Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,057
Hakukuwahi kuwa na kura ya maoni ya kuwauliza wananchi kama wanataka mfumo wa vyama vingi au kuendelea na mfumo wa chama kimoja.
Hakukuwahi kuwa na tangazo lolote la kuwataka wananchi watoe maoni mahali popote kama wanataka mfumo wa vyama vingi.
Kilichofanyika ni kwamba wakati uchumi wa nchi umedorora sana, na nchi inahitaji usaidizi wa mataifa makubwa, na kunyimwa, sababu mojawapo ikiwa uminywaji wa demokrasia, Mwalimu Nyerere alitamka kwenye kikao cha Halmashauri Kuu kuwa tunalazimishwa kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi wakati wananchi hawaoni huo umuhimu. Ebu tuulizane kama kweli kuna haja hiyo?
Kama ilivyo kawaida ya CCM, hufanya mambo kwa unafiki wa kumfurahisha Mwenyekiti wao, wakijua kuwa Mwalimu hataki mfumo wa vyama vingi, wakaulizana humo ndani ya chama, wakamwendea Mwalimu na kumwambia kuwa wananchi hawataki mfumo wa vyama vingi.
Mwalimu Nyerere kwa sababu alijua taarifa ile ni ya uwongo, na wala hakujafanyika kura yoyote ya maoni, na mazingira ya kiuchumi yakiwa yameibana nchi, akayapuuza yale maoni, na kusema nchi itaingia kwenye mfumo wa vyama vingi. Viongozi wanafiki wa CCM, kama kawaida yao wakashangilia na kumpongeza Mwalimu Nyerere kwa uamuzi huo.
Kwa hiyo ni uwongo kusema kuwa wananchi waliulizwa kuwa kama wanataka mfumo wa chama kimoja au vyama vingi, halafu wananchi wakatamka kuwa wanataka mfumo wa chama kimoja. Mahojiano yalifanyika kwenye vikao vya CCM, siyo kwa umma wa wananchi wote.