Mtela Mwampamba
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 537
- 347
Kwa ufupi
Monduli. Kampeni za kuwania nafasi ya udiwani katika Kata ya Makuyuni wilayani Arusha juzi ziliambatana na tukio la kuchekesha baada ya wazee wa huko kupata wakati mgumu kutamka jina la
CHADEMA ambacho ni kifupi cha jina la Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Kata ya Makuyuni ina wakazi wengi ambao kwa kawaida huwa ni wafugaji na hawafahamu vizuri Lugha ya Kiswahili kutokana na maisha yao ya kijadi.
Mzee mmoja aliyetajwa kwa jina la Olengalepo aliwachekesha watu kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Naiti wakati aliposhindwa kutamka jina CHADEMA na badala yake kusema Sabena.
"Hawa Sabena (CHADEMA) kwani wametokea wapi?" alihoji Mzee huyo licha ya Mbunge wa Monduli, Lowassa kumwelimisha kwamba ni CHADEMA na siyo Sabena.
Mzee Olengalepo alichekesha zaidi watu wakati alipomjibu Lowassa."Hiyo hawezi mimi tamka, maana siijui." Jibu hilo lilifanya watu kuangua kicheko zaidi wakati wa mkutano huo ulioanza saa nane mchana kijijini hapo.
Tukio hilo limetokea baada ya Lowassa kuibua staili mpya ya kampeni ya chama chake, ambapo badala ya kuhutubia amekuwa akiwapa nafasi wananchi kupanda jukwaani na kuzungumza.
Lowassa anaongoza kampeni ya CCM ya kutetea kiti cha udiwani wilayani Monduli, ambao uchaguzi wake unafanyika Jumapili hii.
Goodluck Lerunya anawania nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM wakati Japhet Sironga ndiye anapeperusha bendera ya CHADEMA kwenye jimbo hilo.
Chanzo:gazeti la mwananchi
Tar.13/06/2013
- Tukio hilo limetokea baada ya Lowassa kuibua staili mpya ya kampeni ya chama chake, ambapo badala ya kuhutubia amekuwa akiwapa nafasi wananchi kupanda jukwaani na kuzungumza.