu na kumomonyoa demokrasia ambayo tayari imekomaa, imeimarika, inashamiri na kunawiri vizuri sana nchini.
Kama raia wa Tanzania navisihi vyama vya siasa na wanasiasa, vyama vya kiraia, taasisi za dini na makundi mbalimbali ya kutetea haki nchini,
fanyieni vyovyote mfanyavyo kwa mujibu wa sheria.
Lakini chondechonde, matokeo ya hayo yote muyafanyayo iwe ni Amani, Amani, Amani, ya huyu Mama Yetu Tanzania.
wasaalam.....